mmmmh


oo

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

nilivyoteswa na wachawi sumbawanga

Ni dunia ya mikiki mikiki. Kuchelewa kufa ni kuona mengi lakini usiombe kukutana na viroja vya Wachawi wa Sumbawanga. Katika kipindi ambacho nimeishi kwenye ulimwengu ambao wengi wanadhani ni wa kufikirika, nimeweza kuuona uchawi na kujua tafsiri yake.
Fanya ibada unavyoweza ili wachawi wakae mbali na wewe, vinginevyo utageuzwa chakula kilichoungwa viungo vya kupendeza. Namshukuru Mungu nipo hai, nadunda duniani tena navuta pumzi safi, hewa ya oksijeni. Asante Mungu kwa kunipigania.

Leo hii pengine ningekuwa nalima shamba la wenyewe. La, basi ningekuwa marehemu. Chokochoko ndogo ya kukataa kuolewa na Kibabu cha Sumbawanga ndiyo ilisababisha niingie kwenye mapambano na watu ambao wanaamini wao ni wababe kuliko chochote chini ya jua.
Naitwa Helena Nsuzuguye, mzaliwa wa Sumbawanga katika familia iliyoishi kwa imani ya kati, yaani tulimuamini Mungu lakini si kwa kiwango kikubwa. Mama alihudhuria Kanisani kila Jumapili, baba haikuwa muhimu kwake na zaidi ya kushinda kwenye vibao vya kahawa na pombe.
Baba alikuwa mlevi wa pombe za kienyeji, hiyo mara nyingi ikawa inaleta usumbufu nyumbani. Mama ndiye aliyekuwa akijituma kuhangaikia familia yetu. Kutafuta riziki ya kutuwezesha kuweka chochote tumboni, pia kutuhudumia mahitaji ya shule.

Mimi na ndugu zangu watatu, yaani kaka yangu na wadogo zangu wawili kusoma kwetu ilikuwa tabu tupu. Shule tulienda bila kuvaa viatu, sare zimechanika na haikuwa shida sana kwani tulipiga moyo konde na kuendelea na masomo yetu.
Kufika darasa la sita mambo yakabadilika. Kuna kibabu tulichozoea kukiita, Mzee Balinaba (Barnabas), kwa muda wote ambao nimekua na kumuona, alikua hana mke wala mtoto. Nyumba yake ilizungukwa na shamba kubwa la miembe, michungwa, michenza, mistafeli, mipapai na michikichi michache.

Yule mzee ni mkubwa kuliko hata baba yangu, ni kibabu hasa! Nikiwa darasa la sita, siku moja baba aliwahi nyumbani tofauti na kawaida yake. Alionekana mchangamfu na mkononi alishikilia kifurushi. Alikuwa amebeba nyama ya nyati.

Alipofika alisalimia, akataka aonane na wanaye wote. Tukakusanyika, kila mmoja akampa shilingi 50, baada ya hapo akataka wote waende wakalale ila nibaki mimi na mama. Sikuhisi kitu chochote kibaya, kwahiyo nilibaki nikiwa na shauku ya kujua kilichonibakiza.
Baada ya waliotakiwa kuondoka, kilipita kimya cha sekunde kadhaa. Muda wote huo baba alikuwa anatutazama usoni kama vile kuna kitu anataka kutuambia lakini akawa anajishauri jinsi ya kuanza. Alikohoa mara tatu, tukadhani anaweka sawa koo.

Sisi tukabaki kumshangaa na kungoja kwa hamu hicho alichotaka kutuambia. Muda ulipozidi kwenda, ilionekana mama amechoka kusubiri, akaamua kuvunja ukimya: “Hivi Baba Jere umetuweka hapa ili ututazame, maana huongei.”

Mama alipozungumza hivyo, baba alijibu: “Utulivu kidogo Mama Jere, kuna mambo muhimu ya kujadili mimi na ninyi ndiyo maana nimewaambia mningoje na muwe wawili, kwahiyo hatupaswi kuyapeleka mambo kwa haraka.”
Mimi sikutia neno, ningeongea nini wakati wazazi wanalumbana? Nilibaki kimya, huku nikisubiri kwa shauku. Kusema ule ukweli siku hiyo niliiona ni ya ajabu. Haikuwa kawaida baba arudi na kutaka kuzungumza mtu pale nyumbani achilia mbali kubeba kifurushi ambacho ndani yake kuna kitoweo.

“Helena,” baba aliita.
“Abee,” niliitika.
“Umebakiza muda gani umalize shule?” Baba aliniuliza.
“Bado kama mwaka na nusu ila nataka niendelee na sekondari,” nilimjibu.
“Sekondari kufanya nini?”
“Nataka kusoma baba.”
“Nini?”
“Unang’aka nini Baba Jere? Mwanao kasema anataka kusoma zaidi, wewe kama una yako yaseme,” mama aliingilia.
“Ahaa, sasa acheni niseme. Helena umepata mchumba na ni lazima aolewe,” baba alisema.

“Baba Jere acha utani, tena usinitanie kwa wanangu, hujui nahangaika nao vipi. Helena haolewi,” mama alisema kwa sauti ya juu.
Mama alipozungumza kwa sauti hiyo, baba alinyanyuka na kuondoka huku akisisitiza kuwa ni lazima nitaolewa kwa sababu huo ndiyo uamuzi wake kama baba wa familia. Mimi nilibaki sina la kusema nikawa namtolea macho mama yangu ambaye yeye hakuweza kuzungumza chochote zaidi ya kusonya.

Tulitawanyika na kila mmoja kuingia chumbani kwake kulala, palipokucha, baba aliondoka mapema. Siku nzima hakuonekana, aliporudi alikuwa amelewa chakari. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kumvaa mama na kuanza kumpa kipigo.

Alimpiga sana!
Alipoona alivyompiga mama ameridhika, aligeuka kwangu na kuniuliza kama nitaolewa au nimeshikilia kiburi cha mama? Nilimjibu kuwa mimi sipo tayari. Jibu hilo likanichongea, kwani alinigeukia na kunipiga sana. Ni kwa mara ya kwanza nipomuona baba ni katili. Baada ya kuridhika, akaamrisha kila mtu aingie chumbani kulala.

Asubuhi wakati najiandaa kwenda shule, baba alikuwa ananiangalia. Nikavaa sare zangu huku miguuni nikiwa peku, nilipotaka kutoka, akanizuia na kuniambia kuanzia siku hiyo hakuna kusoma. Nilisimama na kumuangalia kama vile sijaelewa vizuri alichoniambia. Akaniambia huo ndiyo msimamo wake kama baba na hakuna wa kumpinga.

Shule hakuna na ibaki kuwa hivyo kwa sababu yeye amekwishapokea pesa na ameahidiwa mali nyingi baada ya kuniozesha. Pale pale nilianguka na kuanza kulia. Kilikuwa kilio cha kusaga miguu. Fikiria mtu unaamini ndoto zako ni kufika mbali kielimu, halafu mzazi wako anatumia nafasi yake kukulazimisha ufanye anavyotaka yeye. Anaamua kukuozesha!
Nililia lakini haikusaidia, nilibaki mnyonge. Hata hivyo yote ikawa tisa, kumi ni siku ambayo nilitajiwa jina la huyo mtu anayetaka kunioa.

Mzee Balinaba. “Mungu wangu, huyo mzee nitampeleka wapi mimi?” Nilijiuliza huku moyo ukinienda mbio kwa hasira.
Mama akaja juu: “Baba Jere umekuwaje? Yaani huyo mzee kila mtu anamuimba ni mchawi ndiyo unataka kumuoza mwanao? Au ndiyo amekuroga?” Mwisho wa sentensi ya mama ikawa ni kipigo cha kuzibwa mdomo ili asizungumze chochote.

Swali la mama halikuweza kupata jibu, baba alinyanyuka na kuondoka. Nilimsindikiza kwa macho

wakati anapiga hatua huku akisema maneno ambayo sikuweza kuyapata kwa mpangilio unaotakiwa.

Nilichojua ni kwamba alifoka na kusonya mfululizo!
Siku ilipita, kesho yake asubuhi baba aliondoka na kuelekea kusikojulikana, mchana alirejea akiwa

ameongozana na Mzee Balinaba (Barnabas). Mama alipowaona aliingia chumbani, nami nilijificha kwa

sababu sikutaka kuonana nao. Niliona aibu!

Baba alimkaribisha mgeni wake mpaka sebuleni, baada ya hapo alimfuata mama akamvaa. Alimlazimisha

atoke kumsalimia mgeni. Mama aligoma lakini pale pale bila kusubiri, baba alianza kumpiga pasipo

kufikiria uwepo wa mgeni ambaye kwake aliamini ni mkwe sahihi.
Pamoja na kumpiga, lakini bado mama aligoma kutoka nje ili amsalimie mzee Balinaba. Alipoona kwa

mama imeshindikana alikuja kwangu. Nami nikiwa na hasira za kulazimishwa kuozwa na kikongwe pamoja

na kipigo alichopewa mama, niligoma kutoka.

Baba akaona dawa pekee ni kunipiga lakini nilishikilia msimamo wangu. Alipochoka alitoka. Baadaye

nikamsikia anazungumza na mzee Balinaba kwamba asiwe na wasiwasi kwa sababu yeye ndiye baba mwenye

nyumba, kwahiyo kila kitu kitakwenda sawa.
Kumbe si mimi peke yangu niliyesikia, hata mama aliweza kuinasa sauti hiyo, kwahiyo baada ya

kumsikia baba akizungumza hivyo, alipaza sauti akamjibu kwamba pale haolewi mtu. Akiwa chumbani,

alizungumza kwa sauti ya juu kwamba mzee Balinaba atafute nyumba nyingine ya kwenda kuoa.
Baba naye akajibu kwa ukali kwamba ni lazima mwanaume ndani ya nyumba ajulikane, kwahiyo kwa

yeyote atakayepinga hiyo ni shauri yake. Sauti yake ilionesha alikuwa anatembea, kumbe alikuwa

anamfuata mama, lakini hakufanikiwa kumfanya chochote kwani alikuta mlango umefungwa.

Mama alikuwa amejifungia. Baba akamgombeza huku akimshinikiza afungue mlango. Kule chumbani mama

aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutofungua mlango. Ni wazi alijua kwamba angethubutu kufanya

hivyo angepokea kipigo. Baba alikuwa na mkono mwepesi kweli!
Wakati baba na mama wanaendelea kubishana, ikasikika sauti ya mtu akikohoa. Huyo alikuwa mzee

Balinaba. Baada ya kuvuta kikohozi kama mara tatu hivi, alianza kucheka. Hapo nyumba nzima ikawa

kimya kumsikiliza anacheka nini. Yamkini kuna kitu alitaka kuzungumza!
“Baba Jere, unahangaika nini?” Aliuliza mzee Balinaba kwa sauti ya kuendelea kucheka.

“Si huyu mwanamke? Nataka afungue mlango nikamchape vibao,” baba alimjibu.
“Hilo tu? Hebu subiri nikuoneshe.”
Mzee Balinaba alipomaliza kuzungumza hivyo, papo hapo kule ndani mama alianza kulalamika kuwa

chumbani kuna simba. Alipiga mayowe mpaka majirani wakasikia. Ili kujiokoa akafungua mlango na

kutoka nje. Ile anamalizia kunyonga kitasa tu, baba aliingia ndani na kumkabili.
Siku hiyo baba alimpiga sana mama, majirani walijaa kushuhudia. Nikiwa chumbani kwangu

nilijiinamia bila kujua cha kufanya. Machozi yalinitiririka kama bomba. Ilikuwa ni aibu kubwa!

Fikiria mtu unashuhudia mzazi wako anaadhibiwa, analia huku majirani wakisikiliza madirishani!

Dakika kama 20 hivi zilipita tangu baba alipoanza kumpiga mama, nikasikia anafungua mlango na baba

akatoka huku akiendelea kuongea kwa sauti ya hasira: “Alaa, ni lazima ajulikane mwanaume ndani ya

nyumba ni nani, mimi niseme na wewe useme nani atamsikiliza mwenzake?”
Baba akiendelea kutembeza ubabe ndani ya nyumba, baadaye alihamia chumbani kwetu. Akagonga, mimi

nikabana kwa komeo, kwahiyo akawa anaita bila mimi kuitika. Alifanya hivyo kama mara nne hivi,

ikabidi apaze sauti na kupiga mlango kwa nguvu zaidi.

Niliendelea kukaa kimya kama vile simsikii. Kwa mara nyingine mzee Balinaba anakohoa mara nne,

halafu akaanza kucheka. Nyumba nzima ikanyamaza kuona nini ambacho anataka kuzungumza, ingawa kwa

upande wangu niliingiwa na hofu, nikikumbuka yale ya mama.
“Na huyo anakusumbua?” Mzee Balinaba aliuliza.
“Mtoto mjinga sana huyu, yaani yupo kama mama yake,” ndivyo baba alivyojibu.

“Unataka atoke ndani huko?” Mzee Balinaba aliuliza tena.
“Siyo kwamba nataka atoke, lengo langu ni aje aonane na wewe, ikiwezekana muondoke leo leo maana

sina hela za kufanya sherehe hapa kwangu,” baba alijibu na kuzidi kunipa hofu.
“Basi ngoja kidogo nimtoe humo ndani.”
Mzee Balinaba alipozungumza hivyo, ghafla pale chumbani nilimuona chui. Alikuwa mkubwa na akawa

ananitisha kama anataka kunirukia. Nilipiga kelele lakini yule mzee akawa anacheka. Bila

kulazimishwa nilifungua mlango ili kumkimbia chui kumbe najipeleka.
Nilipotoka tu, baba alinikokota mpaka kwa mzee Balinaba, akaniweka chini na kunilazimisha nipige

magoti.

Nilitaka kuwa mbishi, lakini nilipoangalia nyuma niliona kiumbe cha ajabu chenye mwili mkubwa.

Nadhani ni zimwi! Likanilazimisha nitekeleze maagizo.
Nilipiga goti haraka! Baba akaniambia nimshike mkono mzee Balinaba. Kwa mara nyingine nilitaka

kugoma, lakini kuangalia nyuma, nikamuona tena yule zimwi, akanitishia kunimeza, kwahiyo kwa hofu

ya kumezwa ikabidi nimpe mkono yule mzee.
Kumshika tu mkono, nikajikuta nabadilika. Mwili ukawa baridi nikawa natamani kumkumbatia mzee

Balinaba. Ni wazi aliniroga, kwa maana hapo kabla sikuwa na hisia zozote za kumpenda. Baba

aliniuliza kama nimekubali kuolewa, nami kabla hajamaliza sentensi yake nikaitika kuwa nimekubali!

Asikwambie mtu, uchawi upo! Jiulize mimi ambaye nilikuwa namchukia mzee Balinaba kiasi kwamba

sikutaka kabisa kumuona, lakini kufikia hapo nikampenda ghafla tena baada ya kushikana naye mkono.

Moyo ulitulia juu yake ndiyo maana sikuendelea kuwa mbishi.
Nilipogeuka nyuma, sikumuona tena yule zimwi, hali ilikuwa shwari. Mama alikuja pale tulipokuwa,

akaniuliza kama nimemkubali mzee Balinaba, nami nikamjibu kwamba nimekubali kwa sababu nampenda

sana. Jibu hilo lilimshangaza sana mama yangu, ni wazi hakulitegemea!
“Wewe mzee umemroga mwanangu siyo? Mzee Balinaba kweli umemroga mwanangu!” Mama alikuja juu.

Mzee Balinaba hakujibu kitu, wakati huo baba akamsukuma mama ambaye alianguka pembeni kama mzigo.
Mama yangu alilia sana, aliumizwa sana kuona nachukuliwa kwenye himaya yake bila ridhaa yake. Hata

hivyo, hakuweza kufanya lolote, niliolewa kienyeji na kibabu cha ajabu mno!
Baada ya shughuli ya ndoa, tuliondoka na mzee Balinaba. Mkono wake mmoja alinishika, mwingine

alikamata mkongojo. Watu waliokuwa wamezunguka nyumba yetu walitushangaa barabarani, wangine

walizomea. Sisi hatukuwajali, tuliingia mpaka nyumbani kwa mzee huyo na kuanza rasmi maisha ya

ndoa.

Ni maisha ya ndoa lakini ambayo ndiyo yaliyonisababishia mateso makubwa maishani. Nikajikuta ni

mke wa mchawi, napika nyama za watu, chakula ambacho mume wangu alikipenda mno. Wadudu, wanyama na

viumbe wa ajabu ndiyo rafiki wa nyumba yetu.

Ni maisha ya ndoa lakini ambayo ndiyo yaliyonisababishia mateso makubwa maishani. Nikajikuta ni

mke wa mchawi, napika nyama za watu, chakula ambacho mume wangu alikipenda mno. Wadudu, wanyama na

viumbe wa ajabu ndiyo rafiki wa nyumba yetu.

SEKESEKE NAMBA MOJA
Tulifika nyumbani kwa mzee Balinaba (Barnabas), akanikaribisha. Hakukuwa na mtu hata mmoja. Nyumba

ilikuwa na giza, mwenyewe akazunguka pale ndani, alipopata kiberiti, aliwasha kibatari. Angalau

mwanga ukawepo.

Wakati huo nilikuwa na hisia za kweli za kimapenzi. Alinishika kweli kweli! Aliniongoza kuingia

ndani, tulifikia varandani ambako niliketi kwenye jamvi. Yeye aliingia chumbani, aliporudi

aliniuliza kama nimeshakula. Nilitabasamu, nikamjibu nitakula baadaye!
Kwanza nilijiuliza, hicho chakula kitakuwa wapi? Alipika nani? Umri wa mzee Balinaba kwa

kumuangalia tu, ilitosha kutoa picha kwamba hawezi kumudu kuingia jikoni. Halafu pale ndani

aliishi peke yake na hakukuwa na dalili ya kutembelewa hata na majirani.

Tabasamu langu lilimvuta, akainama na kusogea pale nilipo. Akaketi jirani yangu, mkono wake wa

kushoto ukapita kwenye bega langu. Alinikumbatia! Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu,

nikasikia hisia za mapenzi, yaani tamaa kufanya tendo la ndoa.
Tangu nizaliwe nilikuwa sijawahi kufanya mapenzi. Kumbuka, nimeachishwa masomo nikiwa darasa la

sita. Simulizi za mapenzi nilikuwa nazisikia kwa kupiga soga na marafiki ambao tulikutana kisimani

kuchota maji au kwenye chemchemi kufua.

Mwili ulinisisimka mpaka nikawa natetemeka. Yule mzee akasogeza kinywa chake kwenye mdomo wangu.

Sikuelewa anataka kufanya nini. Kwangu mimi, nimekuwa nikiamini kuwa harufu ya mdomo siyo nzuri,

kwahiyo mate ya mtu ni kinyaa.
Nikiwa na umri huo, kwa mara ya kwanza nikapata kujua kwamba kumbe mdomo wa mtu ni moja ya viungo

vya kutekeleza mpango mzima wa mapenzi. Kwani aliposogeza kinywa chake, alinipumulia, harufu kali

ya mdomo wake sikuijali, badala yake nilihisi utamu wa kipekee.

Aliponipumulia, ile pumzi yake yenye uvuguvugu ilizidi kunipa wazimu. Nikawa siwezi tena kujizuia.

Nilihangaika na kujinyonga nyonga pale kwenye mikono yake. Nilijiridhisha kwamba mzee Balinaba

anavyoonekana, sivyo alivyo.
Nilijinyonga nyonga mpaka nikaanza kulia. Kile kilio cha utamu. Kilio cha mahaba ambacho

humhamasisha mtendaji badala ya kumfanya awe na huruma. Pale pale kwenye jamvi, mikono yake

ikakosa ustaaraabu, akawa ananishika sehemu tofauti za mwili wangu.

Hapa naomba niseme kwa mkazo kidogo; Mzee Balinaba alikuwa fundi wa kucheza na viungo hatarishi,

kwani alipopeleka mikono mapajani, sivyo alivyofanya pale alipotua kwenye vilima kifua ambavyo

vilikuwa vidogo mno.
“Oooh, mtoto Helena, leo umekuwa wangu, oooh!” Alisema mzee Balinaba kwa sauti ya hisia mno,

wakati anachezea vilima vyangu vya kifuani. Hakuishia hapo, aliliondosha lile gauni nililokuwa

nimevaa. Sikuona aibu kubaki na nguo ya ndani mbele yake.

Yule mzee aliendelea kunikamua kamua. Kuna wakati aliongeza gia, akaninyonya sikio la kulia, ile

kupitisha ulimi tu, nikaruka mpaka nikamponyoka. Mwenyewe hilo hata halikumshangaza, zaidi

lilimfanya ajione mshindi. Akacheka sana!
Unacheka nini babu?” Nilimuuliza.
“Nakucheka wewe, halafu usiniite babu, sawa?” Alijibu kisha naye akauliza.

“Niite mume au unaweza kuniita Balinaba,” alisema.
Baada ya mazungumzo hayo mafupi, tuliendelea na mchezo wetu. Mzee Balinaba akiwa mwalimu wangu.

Aliridhika na kile alichokifanya kwenye masikio yangu yote mawili kisha mimi kuruka na kujikunja

kama kinda la njiwa lililolowa mvua, alihamisha mashambulizi.
Akanilaza chali kwenye jamvi lile lile halafu akaanza kuninyonya matiti. Hakika, hapo ikatosha

kunifanya niamini kwamba kumbe mchezo wa mapenzi ni mzuri. Ndiyo maana watu wanaambiwa kuna ukimwi

lakini hawatishiki, na kila siku wapo wanaofumaniwa!

Aliendelea na mchezo wake, alipoona nipo hoi akaishika nguo yangu ya ndani na kuanza kuitoa. Hapo

nilishtuka kidogo! Niliweka mkono kuzuia asiendelee kuiteremsha lakini baada ya kung’ang’aniza kwa

dakika kadhaa, nilikuwa mpole akaitoa.
Nikiwa sina nguo, mzee Balinaba alininyanyua mpaka chumbani, wakati ananiongoza nilikuwa

nimeinamisha uso wangu chini kwa aibu. Alinifikisha kitandani, naye akavua nguo zote. Siyo siri,

niliogopa mno kumuangalia akiwa hana nguo. Jamani haya mapenzi!

Imani yangu ilikuwa kwamba mtu akishazeeka, hajiwezi kabisa kimapenzi. Mzee Balinaba alikuwa

kikongwe hasa lakini ndiye aliyenitoa bikira. Nikiwa namuangalia kwa wizi wizi huku nikisaidiwa na

mwanga hafifu wa kibatali, alipanda kitandani na kunivaa mzima mzima.
Aliniletea mdomo wake, nikabana meno lakini alinibana mashavu, nilipofunua kinywa changu,

akaingiza ulimi wake. Aliutuliza kwa sekunde chache, nilipoutoa ulimi wangu nje, kumbe ndicho

alichokuwa anahitaji. Alianza kuunyonya kwa kasi ya ajabu.

Kuna raha fulani niliipata wakati ananinyonya ulimi, na ni kitu kingine katika mambo ya kimapenzi

ambayo nilijifunza kwa mzee Balinaba. Aliendelea kunichezea, alipotosheka akaniweka alivyotaka,

akaingia sehemu yenyewe. Niliumia sana na damu nyingi zilivuja.

Bikira yangu ilitoka siku hiyo! Baada ya kumaliza haja zake, huku mimi nikiwa nina maumivu makali,

alinibembeleza, niliponyamaza aliniletea chakula, ilikuwa pilau. Njaa niliyokuwa nayo ilikuwa

kali, kwahiyo nilikula haraka haraka, nilipomaliza alinikanda maji kisha nikalala.
Nilimuona mzee muungwana, asiye na matatizo na mkarimu kwa jinsi alivyokuwa ananikanda maji. Hata

hivyo, usiku wa manene niliona tofauti. Nikathibitisha yale yaliyokuwa yanasemwa kuwa mzee

Balinaba ni mwanga. Nilishtuka usingizini, bila kuchezesha kichwa nikamuona akiwa mtupu na bibi wa

jirani yetu.

Huyu bibi namjua, naye watu wanamsema ni mwanga. Anaitwa Bi. Shede. Walisimama kwa kuangaliana,

wote walikuwa watupu. Wakaulizana, nikasikia mzee Balinaba anasema siwezi kuamka mapema.

Alijidanganya, nilikuwa nawaona! Ghafla wakaanza kufanya mapenzi!
Roho iliniuma lakini niliogopa kusema lolote. Nikawa nawatazama kwa jicho la wizi. Walipofanya

mapenzi wakaanza kucheza kama watoto, mara huyu kampiga hapa, mwenzake kamrudishia. Nikaanza kuona

mapadiliko yao kuanzia miguuni na hatimaye wote wakageuka nyoka.

Mwili wote ukaingiwa na baridi ya woga. Wakiwa wamegeuka nyoka, wakaendelea kucheza mitindo

mbalimbali. Hawakuishia hapo, walipanda kitandani na kuanza kutambaa kunizunguka. Sijawahi

kushikwa na woga kama siku hiyo, nilijitahidi kuendelea kujikausha.
Baada ya kunizunguka miguuni na tumboni, sasa wakawa wanakuja usawa wa kichwa changu.

Nilichogundua, nyoka mmoja alikuwa anataka kunidhuru, mwingine ananipigania. Yule anayetaka

kunidhuru, alikuja usawa wa kichwa na kupanua mdomo kwa lengo la kunimeza. Mungu wangu!
Itaendelea wiki ijayo…



Nimeamua kuanzisha ukurasa huu ili niweze kuwasiliana na Watanzania wenzangu nikijaribu

kupandikiza mbegu ya Ushindi katika mioyo ya wenzangu waliokata tamaa, najua wapo ambao wamejaribu

mambo mengi maishani mwao na hayakutokea kama walivyotaka, wamekata tamaa na kuamua kuacha mambo

yaende kama yalivyo! Wameridhika na umasikini bila kuelewa kuna mtu mkubwa kiasi gani ndani yao.

Kama wewe ni miongoni mwa watu hawa, au ni mtu ambaye unataka kufikia vilele mbalimbali maishani

mwako, basi Waraka huu ni wako, USIKOSE KUUSOMA KILA WIKI

Binafsi nilipoamua safari ya kutafuta mafanikio, kitu cha kwanza nilichochagua kukifanya ni

kujielimisha. Sikuwa na sifa wala elimu ya kutosha kufanya mambo ninayoyafanya leo, kifupi huu ni

muujiza, ndio maana kila siku namshukuru Mungu. Wakati mwingine huwa nalazimika kusema kila kitu

kinachotokea maishani mwangu, pamoja na juhudi zote ninazofanya, bado Neema za Mungu zina nafasi

yake.

Kwa uamuzi wangu wa kujielimisha, nikimaanisha kutafuta maarifa ambayo yangeniwezesha kutoka

kwenye umasikini uliokuwa ukinikabili tangu utotoni na kusonga mbele, nisingeweza kurejea tena

darasani na kujifunza biashara! Yaani mwalimu asimame mbele, nyuma yake kukiwa ubao mweusi na

kuandika juu yake neno “Book Keeping” ndipo nijifunze namna ya kutunza vitabu vyangu vya mahesabu.
Nilichofanya ni kuchukua uamuzi wa kusoma sana vitabu vilivyoandikwa na watu waliofanikiwa katika

jambo nililotaka kufanya, Biashara. Nilisikiliza sana CD na Kanda za Redio za watu kama Les Brown,

Robert Kiyosaki, Jim Rohn na wengine wengi. Hiyo ndiyo ilikuwa kazi yangu; kujielimisha.

Nilisoma vitabu mpaka familia yangu ikahisi nataka kuchanganyikiwa, mpaka leo hii ninavyoandika

waraka huu bado nasoma vitabu sana, mbele yangu kuna kitabu kipya cha mtu aitwaye Robin Sharma,

kiitwacho The Greatness guide, hiki ndicho ninachosoma kwa hivi sasa. P.Funk, mtayarishaji maarufu

wa muziki nchini Tanzania naye amenipa kitabu kingine kiitwacho 48 Laws of Power, nacho pia

nitakisoma baada ya kumaliza hiki cha Robin Sharma.

Hakika maisha yangu ni vitabu, najielimisha kila siku kwa sababu sikupata bahati ya kusoma pengine

kama wewe msomaji wangu, Najiendeleza kwenye lugha ya Kiingereza mpaka Biashara, hakuna siku huwa

nakwenda kitandani bila kujifunza angalau neno moja jipya la Kiingereza, hii ina maana kwa mwaka

mzima ni lazima nielewe maneno mapya 365! Je, hapo nitabaki nyuma? La hasha!

Ndugu zangu,
Kama kuna kitu kigumu duniani kwa mtu kufanya ni kupata nafasi ya kukutana na matajiri au watu

waliofanikiwa maishani na kuzungumza nao juu ya mafanikio yao, hawa ni watu wenye shughuli nyingi

mno na wanaoelewa thamani ya wakati. Unahitaji kuvuja jasho kuwatafuta, uwe uvumilivu wa ajabu na

pengine kibali kutoka kwa Mungu, lakini ni lazima ukutane nao hata kama hawataki na ujifunze.

Jambo hili halikwepeki kama kweli umedhamiria kutafuta mafanikio na unataka kujifunza kutoka kwa

watu unaotaka kufanana nao.

Hebu nikusimulie kisa kifuatacho ambacho kimenipata mimi mwenyewe, kwa muda mrefu sana nilimtafuta

Mama Mheshimiwa Dk.Getrude Lwakatare bila mafanikio, kila siku nilipompigia simu nikiomba kukutana

naye ili tuzungumze alianimbia “Mwanangu, niko Bungeni, nikirejea Dar es Salaam nitakutafuta” au

“Niko kwenye maombi, kwa sasa hatuwezi kuonana”
Hayo ndiyo yalikuwa majibu yake mara kwa mara, mwisho hata simu yangu akawa hapokei! Hayo

yakitokea, moyoni mwangu bado nilitamani sana kukutana na Mwanamke huyu jasiri, ambaye kwa vigezo

vyangu vya uelewa ni Oprah Winfrey wa Tanzania, yaani mwanamke tajiri kuliko wanawake wengi wote.

Kwa usumbufu uliotokea nikiabudu mfumo dume ambao umewafanya wanaume kujisikia wako juu, jambo

ambalo mimi sikubaliani nalo, ningeweza tu kusema “Yule ni mwanamke, nitajifunza nini kutoka

kwake?” Badala ya kufanya hivyo, nikijua kuna jambo la kujifunza kutoka kwa mama huyo niliendelea

kumtafuta nikitaka kufahamu, ilikuwaje akafanikiwa wakati wanawake wengi huona kama si rahisi

kufanya vizuri maishani na huiacha nafasi hiyo kwa wanaume? Anawezaje kuendesha miradi yote

aliyonayo wakati mimi nachanganywa akili na vimiradi vidogo tu kiasi kwamba kuna wakati naona

maisha hayana raha? Ipi hasa siri ya mafanikio yake?”
Hayo yalikuwa ni miongoni mwa mambo niliyotaka kujifunza kutoka kwake, ndio maana kwa muda mrefu

sana nilimtafuta bila kuchoka. Inawezekana kabisa alikuwa hataki kuniona, lakini ilikuwa ni lazima

nikutane naye na kujifunza kutoka kwake, maana nilikuwa na njaa kali ya mafanikio, hakuwa na jinsi

isipokuwa kuniona ili nile na kushiba. Binadamu hutakiwi kukata tamaa mpaka upate unachokihitaji,

huu ni ukweli na ndio niliouamini mimi nikimtafuta mama huyu.

Mmoja wa Wachungaji wangu kanisani, Mchungaji Weria ana mtoto wake aitwaye Genesis, mwenye umri wa

mwaka mmoja na nusu hivi, anapenda sana kupiga ngoma (Drums). Bila shaka akija kukua atakuwa

mwanamuziki mzuri sana wa Injili, mchungaji na mke wake wanatakiwa kulielewa jambo hili na

amwendeleze mtoto wake ili kipaji chake kikue”
Kila siku kanisani hata wakati mahubiri yanaendelea, Genesis hupenda sana kucheza na vyombo vya

kwaya. Jumapili iliyopita, wakati Mtumishi wa Mungu akihubiri, Genesis alikuwa kwenye ngoma,

akipiga mapigo yasiyokuwa na maana, ya kitoto ambayo kwa wengi nikiwemo mimi yalionekana kama

kelele hivi. Mzazi mmoja akanyanyuka na kwenda kumtoa Genesis kwenye ngoma kwa upendo ili watu

wapate kusikiliza neno liwaingie vizuri.

Alichokifanya Genesis akipinga uamuzi huo ni kulia mfululizo huku akionyesha kidole chake kwenye

ngoma, kelele zake zikaonekana kali kuliko ngoma. Hapakuwa na la kufanya zaidi ya kumrejesha

kwenye ngoma aendelee kupiga, kelele za ngoma zilionekana kuwa nafuu kuliko kilio chake kikali,

alipoketishwa tu kwenye ngoma, alitulia na mahubiri yakaendelea vizuri, alipochoka mwenyewe ndipo

akaondolewa.
Pamoja na umri wake mdogo Genesis alinifundisha jambo moja maishani “Hakuna kuacha, pambana kadri

uwezavyo mpaka upate unachokitaka”ndio maana nasisitiza sana watu wajifunze kutoka kwa kila mtu

aliyeko mbele yao, hakuna kukata tamaa, wala kuzuiliwa na mtu mpaka unachokitaka kitokee! Pamoja

na Mama Lwakatare kuonekana hayuko tayari kukutana na mimi, moyoni mwangu nilisema “Sitaacha mpaka

apatikane!”
Usiku wa kuamkia leo Mei 8, 2010, nimemfikiria sana mama huyu na nikauambia moyo wangu “Eric,

kesho, siku ya kesho, lazima Mama Lwakatare apatikane, hutafanya kazi yoyote mpaka umwone na

kuzungumza naye” Nayasema haya ili watu waweze kuelewa kuwa mtu anapokuwa na kiu ya mafanikio

anakuwa na hali gani.

Nataka tu niwakumbushe hapa ya kwamba, ninapoandika waraka huwa siandiki hadithi za kutunga

mlizozoea kuzisoma magazetini bali naandika mambo ya kweli tupu, anayemfahamu Mama Lwakatare

anaweza kumpigia simu na kumuuliza kama kisa hiki ninachokiandika ni kweli au ni uongo.
Kulipokucha nimekwenda kazini ambako nilitoa taarifa kwa Katibu Mhutasi wangu kwamba nakwenda

nyumbani kwa Mama Lwakatare na nikaondoka kuelekea Mikocheni. Sikuwahi kufika nyumbani kwa Mama

Lwakatare kabla, ilibidi niulizie mpaka nikapapata.

Wakati naegesha tu gari mbele ya lango lake, kijana mmoja, ambaye naamini ni mtu wa Usalama,

alinifuata na kuniuliza shida yangu nami nikamweleza kwamba nilikuwa pale kumwona mama Lwakatare.
“Una appointment (Miadi)?” aliniuliza akitabasamu.
“Sina”
“Sidhani kama utamwona”
“Leo lazima nimwone, nenda ndani kamweleze kuwa Shigongo yuko getini na leo anasema hataondoka

mpaka akuone”
Kijana huyo alicheka na kuondoka kwenda ndani aliporejea aliniambia mama alikuwa bado hajaamka na

isitoshe kulikuwa na wageni wengi sana waliokuwa wakisubiri kumwona, hivyo ni bora niondoke niombe

miadi ya kuonana naye siku nyingine.

“Bwana mdogo, hujanielewa? Nimesema leo siondoki mpaka nimwone mama Lwakatare, nenda tu kawaambie

huko ndani, kuna mgeni mwingine nje ambaye leo atakula hapa!”
Kijana alicheka na kubaki amesimama kando ya gari yangu na tukaanza kufanya mazungumzo ya hapa na

pale. Muda mfupi baadaye wazo lilinijia kuwa nimpigie simu mama Lwakatare na kumweleza kuwa nipo

mbele ya lango lake namsubiri na kwamba sitaondoka mpaka nimwone, nikaitafuta namba yake na

kuipata.

“Shikamoo mama”
“Marahaba hujambo mwanangu Eric?”
“Sijambo mama, nimekuja kukuona, niko mbele ya lango la nyumba yako, mama utanisamehe, si kwamba

mimi ni mtovu wa nidhamu lakini leo sitaondoka hapa nyumbani mpaka nikuone na tuzungumze!”
“Heee!Heee!Mwanaaangu, bado nimepumzika, kwanini usiende urudi baada ya masaa mawili?”
“Hapana mama, nitakusubiri!”
“Hutachoka?”
“Mama atafutaye hachoki, akichoka amepata!”
“Haya basi subiri”
Ofisini kwangu watu hunitafuta na kusubiri kuniona, ningeweza kuwa na kiburi na kusema “Ah! Mbona

mimi watu huwa wananitafuta? Mama atanigandishaje kiasi hiki?” kisha nikaondoka zangu, lakini

haikuwa hivyo, nilikuwa natafuta maarifa ya kunisaidia maishani mwangu, hivyo ilikuwa ni lazima

nivumilie!

Huwezi kuamini msomaji, sikukaa masaa mawili tu, nilikaa pale masaa matatu namsubiri Mama

Lwakatare ndipo nikaruhusiwa kuingia ndani ya nyumba yake kuzungumza naye. Simlaumu mama Lwakatare

kwa hilo, mama huyu ana wageni wengi mno wanaokwenda kumtembelea nyumbani kwake tena wenye miadi

naye, hivyo ilibidi mimi nivumilie.
Tulizungumza kwa dakika kumi na tano hivi, maswali yangu yakiwa matatu tu, la kwanza, nini siri ya

mafanikio yako? Ambako mama alijibu kifupi tu ni kutokata tamaa na kuchukulia matatizo kama

kichocheo cha mtu kufika juu. La pili likawa anawezaje kuendesha miradi yote aliyonayo ikiwa ni

pamoja na Kanisa? Nilitaka kujua nini siri ya mafanikio yake na shughuli zake zinakwenda vizuri

huku akifaidi maisha na Baraka alizopewa na Mungu, wakati mimi nachanganywa na vitu vidogo.

“Mwanangu ni rahisi tu, wakati mwingine mimi nashinda hapa nyumbani kwangu, lakini ninachofanya ni

kwamba, nawashirikisha watu wangu kwenye maono niliyonayo na kuwafanya waone maono hayo si yangu

peke yangu bali yetu sote na kuwafundisha jinsi ya kutimiza maono hayo, baada ya hapo nawaacha

wafanye wenyewe nikiwa nimewaamini!” Alimaliza mama Lwakatare, nikawa nimejifunza anawezaje

kuendesha shule zote alizonazo na sasa anaanzisha Chuo Kikuu, bila matatizo yoyote.
Swali la tatu likawa ni kitu gani kinachokutia hamasa ya kufanikiwa zaidi? Jibu lake lilikuwa

rahisi tu “Matatizo.” Hapa alimaanisha kuwa matatizo kwake ni kichocheo cha yeye kusonga mbele,

wakati mwingine anapokuwa hana tatizo, akili yake hudumaa, hivyo anapokuwa na matatizo akili yake

huingia kazini na mwisho wa siku matatizo hayo yakipita, hujikuta amepiga hatua kubwa zaidi

maishani mwake.

Kwanini nimeutoa mfano huu? Hutakiwi kukata tamaa katika maisha yako, lazima uhakikishe kile

unachotaka kitokee kinatokea hata kama dunia nzima imesimama mbele yako kukuzuia na hili

linawezekana kwa mtu aliyeamua, hicho ndicho kilichonitokea mimi, nilitaka kujifunza kutoka kwa

Mama Lwakatare ikaonekana kama haiwezekani, lakini niling’ang’ana hatimaye leo ndoto yangu ya

kukutana na mama Lwakatare imetimia.
Nimepata kile nilichokuwa nakitamani. Huu ndio ukweli kuhusu maisha, lazima kila mmoja wetu

ahakikishe anakutana na kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa maishani mwao, au niseme wale

anaotamani kuwa kama wao. Kama utashindwa kabisa kukutana nao ana kwa ana, isiwe kikwazo, kama

wanaandika vitabu basi tafuta vitabu vyao uvisome, tafuta CD zao usikilize, hiyo itakuwa ni sawa

kabisa na kukutana nao ana kwa ana na kujua jinsi akili zao zinavyofanya kazi.

Wiki iliyopita nilisema nimewahi kukutana na Matajiri wakubwa duniani; Waren Buffet, Bill Gates,

Richard Branson na Donald Trump na kufanya nao mazungumzo. Najua wasomaji wangu wengi walishtuka

na kuona kama nilikuwa nadanganya, ni kweli kabisa, nimekutana na watu hawa lakini si kama

unavyofikiria wewe, nimekutana nao kupitia vitabu walivyoandika, wote watatu nimesoma vitabu vyao

ambavyo ni sawa kabisa na kuketi nao mezani maana wanaeleza siri zote za mafanikio yao na

ninakushauri msomaji uhakikishe unapata vitabu vya watu hawa, hakika uwezo wa akili yako hautabaki

ule ule.

Kwa tajiri Warren Buffet, nimesoma kitabu chake kiitwacho The Warren Buffet’s way na nikajifunza

namna ya kuwekeza fedha katika biashara ya kuuza na kununua, kila kitu kimeelezwa ndani ya kitabu

hicho, ukikisoma ni sawa kabisa na kukutana na tajiri huyo. Kwa Richard Branson nimesoma kitabu

chake kiitwacho Screw It, lets do it.
Ndani ya kitabu hiki tajiri huyu anayemiliki shirika kubwa la ndege liitwalo Virgin Atlantic,

nimejifunza jinsi ya kuanza biashara chini kabisa na kukua bila kuogopa ushindani, kampuni yake

ilianza ndogo akidharauliwa lakini ikafanya vizuri kiasi cha kuyatishia masharika makubwa ya ndege

duniani kama British Airways.

Kwa tajiri William ‘Bill’ Gates nimesoma kitabu chake kiitwacho The road ahead na kujifunza jinsi

ya kuheshimu mawazo yako na kuwa tayari kuanzia sifuri na kusonga mbele, hata kama dunia nzima

itakupinga bila kujali waliokutangulia wamefika wapi. Ndani ya kitabu hiki Bill Gates anaielezea

historia yake na namna alivyoanzisha kampuni ya Microsoft.
Nimesoma pia kitabu cha Thinking big- kilichoandikwa na tajiri aliyewahi kutajirika halafu

akafulia, kisha kutajirika tena mara kumi zaidi yake huyu ni Donald Trump, ambaye ndani ya kitabu

chake hiki nimejifunza sheria moja iitwayo, Hire the best people, but don’t trust them! Hapa

hamaanishi kwamba usiwamini watu, bali linapokuja suala la kuajiri, hakikisha unaajiri watu

wanaoiweza kazi, wenye sifa lakini mwisho wa siku lazima uwakague.

Sio eti kwa sababu umepata Meneja mzuri, Mhasibu mzuri, Mhariri mzuri, Mpishi mzuri, basi wewe

unakwenda nyumbani kulala, hutaki kufanya kazi eti kwa sababu una wafanyakazi wazuri! Wakati

unaamka kutoka usingizini utakuwa kampuni haipo.
Haya ndiyo maisha yangu, kujifunza kila siku kutoka kwa watu mbalimbali walio mbele yangu. Nasoma

sana vitabu kila siku, siwezi kusinzia kabla sijasoma kitabu. Hii ndio desturi ambayo watu

wanaotafuta mafanikio lazima tuipandikize mioyoni mwetu, tusiwe watu wa kuridhika na kujivuna kwa

kidogo tulichokifanya au tulichonacho, dunia inabadilika kila siku, lazima nasi tubadilike pamoja

nayo na tutafute maarifa ya kufanikiwa kadri tuwezavyo, kutoka mahali popote, ndani na nje ya

darasa.

Nikumbushe tu kuwa binadamu siku zote huwa sawasawa na mawazo yake yalivyo, watu wanaomzunguka na

vitendo tunavyovifanya maishani mwetu ndivyo vinavyoamua kesho yetu iweje. Kuna mambo

tunayoyafanya ambayo yanaziita fedha na mafanikio yaelekee katika maisha yetu na kuna mambo

tunayoyafanya ambayo kila siku yanafukuza bahati, fedha na mafanikio kuja kwenye maisha yetu.

Mwisho wa siku hatuna mtu wa kumlaumu, kama yupo basi ni sisi wenyewe. Hivyo huu ni wakati wa

kubadilika na kuanza ukurasa mpya wa maisha.

Baada ya kunizunguka miguuni na tumboni, sasa wakawa wanakuja usawa wa kichwa changu.

Nilichogundua, nyoka mmoja alikuwa anataka kunidhuru, mwingine ananipigania. Yule anayetaka

kunidhuru, alikuja usawa wa kichwa na kupanua mdomo kwa lengo la kunimeza. Mungu wangu!

Kitu ambacho najishangaa mpaka leo ni ujasiri ambao niliuonesha siku hiyo. Nafikiri ni Mungu tu!

Nilitulia bila kuonesha hali yoyote ya kushtuka. Baadaye yule nyoka mwingine akambana shingoni

yule aliyekuwa anataka kunimeza halafu akamvuta nyuma. Wakaendelea kupigana.
Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kushuhudia nyoka wakigombana. Walizungushana pale chini mpaka

wakawa wamechoka, wakabaki kutazamana.

Baada ya muda kidogo, walipanda dirishani wakatoka nje. Ilikuwa ni kama vile nipo kwenye ndoto,

kwahiyo nikiamka kila kitu kitakuwa hadithi.
Walipotoka nje, nilitaka kusimama lakini nikashindwa. Mwili ulikakamaa hata kuinua mkono ikawa

ngumu, Kuna kipindi nilijaribu kugeuza shingo napo ikashindikana. Nilitulia hivyo hivyo lakini

baada ya muda nikaja kugundua kwamba mwili wote haukuwa na hisia. Ungenishika mguu nisingehisi

chochote.

Hilo likanipa uhakika kuwa kumbe ndiyo maana wale nyoka walipotambaa juu yangu sikuhisi chochote.

Hata yule mmoja alipotaka kunimeza, hakuna uoga wowote ambao ulinishika. Ilikuwa ni sawa na

kukutana na sanamu, kwamba hata ukimuingizia mkono hakuna lolote baya linaloweza kukupata.
Macho yangu yaliendelea kuganda pale dirishani, mara nikamuona nyoka mmoja anaingia, nikashindwa

kufananisha kama ni yupi kati ya wale waliotoka muda mchache uliopita. Alipomalizia kuingia,

mwingine naye akafuata. Nikajua ni hao hao, ila haikuwa hivyo. Ikawa baada ya huyu anafuata

mwingine.

Walikuwa nyoka wengi mno! Waliingia mpaka wakaanza kupandana. Wakajaa chumbani! Alianza mmoja

kuniangukia, wakawa wawili, kutahamaki nikawa nimewekwa katikati ya nyoka. Nikafunikwa gubigubi.

Kidogo kidogo nikaanza kukabiliwa na uhaba wa hewa, baadaye nikashindwa kabisa kuvuta pumzi.
Wale nyoka walikuwa wanacheza cheza juu yangu. Wakati mwingine wanatambaa, wengine niliwasikia

kabisa wanapita usawa wa kichwa na macho. Naweza kusema kuwa ni usawa wa kichwa tu ndiyo nilikuwa

naweza kuhisi kitu kwa sababu kuanzia shingo kushuka mpaka kwenye miguu nilibaki kama gogo.

Hali ya kukosa hewa ilinisumbua kadiri muda ulivyosogea mbele. Kifua kikabana nikahisi naelekea

kabisa kupoteza maisha. Kiwango changu cha ufahamu kikawa kinashuka taratibu mwisho kabisa nikawa

sijielewi. Nilizimika na kupoteza fahamu nikiwa katikati ya wale nyoka ambao wote walikuwa weusi.
Mapema asubuhi nilizinduka, mzee Balinaba (Barnabas) alikuwa ameketi kwenye kitanda cha miti

ambacho kinaitwa samadari kwa lugha fasaha ya Kiswahili. Mwanzoni nilimuona kama vile anajikagua

maungo yake lakini nilipomuangalia vizuri, nilijua kuna tatizo ambalo alikuwa anashughulika nalo.

Hakika! Nilipomuangalia vizuri, niligundua alikuwa na kitambaa ambacho alikitumia kufuta eneo la

pajani kwake. Na wakati akifanya hivyo alikuwa akigugumia maumivu. Kwa haraka haraka nikahisi ni

jipu, kwahiyo pale alikuwa analikamua na kujivuta. Hata hivyo haikuwa jibu sahihi!
Mzee Balinaba alikuwa na kidonda kikubwa kwenye paja lake na hilo nililigundua baada ya kuibuka

pole pole na kumtazama bila yeye mwenyewe kujua. Nilishtuka nilipoliona na nilijisikia kinyaa

lakini nilivumilia na kurudi taratibu mpaka pale nilipokuwa nimelala, halafu nikavuta kohozi kama

vile ndiyo naamka.

Aliposikia sauti ya kohozi langu alishtuka na kufunika paja lake, yaani alishusha suruali

aliyokuwa amevaa. Aligeuka akanitazama, bila shaka alitaka kuhakikisha kama nimeona alichokuwa

anafanya. Akawa anapumua kwa nguvu kisha akaniuliza nimeamka saa ngapi.
“Sasa hivi,” nilijibu huku nikibenua midomo. Ile picha ya kidonda kilichopo kwenye paja lake!

“Kuna kitu umeee… aah basi, vipi usiku ulikuaje?” Aliuliza tena.
“Usiku ulikuwa mzuri tu,” nilimjibu huku nikiinuka kitandani.
Akiwa katika hali ya kujishtukia, aliinama kisha akachukua kile kitambaa alichokuwa anakitumia

kufuta kwenye donda lake, akakikunja mkononi. Bila shaka alitaka nisikione. Alikuwa anahema kwa

nguvu na macho yake yalionesha wasiwasi mwingi. Nami nikawa namuangalia kama vile sijui

kinachoendelea.
Nilishikwa na kinyaa, nikajiuliza nilivyoweza kufanya mapenzi na mtu ambaye ana donda kubwa kwenye

paja bila kumuona. Nilijisikia vibaya. Kusema ule ukweli, zile hisia nilizokuwa nazo jana yake,

zilibadilika, nilianza kuona nimeuzwa kwa mzee huyo mchafu, havutii wakati mimi ni binti mdogo.

Kumbukumbu ya kukatishwa masomo ikarejea, kilio cha mama kwamba mzee Balinaba ameniroga

nilikikumbuka, nipofikiria kidonda chake nilichoka. Ukijumlisha na kuona ukweli kwamba ni huyo

huyo ndiye aliyenitoa bikira, niliumia mara kumi zaidi. “Oooh, Helena mimi maskini!” Niliwaza kwa

kujihurumia.
Machozi yalianza kunitoka, bila aibu yule mzee akanisogelea na kuanza kunibembeleza. Kwa hali

ilivyojionesha, ni wazi kwamba maisha yangu yaliishia hapo. Hiyo ilikuwa ngumu kuamini na kichwa

kikawa kama vile kimejaa mawazo. Nilikuwa na hasira kali lakini nikawa nashindwa moja kwa moja

kumkabili.

Ningewezaje? Yule mzee ni mchawi aliyekubuhu, niliyoyaona usiku peke yake yanatosha kutoa ushuhuda

wa jinsi alivyo mtu hatari. Mtu kugeuka nyoka! Nilijisikia kinyaa alivyofanya mapenzi na yule bibi

kizee wa jirani yetu kule kwa mama tena mbele yangu. Nilimchukia mpaka mwisho.
Ilikuaje akanioa? Ni swali ambalo nilijiuliza kisha nikakumbuka jinsi nilivyoingiwa na hisia za

kumpenda ghafla baada ya kunishika mkono. Hiyo ilizidi kunifanya nimuone yule mzee ni hatari mno,

kwani kama aliweza kuniroga mimi nikampenda na nikakubali anioe kisha tukafanya mapenzi,

anashindwaje kwa wengine mtaani?

Alinishika mkono akanitaka tutoke nje. Jua la asubuhi lilikuwa linawaka. Tuliketi chini ya miti

iliyopo uani kwenye nyumba yake. Kivuli na hewa safi vilinifariji kidogo. Aliniuliza kama nipo

tayari kwa kula, nikamwambia siwezi mpaka nisafishe mdomo, yaani nipige mswaki.
Eti jibu langu likawa kituko, mzee Balinaba alicheka sana. “Kupiga mswaki, eeh, kweli watoto wa

siku hizi mna mambo ya kizungu!” Aliongea kwa mtindo wa kushangaa, mzee huyo ambaye mtaani kwetu

tulizoea kumuita Mzee Mzungu kutokana na jinsi alivyokuwa mweupe, wengine walimwita Mgiriki.

Akiwa ananishangaa, nilisimama na kukata kitawi kidogo cha mchungwa, nikamuomba anioneshe maji,

akaniambia nisubiri, alikwenda ndani kuniletea. Nikiwa nimebaki pale nje peke yangu, mara upepo

mkali ukavuma na baada ya muda nikaona watu wawali wachafu sana wanapita wakiwa uchi.

Nilipigwa na butwaa! Wale watu walikuwa na kucha ndefu na nywele nyingi ambazo pia zilikuwa chafu

kupindukia. Macho yao yalikuwa mekundu. Waliingia ndani haraka na walipita kama umeme. Pale

nilipokuwa, nilijikunyata kwa woga. Walikuwa ni watu waliokufa zamani. Misukule!
Muda mchache baadaye mzee Balinaba alikuja akiwa ameshika kikombe cha maji. Nilitazama, yalikuwa

ni maji kweli kwa macho, nikayapokea huku nikamuangalia usoni kwa wasiwasi. Nikapiga hatua mbili

mbele na kuanza kupiga mswaki, nilipoanza kusafisha mdomo, nilishangazwa na harufu ya yale maji.

Yalikuwa yananuka damu, nilipogeuka kumuangalia mzee Balinaba, alikuwa anaishilizia ndani.

Nikayaangalia yale maji kwa mara nyingine. Tayari yalikwishabadilika rangi na kuwa mekundu.

Nikashtuka, nikakitupa kile kikombe. Ilikuwa ni damu!
Nikasisimka kwa woga!

Kauli hiyo ikanishtua. Nikakumbuka kwamba ni baba huyo huyo ambaye nilimuacha kwenye mtungi, pale

kwa mzee Balinaba, akiwa amechomwa kisu kifuani kilichopita usawa wa moyo wake. Nikamwambia mama

kwamba baba anauawa na anayemuua ni mzee Balinaba.

Niliingia mpaka subuleni. Nikawakuta baba na mama wakiwa wamekaa subuleni. Baba alionekana ni

mgonjwa sana, huku mama akiwa akiwa amejikunyata. Mama aliponiona, alinyanyuka na kunikumbatia.

Akaanza kulia. Nilimuuliza kilio chake, akanijibu ni baba, kwa sababu hawezi kuongea, hali wala

kunywa.

Kauli hiyo ikanishtua. Nikakumbuka kwamba ni baba huyo huyo ambaye nilimuacha kwenye mtungi, pale

kwa mzee Balinaba, akiwa amechomwa kisu kifuani kilichopita usawa wa moyo wake. Nikamwambia mama

kwamba baba anauawa na anayemuua ni mzee Balinaba.
“Unasemaje mwanangu?” Mama aliniuliza katika katika hali ya mshtuko.
“Eeh mama, baba anauawa, nimemuona sasa hivi kule kwa mzee Balinaba akiwa amechomwa kisu kifuani,”

nlimwambia mama huku nikiwa bado na macho ya wasiwasi.

Bado niliamini kwamba lile dubwasha lilikuwa bado linanifuatilia, lakini kwa muda wote nikiwa pale

sebuleni, sikuweza kuliona. Kuna wakati niliamini labda baada ya kunikosa lilikuwa limeondoka na

kurudi kwa mzee Balinaba. Masahibu yote hayo, niliyachukulia kama kisa cha kujitakia cha baba.
“Niambie vizuri, baba yako anauawa kivipi?” Swali la mama lilinirudisha pale ndani.

“Aam, mama we’ acha tu! Kwa macho yangu nimeshuhudia,” nilijibu kwa kukurupuka, jibu ambalo

halikumpa msaada wowote mama.
“Unaniacha njia panda Helena, unasumbuliwa na nini? Sikuelewi na huniambii baba yako anataka

kuuawa na mzee Balinaba kivipi?”
Kufikia hapo nikatulia ili nianze kumsimulia mama kile nilichokishuhudia kwa mzee Balinaba lakini

ile kutaka kufunua kinywa tu, mambo yakawa magumu. Sauti haikutoka licha ya kujaribu kwa dakika

kadhaa. Hali hiyo ilimtisha hata mama, kwahiyo akamuacha baba na kuja kunipa msaada.

Mama alijitahidi kunisaidia lakini haiwezekani. Moyo wake mwepesi wa kike, alishindwa kumudu yote

hayo, alianza kulia mfululizo, kisha akapoteza fahamu. Niliumia mno kwa sababu nilishuhudia jinsi

alivyohangaika wakati anaelekea kupoteza fahamu. Nilimuangalia baba, naye alikuwa anagugumia

maumivu makali.
Hisia kuwa matatizo yote yale yalisababishwa na baba, yaliyeyuka. Uchungu wa mzazi anaujua mwana.

Niliteswa mno na ile hali aliyokuwa nayo. Ingawa nilikuwa siwezi kuzungumza sauti ikatoka,

nilisimama hadi pale alipokuwa ameketi baba na kuanza kujitahidi kumhudumia. Alitia huruma kweli!

Ni wazi baba alikuwa kwenye mateso makubwa. Nikawa nachanganyikiwa bila kujua cha kufanya. Baba

anaumwa, mama hana fahamu. Kama mtu angeniona, bila shaka angedhani nimewehuka kwa maana kila

nilichofanya hakikuwa na tafsiri yenye kueleweka. Mara nimshike mama namuamsha kwa kumtikisa,

baada ya sekunde narudi kwa baba.
Nani anasema uchawi haupo? Mimi nimeona ndiyo maana nasimulia haya; Nikiwa nahangaika kumuamsha

mama na wakati huo huo nikifuatilia kwa ukaribu hali ya baba, kumbe lile dubwasha lilikuwa

linatazama ndani na kushuhudia kila kitu. Jicho lake moja, lilitosha kuonesha kwamba halikuwa na

mzaha hata kidogo.

Kwa woga, nilimfuata mama na kulala nikiwa nimemkumbatia. Sikutaka kukutanisha macho na dubwasha

hilo, ingawa kila wakati nilipoinua kichwa, bado lilikuwa limeganda dirishani likiangalia ndani.

Nami nikawa nikimuona tu, narudi kujificha haraka sana. Ni vema kusimuliwa, ukiliona linatisha

kweli kweli!
Zilipita dakika nyingi moyo wangu ukiwa unauma kutokana na mauvimu ya hofu, mara nikamsikia mama

anapiga chafya. Naam, alikuwa anazinduka! Alipiga chafya mara tatu, kisha akainuka. Nami nikawa

namfuatilia hatua kwa hatua. Alianza kupepesa macho huku na huko alipokutanisaha na yangu

akatulia.

Kwa wakati huo, kumbukumbu zake zilikuwa hazijawa sawasawa, kwahiyo akawa hajui ni nini hasa

kilichompata ndiyo maana baada ya kukutanisha macho na kutazamana kwa muda, swali la kwanza

kuniuliza lilikuwa ni: “Kuna nini kimetokea?” Kabla sijajibu akasema tena: “Mbona sijielewi elewi?
Bado nikaendelea kuwa kimya, hali hiyo ikamfanya aondoe macho kwangu na kuyaelekeza kwa baba. Hapo

picha ikaanza kurudi, kwani alimuangalia mara moja kisha akarudisha macho kwangu. Machozi yakaanza

kumtoka akanisogelea na kutaka kunikumbatia. Alikunjua mikono kutaka kufanya hivyo.

Hata hivyo, badala ya kumpokea alipotaka kunikumbatia, nilimuonesha ishara ili atazame dirishani.

Alinielewa na papo hapo aligeuza kichwa kutazama. Ooh Mungu wangu! Nadhani nilikosea kwa sababu

woga uliomshika mama si wa kawaida. Alipiga kelele lakini mayowe yake hayakusaidia.
“Nini hicho Helena… nini hicho… ni nini jamani?” Ni sehemu ya maneno ya mama ambayo yalionesha

jinsi alivyokuwa anatapatapa.
Tuliendelea kufarijiana kwa jinsi tulivyoweza. Muda ulienda taratibu mno. Swali kubwa ambalo

nikawa najiuliza ni uwepo wa majirani, kwani katika hali ya kawaida, tukio lile lilitosha

kukusanya idadi kubwa ya watu lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza. Utadhani mtaa mzima ulikuwa

umehama.

Hata barabarani nilipokuwa nakimbizwa na lile dubwasha, kutoka kwa mzee Balinaba hadi nyumbani,

sikuweza kukutana na mtu yeyote yule. Kuna wakati nilihisi mkusanyiko wa yale matukio ni ndoto za

usiku lakini bado picha kamili ilionesha ni mambo ambayo yalichukua nafasi katika ulimwengu wa

kawaida.
Tukiwa tumekwishahangaika kwa muda mrefu, tukasikia mlango wa uani unasukumwa. Woga ukazidi

kutushika, tukashikana na mama na kukumbatiana kwa nguvu kungoja hicho ambacho kingetokea. Kusema

ukweli, kipindi hicho hakuna kati yetu aliyemuwaza baba ambaye alikuwa kwenye maumivu makali.

Kila mtu alitaka kunusuru maisha yake. Tukangoja hicho kilichosukuma mlango wa uani. Nyayo za

binadamu zikasikika zikisogelea kabisa pale sebuleni. Kumbe alikuwa mzee Balinaba, alipofika,

badala ya kutuhurumia, alianza kucheka na kuzungumza maneno ya kejeli ambayo yalinilenga mimi.
“Aliyekwambia ufunue vitu visivyokuhusu ni nani? Siku nyingine utapata matatizo makubwa,” alisema

mzee Balinaba na kuongeza:
“Haya inuka twende.”

Niligoma kunyanyuka lakini akanitisha kwamba kama nisipotii kauli yake, baba angefariki ndani ya

muda mchache. Nilidhani utani au vitisho tu peke yake, kwahiyo nikaendelea kukataa. Baada ya kuona

nimegoma, aliondoka huku akisema nitajuta. Akatoka, nikamuona kwa dirishani akiliongoza lile

dubwasha.

Niliwashuhudia wakianza kuondoka, lile dubwasha mbele, mzee Balinaba nyuma. Nikiwa naendelea

kuwashangaa, wanavyoondoka, nilishtuliwa na kelele za kutapatapa za baba ambaye alikuwa anarusha

miguu huku na huko na kujipiga mfano wa mtu anayekaribia kukata roho. Moyo ukapiga paa! Nikajua

nampoteza baba!

Hata barabarani nilipokuwa nakimbizwa na lile dubwasha, kutoka kwa mzee Balinaba hadi nyumbani,

sikuweza kukutana na mtu yeyote yule. Kuna wakati nilihisi mkusanyiko wa yale matukio ni ndoto za

usiku lakini bado picha kamili ilionesha ni mambo ambayo yalichukua nafasi katika ulimwengu wa

kawaida.
Tukiwa tumekwishahangaika kwa muda mrefu, tukasikia mlango wa uani unasukumwa. Woga ukazidi

kutushika, tukashikana na mama na kukumbatiana kwa nguvu kungoja hicho ambacho kingetokea. Kusema

ukweli, kipindi hicho hakuna kati yetu aliyemuwaza baba ambaye alikuwa kwenye maumivu makali.

Kila mtu alitaka kunusuru maisha yake. Tukangoja hicho kilichosukuma mlango wa uani. Nyayo za

binadamu zikasikika zikisogelea kabisa pale sebuleni. Kumbe alikuwa mzee Balinaba, alipofika,

badala ya kutuhurumia, alianza kucheka na kuzungumza maneno ya kejeli ambayo yalinilenga mimi.
“Aliyekwambia ufunue vitu visivyokuhusu ni nani? Siku nyingine utapata matatizo makubwa,” alisema

mzee Balinaba na kuongeza:
“Haya inuka twende.”

Niligoma kunyanyuka lakini akanitisha kwamba kama nisipotii kauli yake, baba angefariki ndani ya

muda mchache. Nilidhani utani au vitisho tu peke yake, kwahiyo nikaendelea kukataa. Baada ya kuona

nimegoma, aliondoka huku akisema nitajuta. Akatoka, nikamuona kwa dirishani akiliongoza lile

dubwasha.
Niliwashuhudia wakianza kuondoka, lile dubwasha mbele, mzee Balinaba nyuma. Nikiwa naendelea

kuwashangaa, wanavyoondoka, nilishtuliwa na kelele za kutapatapa za baba ambaye alikuwa anarusha

miguu huku na huko na kujipiga mfano wa mtu anayekaribia kukata roho. Moyo ukapiga paa! Nikajua

nampoteza baba!

Kuona hivyo, nikatoka mbio na kumfuata mzee Balinaba (Barnabas). Nilipotoka nje, nilimuona akiwa

anazidi kutokomea akiwa na dubwasha lake. Nikapiga mayowe! Akageuka, nikamuonesha ishara ya mkono

kumuomba arudi. Hata hivyo, naye alikataa, akaendelea na safari yake.
Nilitamani kumpuuza ili aende zake lakini taswira ya kumpoteza baba huku namuona ilinirudia.

Nikakakimbia mbio kumfuata mzee Balinaba. Nilipomfikia nilimshika mkono, nikapiga magoti kuomba

asaidie kumponya baba. Akaniangalia kwa jicho kali ambalo lilitoa tafsiri ya kama mtu anasema: “Si

ulikuwa unajifanya mjanja?”
Akasema: “Jiangalie sana Helena, wakati mwingine siyo wa utani, umenikosea sana kwenye vitu vyangu

nyumbani, halafu unaleta jeuri.”

Aliposema hivyo, aliinua kidolea akawa kama mtu anayeandika maandishi fulani angani, baada ya hapo

akanishika mkono na kuniambia tuondoke kwa sababu kila kitu tayari. Nilipingana na kauli yake,

nilijua ananidanganya, kwahiyo nikazidi kumuomba kwa huruma yake amponye baba.
Hapa naomba nikiri kuwa, kuna wakati watu tunamkosea Mungu, tunamkufuru na kuwaabudu binadamu

wengine kutokana na matatizo ambayo tunakumbana nayo. Mfano ni mimi, kwa wakati huo sikufikiria

kama Mungu ni sababu ya kila kitu. Nilimuona mzee Balinaba ndiye mkombozi.

Wakati mimi niliendelea kutokumuamini mzee Balinana na kumchukulia kama mtu anayetumia hila ili

kuyakatisha maisha yangu. Yeye alinishangaa kwa kutokumuamini. Eti pale alipo, alikuwa

amekwishamtibu baba yangu, kwahiyo akaniona mimi mbishi, nisiyemuamini kwa nguvu alizonazo.
“Nifanyeje ili uniamini? Sawa, ngoja nimuite aje hapa,” alisema mzee Balinaba na kupuliza viganja

vyake, baada ya muda, nikamuona baba anakuja pale tulipo. Lilikuwa tukio la kushangaza, kwani baba

ambaye nilimuacha hoi, hajiwezi, eti ndiye alikuwa anatembea mzima bila wasiwasi.

Nilimuangalia mzee Balinaba kwa macho ya wasiwasi, wakati huo yeye hakuwa na shaka ya aina yoyote.

Alipofika pale tulipo, alimsalimia mzee Balinaba kwa heshima zote, kisha akanigeukia mimi.

Akaniuliza naendeleaje na maisha ya ndoa? Hii ilinipa picha kwamba hakuna chochote

alichokikumbuka.
Zaidi alinishangaza pale aliposema: “Mwanangu nilikwambia huyu mumeo ni mtu mwema sana, utapata

vingi ukiwa na yeye.”
Alizungumza mfululizo, kwani hata pale aliponiuliza naendeleaje na mume wangu, kabla ya kumjibu

alidakia mada nyingine ya kumwagia sifa za utukufu mzee Balinaba. Ni wazi kuwa baba yangu alikuwa

amerogwa kwa kiasi kikubwa. Hakuwa na uwezo wa kupambanua lolote, yaani hata alivyokuwa anateseka

na kukaribia kufa hakukumbuka.

Katili mzee Balinaba aliamua kumfanya anavyotaka. Mwanzoni nilikuwa nawaogopa na kuwachukia

wachawi lakini kufikia hapo, niliwachukia mpaka kiwango cha mwisho. Chuki yangu iliongezeka

kutokana na matukio mfululizo. Laiti ningeweza, ningehakikisha nawasambaratisha wote dunia nzima.
Bila kupenda, huku nikiwa na mawazo mengi, niliagana na baba kisha nikaongozana na mzee Balinaba

hadi nyumbani kwake. Wakati wote huo, lile dubwasha lilikuwa mbele yetu. Tulipofika kwa mzee

Balinaba, aliliongoza kuingia kwenye mtungi ambao niliufunua likatoka, kisha akaweka mfuniko.

Baada ya hapo alinigeukia na kuanza kunisema. Hiyo ilikuwa siku ya kwanza mzee Balinaba kunionesha

sura ya ukali. Aliniambia kuwa amechoka kunibembeleza kwa sababu ni muda mrefu amejitahidi

kuninyenyekea na kunibembeleza lakini nimejidai kiburi, kwahiyo anachotaka kufanya ni kunionesha

yeye ana nguvu kiasi gani.
Aliposema hivyo, mara radi kali zikaanza kupiga. Zilinigonga pale pale. Zilipiga kama kumi

mfululizo. Msomaji, nikikwamba radi naomba upate picha halisi ya ninachokizungumza. Si radi za Dar

es Salaam, huko hakuna. Nazungumzia zile za Sumbawanga ambazo zikipiga, unasikia mwili mzima

unatikisika.
Nilifikiri zimetumwa na mzee Balinaba ili kuniadhibu kama alivyosema lakini kumbe haikuwa hivyo.

Zilimpiga hata yeye, akalala chini akapiga kelele. Yalikuwa ni mayowe ya kusikilizia maumivu hasa.

Pala pale akaniamrisha nitoke chini ya mti, nipande kwenye mtungi.

Akasema ni kisasi, kuna wapinzani wake wa mambo ya uchawi wanataka kumuangamiza. Baada ya

kuzungumza hivyo nilipanda kwenye mtungi. Mzee Balinaba alibadilika na kuwa kondoo. Niliwahi

kusikia kabla kwamba radi huwa haifanyi kazi kwa kondoo, siku hiyo nikaamini. Nilishuhudia

vimbwanga vya wachawi.

ILIPOISHIA “Inamaana kumbe huwa nakula nyama za watu!” Niliongea kwa kushangaa.
“Usijifanye ulikuwa hujui. Unafahamu sana ndiyo maana ukawa unasifia, kwahiyo chagua moja,” mzee

Balinaba alisema kwa msisitizwachawi.

Nilitafakari mengi lakini mawili yaliniumiza sana kichwa. Kugundua kwamba kumbe siku zote nilikuwa

nafurahia kula nyama ambazo ni za binadamu, pili ni kulazimishwa kumtoa ndugu yangu mmoja kafara

ili aliwe nyama na wachawi. Nilijiapiza kuwa ningepambana mpaka mwisho, kuona familia yangu

haipati madhara ya aina yoyote.

Siku hiyo usingizi ulikuwa wa shida sana. Licha ya kujitahidi sana lakini iliniwia vigumu kuupata.

Usiku ulikuwa mzito na mrefu sana. Katikati nilitokewa na taswira ya bibi yangu mzaa mama, anaitwa

Bi. Shuwena. Alikuwa marehemu aliyetangulia mbele za haki tangu nikiwa darasa la pili. Hii

inamaana kuwa ilikuwa miaka minne kabla ya usiku huo.

Bi. Shuwena akiwa kwenye mavazi meupe, moja kwa moja niliamini ni mzimu wake kutokana na habari

ambazo nilikuwa nikisimuliwa. Alikuwa katika sura ya upole huku akinihurumia mno. Alisogea mpaka

jirani yangu kabisa na kunyoosha mkono wa kulia, lakini nilipoinua wa kwangu kutaka kumpokea

akatoweka. Nilibaki nashangaa!

Kwa muda mrefu nilibaki natafakari tukio hilo, nikawa najumlisha na lile la kulazimishwa na mzee

Balinaba kumtoa sadaka ndugu yangu mmoja, auawe na wachawi ili wamle nyama. Ni wazi niliona dunia

inanikamata upande mbaya. Sikuona wa kunitetea, niliamini wachawi wana nguvu ambayo hakuna hata

kiumbe mmoja aliyeweza kuwazuia wakiamua.

Ilipofika kama saa 10 usiku hivi, nilisikia upepo mkali unavuma nje ya nyumba. Paa likawa

linatikisika na hata kitanda kutetemeka. Hali ilikuwa ya kutisha mno na ilidumu kwa takriban

dakika 25. Ungeweza kudhani mvua kali ya upepo ingefuatia lakini haikuwa hivyo. Nikiwa kitandani

giza totoro baada ya kibatali kuzimika kutokanba na upepo, nilijikunyata kama kinda la njiwa

katika ya mvua.

Upepo ulisumbua kwa muda huo, mwisho nilisikia kishindo kikubwa, yaani kitu kizito kilidondoka

pale chumbani. Hofu kubwa ilinishika, nikasogea karibu na mzee Balinaba lakini badala ya kugusa

mtu nikashika kitu kigumu. Ilikuwa ni kinu kikubwa! Nilijiuliza ilikuaje, kwa maana pale alikuwa

amelala mzee Balinaba lakini alitoweka na pale alipokuwa kilikuwepo kinu.

Uchawi upo jamani! Kumbe mzee Balinaba aliondoka siku nyingi na kwenda kwenye mizunguko yake ya

kichawi na pale aliacha kinu. Mimi nikiwa nimefumbwa kwa kiinimacho, sikujua hilo, nilidhani ni

yeye lakini baada ya ile patashika, ndiyo nikaweza kugundua kwamba pale alipokuwepo, badala yake

kulikuwa na kinu kikubwa!

Hapa nifafanue kitu kwamba unaweza kila siku kulala na mchawi chumba kimoja lakini usijue. Kila

siku anafanya shughuli zake na wewe usitambue chochote. Upo naye kitanda kimoja lakini kila

ukigeuka unamuona. Pale anakuwa siyo yeye, ni kinu! Kinawekwa kimazingara halafu unazugwa kwa

kiinimacho kwamba hata ukishtuka kwa bahati mbaya, umuone yupo kumbe siyo!
Wapo watu wanaishi na waume au wake wachawi lakini hawajui chochote. Usiku wanalala wote, kila

akipeleka mkono anamshika na akitazama anamuona. Yeye anadhani wapo wote kwamba mwenzake anaogelea

usingizini, wakati hayupo pale. Yupo mbali kwenye harakati za kichawi na wachawi wenzake. Ni siri

kubwa lakini ukiwa mtu wa Mungu ni rahisi kumbaini.

Kuna dalili hizi ambazo ni vema niziweke wazi. Ikiwa unalala sana usiku na kujikuta unashtuka

ghafla alfajiri baada ya kuota ndoto ndefu isiyoeleweka, hapo ni vizuri kuelewa kuwa ama

ulichukuliwa na wachawi kwenda kufanya kazi zao za kilimo na nyinginezo usiku au unaishi na mchawi

ambaye hukupaka dawa ili ulale sana mpaka atakaporudi kwenye shughuli zake.

Aidha, unaweza kuwa unalala na mtu ambaye anapotelea usingizini kwa muda mrefu, unamuamsha haamki

mpaka pale anapogutuka mwenyewe. Hapo pia unapaswa ufahamu kwamba huyo anaweza kuwa mchawi

amekwenda kwenye harakati zake na wachawi wenzake au ni mtu ambaye amebebwa na wachawi. Asikwambie

mtu, wachawi wana matukio mengi usiku!
Hivyo basi, baada ya kile kishindo cha pale chumbani, nilitulia kwa muda kidogo. Hali ya hewa nje

ikatulia. Ikawa kimya, hapo sasa nikaanza kusikia mtu akikoroma pale ndani.

Nilipata shauku ya kujua ni nani lakini ikawa inaniwia ugumu wa kuamka na kwenda kumuangalia. Kuna

kipindi nilihisi ni mnyama mkali, kwahiyo ningemsogelea angenijeruhi vibaya.
Nilipata kigugumizi kwa muda, nikawa nimetulia kitandani huku nikiendelea kujikunyata. Ile sauti

ya kukoroma ikabadilika, sasa akawa kama mtu ambaye analia kwa mbali. Niliendelea kushikwa na

shauku ya kutaka kujua mbivu na mbichi lakini bado woga ukawa unanizuia kufanya chochote. Nilibaki

nasikilizia ila muda ulipozidi kwenda niliamua.

Nilishuka kitandani na kutafuta kiberiti. Taratibu nikiwa natembea kwa kupapasa ukuta huku

nikihofia kugongana na hicho kitu kilichodondoka chumbani, nilipata kiberiti na kuwasha kibatali.
Mungu wangu! Kumbe ni mzee Balinaba. Alikuwa hoi, uchi wa nyama, pembeni yake kukiwa na ungo

pamoja na tunguri nyingi. Ni wazi alikuwa kwenye shughuli zake za kichawi.

Nilitafakari mengi lakini mawili yaliniumiza sana kichwa. Kugundua kwamba kumbe siku zote nilikuwa

nafurahia kula nyama ambazo ni za binadamu, pili ni kulazimishwa kumtoa ndugu yangu mmoja kafara

ili aliwe nyama na wachawi. Nilijiapiza kuwa ningepambana mpaka mwisho, kuona familia yangu

haipati madhara ya aina yoyote.

Siku hiyo usingizi ulikuwa wa shida sana. Licha ya kujitahidi sana lakini iliniwia vigumu kuupata.

Usiku ulikuwa mzito na mrefu sana. Katikati nilitokewa na taswira ya bibi yangu mzaa mama, anaitwa

Bi. Shuwena. Alikuwa marehemu aliyetangulia mbele za haki tangu nikiwa darasa la pili. Hii

inamaana kuwa ilikuwa miaka minne kabla ya usiku huo.

Bi. Shuwena akiwa kwenye mavazi meupe, moja kwa moja niliamini ni mzimu wake kutokana na habari

ambazo nilikuwa nikisimuliwa. Alikuwa katika sura ya upole huku akinihurumia mno. Alisogea mpaka

jirani yangu kabisa na kunyoosha mkono wa kulia, lakini nilipoinua wa kwangu kutaka kumpokea

akatoweka. Nilibaki nashangaa!

Kwa muda mrefu nilibaki natafakari tukio hilo, nikawa najumlisha na lile la kulazimishwa na mzee

Balinaba kumtoa sadaka ndugu yangu mmoja, auawe na wachawi ili wamle nyama. Ni wazi niliona dunia

inanikamata upande mbaya. Sikuona wa kunitetea, niliamini wachawi wana nguvu ambayo hakuna hata

kiumbe mmoja aliyeweza kuwazuia wakiamua.

Ilipofika kama saa 10 usiku hivi, nilisikia upepo mkali unavuma nje ya nyumba. Paa likawa

linatikisika na hata kitanda kutetemeka. Hali ilikuwa ya kutisha mno na ilidumu kwa takriban

dakika 25. Ungeweza kudhani mvua kali ya upepo ingefuatia lakini haikuwa hivyo. Nikiwa kitandani

giza totoro baada ya kibatali kuzimika kutokanba na upepo, nilijikunyata kama kinda la njiwa

katika ya mvua.

Upepo ulisumbua kwa muda huo, mwisho nilisikia kishindo kikubwa, yaani kitu kizito kilidondoka

pale chumbani. Hofu kubwa ilinishika, nikasogea karibu na mzee Balinaba lakini badala ya kugusa

mtu nikashika kitu kigumu. Ilikuwa ni kinu kikubwa! Nilijiuliza ilikuaje, kwa maana pale alikuwa

amelala mzee Balinaba lakini alitoweka na pale alipokuwa kilikuwepo kinu.

Uchawi upo jamani! Kumbe mzee Balinaba aliondoka siku nyingi na kwenda kwenye mizunguko yake ya

kichawi na pale aliacha kinu. Mimi nikiwa nimefumbwa kwa kiinimacho, sikujua hilo, nilidhani ni

yeye lakini baada ya ile patashika, ndiyo nikaweza kugundua kwamba pale alipokuwepo, badala yake

kulikuwa na kinu kikubwa!

Hapa nifafanue kitu kwamba unaweza kila siku kulala na mchawi chumba kimoja lakini usijue. Kila

siku anafanya shughuli zake na wewe usitambue chochote. Upo naye kitanda kimoja lakini kila

ukigeuka unamuona. Pale anakuwa siyo yeye, ni kinu! Kinawekwa kimazingara halafu unazugwa kwa

kiinimacho kwamba hata ukishtuka kwa bahati mbaya, umuone yupo kumbe siyo!
Wapo watu wanaishi na waume au wake wachawi lakini hawajui chochote. Usiku wanalala wote, kila

akipeleka mkono anamshika na akitazama anamuona. Yeye anadhani wapo wote kwamba mwenzake anaogelea

usingizini, wakati hayupo pale. Yupo mbali kwenye harakati za kichawi na wachawi wenzake. Ni siri

kubwa lakini ukiwa mtu wa Mungu ni rahisi kumbaini.

Kuna dalili hizi ambazo ni vema niziweke wazi. Ikiwa unalala sana usiku na kujikuta unashtuka

ghafla alfajiri baada ya kuota ndoto ndefu isiyoeleweka, hapo ni vizuri kuelewa kuwa ama

ulichukuliwa na wachawi kwenda kufanya kazi zao za kilimo na nyinginezo usiku au unaishi na mchawi

ambaye hukupaka dawa ili ulale sana mpaka atakaporudi kwenye shughuli zake.

Aidha, unaweza kuwa unalala na mtu ambaye anapotelea usingizini kwa muda mrefu, unamuamsha haamki

mpaka pale anapogutuka mwenyewe. Hapo pia unapaswa ufahamu kwamba huyo anaweza kuwa mchawi

amekwenda kwenye harakati zake na wachawi wenzake au ni mtu ambaye amebebwa na wachawi. Asikwambie

mtu, wachawi wana matukio mengi usiku!
Hivyo basi, baada ya kile kishindo cha pale chumbani, nilitulia kwa muda kidogo. Hali ya hewa nje

ikatulia. Ikawa kimya, hapo sasa nikaanza kusikia mtu akikoroma pale ndani.

Nilipata shauku ya kujua ni nani lakini ikawa inaniwia ugumu wa kuamka na kwenda kumuangalia. Kuna

kipindi nilihisi ni mnyama mkali, kwahiyo ningemsogelea angenijeruhi vibaya.
Nilipata kigugumizi kwa muda, nikawa nimetulia kitandani huku nikiendelea kujikunyata. Ile sauti

ya kukoroma ikabadilika, sasa akawa kama mtu ambaye analia kwa mbali. Niliendelea kushikwa na

shauku ya kutaka kujua mbivu na mbichi lakini bado woga ukawa unanizuia kufanya chochote. Nilibaki

nas

visitors comments