mimi ni Neema Idabu au mama Irene nimezaliwa iguguno singida nilizaliwa mwaka 1984
Toka nazaliwa mpenzi msikilizaji niliishi singida kwa maisha ya tabu sana kutokana na mazingira ya kuzaliwa kwangu yaani ni aibu sana na roho huwa inaniuma sana kila nikikumbuka yote yaliyopita ktk maisha yangu kutokana na jinsi ambavyo nimezaliwa najiona kama si mmoja wa binadamu kwanini nilizaliwa hivi
Mpenzi msikilizaji wa mikasa ya maisha mpaka nafikisha miaka 6 nilikuwa nikiishi singida kwa maisha ya tabu sana hapa mama yangu alikuwa akiishi na bibi yangu na babu ila huyu babu hakuwa baba yake mama yangu wa kumzaa kwakua bibi alibakwa na mwanaume wakati wa utoto wake na ndipo akazaliwa mama yangu kwahiyo baadae bibi aliolewa na babu anayeishi nae sasa na babu huyu akakubali kumlea mama yangu hivyo mama yangu hamjui baba yake
Wakati mama anakaa kwa bibi siku moja kuna babu alikuja kwa bibi na kwakati huo mama alikuwa nyumbani pekee babu akamlazimisha mama kufanya nae mapenzi mama akakataa ndipo babu akamwingilia mama kwanguvu na kumwondoa usichana na mama akabeba mimba yangu nikazaliwa mimi mpenzi msikilizaji wa mikasa ya maisha haya yote nilikuja kuhadidhiwa na mama yangu mzazi
Baada ya kubeba ujauzito bibi yangu yaanii mama yake na mama yake alimuuliza mama kuwa imba ni ya nani alishindwa kueleza kwakua ilikuwa vigumu kwake lakini alivyoteswa sana ikabidi tu kusema ukweli kwa bibi yangu yangu kwamba ni babu alimbaka kwa nguvu na kumsababishia ujauzito baada ya kusema tu hivyo bibi alistuka na kuanguka chini akapoteza fahamu
Baada ya siku moja bibi alizinduka na akaanza kulia sana alilia sana msikilizaji kila mara alipokuwa akimwona babu alikuwa akilia sana kwanini babu alimbaka mama yangu au kwakua si mototo wake wa kumzaa bibi alikuwa akilaumu na kulia sana huku akijuta kukubali kuishi na babu na akipiga kelele na kusema laana sasa imeingia ktk ukoo wetu bibi alilia sana hata wakati mama ananisimulia haya nay eye machozi yalikuwa yakimtoka lilikuwa ni jambo la kuumiza sana mpenzi msikilizaji na mtangazaji
Baada ya maumivu ya mda mrefu bibi alimuuliza babu kwanini aliamua kufanya kitendo hicho babu aliomba msamaha sana na kusema kuwa ni shetani tu alimpitia na akamwomba sana bibi amsamehe pia mama yangu amsamehe babu alipokubali kuwa alimbaka mama yangu bibi alilia sana na hakuamini kweli kama kitendo kile kingeweza kufanywa na mume wake mwishoe ukoo ukakaa na babu akaomba msamaha bibi akadai ni vigumu sana kumsamehe babu kwani inamkumbusha jinsi yeye alivyobakwa
2
Na sasa mototo wake na yeye kabakwa tena na mtu ambaye alikuwa akimtegemea kuwa mlinzi wa motto wake leo kageuka bibi alilia sana tene kwenye kikao hicho mwishoe kikahairishwa kwakua bibi hakuwa tayari kumsamehe babu
Ilikuwa uchungu sana basi bibi akaamua kumuua babu siku hiyo bibi alipika chakula akakitia dawa ya kuua panya akamwekea babu ktk chakula baada ya kula babu alianza kuumwa sana na tumbo sana na alipokua anahitaji msaada bibi hakuangaika badala yake akamwambia hayo ndo malipo yako kwa ulichokifanya kwa kumbaka motto wangu zawadi iliyokuwa ikikungoja kwa muda mrefu ni kifo na sasa umekipata
Kwakua ilikuwa usiku babu hakupata msaada wowote alifia pale mama yangu akimtizama lakini bibi aliondoka usiku ule ule na mpaka sasa hajaonekana ndivyo mauti yalivomfika babu yangu kwa bibi kuamua kumuuua babu na akatoroka mpaka leo sijui bibi yangu alipo na sielewi yuko wapi nab ado yupo hai ama la baada ya hapo mama alibaki peke yake akilea mimba yangu wakati huo mimba ilikuwa na miezi minne
Nliishi kwa shida kubwa kwakua alikuwa akiishi peke yake watu wote wa kijijini pale walimtenga wakisema kuwa ni motto wa muuaji hivyo aliteseka sana na pia kwakua hakuwa na kazi yeyote pale kijijini mpaka miezi tisa ya kujifungua lipofika alipojifungua tu aliona maisha kuwa magumu sana na aliendelea kutengwa kwa kuonekana sababu ya mauaji ya babu yangu na motto wa muuaji hivyo akaamua kuondoka singida na akaondoka na kwenda babati na akafikia kwa mama anaitwa mama pendo akatupokea
Mama pendo alikuwa anafanya kazi ya kuuza chakula mama lishe na mama yangu akawa msaidizi wake pale ktk mama lishe yake maisha yakaendelea ila wakati tunatoka singida nilikuwa na umri wa miezi minne kwa mujibu wa mama yangu mzazi na hapa kwa mama pendo tulikakaa hapo kama miaka mingi sana na nakumbuka wakati huu nilikuwa darasa la nne ndipo hapo mama aliponiambia kuwa tuondoke amenipatia baba yangu na atanilea kama mwanae
Tukaondoka pale babati na kwenda kuishi kwa baba aliyenipatia mama sikujua alimpataje ila alimuaga mama pendo na tukaondoka na kuelekea Simanjiro
Baadae mama na mimi takaanza maisha mapya simanjiro baada ya kufika simanjiro maisha yakabadilika sana mama aliniambia kwa nitapelekwa shule lakini haikuwa hivyo baba yaani mume wa mama alikuwa akinitesa sana alinipiga sana na pia kuna wakati alikuwa akininyima chakula licha ya umri mdogo niliokuwa nao mpenzi msikilizaji lakini kila mara nilimkumbuka sana mama pendo kwakua tulikuwa tukiishi vyema sana
3
Nilipokuwa kwa mama pendo kwake na alinipenda sana ila mateso ya huyu baba yalikuwa makali mno hata mama hakuweza kusema kwani alipotaka kunisaidia aliambiwa kuwa hakuolewa yeye na motto yaani mama na mimi hivyo kama anataka anirudishe aliponitoa roho iliniuma sana mpenzi msikilizaji sana sana
Wakati mwingine baba akijisikia tu kuninyima chakula bila makosa na kunipiga alikuwa akininyima lakini pia kunawakati ininilazimu kula mabaki ya chakula walichokuwa wanakula watu kutokana na njaa na mateso niliyokuwa nayapata licha ya umri mdogo niliokuwa nao mama hakuwa na jinsi mtangazaji niliteseka sijawahi kuona namuogopa sana mume wake ,tuliishi pale miaka kama minne baadae huyo baba alianza kumchukia mama kwa vile hakuwa na motto.
Na hakupata motto na yele baba hivyo manyanyaso na mateso sasa pia yakaanza kwa mama yangu hata ndugu za baba walimwita mama yangu mchawi kutokana na kudai kwanini hazai na anamfilisi ndugu yao losiok eti maendeleo yake yameshuka na mama ndiye sababu ya hayo
Tuliishi kwa shida sana kila kitu kwetu kilikuwa tabu. lakini mama aliendelea kuvumilia kwakua hatukuwa na pakwenda yalikuwa ni mateso ambayo kila nikikumbuka machozi hunitoka mpenzi msikilizaji na mtangazaji naomba nisiendelee kukumbuka haya kwakua yananitia uchungu mkubwa.Nakumbuka siku ambayo sitsisahau baba alikujamchana mama akamkaribisha chakula
Baba yangu wa kimasai akamwambia mimi sili chakula cha mgumba kamwe kutoka sasa akakichukua kile chakula na kumtupia usoni kasha akamwambia kutoka sasa sstaki kukuona kwangu mgumba na mchawi mkubwa wewe mama alianza kulia sana na kumwomba baba amsamehe lakini baba alimfuata na kumkaba sana akamwambia usipoondoka leo usiku huu nitakuua
Mama aliogopa sana ikabidi mama na mimi kuondoka yaani baba hivyo huyo baba aliamua kumfukuza mama usiku sana hatukujua wapi tuelekee usiku huo ilibidi tulale hapo kwake jikoni kwakua mama aliogopa kuwa baba kweli anaweza kumuua
Asubuhi na mapema tuliondoka kabla yeye hajaamka tukawa tunatembea tu bila kujua wapi pakuelekea,tulitembea masaa kama sita na miguu na njaa nayo iliuma sana .Nililia sana ila mama hakuwa na jinsi ya kufanya,alipita mtu mmoja na gari mama akamwambia hatukuwa na pesa akatusaidia lifti hadi mjini arusha na pia pa kufikia tulikuwa hatujui .
Tulifika jioni sana tulitembea kama kuelekea kijenge njiani mama aliongea na bibi mmoja na kumuelezea hali halisi ,bibi huyo alikubali kutusaidia kwa masharti sana kuwa tunalala tu usiku ule asubuhi tuondoke na hatukuwa na chakula hakutupatia nilihisi nakufa kwa ajili ya njaa .
4
Tulifika kwake sahemu inaitwa Mwanama kweli akatukaribisha vizuri sana alikuwa mkarimu sana tuliingia ndani tukakaa akatuonyesha pakulala nikamwambia mama usiku naweza kufa kwa ajili ya njaa alitoka nje na nlikuwa nikilia sana baadae alirudi kabeba mkate na maziwa sikuamini niliona kama muujiza nilikula na kushiba vema nikamshukuru sana mungu sikuwai kula mkate na maziwa kwa muda mrefu sasa nakula vizuri kweli niliamini mungu ni mkubwa sana
Asubuhi na mapema niliamka nikatazama kitandaani nipo peke yangu nikafikiri kuwa mama labda yupo nje niliamka na kutoka nje nikawauliza wenyeji wetu mama yangu yuko wapi kwakua sikumkuta mama kule ndani nikajua labda yuko nje,nilitoka nje pia sikumuona nilimuuliza Yule bibi lakini naye hakumwona
.Huo ndio ukawa mwisho wa kumwona mzazi wangu hadi leo msikilizaji nililia bila mafanikio sikujua naelekea wapi kwa muda huo.na sikujua kwanini mama kafanya hivi na kaamua haya baadae Yule bibi aliniambia kuwa itabidi niondoke nikamtafute mama yangu nilimwambia kuwa mimi ni mgeni hapa arusha ni simfahamu mtu yeyote Yule hapa arusha akaniambia kuwa nakuomba NEEMA nakupa muda mdogo tu wakufikiri na kuchukua maauzi msikilizaji unajua aliniambia nini?
Bibi Yule akaniambia nakupa masaa 4 uondoke hapa haraka sana,nilkuwa naumia sana zaidi nilitoka pale nikaenda kwa jirani nikamueleza yote yalinonipata na jinsi mama yangu alivyoniacha akanionea huruma sana na akaniambia kuwa hali yake ni nzuri sana angeweza kunisaidia ila huyo jirani baada ya kumweleza nia yangu ikiwa kujaribu kutafuta msaada .
Kweli alinisikiliza na kusema atanisaidia.Kesho yake akaniambia ana mdogo wake anakaa mianzini Anaitwa mama ritha anataka mtu wa kazi je nitakuwa tayari? Kwakua sikuwa na mahali pa kufikia nilikubali kwenda kufanya kazi kwa huyo ndugu wa jirani ili tu niweze kupata hifadhi na mahala pa kula na hata kulala ukizingtia Arusha nilikuwa mgeni na sikuwa na ndugu hata mmoja
Ikanibidi kukubali kwa haraka sana kwani niliona huu ni okombozi mkubwa kwangu sasa nilikubali kwa haraka kwani nilijua iyo ilikuwa mojawapo ya msaada pekee kwangu kwani sikujua mama ameelekea wapi lakini pia kwanini mama alikimbia na kuniacha kwa Yule bibi nilizidi kuumia kama ni mateso mbona mimi sikumkimbia kwa mume wake kwanini mama kanikimbia niliumia sana na nikaona nikubaliane nae tu ili nipate sehemu ya kujihifadhi.
Asubui ya siku inayofuata nikachukuliwa na kupeekwa kufanya kazi nilipelekwa mianzini kuanza kazi Yule anayetafuta mfanyakazi kweli alinikubalia nilikaa pale miezi sita alikuwa na mototo mmoja na alikuwa akiishi na mume wake nilifanya kazi kwa juhudi japoNILILIPWA KIASI CHA SHILINGI ELFU KUMI Kwakua sikuwai kushika kiasi hicho cha hela nilikiona kuwa kikubwa nikakubali na kuanza kazi nilifanya kazi kwa kujituma sana na nikawa namwomba mungu sana ili aweze nami kuniondoa ktk shida hizi zinazonikabili mpenzi msikilizaji.
5
Muda ukazidi kwenda na miezi mitano sasa ikawa imepita toka nianze kazi kwa Siku moja dada alisafiri nikabaki na mume wake tuko wawili tu.Ilikuwa jioni tunakula akaniuliza nina mpenzi nikamwambia sina akanambia unaonaje ukanipa nafasi niwe mpenzi wako ili niweze kukusaidia?NIKASTUKA SANA NA KUMWAMBIA BABA RITH HAPANA SITA WEZA NAKUOMBA NIACHE NAKUOMBA KAMA UNATAKA KUNISAIDIA NISAIDIE TU LAKINI UNACHOTAKA HAPANA
Nilimshangaa sana mume wa dada nikamwambia siwezi nikamsimulia shida zote nilizopitia msikilizaji nililia sana nikakumbuka yaliyompata bibi na mama yangu kubakwa na kupewa ujauzito nikaanza kutetemeka sana
Niliogopa sana kwani sikutegemea angeweza kuongea hivyo nikamwambia hakika siko tayari nikakimbia chumbani huku natetemeka.Alinifuata na kunibembeleza sana nilimkatalia katakata baadae akaniambia sasa nitakushika kwa nguvu,nililia bila msaada wowote Akanishika na kunibaka na pia kuondoa bikira yangu yalikuwa maumivu makali sana niliumia wakati akiendelea kuniingilia nilikumbuka habari za bibi kubakwa akazaliwa mama mama akabakwa nikazaliwa mimi mawazo yalipofika hapo nilihisi usingizi mzito na kichwa kikawa kizito sana na kutoka hapo sikujua kilichokuwa kinaendelea mpaka saa mbilia.
Asubuhi nilipozinduka na nilipojaribu kuteremka kitandani sikuweza nilihisi maumivu makali sehemu za siri na chini ya kitovu huku nikiwa nimelowa damu mguuni siujua kumbe ndo bikira yangu ilikuwa imeondoka ikaanibidi kukaa kitandani roho iliniuma nililia sana na nikaona ni bora kufa kwanini yamenipata haya mungu kwanini ameyaruhusu haya yanipate na mimi nilianza kumchukia mungu na kuona si msaada kwanini asinisaidie kwanini nateseka kiasi hiki nikiwa kitandani sikumuona Baba Ritha nilishinda kitandani nimelala nikilia jioni ya siku hiyo
Baba ritha alikuja na kunibembeleza sana akaniambi kuwa atanisaidia nilikuwa nikilmtazama na hapa ndipo niligundua kuwa kumbe bibi hakuua kwa makosa wanaume kaka baba Ritha hawapaswi kuishi kabisa ktk hii dunia nilijikuta nikilia akaondoka na kurudi sebuleni siku inayofuata niliwahi kuamka hapa nilikuwa na maumivu kawaida kabisa japo moyo wangu bado ulikuwa unaniuma sana nikaanza kufanya kazi muda mfupi maumivu yale ya jana yakarudia kwa nguvu ilikuwa maumivu makali nililia na kuacha kazi nikarudi itandani
Nikiwa kitandani nikaanza kumlaumu mama asingnikimbia huenda haya yasingenipata kwanini alinikimbia je anipendi ama ni ugumu wa maisha ulimfanya anitoroke Baada ya hapa sasa ikawa kawaida ya baba ritha kila aliporudi kazini alitaka kuniingilia jambo hili liliniumiza sana lakini sikuwa na jinsi ya kufanya wala sikuwa na pakwenda nikageuzwa kuwa kifaa cha kujifurahisha cha Baba Ritha akawa kila akija ananichukua na kunitumia akinigeuza geuza mimi sikuwa na jinsi mungu wangu tu nilikuwa nikimuomba na kuona nay eye hana msaada wowote kwangu kwanini anayaruhusu haya ktk maisha yangumhapa tena wazo la mama nikaanza sasa nkakamkumbuka sana mama yangu veronica mama kwanini ulinikimbia mwanao sasa ni chombo cha sarehe za watu
6
Mama Ritha ALIKAA kwao kwa muda wa wiki tatu na aliporejea nilitamani sana kumweleza yote aliyonifanyai meme wake baba ritha lakini nikaogopa kuwa je kama atanifukuza nitakwenda wapi roho ilikuwa ikiniuma sana sasa mchezo ukabadilika wakati mkewe aliporudi alikuwa akitegea mkewe wakati hayupo nyumbani ametoka yeye huja kuniingilia kimapenzi na mimi niliumia sana kwani wakati mwingine huniingilia hata kinyume na maumbile ya tendo hilo yaani sehemu ya haja kubwa .Niliteseka sana nikaona bora nimwambie mke wake kuliko kuteseka
Nikaamua liwalo na liwe kwani sasa nilikwishaaribika sehemu ya haja kubwa na ikaanza kutoa harufu mbaya mpenzi msikilizaji wa radio five nikaamua tu kujikaza nikamwelezea mama Ritha Kutoka mwanzo mpaka mwisho kuhusu yote ambayo yametokea ktk maisha yangu ambaya mume wake amenifanyia
kwa muda wote ambao akuwepo na hata wakati huu ambao yeye yupo ila akitoka ninayofanyiwa alisikitika sana kwa wakati huo,jioni mumewe alipokuja alimuuliza lakini alikataa kabisa nakudai kuwa mi pepo ninayetaka kuvunja ndoa yao na tena akaniambia mimi ni shetani na hataki kuniona tena kwake akasema wafanyakazi wengi ni maajenti wa shetani na mimi eti nimetumwa kuvuruga ndoa yao roho iliniuma sana mwana mikasa
Baada ya mumewe kuambiwa hayo aliamua kumuamini mke wake na kuniona kweli mimi mbaya .Mke wake alimuamini mumewe sana na kwa pamoja wakaanza kunipiga usiku hou walinipiga san asana siwezi kusimulia na kunifukuza,sikujua nielekee wapi hivyo baadae nilirudi taratibu nikalala barazani na asubuhuhi na mapema niliondoka wasinikute nikaelekea kama sanawari na sikujua naelekea wapi mpenzi msikilizaji nililia sana nikawa natembea nikilia barabarani
.Njiani nilikutana na dada mmoja akajitambulisha kwangu anaitwa UPENNDO akaniita na kuniuliza mbona unalia?nikamweleza kila kitu akanambia mimi nasafiri ila kuna mtu nitakukabidhi akupeleke kwetu ukakae mpaka nitakaporudi ndio tujue tunafanya nini.
Kweli alinipeleke mpaka stendi akanikabidhi kwa kaka mmoja akamwambia mpeleke huyu binti kwa mama yangu mwambie ni mgeni wangu akae mpaka nitakaporudi.nilitoka pale na Yule kaka tukapanda magari yaendayo mererani ,tulifika mererani kasha tukaelekea sehemu inayoitwa makiba tukatembea na miguu mwendo wa saa 3 tukafika.
Nilijua naenda kwa kina DOREN Yule dada likini kumbe akanipeleka kwake porini sana mpaka nikawa naogopa akanikaribisha,akanipa na chakula na baadae akaniambia amependa kunileta kwake ili tuje tuishi kama mke na mume
7
Msikilizaji nilijiona kama ndoto maisha yangu mbona kama hayaeleweki kwanini mungu amenifanyia haya jamani kwanini lakini mungu ni mkuu wa yote sikujua nifanye nini maisha yangu yalikuwa yaajabu sana nilicheka sana kicheko cha uchungu na machozi yalinidondoka mwanamikasa.Sikuwa na jinsi ilibidi nikubaliane nae tu na nijilazimishe kupenda maana sikuwa naelewa tena pakwenda na sasa sikuwa na matumaini yeyote ktk maisha yangu .
Tuliishi ivyo ivyo kwa miezi 7 na tayari nilikuwa na ujauzito kwakua tulipokuwa tukiishi hakukuwa na kitanda wala chochote tulikuwa tukilala kwenye majani chini na mabox na kigodoro chembamba sana nikamwambia JOHN ABDALA Mume wangu unaniona nina mimba itakuwaje na hapa hakuna hata kitanda?alicheka na hakujibu kitu. Roho iliniuma sana alipocheka sikujua kwanini licheka
Siku zilizidi kwenda kweli maisha yake sikuwa nayaelewa hata kidogo. Kutoka siku hii JOHN ABDALA akabadilika sana maisha yakazidi kuwa ya mateso sana na baadae akabadilika akawa ananipiga vibaya sana,aliniumiza ajabu bila kosa hadi ikafika wakati wa kujifungua mateso mengi yalizidi mpenzi msikilizaji wa mikasa roho iliniuma sana hata chakula na humuma za mama mjamzito sikupata niliteseka sana wakati wa kujifungua namshukuru mungu kwani mungu alinisaidia nikajifungua salama.
Pale pale nyumbani nikisaidiwa na wakunga wa jadi pamoja na majirani ambao walikuwa eneo lile kwakua sikuwa na uwezo wa kwenda hospitali ila namshukuru mungu wakunga walinisaidia sana sana
Nilipotimiza mwezi aliondoka siku moja asubuhi na mpaka sijamwona tena.Niliishi kwa kuomba omba huku nikiwa na mototo wangu,niliteseka mpaka mpaka nikatamani kufa sikujua nini nifanye.Nyumba ilikuwa ya nyasi mvua ikinyesha mimina mwanangu ilitubidi kusimama na kunyeshewa hadi asubuhi.kwakua sikuwa na jinsi yeyote na pakwenda ilinibidi kuvumilia
Maisha yaliendelea kwa mateso mpenzi msikilizajikuna kitu kilitokea kama upele mguuni niliendelea kuumwa na kutengeneza usaha na gafla kikawa kidonda kikubwa.Kilinitesa sana ikawa kama mguu unataka kuoza,kadri siku zinavyozidi kwenda kidonda nacho kinazidi kuwa kikubwa
.Niliamua kwenda hospitali ya jirani inyoitwa mbuguni lakini waliniambia niende Mt.Meru.Nilirudi nyumbani kwani sikuwa na uwezo wa kwenda Mt.Meru mpaka sasa mguu umeoza sana na sina msaada wowote mwanaume amekimbia na pia sina kazi yeyote nateseka sana naona labda nimuue huyu motto na mimi nijiue ili nipumzike kuteseka
Kidonda kiliendelea kunuka kama vile kimeoza, ilibidi nirudi tena mbuguni,nilirudi mbuguni wakao niambia hawawezi kwa sababu ile ilikuwa ni kansa hivyo hawakuwa na njia ya kunisaidia na kunitaka tena niende mt.meru.
8
Uwezo wa kwenda mt.meru sina naishi kwa shida kula kwa shida,pengine ningejua mama yangu alipo angenisaidia MAMA YANGU VERONIKA IDABU KWANINI UMENIKIMBIA MWANAO NAESEKA SANA MUME WANGU KWANINI UMENITELEKEZA JOHN ABDALA .Msikilizaji naona siku zangu za kufa zimekaribia nitamwacha mwanangu kwenye mazingira gani? Naona bora nife na nimuue motto Baba yake sijui alipo,sina ndugu, naombeni msaada wenu angalau niweze kujitibu na kumlea mwanangu
.Kama serikali inanisikia naomba inisaidie kwani hali yangu ni mbaya.Nichangie chochote na mimi nitakushukuru.Ni mimi Mama Irene naona ni bora nife kwakweli kwanini mungu amenipitisha ktk haya naumia sana pia nikipata mahala pa kukaa na matibabu tu na niweze kumlea mwanangu nitashukuru
lakini kwa hali hii naona bora kufa kuliko haya nayopitia naumia sana kwa sasa moyo unaniuma sana naroho inaniuma sana kwa haya nayopitia na ambayo yamepita ktk maisha yangu nateseka sana ktk maisha yangu sijawai kupata tumaini lolote mungu nisaidie mwana mikasa nisaidie hakika nateseka sana sioni faida ya kuishi kutokana na yanayonipata ktk maisha yangu
MUNGU NA AWASAIDIE WOTE AMBAO MTAJITO KUNISAIDIA NAHITAJI MSAADA NIMEFIKA MWISHI UVUMILIVU SASA UMENISHINDA NATESEKA SANA SIJUI NIFANYE NINI MPENZI MSIKILIZAJI WA MIKASA YA MAISHA NAKUOMBA MSAADA WAKO MWENYEZI MUNGU ANANIJUA JAPO NAONA DUNIA IMENIELEMEA

No comments:
Post a Comment