Ndege iliyombeba mzee Albano mwakatala ilipunguza kasi taratibu na hatimaye ikasimama.Tayari gari la wagonjwa lilikwisha fika na wauguzi na madaktari walikuwepo tayari kuhakikisha mzee Albano anapatiwa kila kitu kinachohitajika wakati akishushwa toka ndegeni na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.Kiongozi wa msafara ule wa madaktari toka hospitali kuu ya Patrick Sr memorial hospital ,Dr.Henry Mgumbwa alikuwa pembeni akipewa taarifa na madaktari wa Mzee Albano.
Kutoka serikalini alikuwepo mheshimiwa waziri wa afya akiiwakilisha serikali ,pamoja na viongozi mbali mbali,vile vile walikuwepo viongozi wa dini toka madhehebu mbali mbali, na viongozi wa kisiasa pia walikuwepo.Ilimradi kila nyanja ambayo iliguswa na taarifa za kurejeshwa nchini mzee Albano ilituma mwakilishi wake.
Familia ya mzee Albano ilishuka ndegeni ikiongozwa na mke wake na binti zake wawili,wakasalimiana na kufarijiwa na viongozi kadhaa wa serikali waliokuwa pale uwanjani pamoja na viongozi wa dini.Ilikuwa ni hali ya simanzi kubwa.Huko nje ya uwanja kulikuwa na umati mkubwa wa watu na magari ambao wote walionyesha jinsi gani mzee Albano alivyokuwa mtu wao wa muhimu.
Taratibu zote zikakamilika kisha mzee Albano huku akiwa hajitambua ,akapakiwa katika gari la wagonjwa na safari ya kuelekea hospitali ikaanza.Ulikuwa ni msafara mkubwa wa magari kuelekea Hospitali.Polisi wa usalama barabarani walijitahidi kufanya kazi ya ziada ili kufanikisha zoezi la kuelekea hospitali lisiwe gumu sana ,hasa kutokana na msongamano wa magari katika jiji hili la Dar.
Taarifa za kurejeshwa nchini Mzee Albano Mwakatala zilisambaa karibu kila kona ya nchi.Magazeti yaliandika kwa kirefu juu ya kushindikana kupona huko nchini India na kisha madaktari Bingwa kushauri arejeshwe nyumbani ,kwa sababu hakukuwa na tumaini tena la kupona,kilichosubiriwa ni siku ya kufariki kwake.Madaktari katika hospitali kubwa nchini India walijitahidi kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja katika kujaribu kuutibu ugonjwa wa mzee Albano bila mafanikio.
Mzee Albano alikuwa ni mmoja kati ya watu wenye heshima kubwa sana nchini Tanzania.Alikuwa mmoja kati ya wawekezaji wakubwa wazawa,ambaye alikuwa na viwanda karibu kila mkoa na siku zote alikuwa akijitahidi na kupigia kelele sana juu ya kuongeza ajira kwa wazawa.Hii ilimfanya ajulikane na kupendwa .Pamoja na kuwa mmoja kati wa wawekezaji wakubwa nchini,ambaye alichangia kupatikana kwa ajira lukuki,alikuwa ni kimbilio kubwa kwa wale watu wenye matatizo mbali mbali.Karibu kila mwezi alikuwa akilipia gharama za operesheni kubwa kubwa za watu mbali mbali wasiokuwa na uwezo,achilia mbali kulipia gharama za elimu kwa watoto ambao wazazi wao hawakuwa na uwezo wa kuwasomesha,vile vile aliweza kuvisaidia vikundi vingi vya akina mama na vijana katika kujikwamua kimaisha.Ni mzee aliyekuwa na heshima ya pekee katika jamii ya watanzania.
Albano mwakatala ,ambaye baba yake alikuwa na asili ya Ureno alizaliwa mkoani Mbeya wakati huo baba yake akiwa mwekezaji mkubwa katika kilimo cha mpunga mkoani humo.Baba yake alioa mwanamke mweusi kutoka mkoani mbeya na wakafanikiwa kupata mtoto mmoja tu ambaye ndiye yeye mzee Albano.Alikulia mkoani Mbeya hadi alipomaliza elimu ya sekondari na kujiunga na chuo kikuu cha Kilimo ambako alihitimu shahada ya kilimo.Akaenda tena kuendelea na masomo nchini Japan katika kilimo cha Mpunga kwani alitaka kuendeleza kazi aliyokuwa akiifanya baba yake.Ni wakati huo ndipo alipopatwa na pigo kubwa la kuondokewa na wazazi wake wote wawili waliofariki kwa ajali ya gari.Alirudi nchini baada ya kumaliza masomo yake nchini Japan ,akaendeleza miradi ya kilimo aliyoiacha baba yake kwa ufanisi mkubwa. Ndani ya miaka miwili alikuwa amepiga hatua kubwa na kuongeza mtaji mara dufu ya ule wa baba yake.Hii ikamfanya ajikite tena zaidi katika uwekezaji mwingine.Akawa akifungua viwanda karibu kila mkoa ili kuyaongezea thamani mazao ya wakulima.Akawa tegemeo kubwa la mazao ya wakulima.Biashara yake ikawa kubwa sana na sasa akawa mmoja kati ya wawekezaji wakubwa na hapo ndipo alipoamua kuhamia mkoani Dar es salaam kwa sababu za kibiashara.
Alioa mke wake aliyekuwa mzaliwa wa Mbeya ambaye walikutana masomoni nchini Japan.wakafanikiwa kupata watoto wawili wa kike.Serena na Isabela.Watoto aliowapenda kuzidi maelezo.
Akiwa katika safari zake za kibiashara alipata ajali ya gari na hivyo kumsababishia tatizo katika ubongo wake.mwanzo lilidhaniwa ni tatizo dogo ambalo lingeweza kutibiwa kwa kunywa dawa za kawaida.Muda ulivyozidi kwenda ndivyo hali yake ilivyozidi kuwa mbaya,ikabidi apelekwe nchini India katika hospitali moja kubwa yenye mabingwa wa masuala ya vichwa na ubongo.Uchunguzi ulifanywa na jopo la madaktari bingwa kwa muda wa siku saba wakijaribu kutafuta namna ambayo wangeweza kufanya upasuaji na kuondoa sehemu ya ubongo ambayo kutokana na kuchelewa kufanyiwa upasuaji ilikuwa imeanza kuharibika..Hatimaye waliiita familia yake na kuileza ukweli kuwa operesheni hiyo ilikuwa ni Ngumu kufanyika kwani kwa vyovyote vile kama ingefanyika uwezekano wa kupona Mzee Albano ulikuwa mdogo sana.Ni lazima angekufa.Suala la kufariki baba yao lilikuwa ni msamiati mgumu kwa familia hii,hivyo wakataka kumuhamishia nchini Marekani katika hospitali kubwa zaidi,lakini wakapewa ushauri na madaktari kuwa hata kama wakimpeleka huko hakuna hospitali inayoweza kuutibu ugonjwa ule ,mzee Albano ni mtu anayesubiri siku zake.
Mzee Albano baada ya kupata taarifa ile ,alimshukuru Mungu na akaiomba familia yake isiendelee na matibabu sehemu nyingine tena bali warudi nyumbani ili akafie katika ardhi ya nyumbani.Uamuzi huu uliiliza mno familia hii na wote waliompenda mzee Albano.Kwa muda wa wiki nzima vyombo vya habari vilipambwa na taarifa za maamuzi ya mzee Albano.SIKU ZA ALBANO ZINAHESABIKA,KABURI LA ALBANO LAANDALIWA,TAIFA LAJIANDAA KUOMBOLEZA,hivi ni baadhi tu ya vichwa vya habari vilivyokuwa vikipamba magazeti ya kila siku,hali iliyoamsha hamasa kwa jamii ya kitanzania kufuatilia kwa karibu hali ya mzee huyu kipenzi cha wengi.
Serikali kupitia kwa balozi wake nchini India ilijaribu kuishawishi familia yake ikubali serikali igharamie matibabu ya Mzee Albano katika nchi nyingine ,ikiwa ni kuonyesha shukrani kwa mzee huyu kwa mambo aliyoyafanya,lakini bado ikawa ngumu.Mzee Albano pamoja na kuwa kitandani bado alikataa kata kata kupatiwa matibabu zaidi,kwa sababu alikwisha hakikishiwa kuwa hawezi pona tena.
Siku zikazidi kusonga mbele na hatimaye siku ya kurudishwa nyumbani kwa mzee Albano ikawadia.Siku iliyokuwa na majonzi tele.Ukiwaona watu waliokuwa hapo uwanjani ni kama vile walikuwa msibani.Maongezi yalikuwa ni ya chini chini kila mmoja akionyesha huzini aliyonayo.Pamoja na kuwa ni siku ya kazi lakini huwezi amini umati wa watu uliokusanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar .
Patrick Sr memorial hospital ni moja kati ya hospitali kubwa kuwahi kujengwa nchin Tanzania.Ilikuwa ni hospitali ya aina yake kwa kuwa ilikuwa na uwezo wakutibu karibu kila ugonjwa.Hospitali hii ilijengwa mahususi kwa ajili ya kumbukumbu ya Patrick Sr mmoja kati ya madaktari waliojitolea maisha yao katika kuwasaidia watu masikini.Katika kuuuenzi mchango wa baba yake ,Patrick Jr akaamua kujenga hospitali hii kubwa na ya aina yake ili kutoa matibabu kwa watu wote na hasa yale magonjwa makubwa yaliyoshindikana katika hospitali nyingine zote hivyo kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya upasuaji.Hospitali hii iliyosheheni mabingwa wa kila fani ilihudumia si tu Tanzania bali hata nchi zote zinazoizunguka.
Eneo lote la kupaki magari katika hospitali hii kubwa lilijaa magari kwa mara ya kwanza toka hospitali hii imefunguliwa.Watu wote hawa walikuwa wamekuja kuonyesha mshikamano wao kwa mzee Albano na kumtakia afya njema.Gari la wagonjwa lililombeba Mzee Albano likaingia hospitalini hapo,likaingizwa mpaka ndani kabisa na mzee albano akiwa bado hajitambui akapokelewa na kupelekwa katika chumba maalumu kwa ajili ya kupatiwa uangalizi .
Kila kitu kilifanyika kwa haraka na kwa umakini wa aina yake.Dr Henry alikuwa bega kwa bega na madaktari wake kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda kama kuilivyopangwa.Baada ya kuhakikisha kila kitu kiko safi na tayari Mzee Albano anaendela kupatiwa matibabu akaelekea ofisini kwake.Akabonyeza namba kadhaa katika simu yake ya mezani
“Hallow Dr Henry hapa toka Patrick Sr memorial hospital,Naomba kuongea na Dr Jason tafadhali” Akasema Dr Henry
“ Dr jason kuna kazi anaifanya.Baada ya kama dakika kumi hivi atakuwa amemaliza”
“Ok akitoka mwambie anipigie ni muhimu mno”
Akakata simu kisha akapiga simu mapokezi na kuomba mke wa Mzee Albano na wanae waweze kupandisha ofisini kwake.
“Karibuni sana jamani.” Akasema Dr Henry baada ya mke wa mzee Albano na wane kuwasili ofisini “Kwanza napenda kuwapa pole nyingi sana kwa kazi kubwa mliyoifanya ya kumuuguza huyu mzee wetu mpaka katika hatua hii aliyofikia .mama na wanao mnastahili pongezi kwa ujasiri mkubwa mliouonyesha.papo hapo bado tunazidi kuwaomba mzidi kuwa wavumilivu kwa sababu hali ya mzee wetu bado si nzuri sana kama wenyewe mnavyoona na kwa mujibu wa taarifa za kidaktari.Sisi hapa tunaahidi kufanya kila tunaloweza ili kumpa tiba inayostahili mzee wetu mpaka hapo baadae.Kwa sasa hatuwezi kumruhusu akae nyumbanio kwani pamoja na hali yake hii bado anahitaji sana uangalizi mkubwa wa madaktari.Tunaye Daktari wetu bingwa wa mambo haya ya neva za ubongo na uti wa mgongo,kwa sasa yuko Dodoma kikazi ,nimempigia simu sasa hivi nikakuta bado yuko kazini hivyo muda wowote atapiga simu hapa ,nataka naye nimuite arudi mara moja leo hii hii ili aongoze jopo la madaktari katika kumpa tiba mzee wetu.Hata kama huko Nje ya nchi wameshindwa sisi hatuwezi kukata tamaa kirahisi ,tutazidi kumpa kila aina ya matibabu na tutafanya kila tunaloweza ili kuokoa au kuongeza zaidi siku za kuishi…….”kabl;a hajaendelea simu ikaita akaipokea
“Hallow,Dr Henry hapa”
“Dr Ni mimi Jason.Nimepata ujumbe wako.Poleni sana na shughuli nasikia leo kuna pilika pilika hapo.”
“Yah! Leo Mzee Albano amerudishwa kutoka India hivyo Serikali ikatukabidhi sisi jukumu la kuhakikisha tunampatia huduma zote muhimu za kitabibu.Hapa tunapoongea niko na familia yake.Ninachoomba ni kwamba itatumwa ndege yetu leo saa kumi na mbili jioni ije ikuchukue ili uongoze jopo la madaktari katika matibabu ya mzee Albano kwa sababu wewe ndio biongwa wa neva za ubongo na uti wa mgongo.”
“Ok Dr Henry hakuna shida,nafurahi kukabidhiwa jukumu la kumuangalia mzee huyu muhimu japo sijawahi hata kumuona kwa sura.Nitakuwa tayari muda huo ndege itakapofika”
“ Ok Dr.see you then.Bye” Akakata simu nakuendela na maongezi na familia ya mzee Albano.
Saa kumi na mbili za jioni ndege inayomilikiwa na hospitali ya Patrick Sr memorial ilitua katika uwanja mdogo wa hospitali hiyo uliopo pembezoni mwa majengo ya hospitali.Ni ndege iliyomleta Dr Jason bingwa wa neva za fahamu za ubongo na uti wa mgongo.Ni mmoja kati ya madaktari bingwa wachache sana katika fani hii kwa ukanda huu wa Afrika.
Dr Jason akapokelewa na Daktari mkuu Dr Henry kisha kwa mwendo wa kasi wakaanza kuelekea hospitalini.
“Mgonjwa anaendeleaje? Akauliza Dr Jason
“mgonjwa hali yake bado si nzuri.Mpaka sasa hivi bado hajarejewa na fahamu” Akasema Dr Henry
Moja kwa moja wakaelekea katika chumba cha wagonjwa mahututi alimolazwa Mzee Albano.Madktari na wauguzi walikuwa wakiendelea na kila linalowezekana ili kumsaidia mzee Albano aweze kurejewa na fahamu.Alipoingia Dr Jason mle ndani kila mmoja aliyekuwemo alionyesha tabasamu la matumaini usoni.Hii ilionyesha ni jinsi gani walivyokuwa na imani na Dr Jason.Kwa haraka akapewa taarifa ya maendeleo ya mgonjwa,akaomba apewe na faili la mzee Albano,kisha akaelekea ofisini kwake.
Ni saa tatu za usiku sasa,masaa matatu yameshapita tangu Dr Jason alipoanza kulipitia faili la Mzee Albano.Alilipitia kwa umakini mkubwa sana na alilirudia mara ya pili na ya tatu.aliporidhika akainua simu na kumpigia Dr Henry ambaye hakupoteza muda akafika ofisini kwa Dr Jason.
“DR Henry nimelipitia kwa makini faili la mgonjwa,ila kuna hivyo vipimo nimeviorodhesha hapo ninataka vichukuliwe mara moja.Ni vipimo muhimu sana ambavyo vitatusaidia kuona jinsi ya kuanza kumsadia mgonjwa”
Dr Henry akaichukua karatasi ile yenye vipimo akaiangalia kisha akasema.
“Ok Dokta nafikiri timu nzima ya vipimo ipo tayari,ngoja watuletee vipimo hivyo”akatoka na kumwacha Dr Jason bado akiendelea kulipitia faili lile.
Saa moja baadae Dr Henry alirudi akiwa na faili lenye vipimo vyote alivyovihitaji Dr Jason.
“Kila kitu kiko humu Dokta.Kama kuna kitu kingine unahitaji niko ofisini”
Jason akaliweka faili alolikuwa akisoma pembeni kisha akaanza kulipitia lile faili lenye vipimo alivyokuwa akivihitaji.Dakika zaidi ya arobaini alizitumia kuyapitia majibu yale ya vipimo alivyovitaka.Akasimama na kuzunguka humo chumbani huku akiangalia juu.Ni wazi kuna kitu kikubwa alichokuwa akikifikiria.Mwishowe akaamua kumwita Dr Henry.
“Dr nimepitia kwa umakini faili la mgonjwa na baadae vipimo hivi ulivyoleta.”
“yes Dr.” Akajibu Dr Henry kwa shaukui ya kutaka kujua nini alichoitiwa
“Dr Henry kuna kitu nimekigundua katika uchunguzi wangu ambacho hawa wenzetu kule India walishindwa kukigundua.Pamoja na kwamba mabingwa wenzangu huko India walisema haiwezekani kwa mgonjwa kufanyiwa upasuaji lakini bado sijakubaliana nao kutokana na majibu ya vipimo nilivyovitaka.Nina kila sababu ya kukwambia kuwa tunaweza kuifanya operesheni hii na kuokoa maisha ya mgonjwa.”
Dr Henry alibaki mdomo wazi akiwa hana la kuongea.Alimuamini Dr Jason kupita kiasi kwani ni mmoja kati ya madaktari wenye uwezo na akili ya ajabu sana.Lakini kwa hili alionyesha mstuko wa dhahiri.
“najua utakuwa umestuka sana baada ya kusikia hivyo, na siwewe tu,kila mtu anaweza akastuka akisikia kauli yangu,lakini ukweli ni kwamba mgonjwa bado anayo nafasi ya kuishi iwapo tutamfanyia upasuaji wa haraka.Nashindwa kuelewa kwa nini hawa madaktari wa India walishindwa kuligundua hili na kusema kuwa mzee huyu hawezi pona
Saa nzima ilitumika kwa Dr Jason kumwelezea na kumfafanulia Dr Henry juu ya kile alichokigundua katika vipimo na sabab ya kutaka opereshi ile ifanyike.Dr Henry bado hakuwa na uamuzi hivyo akaamuru kuitishwa kikao cha dharura usiku huo cha madaktari ili kuona kama kuna ulazima wowote wa kufanya operesheni hiyo.
Haraka haraka ujumbe ukasambazwa kwa timu yote ya madkatari na kwa muda wa dakika kumi wote wakawa wamekusanyika katika chumba cha mikutano.Mkutano huu ulichukua zaidi ya masaa manne ndipo wote waliporidhika kuwa kweli kuna ulazima wa mzee Albano kufanyiwa upasuaji katika ubongo wake.
Ilipata saa tisa za usiku wakati Dr Henry alipompigia simu mke wa mzee Albano na kumtaka yeye na familia yake wafike hospitali hapo asubuhi na mapema kuna jambo la muhimu wanataka kuelezwa.
**********************************************************
Asubuhi ya saa mbili ndipo Dr jason alipowasili hospitali.Moja kwa moja akaelekea katika chumba cha mgonjwa ,akapewa taarifa ya maendeleo ya mgonjwa.hali yake ilikuwa si mbaya sana kuliko alivyokuwa ameletwa.Alipohakikisha kila kitu kiko safi akatoka na kuelekea ofisini kwake tayari kwa kukutana na familia ya mzee albano ili kuielezea kwa ufasaha juu ya uamuzi wake wa kufanya operesheni.
Aliingia ofisini kwake,siku hiyo hakutaka kujishugulisha na kazi nyingine yeyote licha ya kukuta mafaili kadhaa ya wagonjwa hapo mezani kwake.akainua simu na kumpigia Daktari mkuu Dr Henry.
“Dr habari za asubuhi.’
“Nzuri Dr Jason.habari za toka jana?”
“Nzuri tu Dr Henry.Mi tayari nimeshafika ofisini ,nimetoka kumuangalia mgonjwa na hali yake inaendelea vizuri.Maendeleo yake yanatia moyo sana.”
“Yah hata mie nilipita asubuhi,hali yake inatia matumaini.”
“Ok Dr Henry mi niko ofisini iwapo utanihitaji”
“Uhhm nafikiri tunaweza kukutana sasa na familia ya Mzee Albano pale katika chumba kidogo cha mikutano ili tuongelee suala hili la mzee wao,manake nilipata taarifa kuwa walikwisha fika muda mrefu sana na nikaelekeza wapelekwe kule ili tukaongee nao.”
“Ok Dr naja sasa hivi” Akajibu Dr Jason na kukata simu kisha akatoka na kuelekea katika chumba kidogo cha mikutano.
Muda mchache baadae tayari alikwisha fika ,akakinyonga kitasa na kuingia ndani.Ile amiengia tu ndan ya chumba kile akakutana na kitu ambacho hakukitegemea kukiona.
“Serenaaa…….!!!!!!. Akasema Dr Jason kwa mshagao mkubwa.
Kila mtu mle chumbani akabaki akishangaa.Serena ambaye alikuwa ameongozana na mama yake naye akabaki ameduwaa akishangaa.
*********************************************************
Ni milio ya ndege wa aina mbali mbali walioruka katika miti na bustani nzuri za maua zilizopo ndani ya jumba hili la kifahari ndizo zilizokuwa zimetawala.Ukimya mkuu ulikuwemo ndani ya jumba hili.Katika ghorofa ya juu kabisa kikao kizito kilikuwa kikiendelea.Mzee Bryson kamutere,mzee mwenye utajiri wa kutisha nchini Tanzania alikuwa ndiye mwenyekiti wa kikao hiki.Pembeni yake alikuwepo binti yake ,mbunge mdogo kuliko wote katika bunge la jamhuri ya muungano Stella kamutere.,halafu wakawepo na watu wengine tisa wenye nyadhifa mbali mbali serikalini na mashirika binafsi.
“Ndugu wajumbe wa kikao hiki,nawashukuruni sana kwa kuitikia wito huu wa dharura japo si wote mliohudhuria lakini mliopo mnatosha sana kuendesha kikao hiki.”
Alifungua kikao Mr Kamutere.
“Jambo tunaloenda kulizunumza ndugu zanguni ni jambo zito.nafikiri wote mnazo taarifa za kurejeshwa nchini Mzee Albano.Mpango wetu ulikwenda vizuri sana kule India,madaktari walifanya kama vile tulivyowataka wafanye.Kazi Nzuri sana uliifanya Bw.Kumzaya.Kwa sasa dunia nzima inaelewa kuwa mzee Albano hawezi kupona na hana siku nyingi za kuishi.Ni kweli kwa mujibu wa madaktari ni kwamba kama hatapatiwa tiba muafaka kwa muda wa wiki moja basi mzee Albano atafariki na hilo ndilo hasa lengo letu.Si kwamba kule India hawakuwa na uwezo wa kumfanyia mzee Albano upasuaji na kuokoa maisha yake,la hasha.Uwezo huo walikuwa nao lakini lengo letu sisi lilikuwa ni kuwarubuni wale madaktari kwa fedha nyingi ili wafanye kama tunavyotaka sisi na kutoa taarifa kuwa mzee Albano si wa kupona.Kazi yetu ingekuwa rahisi kama familia yake ingekubali afanyiwe upasuaji kwani ingejulikana amekufa katika operesheni.Lakini mzee Albano mwenyewe akakataa kufanyiwa upasuaji na kuomba arudishwe nyumbani.Kurudishwa kwake nyumbani kulikuwa na lengo moja tu kuja kutulipua.Anajua hana maisha marefu ,hivyo alichotaka kukifanya ni kutuanika hadharani.Bilioni 700 tulizochukua toka serikalini kwa mradi hewa wa umwagiliaji ni nyingi sana,na ni yeye ndiye amekuwa mstari wa mbele tangu alipokataa kushiriki katika mradi huu, kusisitiza kuwa tuzirudishe fedha hizo.Iwapo kila kitu kitawekwa hadharani itaamsha hasira kwa umma wa watanzania na kuiweka nchi katika wasiwasi hasa katika kipindi hiki wananchi wanapokabiliwa na matatizo mbali mbali likiwemo hili la ugumu wa maisha.
Kama wote tunavyomfahamu mzee Albano ni mtu mwenye uchungusana na nchi hii na yuko tayari kufanya lolote kwa ajili ya maslahi ya Tanzania.kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani toka hospitali ya Patrick Sr Memorial amabako amelazwa baada ya kurudishwa toka India,hivi tunavyoongea ,madkatari na familia ya Mzee Albano wako katika kikao.Kuna uwezekano mkubwa mzee Albano akaendelea kuwa hai.Kuna huyu daktari bingwa wa neva za fahamu za ubongo na uti wa mgongo anaitwa Jason charles kasima,ambaye anataka kufanya upasuaji katika ubongo wa mzee Albano na kuna kila imani kuwa iwapo atafanyiwa upasuaji huu basi ni lazima apone.daktari huyu ni mmoja kati ya madaktari wachache wa kutumainiwa katika upande huu wa neva za fahamu,si hapa tu bali duniani..Tunachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuhakikisha hilo halitokei kwa gharama zozote zile.”Mzee Bryson akatulia akavuta pumzi na kuwaangalia wajumbe ambao pamoja na kuwa chumba walichokuwamo kuwa na kiyoyozi lakini bado nyuso zao zilionyesha kuvuja jasho.
“Baba umesema Dr Jason Charles Kasima ndiye anayetaka kufanya huu upasuaji?” Stella akauliza kwa msisitizo huku akimtolea baba yake macho ya shauku
“Yes my dear.Ni huyu huyu mchumba wako Dr Jason”
Saa kumi na mbili za asubuhi Dr Jason alikwisha amka.Kama kawaida yake akafanya mazoezi mepesi ya viungo halafu akaingia bafuni kujimwagia maji.Baada ya kujiweka safi akawasha simu yake ambayo alikuwa ameizima toka jana yake alipopigiwa simu na Stella.Jumbe zaidi ya kumi za maneno zikaingia katika simu yake mfululizo.Tisa kati ya hizo zilitoka kwa Stella na zote zilikuwa zikilaumu kwa kitendo cha Jason kuzima simu yake na kumkumbusha ni jinsi gani anavyomuhitaji katika maisha yake.Dr Jason akatabasamu.
“I’m sorry Stella.”Akajisemea kwa sauti ndogo.
Dr Jason akampigia simu Dr Anna maria na kuuliza maendeleo ya mgonjwa.Mgonjwa alikuwa akiendelea vizuri.Akapumua kwa nguvu baada ya taarifa ile.
“Ee Mungu nisaidie niweze kuokoa maisha ya huyu mzee” Akaomba Dr Jason.Akakaa sofani na kutafakari.Siku hii Dr Jason alionekana mwingi wa mawazo.
Akiwa bado katika tafakari mlango wake unagongwa.Akainuka na kwenda kuufungua mara akajikuta akichanua tabasamu pana sana baada ya kukutana na sura ya kiumbe malaika iliyokuwa imesimama pale mlangoni.Alikuwa ni Serena akiwa ndani ya tabasamu pana
“Habari za asubuhi Jason”Akasalimu Serena
“Nzuri tu Serena.Umeamkaje?
“Nimeamka salama Jason.I had a wonderfull night full of sweetdeams.what about you”
“ouh safi sana.hata mimi nilikuwa na usiku mzuri kwa sababu kulala hoteli moja na mrembo kama wewe ni bahati kubwa” Akasema Jason huku akicheka na kumfanya Serena naye acheke.
“mama kanipigia simu asubuhi anataka kujua ni wapi nimelala.Nimemdanganya kuwa nilichelewa sana kutoka hospitali hivyo Ikanilazimu kuchukua chumba katika hoteli yenye usalama.Alikuwa na wasi wasi sana lakini nimejitahidi kumtoa wasi wasi ila kinachotakiwa ni mimi kumuwahi pale hospitali kabla hajafika asubuhi hii.”
“Ok Serena sasa itabidi nikupeleke hadi Rosela Restaurant ulikoacha gari lako jana jioni halafu mimi nitaelekea nyumbani kwanza na baadae nitakuja hositali.Unajua watu wakiona tukiingia katika gari moja na hasa mama yako wanaweza kuwa na maswali ya kujiuliza kulikoni.Leo nitakuwa na shughuli nyingi za kufanya ila kama utakuwa na nafasi mchana ningeomba tupate lunch pamoja.Would you love that?
“Ouh Jason I always love to spend times with you.Nitaangalia kama nitakuwa na nafasi nitakufahamisha.” Akasema Serena huku akicheka na kumfanya Jason atabasamu.
Walitoka hapo hotelini na kuelekea moja kwa moja Rosela Restaurant ambako Serena aliliacha gari lake jana jioni wakati wakipata chakula.
“Serena siwezi elezea furaha niliyonayo kwa kupata wasaa wa kula nawe chakula cha usiku na kupata wasaa wa kuongea nawe mawili matatu.Nimefurahi sana kusema ukweli.I’m real happy” Akasema Dr Jason wakati akimshusha Serena ili aingie katika gari lake.
“Me too Jason.Nimefurahi sana kupata wasaa wa kuongea na wewe.You are such a wonderfull doctor.Hope we can spend more time together pindi mambo haya yatakapokwisha..”
“Ok Serena natumai tutaonana baadae.Please take a good care of yourself.”
“You too Jason”
Dr Jason akamshika mkono Serena wakaagana Serena akaingia katika gari lake na kuondoka.Dr Jason akaliangalia gari la Serena likiondoka hadi lilipopotea kabisa katika upeo wa macho yake.
“I love you Serena.Nitafanya lolote niwezalo kwa ajili yako..I don’t want to loose you this time” Akawaza Dr Jason naye akawasha gari na kuondoka.
Kabla hajaenda sehemu yoyote alipita kwanza nyumbani kwake.Akafunguliwa geti na kuingia ndani.Mtumishi wa ndani akamsalimu na kumpatia ujumbe.
“mama Stella amepiga simu usiku zaidi ya mara tano akiulizia kama umerudi.Aliacha ujumbe kuwa ukirudi umpigie”
“Ok Mona ahsante nitampigia.Kila kitu hapa nyumbani shwari lakini? Akauliza Dr Jason
“Ndiyo bosi kila kitu kiko safi hakuna tatizo lolote”
Dr Jason akaingia chumbani kwake akabadili nguo na kuvaa suti nzuri nyeusi iliyomkaa vema.Akajitazama katika kioo na kuhakikisha amependeza akafunga mlango wake na kupanda gari akaondoka.
Saa mbili na dakika ishirini aliwasili nyumbani kwa Stella akafunguliwa geti na kuingia ndani.Akashuka garini na moja kwa moja akaelekea chumbani kwa Stella.Akabisha hodi na sauti toka ndani ikamruhusu kuingia.Ile ameingia tu akakutana na sura iliyosawajika ya Stella Macho yalikuwa mekundu na yamevimba kuonyesha kuwa alikuwa akilia.Stella alikuwa amekaa kitandani akiwa ameushika mto.
Walitazamana kwa muda wa dakika tatu nzima bila kuongea kitu chochote.Stella machozi yalikuwa yakimtoka.
“So tell me what is this Jason? Akasema Stella huku akilia.
“Stella I’m sorry.najua umeumia sana.I’m real sorry.Ulinipigia simu jana lakini ikazima kwa kutokuwa na chaji ya kutosha.hata hivyo nilikuwa busy sana kiasi sikuweza kupata muda wa kukupigia tena” Akasema Dr Jason huku akienda kukaa kitandani karibu na Stella.
“Tangu lini simu yako imekuwa na matatizo ya chaji?
“Toka jana mchana simu ilikuwa na chaji kidogo ,nikajua nitachaji jioni lakini sikufanya hivyo hadi pale uliponipigia nayo ikazima.
Stella akamtazama kwa jicho kali sana akafuta machozi na kusema
“what a liar.Jason tangu lini umeanza kunidanganya?”
“Kukudanganya?? Akauliza kwa mshangao Dr jason
“Ndiyo .Nakuuliza tangu lini umeanza kunidanganya?I do trust you with my life Jason na sikutegema kama itafika siku ambayo utanidanganya”
“Mbona sikuelewi Darling? Siwezi kukudanganya unajua.Siku zote nimekuwa mkweli na sijakuficha hata kitu kimoja.And why should I lie to you my angel? Please trust me darling.Ninayokwambia ni ukweli mtupu..”Dr Jason akajitetea.
Stella akamtazama tena kwa macho ya ukali yaliyoonyesha hasira ya wazi wazi.
“Jason do you love me? Akauliza Stella.Dr Jason akamtazama kwa makini usoni.
”Kwa nini unauliza hivyo wakati ukweli unaujua kuwa wewe ndiye pekee nikupendaye?
“Say Yes or No Jason.Do you real love me?”
“Yes I do love you”Akajibu Dr Jason
Stella akaina akatika mto aliokuwa ameuweka mapajani mwake.Dr Jason akamshika nywele .
“No don’t touch me Jason.U don’t love me at all” Akasema Stella kwa ukali
“Ouh baby don’t go there.Huko sasa unakoenda ni mbali mno.I love you and you know that.I’m sorry about last night I knew u needed me but I’m a doctor Stella na muda mwingi ninautumia kuhudumia wagonjwa.Nisingeweza kuja kwako jana Stella.Trust me I love you and I can do anything for you,anything…..
“Stop it Jason.Nimegundua unanidanganya.kama ungekuwa unanipenda kweli usingelala jana na Serena binti wa mzee Albano Panavoc hotel.Nimelia sana Jason.Sijalala usiku wote nilikuwa nalia.kwa nini unifanyie hivi? U don’t know how much I do love you Jason. I Love you more than my own life.Ulifikiri sintajua??…….
Dr Jason akabaki mdomo wazi.hakujua ajibu kitu gani.Akamwangalia Stella ambaye alikuwa akimtazama kwa hasira.Alihisi miguu kuisha nguvu.
Akajitahidi kukusanya nguvu na kujibu
“baby that’s not true.kama kuna mtu aliyekwambia mambo hayo amekudanganya.Please amini kile ninachokwambia mimi.” Jason akajaribu kujitetea huku moyo wake ukienda mbio na kijasho kumtiririka kwa mbali.
“Jason ,Jason usije ukajaribu kunidanganya.Mimi nafahamu kila unalolifanya.Huwezi nidanganya kitu.Nina uhakika na ninachokisema na kama ukitaka nitakutajia hata chakula mlichokula .Si mlikula maini nyie,au mie mwongo? Kataa na hilo.”
Dr jason akashindwa kukataa akabaki akimwangalia Stella huku akihema kwa nguvu.hakuwa na sababu ya kubisha tena kwa sababu ilionekana tayari Stella ana taarifa kamili.
“Jason Darling kwa nini lakini ukanifanyia hivyo hali unajua kuwa wewe ndiye kila kitu kwangu? Huyu binti wa mzee Albano , Serena yeye ana kitu gani cha tofauti na mimi??? Answer me jason” Stella akasema kwa uchungu
“Stella una uhakika gani kuwa nilikuwa pale Panavoc hotel na Serena? Akauliza Dr Jason
“Jason mimi nina vyanzo vingi vya taarifa kwa hiyo usije jaribu kunidanganya hata siku moja.Ninajua kila unachokifanya.Kila unakoenda.I know every minute of you” akasema Stella
“Kwa hiyo umeweka watu wa kunifuatilia siyo? U don’t trust me right? Akauliza Jason
Stella akamuangalia usoni bila kujibu lolote
“Nakuuliza Stella umeweka watu wa kunifuatilia mimi siyo?
“For your own safety Jason”Stella akajibu
“My own safety??? Unamaanisha nini?
“Jason I don’t want you to get hurt ndio maana nimeweka watu wa kukufuatilia na kukulinda”
Dr Jason akastuka akasimama na kuuliza.
“Kunilinda? Kwa nini uweke watu wa kunilinda?kwani kuna tatizo gani?Na kama lengo lako lilikuwa ni zuri kwa nini basi usiniambie?
“Jason sit down first.We need to talk.”
Dr Jason huku kijasho kikimtoka na moyo kumwenda mbio akakaa kitandani kama alivyoombwa na Stella.
“haya nambie unalotaka kuniambia” Akasema Dr Jason
“Jason mchana wa leo tunasafiri.Don’t ask why and where we’re going.Kila kitu kiko tayari kwa safari.Kama kweli unanipenda kwa dhati ya moyo wako mchana wa leo tunasafiri.” Akasema Stella
Dr Jason akasimama akazunguka mle chumbani na kupumua kwa nguvu.
“Stella sijakuelewa unasema nini?
“Ninasema mchana wa leo tunasafiri.Kuna safari ya dharura sana imetokea hivyo inatulazimu mimi na wewe tuondoke mchana huu wa leo.”
Dr jason akahisi joto akavua koti na kulitupa sofani.Shati lake lilikuwa limeanza kulowa jasho ambalo sasa lilikuwa limeanza kumtiririka kwa kasi.
“No Stella I cant go.”
Stella naye akainuka pale kitandani na kusimama karibu na Jason.
“Jason unasemaje?
“Nasema siwezi kwenda hiyo safari.tangu lini kukawa na safari ya kustukiza namna hii? halafu unaelewa kabisa kwamba niko katika kipindi kigumu sana cha kuokoa maisha ya mzee Albano.Operesheni hii ni kubwa sana kuifanya katika maisha yangu.Mimi ndiyo tumaini pekee la maisha ya mzee yule.Stella mbona sikuelewi darling?
Stella akamsogelea karibu zaidi akamtazama usoni na kusema
“Jason please u don’t have to do that.Achana kabisa na operesheni hiyo.”
Dr Jason akarudi nyuma hatua kadhaa akamkazia macho Stella.Hakuamini alichokisikia
“ Stella unasema nini???? Akauliza
“Jason u don’t have to do that operation.We have to leave the country this afternoon”
Dr Jason akamtazama Stella kana kwamba ndiyo anamuona kwa mara ya kwanza.
“Stella siamini kama ni wewe ndiye unayeniambia maneno haya leo.Stella umekuwa mstari wa mbele kila siku kunihimiza nizidi kuokoa maisha ya watu leo umegeuka na kuniambia nisifanye operesheni ya mzee Albano??? Unataka mzee Albano afariki? Mbona sikuelewi ???
“yah huwezi kunielewa Jason.Lakini nakwambia kwamba from this moment achana kabisa kujishughulisha na kitu chochote kinachohusiana na mzee Albano.Jason darling nakupenda mno na sitaki uingie katika matatizo ndio maana nafanya kila ninaloweza kukulinda usije dhurika.” Akasema Stella kwa sauti ya upole huku akimkaribia zaidi Dr Jason
“Stella I cant back off now.Siwezi kukataa kufanya operesheni hii hata kama angeniambia nani.Hii ni taaluma yangu ambayo niliapa kufuata misingi yote ya taaluma hii.Mr Albano will die nisipomfanyia operesheni hii,kitu ambacho katu hakiwezi kutokea.Niko tayari nife mimi lakini mzee albano apone”
Stella akatulia akapumua kwa nguvu halafu akasema
“Its because of her,right? Ni kwa sababu ya Serena ndio maana uko tayari hata kuhatarisha uhai wako kwa ajili ya baba yake.Amekupa nini Serena Jason mpaka umfanyie hivi.????
Dr Jason hakujibu kitu akaendelea kumwangalia Stella kwa jicho la ukali
“Tell me Jason Serena amekupa kitu gani????????????.Akauliza Stella kwa sauti ya juu ya ukali
“I promised to save her father” Akajibu Dr Jason naye kwa ukali.
“I’ll do everything I can to keep my promise.I gave her my word”
Dr Jason akachukua koti lake pale sofani akatoka mle chumbani kwa hasira akaubamiza mlango.
“Jason!!!!!!” Akaita Stella lakini Dr Jason hakugeuka.Akaenda lilipo gari lake akaingia na kuondoka kwa kasi.
Huku machozi yakimtoka Stella akajitupa kitandani .
“Jason ,Jason why you are hurting me like this.Kitu gani nimemfanyia Jason kiasi cha kunitesa namna hii?I love Jason and I’m not gonna loose him.This girl Serena……..atanitanmbua mimi ni nani.Kwa sasa naingia mwenyewe vitani.Kwanza kumlinda Jason asidhuriwe na mtu yeyote yule hata awe baba yangu na pili nataka nimtafute huyo Serena nimuonyeshe kuwa mimi si mtu wa kuchezea.I swear ,Serena I’ll teach you a lesson.Get prepared.You must pay for this.
Saa kumi na moja jioni waliwasili katika jiji la Mbeya ambalo kwa jioni hii lilipendezeshwa na kijua kitamu cha jioni na kiubaridi kwa mbali. Alishuka garini akachukua taksi ambalo lilimpeleka moja kwa moja hadi maeneo ya Block T katika nyumba moja kubwa yenye geti jeusi ambako kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa hapo ndipo nyumbani kwa akina Ray.
Akalisogelea geti na kubonyeza kengele ya getini, na baada ya dakika kama tatu hivi mlango mdogo ukafunguliwa na dada mmoja akajitokeza.
“Habari yako dada” Jason akamsabahi yule dada.
“Nzuri karibu”
“Ahsante.Naomba kuuliza eti hapa ndio kwa akina Ray?
“Ndio hapa unamtafuta nani?
“Mimi ni mgeni wao nimetoka Iringa.Naitwa Jason ninasoma shule moja na Ray.”
Yule msichana amabaye bila hata kuuliza aalionekana kuwa ni bintio wa kazi akamwambia Jason asubiri hapo hapo getini.
Baada ya dakika mbili akarejea akiwa ameongozana na mama mmoja mnene mweupe.
“karibu sana baba” Alisema mama yule ambaye bila hata kutambulishwa Jason alijua alikuwa ni mama yake Ray kwa jinsi walivyofanana.
“mama shikamoo” akasalimia Jason
“Marahaba baba .Pole na safari”
“Ahsante sana mama””
“We Mbutolwe hebu chukua mizigo ya kaa yako ipeleke chumbani”Yule msichana wa kazi mara moja akachukua mabegi ya Jason na kuyapeleka ndani.
“ Vipi hukupata taizo lolote njiani? Ray kanipigia simu mida ya kama saa sita hivi akasema uko njianI , mpaka saa hizi nikawa na wasi wasi labda mmepata matatizo njiani.
“Hapana mama sikupata taizo lolote njiani safari ilikuwa nzuri tu.Gari ndio lilikuwa likienda taratibu sana.
baada ya maongezi mawili matatu akapelekwa katika chumba cha Jordan kwa ajili ya mapumziko.Kilikuwa ni chumba kikubwa chenye kila kitu ndani.Akaingia bafuni kujumwagia maji kIsha akajitupa kitandani usingizi ukampitia.
*************************************************************
Mtu aliyekuwa akigonga mlango ndiye aliyemstua Jason toka usingizini.Mwanzoni alihisi ni kama anaota vile lakini baada ya kufumbua macho yake na kutega sikio kwa makini akagundua ni kweli kuna mtu alikuwa anagonga mlango.Akainuka na kwenda kufungua mlango.
“Samahani kaka,mama anakuita sebuleni” Alikwa ni Mbutolwe yule msichana wa kazi
“Ok dada nakuja”
Alipotazama saa ilipata saa moja na nusu hivi.Alikuwa amelala sana kwani jana yake hawakuweza kulala hata kidogo kutokana na furaha ya kufunga shule.Muda huo hali ya hewa ilikuwa ya kiubaridi baridi kama ilivyokawaida ya jiji la Mbeya.
“Karibu baba” Alisema mama Ray baada ya Jason kuingia sebuleni.
“Ahsante sana mama nimeshakaribia.”
“Nimeona umelala sana nikaona bora uamshwe ili utupe habari za shule.Vipi Ray anaendeleaje huko? Akauliza mama yake Ray
“Ray anaendelea vizuri tu mama,kwa sasa amekwisha zoea mazingira ya shule na hata maendeleo yake pia ni mazuri” Akajibu Jason
“Lakini vipi masomo?walimu wapo wa kutosha, na wanafundisha kweli?
“Ndiyo mama ,walimu wapo wa kutosha na kufundisha wanajitahidi sana.Ni shule nzuri kusema ukweli”
“Nafurahi kusikia hivyo.”
Wakati wakiongea mara akaingia msichana mmoja mweupe mzuri,mrefu na mwenye umbo lakuvutia.Jason akatupa jicho pembeni kumuangalia dada yule.Mara moja akagundua kuwa alikuwa ni Nange dada yake Ray kwani alikwisha muona katika picha za Ray.
“Nange huyu ni kaka yako anaitwa Jason.Amefika jioni hii kutoka shule.Anasoma shule moja na Ray.Jason huyu ndiye dada yake Ray anaitwa Nange.”
“Ouh kaka Jason karibu sana.Ray alinipigia simu kuwa utapita hapa kwetu .Karibu sana” Nange alikuwa ni binti mchangamfu .Alipotabasamu ndio uzuri wake ukaongezeka.
“Ouh Mungu wangu niepushe na majaribu haya” Jason akajisemea kimoyo moyo.
“Ahsante sana nange nimekwisha karibia.”
Maongezi ya hapa na pale yakaendelea kisha wakapata chakula cha usiku wote halafu mama yake Ray akawaacha sebuleni wakiendelea kutazama filamu yeye akaenda zake kulala.
“Enhee kaka Jason ,Ray alisema amekupa maagizo yangu” Alianzisha mazungumzo Nange baada ya mama yake kuondoka na kumuacha na Jason sebuleni pamoja na msichana wa kazi.
“yah! alinipa maagizo yako ,ngoja nikuletee”
Jason akainuka akelekea chumbani na kurudi na kifurushi kidogo pamoja na barua.Nange akaifungua barua akaisoma kisha akatabasamu na kutoa kicheko kidogo cha chini chini.
“ Ray bwana,amesema nifanye kila ninaloweza nikukutanishe na Serena umuone,hahahaha…” Akacheka kicheko kikubwa huku Jason akitabasamu
“Amekwambia nini kuhusu Serena? Mbona ameweka msisitizo mkubwa namna hii…” nange akauliza.
Huku akitabasamu Jason akajibu.
“Uhhmm ni maongezi ya kawaida tu ila alipenda nimuone Serena ,walau nimsalimie.”
Nange akacheka tena kicheko kikubwa.
“Ok haina shida nitamleta akusalimie.halafu bora umekuja .kesho kuna rafiki yetu ana birthday party yake na ametuomba tusikose mimi na Serena.Nilikuwa na wasi wasi sana kuhusu kuruhusiwa kwenda huko kwa sababu mimi huwa siruhusiwi kuwa nje ya nyumba baada ya saa kumi na mbili jioni labda nikiwa na Ray.Sasa kwa vile wewe utakuwepo itabidi twende wote ili iwe rahisi mimi kuruhusiwa .Halafu huko ndo itakuwa rahisi kuonana na Serena manake naye atakuwepo.Sherehe yenyewe itaisha saa mbili usiku.”
Hakuna mtu aliyeweza kuona furaha ya Jason kwa kauli ile ya Nange.kwa sasa kitu pekee alichokuwa akikihitaji ni kumuona Serena.homa ya jiji la Mbeya.
“Hakuna shida nange, weka mambo safi ili kesho tuhudhurie hiyo sherehe.”
**********************************************************************8
Saa kumi na mbili na dakika tano tayari Nange na Jason walikwisha wasili nyumbani kwa akina Sasha ,binti mrembo ambaye leo hii alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.Tayari baadhi ya waalikwa walikuwa wamekwisha fika na wengi wao wakiwa ni wanafunzi anaosoma nao shule moja.Dereva alipaki gari kisha Jason na nange wakashuka.
“waooh karibuni sana nange” Binti mmoja alikuja kuwapokea kwa furaha huku akikumbatiana na Nange.
“ahsante sana Nancy”
“Jason huyu ni nancy mdogo wake na Sasha..Nancy huyu ni kaka yangu anaitwa Jason.” Nange akawatambulisha
“waoo Jason karibu sana “ Akasema Nancy kwa furaha.Binti huyu alijaaliwa sauti nzuri laini yenye kuvutia.
“Mi nilipowaona nikadhani labda leo umekuja na shemeji kwa sababu sijawhi kumuona pale kwenu mara zote ninazokuja na Sasha.Mi namfahamu Ray peke yake”
Wote wakaangua kicheko huku wakielekea ndani ambako ndiko sherehe ilikuwa inafanyikia.Baada ya kusalimiana na watu kadhaa Nange akamuacha Jason katika meza iliyokuwa pembeni kabisa yeye akapanda juu ghorofani ambako ndiko alikokuwa Sasha binti anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa.Ukumbini kulikuwa na watu wa kutosha na sura nyingi zilionyesha kuwa ni za wanafunzi.Kwa mujibu wa maelezo ya Nange wazazi wa Sasha hawakuwepo,walikuwa safari nje ya nchi .
Sherehe ilianza rasmi saa moja kasoro robo.Ilikuwa ni sherehe ndogo lakini liyoandaliwa vizuri sana.Watu walikula na kunywa vilivyo.Ilipofika saa mbili kama na robo hivi Jason akaamua kutoka nje ili apate upepo kidogo manake ndani kilichokuwa kikiendelea ni kucheza mziki .hakuwa na mtu wa kucheza nayekwani Nange alijichanganya na kundi la wanafunzi wenzie kucheza.Kilichomshangaza zaidi ni kushindwa kumuona Serena pale ukumbini hali alihakikishiwa na Nange kuwa ni lazima angekuwepo pale.
“Anyway kama leo hayupo nitamuona hata siku nyingine” akajisemea kimoyo moyo Jason huku akiufungua mlango na kutoka nje,akakaa katika kibaraza huku akiifurahia mandhari nzuri ya hapo nje.
“Sijui ni kwa nini Serena ananijia akilini namna hii? Toka nimeziona picha zake siku ile kwa Ray basi amakuwa akinijia akilini mara kwa mara.Do I have any feelings for her au ni tamaa tu ya uzuri wake.No.. si tamaa.Mtoto yule tayari ameanza kuingia katika mishipa yangu ya damu taratibu.Inabidi niidhibiti hali hii mapema kwa sababu inaweza kuniletea shida siku za usoni nikapoteza dira na mwelekeo wa maisha yangu.Hawezi kunikubali mtu kama mimi ambaye familia yangu hailingani kiuwezo na yake…”
Akiwa bado katika mawazo yake hayo mlango ukafunguliwa akageuza shingo kuangalia,hakuamini kile alichokiona.
“oh My God is this true?….Akajisemea mwenyewe
Alikuwa ni Serena akizungumza na simu.Serena hakuweza hata kuangalia kama pale katika kibaraza kulikuwa na mtu amekaa,yeye akaendelea kuongea na simu.
“Ndio mama tunakaribia kufunga sherehe,muda wowote tunarudi”
“ndyo mama,,……..”
“Its ok mom…see you soon.Bye”
Akakakta simu.Alikuwa akiongea na mama yake.
Alipokata simu aliinama kidogo kisha akaiweka simu yake mfukoni akawa tayari kurejea ndani ndipo alipokutana macho na Jason ambaye kijasho kilikuwa kikimtoka.
“haaa!!!! Sikujua kama kuna mtu huku.Mbona uko nje peke yako” Serena akauliza kwa mshangao
Jason akapata kigugumizi kidogo kujibu.Akabaki amemkodolea macho binti yule mrembo ambaye kwa leo uzuri wake ulikuwa hauelezeki.
“nime….nimekuja kupata hewa kidogo manake ndani I feel bored kwa sababu zaidi ya Nange hakuna anayenijua .”
Serena akamkazia macho na kuuliza
“Nange!!! We ni ndugu yake Nange?
“ Hapana si ndugu ila nimekuja leo toka shule,naelekea Tunduma hivyo nimefikia pale kwao.Ninasoma shule moja na kaka yake Ray”
“Ouh ! karibu sana.Kumbe uko shule moja na Ray.Mi Nange ni rafiki yangu mkubwa sana pamoja na huyu Sasha anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.Tunasoma shule moja pia wote.Nange mbona hajatutambulisha? Kafanya vibaya sana…..”
“By the way Naitwa Serena”
“Mi naitwa Jason”
Jason akatabasamu .Tayari uoga ulikwisha anza kupungua.
“Sherehe imefana sana kwa hiyo sidhani kama hata anakumbuka kunitambulisha kwa rafiki zake.”
Serena akacheka kidogo
“Kweli sherehe imependeza sana.Imeandaliwa vizuri.hata mimi nimefurahi”
Jason akabaki ametabasamu asijue nini cha kuongea.Hali hii ilikuwa ni mara ya kwanza kumtokea.
“Kwa hiyo mmefunga shule? Akauliza Serena ambaye alionyesha kutaka kuendelea kuongea na Jason pale nje.
“Yah tumefunga shule.Ray yeye amekwenda Zanzibar na mie naelekea Tunduma kumsalimia kaka yangu afanyanye kazi pale.”
“Kwani we ni mweneyeji wa wapi?
“ Mie naishi Arusha”
“Ouh ok.Nimefika Arusha mara kadhaa.Napapenda sana,ni pazuri.Unaishi maeneo gani pale Arusha?”Serena akauliza.
“Pale ninaishi sehemu moja inaitwa Kisongo.”
“Ok fine.Nitapanga siku moja nije nitembee vizuri Arusha na rafiki zangu.I hope utakuwa mwenyeji wetu..”Akasema Serena huku akiachia tabasamu pana na kuufanya uso wake uzidi kung’ara na kupendeza.
“Msijali karibuni sana Arusha.Muda wowote nitakuwa mwenyeji wenu..
Mlango ukafunguliwa akatokea binti mmoja mwembaba mrefu kidogo aliyevaa gauni refu la usiku,akitembea kwa maringo kuelekea alipokuwa Serena.
“Tulikuwa tunakutafuta ndani kumbe uko huku nje” Akasema binti yule ambaye naye alikuwa mzuri kupindukia.Aliposimama na Serena alionyesha kumzidi urefu kidogo.
“Duh!! Haya sasa majaribu jamani,watoto wazuri namna hii!!!!!…”Akawaza Jason
“Jason huyu ni mdogo wangu anaitwa Isabela..Isabela huyu ni mgeni wetu yuko kwa akina Nange anasoma shule moja na Ray.”
“Ouh karibu sana brother.Karibu sana Mbeya.”
Akasema Isabela huku akimpa mkono Jason”
“Ahsante sana Isabela.”
“Vipi kitu gani kinachoendelea huko ndani? “Serena akamuuliza Isabela.
“Ni muziki tu ndio watu wanacheza.nadhani ni muda wa kujiandaa kuondoka sasa.”
“Jason ngoja tukaage ndani tunataka kuondoka.Kama bado upo tutaendelea kuonana.Nitakuja kwa akina Nange ,kesho au keshokutwa.Pale ni kama nyumbani.”
“Ok Serena safari njema nadhani tutazidi kuonana.Sina haraka sana ya kuwahi huko Tunduma.”
Serena na Isabela wakamuaga Jason ,wakaingia ndani ilikuaga wenzao tayari kwa kuondoka.
Dakika kama tano baadae wakatoka wakiwa na kundi la wasichana wengine kama watato hivi na mmoja wao ni Nange.Walikuwa ni kama wakibishana kitu Fulani huku wakielekea moja kwa moja alipokuwa amesimama Jason.
“Jason nimemleta nange atueleze kwa nini amekataa kututambulisha kama kuna mgeni amekuja ” Akasema Serena.
“jamani nimeshawaambia nilipitiwa tu ,lakini lengo likuwa kuwatambulisha .Haya jamani huyu anaitwa Jason anatokea Arusha ,anasoma na Ray na hivi sasa wamefunga shule kwa hiyo yupo nyumbanio kwa siku chache.Jason hawa ni rafiki zangu niliokuambia.Huyu ni Serena ambaye nadhani umekwisha mjua,huyu ni Sasha ambaye amezaliwa leo,na huyu ni mdogo wake Serena anaitwa Isabela,huyu ni mdogo wake Sasha anaitwa Nancy.haya madada kesi imeisha”
Wote wakacheka ,wakaagana kisha Serena na mdogo wake ,wakaingia katika gari lao dereva wao akaliondoa gari kuelekea nyumbani.
Hawakukaa sana ,Jason na Nange nao wakaondoka hapo shereheni.
“Mhh ..unajua leo kuna kitu strange sana kwa Serena.Sijawahi kumuona akiwa amefurahi namna hii.Cha ajabu sijawahi muona akiongea na mvulana yeyote kama alivyoongea na wewe leo hii…..”Akaanzisha mazungumzo nange wakiwa njiani kuelekea Nyumbani.Jason akatabasamu , akasema.
‘yawezekana leo aliamka vizuri,ndio maana amekuwa mtu wa furaha sana”
“Yawezekana,lakini nimekaa na Serena kwa muda mrefu sana ,I know her better than anyone.Lazima kuna kitu kimemfurahisha”..nange akazidi kukazia.
Jason hakujibu kitu,mawazoni mwake aliamini furaha aliyokuwa nayo Serena ilikuwa ni kutokana na sherehe ile iliyofana sana.Moyoni alikuwa ni mwingi wa furaha hasa baada ya kutimiza ndoto yake ya kuongea na Serena na hata kushikana mikono naye,kitu ambacho watu wengui wanakitafuta bila mafanikio.
“Ray was right,Serena is hot.si mtoto wa kawaida.” Alizidi kuwaza.
Ulikuwa ni usiku mrefu sana kwa Serena.Alikuwa amekaa kitandani pake akisikiliza muziki laini alioufungua kwa sauti ya chini.Ni kitu kimoja tu kilichokuwa kikizunguka akilini mwake kwa wakati huo.haijawahi kumtokea katika maisha yake kuwa katika hali kama hii aliyonayo.Kila mara sura moja ilikuwa ikija na kuondoka na kumwacha katika fikara nzito.Hii ni sura ya Jason.
“Why this is happening to me.Am I right with my feelings? No ..No!!! something isn’t ok with me” Akasema Serena kwa sauti ndogo akiwa sasa amekaa.
“Haijawahi kunitokea katika maisha yangu kuvutiwa na mvulana kama alivyonivutia Jason.Well he’s handsome and he got everything I need in my dream man.Is this what they call love at first sight? Labda ndio hii yaani unatokea kumuona mtu na kwa wakati huo huo unatokea kumpenda kupindukia.”
Bado mawazo mengi yalizidi kumsonga Serena .
“Ana kitu Fulani cha pekee tofauti na wavulana wengine.When he laughs…ouh he’s amazing..Akiongea ndio basi kabisa,utatamani asiache…ouh my…”
Akashika kichwa tena .
“No Serena don’t be stupid, its just feelings. Just normal feelings nothing more…U can fight this Serena,u can fight this.You are strong girl” Akajisemea mwenyewe huku amesimama akijipa moyo wa kulishinda jaribu hili gumu kwake.Alikuwa akisikia tu kwamba mtu ukitokea kumpenda mtu unakuwa kama chizi,alizoea kuyaona haya katika filamu lakini leo hii ilikuwa zamu yake.
“Help me God to fight this.Its so hard for me.I don’t know what I should do…”
Aliendelea kujigeuza pale kitandani bila usingizi hadi ilipofika mida ya saa nane ndipo usingizi ukampitia.
Saa nne asubuhi akagongewa mlango na mama yake ambaye alitaka kujua ni kwa nini leo hakwenda kanisani hali si kawaida yake.
“Samahani mama ,sijisikii vizuri leo,ndio maana nimechelewa kuamka .” Serena akajitetea.
“Ok jiandae basi tukamuone daktari haraka”
“No mama I’ll be fine.I just need some rest”
mama yake akanyamaza huku akimwangalia mwanae kwa makini.
“Serena hebu nambie una tatizo?….
“hapana mama sina tatizo lolote.Nadhani ni uchovu wa jana tu .I had a little dance with girls.”
“Ouh ok kama ni hivyo then have some rest.Ukiamka oga halafu upate chai”
“Ok mama I wont take long”
mama yake akafunga mlango na kumwacha Serena akiwa bado kitandani.Alimfahamu mwanae vizuri sana hivyo akahisi ni lazima kuna kitu kinamsumbua.Moja kwa moja akamfuata Isabela ambaye ndio kwanza alikuwa amerejea toka kanisani ambako aliwahi ibada ya kwanza.
“Isabela hebu niambie mwanangu.,dada yako anasumbuliwa na nini? Leo hajakwenda kanisani kitu ambacho si kawaida yake,nimetoka kumwangalia anasema anahisi uchovu,hajisikii vizuri..What happened at the party?”
Isabela akanyamaza kimya akajaribu kuvuta kumbu kumbu juu ya ile sherehe ya jana ya kuzaliwa Sasha.
“mama ilikuwa ni pati ya kawaida tu.hakuna kitu chochote kibaya kilichotokea.”
“ mlicheza mziki?
“yes tulicheza mziki”
“Serena alicheza?
“No mama Serena hakucheza.Muda wote alikuwa akitutazama tunavyocheza.”
“Kulikuwa na pombe?
“Yes kulikuwa na pombe lakini Serena hakugusa yeye alikunywa tu maji.Si unamjua Serena mama,Pombe hagusi kabisa.”
“sasa kama ni hivyo kitu gani kinachomsumbua huyu mtoto? Ok hebu jaribu kukaa naye anaweza akakueleza ni kitu gani ambacho kinamsumbua.
“Ok mama”
Isabela akanyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwa serena ,akamkuta bado yuko kitandani.
“Hi sister”Akasema Isabela
“Hi” Akajibu serena
“Vipi mbona mpaka saa hizi bado uko kitandani? Father Kalistus alikuwa anakuuliza baada ya kutokuona katika ibada.”
“Du leo nimechoka sana Isabela.Nimechelewa mno kulala jana.”
“ulikuwa unasoma?
“No wala sikuwa nasoma.Just had deep feelings,ndio maana sikupata usingizi haraka”
“Ulikuwa unawaza nini Sister?
“Mhh we Isabela ni story ndefu sana.It’s my first time to feel this way.It never happened to me.”
“What was that?
“ Ah just love feelings.I feel I’m in love with someone”
“In love……………..!!!!??
Isabela akauliza kwa mshangaoHakuwahi kusikia hata siku moja dada yake akiongelea masuala ya mapenzi.
“Yes ,why? Is it bad to have love feelings?
Isabela akamkimbilia dada yake pale kitandani na kumkumbatia kwa furaha.
“Ouh my sister is in love”
“shhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh……Usiseme kwa sauti mama akasikia.She was here few minutes ago.”
“wow my sister .Nafurahi kusikia hivyo.kwa hiyo ni nani huyo kijana mwenye bahati ambaye amefanikiwa kuziteka hisia zako kwa mara ya kwanza?”He must be a very handsome guy”
Serena akacheka kicheko kikubwa.Akatulia kidogo kisha akasema.
“Ni Jason.Yule aliyekuja na nange jana kwenye sherehe”
“Jason..!!!!!!!!? Isabela akastuka.
“Yes Jason.I think he’s the guy I’ve been dreaming for.Ameweza kunifanya nivunje mwiko wangu na hata masharti ya baba ya kutokupenda mvulana yeyote mpaka hapo nitakapomaliza elimu ya juu.I love him ”
Isabela akamwamngalia dada yake kwa macho makali kana kwamba haamini kile alichokisikia.Serena akaligundua hilo na kuuliza.
“ Kwani Isabela wewe ulivyomwona Jason ana kasoro gani?
“Hapana sister,hana kasoro zozote.If u have true feelings for him then I’m happy for you.I always wants to see my sister happy.”
Serena akamkumbatia mdogo wake kwa furaha.
“Please don’t tell mom.Nitatoka sasa hivi niende kwa akina Nange ili nimuone Jason.”
“Ok sister don’t waste time just go” akasema Nange.
Haraka haraka Serena akaoga ,akajiweka safi na kumpigia simu dereva wao aandae gari anataka kutoka.Akamfuata mama yake na kumuaga kuwa anataka kwenda kumuona Nange.mama yake akamruhusu lakini akiwa na mashaka Fulani.
Baada ya Serena kuondoka mama yake akamfuata Isabela na kuanza kumdadisi ili ajue kama Serena alimwambia jambo lolote..Baada ya kbanwa sana na maswali ya mama yake hatimaye Isabela akammwabia mama yake ukweli halisi kuhusu Serena.mama yake akajishika kichwa kwa mshangao kisha haraka haraka akampigia baba yake Serena simu na kumweleza kila kitu.Taarifa hii ilkuwa ya mstuko kwa baba yake pia..Uamuzi ukafanywa haraka haraka kuwa kabla hajafika huko kwa akina Nange kwa minajili ya kuonana na Jason aitwe nyumbani mara moja na akifika wafunge mizigo yao haraka yeye,Isabela na mama yao waondoke kuelekea dar es salaam ambako watapanda ndege kuelekea Nairobi ili kumuona baba yao ambaye amepatwa na matatizo.Yote hii ilitungwa ili kumfanya Serena awe mbali na Jason na asiweze kumuona tena.
Akiwa ndani ya gari yeye na dereva wao akielekea Block T kwa akina Nange Simu yake ikaita .Kuangalia alikuwa ni mama yake.Akabonyeza kitufe cha kupokelea simu na kuiweka sikioni.
“Haloo mama”
“Serena samahani mwanangu kama ulikuwa na safari zako lakini kuna taarifa tumeipata hapa si nzuri baba yako anaumwa sana yuko Nairobi kwa hiyo tunatakiwa wote tuondoke sasa hivi kuelekea dar es salaam ili kesho tupande ndege tuende kumuona baba yenu.Rudi nyumbani haraka sana ili tuweze kuondoka mara moja”
Kijasho kilianza kumtoka binti huyu mrembo.Alimpenda mno baba yake.Taarifa ya kuumwa kwa baba yake ambaye alikwenda Kenya kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara ilimstua mno.hakuwa na jinsi tena akamwambia dereva wao ageuze gari warudi nyumbani.Dereva akatii na kugeuza gari kisha Serena akaamua kumpigia simu Nange .
“Shosti nilikuwa njiani kuja kwenu lakini nimepigiwa simu sasa hivi kuwa ninatakiwa kurudi nyumbani sasa hivi kuna matatizo yametokea.baba mgonjwa sana amelazwa Nairobi kwa hiyo yatubidi tuanze safari mara moja kwa kuwa hakuna ndege ya haraka hapa Mbeya ya kutufikisha Dar es salaam inatubidi tuanze safari kwa gari mpaka dar halafu ndo tupande ndege.Msalimu sana Jason,kama tukiwahi kurudi nitakuja kumsalimu.Hivi ana simu?
“ mhh shosti mbona Jason asalimiwe peke yake,wakati hapa nyumbani kuna watu wengine? Au…hahahahah.Usijali Serena nitazifikisha bado yuko kanisani.Pole sana best yangu tuzidi kuwasiliana”
“Ok Nange nitakupigia tukifika Dar”
***********************************************************
Gari aina ya BMW nyeusi ilikata kona na kuingia katika geti la hoteli moja kubwa ya kifahari ya nyota tano mjini Nairobi.Savannah Paradise hotel ilikuwa ni moja kati ya hoteli mpya na tishio katika ukanda huu wa Afrika.Ilimilikiwa na tajiri mmoja wa kiasia aitwaye Rajesh patel.Rajesh ni mmoja kati ya watu wachache wenye kunuka utajiri nchini Kenya .Ni mmoja pia kati ya wawekezaji wakubwa nchini Kenya na Tanzania.
Gari lilielekezwa sahemu ya kupaki ambayo ni maalumu kwa watu maalum kama vile marais na watu wengine wenye uwezo mkubwa kifedha.Hili ndilo gari lililokuja kuwachukua Serena ,Isabela na mama yao pale uwanja wa ndege.Serena ndiye aliyekuwa wa kwanza kushuka kisha mamayake na Isabela.Pamoja na kuwa na mawazo mengi juu ya afya ya baba yao lakini Serena alishindwa kujizuia kuufurahia uzuri uliokuwapo hapo hotelini.
“what a paradise…mama daddy akipona inabidi tukae naye hapa kama wiki nzima.”
“yah nafikiri hilo litakuwa jambo jema sana”akasema mama yake.
Akasema huku akitabasamu.Mama yake pia akatabasamu.
Muhudumu alikuwepo tayari akawapokea na kuwaongoza hadi katika mahala walipokuwa wameandaliwa.Wakakaaa pale huku wakiendela kuustaajabia usuri wa hoteli hii.Kulikuwa na kila aina ya urembo.
Wakati wamekaa pale wakiburuka kwa mandhari safi na vinywaji mara mlango unafunguliwa na mzee Albano mwakatala akiwa mwenye tabasamu pana anaingia.
Kila mmoja mle ndani anashikwa na mshangao kwa maana walitegemea kutoka hapo waelekee hospitalini kumuona.
Huku akilia machozi ya furaha Serena akakimbia na kumkumbatia baba yake kwa nguvu.
“Ouh my best daddy”
Kwa muda wa dakika kama mbili hivi Serena na isabela bado wamemkumbatia baba yao huku mamayao akicheka na kufurahi.
“Daddy how do you feel now? Akauliza Isabela’
“Tulistuka sana tulipopata taarifa ya kuumwa kwako”
Huku akitabasamu akawavuta binti zake wawili kwake akawaangalia kisha akasema.
“Mimi sio mgonjwa wanangu”
“what……..? serena akauliza kwa mshangao.
“I’m sory kwa kuwapa wakati mgumu wanangu ni kwamba nilikuwa najisikia upweke mno kuwa huku Nairobi peke yangu hivyi nikaona njia pekee na ya haraka ni kutumia ugonjwa ili muweze kufika hapa haraka.I love you my daughters.I love you all very very much.Ndio maana nakuwana wakati mgumu sana pale ninapokuwa mbali nanyi.Naomba mnisamehe kwa hili la kuwastua.
Isabela na Serena wakamkumbatia tena baba yao kwa nguvu..
“ Please daddy don’t do this again.You know we love you so much.’ Akaseam Serena huku machozi yakimtoka.
Ni moja kati ya bustani nzuri kuwahi kuwepo katika ukanda huu wa afrika.Ndege wa kila aina wakubwa ka wadogo walikuwa wakizunguka,wakiruka na kutoa sauti zenye kuvutia mno.Maji yalibubujika toka katika chemchem zilizoko katika bustani hii.wanyama wale wasiodhuru binadamu walikuwa wakizunguka zunguka na kupafanya mahala hapa pawe kama ni moja kati ya sehemu za kipekee kabisa .
Ni mida ya saa kumi na mbili za jioni Mzee Albano mwakatala na familia yake walikuwa wamekaa ndani ya bustani hii mwanana wakipata vinywaji na kufurahi.Pembeni yao ndege wakubwa wenye mikia mirefu na rangi za kuvutia walikuwa wakizunguka na kumfanya Serena atabasamu kila sekunde.
“wanangu wapendwa nimeamua kuwaiteni hapa leo kwa sababu kuna jambo la muhimu sana ambalo nataka niwafahamishe.Kuna kipindi miaka kama kumi hivi iliyopita niliwahi kuingia katika mgogoro wa kiuchumi.kampuni zetu zilikuwa haizalishi vya kutosha na hivyo kuchelewa kulipa mkopo wa benki wa shilingi bilioni kumi na tatutatu.Kwa kuniepusha kufilisiwa na benki,rafiki yangu mkubwa Bw Rajesh Patel alikubali kunidhamini na kunilipia deni hilo kubwa la mamilioni ya fedha kwa makubaliano kuwa nimlipe kwa miaka mitano.Nimejitahidi kulipa deni hilo kwa kipindi tulichokubaliana lakini mpaka mwisho nilifanikiwa kulipa kiasi cha shilingi bilioni saba tu..Siku za karibuni kumekuwa na kuporomoka kwa bei za mazao katika soko la dunia hivyo uuzaji wetu ndani na je ya nchi umeshuka sana kitu kinachopelekea kuendesha biashara kwa hasara.Mr Rajesh aliniongeza tena bilioni kumi ili kukuza mtaji na kwa kweli sasa hivi mambo si mabaya.Biashara imeanza kwenda vizuri tena na kidogo tumeanza kutengeneza faida”.
Alitulia kidogo akawatazama wanae wliokuwa makini wakimsikiliza kisha akaendelea.
“ Mr Rajesh aliniongezea kiasi hiki kikubwa na kuirudisha kampuni yetu katika mstari kwa makubaliano ambayo leo nataka niyaweke wazi.Mr rajesh kuna kitu alikihitaji kama fidia kwa fedha alizotupa na kutuepusha na aibu ya kufulisiwa na benki.Kitu hiki akitakacho kimekuwa kikiniliza kila siku na kunifanya nijione mjinga na mkatili.Naomba leo niweke wazi kila kitu kwa sababu muda unazidi kwenda na kila siku mambo yanabadilika na Mr Rajesh anasubiri jibu langu kama niko tayari kutekeleza matakwa yangu au kama la nizirejeshe pesa zake kitu ambacho ni kigumu kwa sasa na kama nikishindwa basi hakutakuwa na jinsi zaidi ya kuipiga mnada kampuni yetu kwa kushindwa kulipa deni hilo.”
Wote walikuwa kimya wakimkodolea macho baba yao ambaye ni wazi ile furaha yote aliyokuwa nayo dakika chache zilizopita ilikuwa imetoweka.Huku kijasho chembamba kikimtoka na machozi kumlenga lenga akasema
“Mr Rajesh anataka…………..anamtaka Serena………….anataka mwanae anayeishi Marekani amuoe Serena.”
Kimya kikuu kikatanda hapo mezani.Kila mmoja alikuwa amestushwa mno na taarifa ile.Serena alikuwa ameinamia meza akilia kwa kwikwi..
Ilichukua zaidi ya dakika tano kwa mzee Albano kupata tena nguvu ya kuendelea kuongea.Familia nzima ilikuwa imesawajika mno
“Mr Rajesh ana mtoto wake mmoja wa kiume aitwaye Kenneth Mclay Patel aishiye nchini Marekani ambaye amezaa na mwanamke mmoja toka Puerto rico.Kenneth amechanganya damu hivyo haonekani kama muhindi.Aliwahi kuja nyumbani na baba yake ndipo hapo alipofanikiwa kumuona Serena na kumpenda kisha akamweleza baba yake kuwa katika zawadi kubwa ambayo angempatia basi ni kumsaidia kumpata Serena.Mr Rajesh amekuwa akinikumbusha na kunisisitiza kila siku ila nimekuwa muoga wa kumpa jibu lolote lile kwa sababu naelewa mwanangu wewe kwa sasa ni binti mkubwa na kwa hali halisi ilivyo najua unahitaji kwa na rafiki wa kiume.Nafahamu kuwa unahitaji kuwa na rafiki wa kiume ambaye unampenda toka moyoni.Jana mchana tulipata taarifa kuwa kuna mvulana unayempenda lakini bado hajui kuwa unampenda.Tulipanga plani hii ili uje huku Nairobi niweze kukueleza kila kitu bila kukuficha kabla haujaingia katika mahusiano na huyo kijana.Naumia sana mwanangu kwa sababu nataka uwe na furaha katika maisha yajko,nataka uishi na mtu umpendaye.Hivyo mwanangu hapa nilipo baba yako niko kwenye mtihani mkubwa nini cha kufanya.wewe ndiye mwenye uamuzi wote kwa sasa kwani iwapo hautakuwa tayari basi mali zetu zote zitataifishwa na tutarudi katika maisha ya chini kitu amabcho sijawahi kukiota kama kinaweza kutokea maishani mwangu.”..
Mzee albano akashindwa kuizuia na mahozi yakaanza kumtoka.Ilikuwa ni hali ya simanzi kubwa.Mke wake akatoa kitambaa na kumfuta machozi.
Ukimya mkuu ukatawala meza hiyo kwa dakika kama kumi na tano hivi bila mtu yeyote kuongea.Serena akainua kichwa na huku macho yake yamejaa machozi akakohoa kidogo na kusema.
“Baba nimekusikia na kukuelewa.You are the best daddy I’ve ever seen in this world.wewe ni mzazi wa kipekee kabisa.Ni kweli najua unataka mimi na mdogo wangu tuishi kwa furaha nan amani katika maisha yetu .Umefanya mambo mengi mno kwetu sisi.Hata hili deni unalodaiwa ni kwa ajili yetu.Please daddy usijione kama una makosa.Yes nina haki ya kuwa na mtu ninayempenda kwa maisaha yangu.Lakini kwa hili baba yangu siwezi kukupinga.I love you my daddy more than you can imagine.Ninakubali kuolea na Keneth nitakapomaliza masomo yangu ya juu.Nataka nikuonyeshe baba jinsi gani ninavyokuthamini.Sitaki uaibike au upate shida yoyote.I’ll sacrifice my happiness for you my daddy.Simjui Kenneth,simpendi but I’ll be with him kwa ajili yako daddy……..”
Serena akashindwa kuendelea kuongea ,uso ulikuwa umejaa machozi.Mzee Albano akainuka na kwenda kumkumbatia huku wote wakilia.
*****************************************************************
Serena hakutaka tena kuendelea kukaa pale mezani akainuka bila kuaga mtu na kuondoka kuelekea chumbani kwake.Hakuna aliyemsemesha.Isabella naye akainuka kumfuata kwani hali aliyokuwa nayo Serena ilimpa wasiwasi.
Alipojaribu kuufungua mlango wa Serena ulikuwa umefungwa kwa ndani.Akagonga.
“ Serena ni mimi Isabella.Nifungulie mlango”
“Go away Isabela.I don’t wanna see you.U betrayed me.” Akasema Serena toka ndani chumbani kwa sauti ambayo ilionyesha dhahiri alikuwa akilia.
Isabella naye machozi yakaanza kumtoka.Ni wazi alivunja makubalianao aliyokubaliana na dada yake ya kutokumwambia mama yao juu ya Serena kumpenda Jason.
“Sister I’m sorry.Nisamehe dada yangu sikujua kama yatatokea haya.Please open the door Serena we need to talk”
Serena hakujibu akaendelea kulia.Isabella akaendelea kugonga mlango kwa nguvu.Hatimaye serena akaamua kuuufungua mlango.Hakutaka kumtazama mdogo wake usoni akakaa kitandani huku akilia.
“Serena I’m sorry .Please usilie” Akaseam Isabella huku akimfuta machozi.
“What a cruel father….”Akasema Serena kwa hasira
“All these days he pretended to love us…….”Akashindwa kuendelea akazidi kulia.
“Ndio maana amekuwa kila siku ananisisitiza kutojihusisha na masuala ya mahusianao kumbe alijua anachokitafuta…”
“ Calm down serena.”
“I wont calm down wakati my own father ananitumia mimi mwanae kwa manufaa yake”
“Serena ulikubali kiurahisi sana matakwa ya baba” Isabella akasema
“Ulitakiwa kusimama Imara Serena.Hukutakiwa kuonyesha udhaifu.This is your own life my sister,no one should……….”
“save your breath Isabella.wewe ndo chanzo cha haya yote.Lakini anyway imesaidia kujua nini kilichokuwa nyuma ya pazia.Nilikubali kiurahisi kwa sababu sikutaka Jason apate shida yoyote.Iwapo ningekataa ombi la baba basi Jason angekuwa katika matatizo makubwa na pengine hata kuuawa.I know our father very well.Kwa hatua aliyofikia ilikuwa ngumu kukataa.Nina imani dunia nzima itanishangaa kwa uamuzi wangu lakini I have to protect Jason even if it costs my life.” Akatulia nakufuta machozi kisha akainua kichwa na kusema
“ I’ll do what he wants lakini Jason will be the one I love and someday he’ll be mine.I wont stop loving Jason not for one second.For now let me do what he wants.I hate him so much”
“ Sister kwa nini usimwambie tu kuwa umebadili uamuzi?” Isabela akasema
“No Isabella siwezi kwa sasa.Nimekwambia I don’t want Jason to get hurt.Nikikataa matakwa yake ni lazima Jason apate matatizo.Jason hana kosa and above all he doesn’t know that I love him sasa kwa nini apate matatizo?Let this be…He exchanged me for money…money.!!!!!!!!.Serena akasema kwa hasira huku akilia.
MWAKA MMOJA NA NUSU BAADAE
Ni asubuhi ya kuamkia siku ya mahafali ya kidato cha sita.Siku iliyokuwa na kila ain