“Patrick amka basi darling inakaribia saa nne sasa”Alisema Veronika kwa sauti laini ya
kubembeleza.
‘Mmmmhhh”Aliguna Patrick ,akajigeuza upande wa pili na kulivuta zaidi shuka.
“Amka basi bwana uende ukaoge”Alizidi kubembeleza Veronika
Kwa uchovu mwingi Patrick akaamka na kunyoosha mikono yake juu huku akijipinda
“Loh !I’m veeery tired”Akasema kwa uchovu.
“lakini ukishaoga uchovu wote utaisha my darling “Akadakia Vero.
Kwa uvivu Patrick akajiinua kitandani na kuelekea bafuni .Dakika chache baadae alitoka akiwa
amechangamka.MISS TANZANIA
‘Kweli maji ni dawa nzuri ya uchovu.Sasa najisikia saafi kabisa.Nadhani itabidi kwa sasa nipunguze
muda wa kufanya kazi .Nimekuwa nikifanya kazi kwa masaa mengi sana kwa siku kiasi kwamba nakosa
hata muda wa kupumzika.naogopa tukija kuonana nisije kuwa nashindwa kutimiza majukumu yangu kama
mume kwa sababu ya uchovu”
Vero akatabasamu halafu akatoa kicheko cha chini chini na kusema
“Kweli mpenzi jitahidi kwa sasa kujaribu kupata muda wa kutosha wa kupumzika.”
“Nitajitahidi baby”
Baada ya kuhakikisha sasa yuko safi Vero akamshika mkono Patrick na kumpeleka sebuleni kupata
stafstahi.
“Patrick dear nataka unisindikize Supermarket nikafanye manunuzi ya vitu vya ndani .Si unajua
kesho Andrew na vicktoria wameahidi kututembelea”Alisema Veronika wakati wakiendelea kupata chai.
“Mhh Vero we nenda tu mwenyewe mi niache nipumzike bwana”Patrick akajibu
“jamani dear usifanye hivyo naomba bwana unisindikize ,mi naona uvivu kwenda peke yangu”
‘haya mama ,tumalize twende ili tuwahi kurudi”
“Nashukuru dear”
Katika vitu ambavyo Veronika alibarikiwa kuwa navyo ni uwezo wake mkubwa wa kushawishi.
******************************************************************
Veronika Rugi alikuwa ni binti mrembo mwenye mvuto wa aina yake.Binti huyu licha ya kujaaliwa
kichwa kizuri chenye nywele laini ,nyingi na ndefu ,alikuwa na uso mpana wa mviringo ulionakshiwa
na macho mapana yenye kurembua muda wote.Midomo mizuri ,laini ambayo akikupiga busu hutatamani
abanduke.Mtoto huyu alijaaliwa shingo murua ambayo iliungana na kiwiliwili kilichokuwa na kifua
chenye kupendeza kilichobeba chucu changa zenye kusisimua,zenye kuwatoa udenda wakware.Kimwana
huyu mwenye uzuri usiopimika alijaaliwa umbo la utatanishi kuanzia kiunoni kushuka chini.Ni
mabinti wachache sana waliopewa upendeleo wa namna hii na manani..
Pamoja na sifa hizo zote za nje lakini bado alikuwa na sifa lukuki za ndani.Kikubwa zaidi
kinachomfanya apendwe na kila mtu ni uwezo wake mkubwa wa uelewa .Ni binti mwenye roho nzuri ya
huruma na upendo asiyependa kujivuna wala kujikweza licha ya uwezo mkubwa familia yake ilionao.Ni
binti mwenye heshima kwa watu wa rika zote ,mcheshi,asiyependa ubinafsi na zaidi ya yote ni mtu
anayejua kupenda.
Veronika ambaye bado anaishi na mama yake mzazi baada ya baba yake kufariki miaka kadhaa iliyopita
,alikuwa ni mtoto wa tatu na wa mwisho katika familia ambayo haikubahatika kuwa na mtoto wa
kiume.Dada mkubwa wa Veronika aliyeitwa Loniki hivi sasa anafanya kazi katika shirika la ndege la
British airways ,ameolewa na anaishi nchini Uingereza.Mtoto wa pili kuzaliwa katika familia hii ni
ni binti mrembo sana Sarah ambaye aliwahi kushika nafasi ya tatu katika kinyan’anyiro cha kumsaka
mrembo wa taifa.naye amekwishaolewa na ni afisa mahusiano wa benki moja mpya kabisa nchini iitwayo
African meckat bank.Mtoto wa tatu na wa mwisho ni Veronika ambaye bado hajaolewa ,ila alikuwa
katika hatua za mwisho za kukamilisha maandalizi ya ndoa yake na mchumba wake Patrick.Ni hivi
karibuni tu amehitimu shahada yake ya kwanza ya biashara katika chuo kikuu cha dar es salaam.Yeye
ndiye msimamizi mkuu wa miradi yao yote ya familia kwa sasa.
******************************************************************
“basi nikwambie mpenzi nilisahau kukwambia toka mapema kuwa dada Loniki alifurahi sana kusikia
kuwa tunataka tukafanye shopping ya harusi yetu nchini Uingrereza,nakwambia alifurahi huyo na
akaahidi kuwa yeye na mumewe watagharamia safari nzima ya kwenda na kurudi na gharama zote za
manunuzi.Amesisitiza kuwa tusitumie hata shilingi yetu.Kwa maana hiyo wiki hii nataka niende tena
kufuatilia yale maombi yetu ya viza pale ubalozini.Nadhani kama Mungu akijaalia basi ndani ya wiki
mbili zijazo tutakuwa tumeshakamilisha taratibu zote zinazotakiwa.”
Alisema Vero huku akijiegemeza karibu zaidi na kifua cha Patrick.Muda huo ilipata saa mbili za
usiku na bado walikuwa wakipunga hewa safi baada ya mlo wa jioni.
“Wow! Hongera sana Vero kwa kuwa na ndugu wakarimu na wenye upendo wa hali ya juu sana kama ulivyo
wewe.Tena umeongea kuhusu Loniki nimekumbuka na zile CD alizonitumia wiki iliyopita.Unajua
sijatazama hata moja.Hebu twende ndani nikaitazame ile CD mpya ya Jack bauer.”
Alsema Patrick huku akijiinua toka pale walipokuwa wameketi na kuelekea sebuleni .Vero naye
akakusanya vitu vyote vilivyokuwapo hapo chini naye akaingia ndani.
“Vero mbona ile CD ya Jack bauer siioni hapa?au Andrew aliichukua?Aliuliza Patrick baada ya
kuitafuta CD ile bila kuiona.
“Yawezekana Andrew atakuwa aliichukua kwa sababu siku ile aliing’ang;ania sana.Nakumbuka kuna CD
alizichukua hapo nadhani na hiyo nayo ilikuwapo.”Akasema Vero
Patrick akalifunga kabati ,akaelekea katika friji akafungua na kujimimia Juice katika glasi .Vero
alikuwa ameketi sofani akitazama Luninga.
“basi nakwambia Patrick ,Miss Tanzania ya mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa sana kwa sababu
mabinti ni warembo kupita maelezo.Mhh………..”
Alisema Vero huku amekodoa macho yake katikaLuninga kubwa iliyokuwamo humo sebuleni.
“kwani fainali za miss Tanzania ni lini?”Patrick akauliza
“Ni jumamosi ijayo na itafanyikia pale Diamond Jubilee.Kutapambwa na onyesho kali la machozi
band,vile vile wana Fm academia na wasanii wengine kibao.Nataka kesho nikakate tiketi zetu za V.I
P ili tusikose nafasi siku hiyo”Alisema Vero
Akiwa na juice yake mkononi Patrick akajisogeza taratibu kuelekea mahali alipokaa Veronika .kabl;a
hajafika sofani alisimama akapiga funda la juice kisha akaelekeza macho yake katika luninga
“Naitwa Neema jastin ni mrembo toka kanda ya kaskazini.Ni miss Arusha.napendelea sana muziki wa
dini,kusoma na michezo mbali mbali.Nategemea kuja kuwa mwanamitindo wa kimataifa.Iwapo
nitachaguliwa kuwa miss Tanzania nitajikita zaidi katika kuwasaidia watoto yatima kwani naelewa
mateso na machungu wanayaoyapata kwa kutokuwa na wazazi wao.Naombeni kura zenu namba yangu ya
ushiriki ni ishirini.”Alikuwa ni mrembo wa Arusha akijinadi katika kipindi maalum cha
kuwatambulisha washiriki wa kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania kilichorushwa moja kwa
moja na televisheni ya Taifa.
“Du! Si mchezo”Aliguna Patrick huku akisogelea zaidi Luninga
“nimekwambia Patrick warembo wa mwaka huu si mchezo .Hebu kaa uangalie jinsi watoto
walivyobomba”Alisema Vero
“Naitwa Happy kibaho.Ni mrembo wa wilaya ya Ilala .Napendelea sana muziki laini,kusoma hadithi
,magazeti,kutazama luninga,na wanyama.nategemea kuwa mwanasheria.Iwapo nitachaguliwa kuwa miss
Tanzania nitaelekeza nguvu zangu zote katika kuwasadia vijana wajasiria mali ikiwa ni pamoja na
kuwatafutia wafadhili,nitaitumia kofia yangu kuiomba serikali ielekeze nguvu zake zaidi katika
kuwasaidia vijana hawa katika kuwapatia mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao wanazozizalisha
ili kupambana na ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira.Ninaomba kura zenu ili niweze kulitwaa taji
hili la miss Tanzania kwani nina vigezo vyote vya kulitwaa taji hili .Namba yangu ya ushiriki ni
6.”
“Whaaaat!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!........................”Patrick Alipiga ukelele
mkubwa
“Nooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!..I cant ……………………”alishindwa kuendelea glasi aliyoishika ikamponyoka
na kuvunjika .Taratibu nguvu zikaanza kumwishia akadondokea sofani kisha akapoteza fahamu.
“Patrick ,Patrick what’s wrong!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.........”
Alihamaki Veronika huku akimsogelea Patrick pale sofani na kumtingisha.
“Patrick darling what’s wrong with you?
Alizidi kuuliza Vero huku akimtingisha.
“Oooooh!Nooooooooooo!!!!!!!!Wake up Patriick”Alipiga ukelele baada ya kugundua kuwa Patrick hakuwa
na fahamu.Vero akataharuki asijue afanye nini.hakukuwa na mtu yoyote wa karibu ambaye angeweza
kumsaidia .Alitoka kutaka kwenda kuwaita majirani ,akafika mlangoni na kurudi tena ndani mpaka
sofani alipolala Patrick.
“Patrick ,Patrick dear what’s wrong with you.Whats’s wrong Patrick!!!!!!!!!!!!!!”Vero aliongea
peke yake huku machozi yakimtiririka.Pale pale akapata wazo la kumpeleka Patrick hospitali.Kwa
nguvu zake zote akamuinua Patrick na kumpakia garini ,akakimbia kufungua geti kisha akaingia
garini na kuondoka kwa kasi ya ajabu pasina kufunga mlango wowote wa nyumba.
Kwa kasi ya ajabu Vero aliendesha gari hadi hospitali ya karibu maarufu kama Dr Heneriko
hospital.Si mbali sana na makazi ya Patrick.Huku akilia akapaki gari na kuingia ndani ,akawaomba
msaada wauguzi .Haraka haraka wauguzi wakamchukua Patrick na kumuwahisha katika chumba maalum kwa
ajili ya kumpatia huduma ya haraka.
“Hurry up.hurry up.Ooh Patrick what’s wrong with you?”Alilalamika Vero kuwaomba manesi waliombeba
Patrick waharakishe.Muda wote huo machozi hayakumkauka.
Veronika alizuiliwa asiingie katika chumba cha huduma ya kwanza akaachwa hapo nje na mmoja kati ya
manesi akiendelea kumfariji.
“Jipe moyo dada yangu Patrick atapona tu.Mtumaini Mungu.”Nesi yule alimbembeleza Vero kwa upole.
Dakika kama 20 hivi baadae dokta Heneriko alimwita Vero ofisini kwake na kumuomba awe mvumilivu
wakati wakiendelea kuishughulikia hali ya Patrick.Dokta alitaka kufahamu nini hasa kilichopelekea
Patrick kupoteza fahamu.
“Unajua dokta ,Patrick ni mpenzi wangu na tuko katika maandalizi ya harusi yetu.Mimi siishi naye
kwa sasa ila huja kwake kila mwisho wa wiki .Leo hii toka asubuhi alikuwa akilalamika kuwa alihisi
uchovu mwingi .Tulitoka kidogo kisha tukarudi na akaendelea kupumzika.Usiku tukiwa sebuleni
tukiangalia Tv nikaona mwenzangu akipiga ukelele akaishiwa nguvu na kuangukia sofani akapoteza
fahamu.kwa kweli sina hakika mpaka sasa ni kitu gani hasa kilichopelekea hali ile kutokea.Naomba
Dokta ufanye kila linalowezekana ili ili Patrick apone.Niko tayari kutoa kiasi chochote cha pesa
ili mradi tu apone.”
Vero alishindwa kujizuia akaangua kilio.
“Nyamaza Vero,Hali ya Patrick inaendelea vizuri. nina hakika muda si mrefu atazinduka.Kwa hiyo
yawezekana kuwa kuna habari yoyote aliyoitazama ambayo haikumfurahisha wakati mkiangalia hadi
ikampelekea yeye kupata mstuko ?
“Sidhani dokta kwa sababu wakati tunaangalia Tv hakukuwa na taarifa yoyote ya kutisha au kustusha
inayoweza kupelekea mtu kupata mstuko hadi kupoteza fahamu.Tulikuwa tukiangalia washiriki wa miss
Tanzania wakijinadi.Ni hilo tu”Vero akajibu
Dokta Heneriko akanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema
“Kwa kumbukumbu zako toka umekuwa naye kuna siku yoyote tukio kama hili limewahi kumtokea zaidi ya
leo?
“Hapana dokta tangu mimi nimekuwa naye halijawahi tokea tukio kama hili Patrick kupoteza fahamu.”
“Ok Vero hivi sasa waweza tu kwenda kupumzika na kutuacha sisi tuendelee kumuhudumia mgonjwa
wako.Iwapo kutakuwa na mabailiko yoyote basi tutakupigia simu kukutaarifu.Na kama itahijika
kuhamishwa kupelekwa katika hospitali kubwa zaidi tutakutaarifu pia.akini kwa sasa hali yake
inaendelea vizuri,mapigo ya moyo wake yako sawa na kila kitu kinaonekana kufanya kazi vizuri.Huu
ulikuwa ni mstuko wa kawaida tu ambao unaweza kumtokea mtu yeyote na hasa akiwa na msongo wa
mawazo.”Akasema Doctor Henry.
“No Dokta ,siwezi kwenda nyumbani bila kujua hali ya mpenzi wangu iko vipi.Nitalala hapa hapa
.Nataka niwe wa kwanza kuniona pindi atakapofumbua macho.Samahani dokta naweza kuitumia simu yako
kuongea na mama yangu na kumtaarifu juu ya ugonjwa wa Patrick”
Dokta Heneriko hakuwa na kipingamizi akamruhusu Vero aitumie simu yake.
Vero akampigia simu mama yake na kumtarifu juu ya tukio lile ,halafu akawapigia simu ndugu zake
wote bila kumsahau Andrew rafiki mkubwa wa Patrick pamoja na Aloicy kaka yake Patrick.Wazazi wa
Patrick walikuwa safarini nje ya nchi.
******************************************************************
Ilichukua kama nusu saa hivi toka Andrew apate taarifa ya ugonjwa wa patrick,kuwasili pale
hospitali.Akiwa na mpenzi wake Vick walishuka garini na kukimbia kuelekea mapokezi.Mara tu baada
ya kuingia hapo mapokezi walilakiwa na sura yenye kusawajika ya Vero.Alipowaona Andrew na Vick
wakiingia humo hospitali Vero aliangua kilio ambacho kiliwachanganya zaidi Andrew na Vick.
“Where is Patrick??”Andrew akauliza huku akijikaza lakini ni wazi alikuwa akitetemeka
“Calm down Vero tuambie Patrick yuko wapi?”Aliuliza tena Andrew .Vick akamkumbatia Vero huku naye
machozi yakimtoka.
Andrew alimfuata nesi aliyekuwa mapokezi na kumuuliza juu ya hali ya Patrick.Hakuridhika na jibu
alilolipata ,kwa kasi akakimbia hadi katika ofisi ya Dokta Heneriko lakini hakumkuta.Taratibu
akatoka humo ofisini jaso likimtiririka na kurudi mapokezi.tayari Aloicy kaka yake Patrick
alikwisha wasili hapo hospitali akiwa ameongozana na mke wake nao wote waliungana na Vick katika
kumbembeleza Vero.
Andrew akawasalimia kisha akamvuta mkono alois wakasogea pembeni kidogo.
“Hebu niambie Andrew kitu gani kinachoendelea hapa na Patrick yuko wapi ?
Aliuliza Alocyhuku naye jasho likimtiririka
“Brother Aloicy hata mimi mpaka muda huu sielewe chochote kwani toka nimefika hapa muda mfupi
uliopita sijaweza kuongea lolote na Vero.Ila kwa maelezo niliyoyapata toka kwa nesi ni kwamba
Patrick yuko katika chumba cha huduma ya kwanza akipatiwa matibabu.Nasikia ni mstuko ndio
uliopelekea akapoteza fahamu”
Mara dokta Heneriko akatokea.Nesi aliyekuwapo mapokezi akamtambulisha kwa akina Andrew.
“Dokta hawa ni ndugu zake na Patrick wamefika saa hivi na walikuwa wakitaka kupata taarifa juu ya
maendeleo ya mgonjwa wao’
Dr henry akawasalimu wote halafu akawaomba Alois na Andrew wamfuate ofisini kwake..
“Vijana wangu kwanza poleni sana kwa matatizo ‘
“Ahsante sana dokta tumeshapoa”Walijibu kwa pamoja
“sasa vijana wangu nimewaiteni hapa ili tuongelee zaidi suala la ndugu yenu..Patrick aliletwa hapa
kwangu usiku huu akiwa amepoteza fahamu.Kwa haraka nikisaidiana na madokta wenzangu tumejitahidi
kumpatia huduma ya kwanza na mpaka sasa maendelo yake ni mazuri.Tumejitahidi kurekebisha mapigo ya
moyoyaliyokuwa juu sana na kwa sasa yako kawaida.Taratibu anaanza kurejewa na fahamu zake ingawa
bado anahitaji kupumzika zaidi kwani bado fahamu ahizarejea vizuri.Maendeleo yake ni mazuri na
baada ya muda mfupi ujao basi atarejea na fahamu zake zote.”
Alois alishusha pumzi nzito kwa kusikia taarifa ile ya dokta.akatoa leso na kujifuta jasho
lililokuwa likimtirirka kwa kasi muda huo.
“Thanks God”Alisema Alois huku ameinua mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu
“kwa hivi sasa bado ataendelea kuwapo katika uangalizi maalum mpaka hapo hali yake itakapokuwa
nzuri kabisa.Tatizo lililompata ni mstuko wa moyo.Ni tatizo la kawaida kutokea.Ila hali yake
itakapokuwa nzuri tutamshauri aonane na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ili aweze kumfanyia
uchunguzi zaidi katika moyo wake ”
Baada ya kupata maelezo ya kutosha toka kwa dokta,Aloicy na andrew waliridhika kabisa na dokta
akawa shauri waende kupumzika mpaka kesho .aloicy alikubaliana na wazo hilo lakini akashauri
andrew awarudishe Vero na Vick nyumbani wakapumzike.Yeye atabaki pale kuangalia hali ya Patrick
inavyokwenda.
Wakati wakiendelea kujadili mama yake Vero akatokea.Akawasalimu wote aliowakuta hapo kisha kwa
wasiwasi akataka kujua juu ya hali ya Patrick.alipewa maelezo na mafupi ya hali ya mgonjwa halafu
akaomba aonane na dokta Heneriko,akaongea naye na kupewa kwa muhtasari juu ya hali ya Patrick na
maendeleo yake na akahakikishiwa uangalizi wa hali ya juu.
“Ok jamani sasa utaratibu gani unaoendelea hapa?
Aliuliza Bi stella Rugi mama yake na Vero.
“Tumepanga kuwa Andrew awarudishe nyumbani Vero na vick wakapumzike ,mimi nitaendelea kubaki hapa
hapa na kufuatilia hali ya mgonjwa”Alisema aloicy
“Vizuri ,basi msipate shida ,Vero na Vick nitaondoka nao mimi,halafu Andrew nenda kule kwa Patrick
ukahakikishe usalama .Aloicy utaendelea kubaki hapa kumwangalia mgonjwa .Nitakuwa nakupigia simu
mara kwa mara ili kujua maendeleao ya mgonjwa sawa baba eenh”Alisema mama yake Vero
“sawa mama tumekuelewa .”Andrew na aloicy waliitika kisha wote wakatawanyika na kumwacha Aloicy
hapo hospitali
Saa saba usiku Patrick akarejewa na fahamu zake kamili.Kitu cha kwanza kuhisi ni harufu kali ya
dawa.akageuza shingo kutazama pande zote akatambua kuwa pale alikuwa hospitali.Taratibu akavuta
kumbukumbu za nyuma na mara akakumbuka kitu kilichopelekea yeye kuwepo pale.
“I saw her.Real I saw her.she’s alive”Alijikuta akitamka maneno haya huku jasho likikimtiririka na
mapigo yake ya moyo kwenda kasi .
“I saw her.Real I saw her.she’s alive”Alijikuta akitamka maneno haya huku jasho likikimtiririka na
mapigo yake ya moyo kwenda kasi .Muuguzi aliyekuwa akimuangalia aliingia ndani na kumkuta tayari
Patrick amerejewa na fahamu na amekaa kitandani.Haraka akaenda kumwita daktari.Dk heneriko alikuja
kwa kasi na kumpima akagundua kuwa bado mapigo ya moyo wa Patrick yalikuwa juu sana.
‘Lazima kuna kitu kinamsumbua huyu si bure”Aliwaza dokta Heneriko.
“Patrick “Dokta akamwita baada ya kumaliza kumfanyia vipimo.
“naam dokta”Aliitika Patrick kwa sauti yenye kukwaruza.
“Pole sana “
“Ahsante sana dokta”
“Patrick kijana wangu usijali utapona tu hali yako inaendelea vizuri .Unahitaji kupumzika sasa
mpaka hapo asubuhi tutakapochukua tena vipimo vingine”
“Sawa dokta.”
“Ok pumzika Patrick na iwapo utahitaji kitu chochote nesi yuko hapo nje na atakuwa akija hapa mara
kwa mara kukuangalia.Tena nimekumbuka kaka yako yuko nje muda sasa sijui kama ungependa
kumwona?”Akasema dokta heneriko.
“Yes dokta naomba uniitie..”
Dokta Heneriko akafungua mlango na kutoka.
Alois muda huo alikuwa amesinzia katika sofa lililoko mapokezi Mara akastuliwa na sauti ya Dokta
Heneriko.
“Alois,Patrick amekwisha rejewa na fahamu zake kamili kwa hiyo unaweza kwenda kumwona.Ila
tafadhali usijaribu kumuuliza chochote kuhusiana na kilichopelekea yeye kupoteza fahamu.Ongea naye
maongezi mengine ya kawaida.sawa?”
“sawa dokta”Alijibu Patrick huku akifikicha macho yaliyojaa usingizi.Nesi aliyekuwepo mapokezi
akampeleka hadi katika chumba alimokuwa amelazwa Patrick.
“Vipi brother unajisikiaje kwa sasa?Alisema Alois
“Sasa hivi sijambo brother najisikia vizuri.nashukuru kwa kuja kuniona”
“Usijali Patrick kwa sasa endelea kupumzika.bado unahitaji mapumziko ya kutosha.Mimi niko hapo
mapokezi tutaonana asubuhi”
“Ok brother”
**************************************************************
Baada ya kulia sana hatimaye kiusingizi kikaanza kumchukua na taratibu akajikuta akianza
kulala.Hazikupita hata dakika kumi toka aanze kusinzia simu yake ikaanza kuita na kumstua toka
usingizini.Alipoiangalia simu yake ilikuwa imeandika jina Alois.Aliogopa kuipokea simu ile akabaki
akiiangalia ikiiendelea kuita.Mikono ilikuwa ikimtetemeka .Alihofia pengine simu ile inaweza kuwa
imebeba ujumbe mbaya kuhusu Patrick.Simu iliita ikakatika ,ikaanza kuita tena.Akaamua kuipokea.
“Haloo”Aliita Vero
“Haloo shemeji vipi?Ilkuwa ni sauti ya upande wa pili wa simu ambayo Vero aliitambua moja kwa moja
kuwa ilikuwa ya Alois.
“safi shemeji vipi kwema huko?Alisema vero huku mapigo yake ya moyo yakienda kwa kasi isiyo ya
kawaida.
“Huku kwema tu shemeji.Nataka nikufahamishe tu kuwa Patrick tayari amekwisha rejewa na fahamu zake
na nimetoka kuongea naye muda si mrefu.Kwa hivi sasa anaendelea kupumzika.kwa hiyo shemeji yangu
unaweza ukalala kwa amani sasa.”
Vero akashusha pumzi ndefu akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akamuaga Aloicy na kukata
simu.Alipokata simu akaanza tena kulia kwa kwikwi..Vick ambaye alikuwa katia usingizi mzito
akaamka baada ya kustushwa na kilio cha Vero.
“Vero nini tena?
“Patrick anaendelea vizuri.Alois amenipigia simu sasa hivi na kunifahamisha.”
“sasa kama hajambo unalia nini?
“Huwezi jua Vick ni jinsi gani nisivyopenda kumuona Patrick akiumwa kwa jinsi
ninavyompenda..Ninalia kwa mateso ninayoyapata juu yake.”
Vick alimbembeleza vero hadi akanyamaza kisha akajilaza kitandani na kuanza kutafakari.juu ya
tukio zima..Alikumbuka walikuwa sebuleni wakiangalia luninga ambapo warembo wanaotarajia kuwania
taji al miss Tanzania walikuwa wakijinadi .alivuta picha na kumuona Patrick akiwa katka friji
akijimiminia maji katika glasi ambapo muda huo Miss arusha Neema aliikuwa akijinadi.Alikumbuka
kumuona Patrick alivyovutiwa ghafla na kipindi hicho cha warembo.Toka Neema hakumbuki ni mrembo
gani aliyefuatia kujinadi ila anachokumbuka ni kwamba Patrick alipiga ukelele mkubwa wa kama
anashangaa kitu halafu akaanguka.
“Ni dhahiri ni mstuko ndio uliomfanya Patrick aanguke na kupoteza fahamu .Lakini je ni kitu ganui
hasa ambacho kilimstua Patrick kiasi cha kupoteza fahamu?Je mstuko huu una uhusiano wowote na
kipindi kile tulichokuwa tukikitazama?Lakini hapana Patrick nimekuwa naye kwa muda mrefu sasa na
tabia yake ninaifahamu vizuri.Kuhusu wanawake siwezi kumsemea vibaya hana tabia hiyo ya kuwa na
wanawake wengine nje ya mahusiano yetu.Nina uhakika na hilo.Sasa ni kitu gani alistuka ?any way
siwezi kupata jibu kwa sasa mpaka hapo atakaponiambia yeye mwenyewe kwani nina hakika hawezi
kunificha kitu chochote.”
Alikuwa akiwaza Vero na taratibu usingizi ukamchukua akalala.
*****************************************************************
Saa kumi na mbili asubuhi iliwakuta Vero ,Vick na mama yake vero hospitali.Hali ya Patrick ilikuwa
ikiendelea vizuri .alfajiri hiyo tayari alikwisha hamishwa toka katika chumba cha uangalizi maalum
na kuwekwa katika chumba cha mapumziko ya kawaida.
Wakiongozwa na alois ambaye alilala hapo hospitali walielekea moja kwa moja chumbani na kumkuta
Patrick tayari amekwishaamka.Bila kupoteza muda Vero akamkumbatia na kumpiga mabusu mfululizo.
“Pole sana my dear.Unajisikiaje kwa sasa?
“Najisikia vizuri sana”
alijibu Patrick huku akijinyoosha nyoosha pale kitandani.baada ya kusalimiana kilifuata kipindi
cha vicheko na utani wa hapa na pale kisha Vick na mama yake Vero wkaomba waondoke kwa ajili ya
kwenda kujiandaa na mishughuliko ya siku.
Vero alimwinua Patrick na kumpeleka bafuni ambako alimwogesha na kumrudisha tena chumbani
,akamwandalia kifungua kinywa .Patrick alijisikia faraja kubwa kwa jisni binti huyu alivyokuwa
kimuhudumia.
****************************************************************
“Andrew kwa kipindi kirefu sasa umekuwa ni msiri wangu mkubwa.Mambo yangu mengi ambayo sihitaji
mtu mwingine kufahamu wewe wayajua.Urafiki wetu ni zaidi ya undugu.Naomba sana kile
nitakachokuambia hapa usimwambie mtu yeyote yule.Itabaki kuwa siri yako mpaka pale muda muafaka
utakapofika.”
Patrick aliongea taratibu huku akijiweka vizuri sofani.Ni siku ya kwanza tangu ameruhusiwa kutoka
hospitali kwa sababu ya mstuko uliopelekea apoteze fahamu.Andrew rafiki mkubwa wa Patrick alikuwa
kimya akiwa na shauku kubwa ya kutaka kulisikia lile ambalo rafiki yake alikuwa tayari kumwambia.
“I saw Happy”alisema Patrick kisha akatulia na kuyaacha maneno yale yamwingie Andrew.
“what” aliuliza Andrew kwa mshangao
“I saw Happy”
Patrick alirudia tena kisha akainamisha kichwa chini na kuzama katika mawazo mazito.andrew
aliinuka na kuanza kuzunguka zunguka mle chumbani huku akionekana dhahiri alikuwa meshtushwa mno
na kauli ile ya Patrick.
“Umemuona wapi?”andrew akauliza huku amejishika kichwa.
‘Nimemuona kwenye tv .Kulikuwa na kipindi cha kuwanandi warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro cha
kumsaka mrembo wa Taifa .Happy ni miss Ilala.”
“are you sure” Andrew akahoji
“Yes I'm sure na ndio kitu kilichonifanya nikapata mstuko na kupoteza fahamu”
Andrew alivuta pumzi ndefu ,akainuka akaanza kuzunguka zunguka humo ndani kisha akakaa.Vijana hawa
wote kwa sasa walikuwa katika wakati mgumu sana.Ni Andrew pekee aliyefahamu kilichokuwa
kikiendelea kati ya Patrick na Happy na ndio maana alichanganyikiwa asijue afanye nini.Alimuonea
huruma sana Patrick kwa wakati huu mgumu alionao.
“Vero aligundua chochote “Andrew akauliza tena
“sidhani kama aligundua kitu chochote.sidhani kama alihisi chochote kwa wakati ule”
“Ok kwa hiyo tufanye nini sasa” Andrew alihoji.
Patrick akainuka na kwenda katika friji akjimiminia maji baridi kwenye glasi akapiga funda kubwa
kisha akavuta pumzi ndefu na kusema.
“Nataka kuonana na Happy”
Kimya kikatanda hapo sebuleni
“Nataka kabla ya kuonana naye kwanza tumfanyie uchunguzi anaishi wapi,na nani anafanya kazi
gani,ana mchumba hana,na chochote kile tunachoweza kukifahamu kuhusu yeye.Uchunguzi huu nataka uwe
wa siri na yeye Happy asiweze kufahamu kuwa anachunguzwa.Ikiwezekana tunaweza hata kuajiri mtu wa
kuifanya kazi hii niko tayari kumlipa kiasi chochote cha pesa anachohitaji.Nakukabidhi kazi hii
Andrew nina imani itafanyika ipasavyo.Tuko pamoja?
“Nimekuelewa Patrick lakini suala hili haliwezi kuathiri maandalizi ya harusi yako ambayo tayari
yamekwishaanza?”
“Hahahah usihofu kuhusu hilo my friend.I know what I’m doing ,ok?”
“Una maana gani Patrick unaposema unajua unachokifanya ?Ninafahamu kuwa ndoto zako za siku nyingi
ni kuwa na Happy katika maisha yako na kwa sasa umekwisha kuwa na uhakika kuwa yupo na kwa wakati
wowote unaweza kumuona .Nina wasiwasi sana na huu ujio wa Happy katikati ya maandalizi ya Harusi
yako unaweza kutibua kila kitu.
“Kwa ajili ya Happy niko tayari kwa lolote linaloweza kutokea.I must fight for her.all these years
I’ve been hurting myself thinking about her na mpaka sasa nimeshindwa kabisa kuifuta kumbukumbu
ya Happy moyoni mwangu.Siwezi kuendelea kuutesa moyo wangu Andrew.I have to face her.” Akasema
Patrick
“Patrick nafikiri unahitaji kufikiri zaidi kuhusu suala hili, si suala jepesi kama
unavyolifikiri.Ni suala ambalo linagusa hisia za watu wengi .Hi…..”
Andrew hakuendela Patrick akadakia.
“Andrew no body’s gonna change my mind.That’s my decision and its final.Nilivyoamua
nimeamua.Nitapambana kadiri ninavyoweza ili kumpata Happy.I love her and I know that she loves me
too.”
“Patrick miaka mingi imepita tangu mpotezane na Happy na kwa sasa bado kama mwezi mmoja na nusu
hivi ufunge ndoa na Vero ,ndoa ambayo sehemu kubwa ya maandalizi yake yamekamilika.Huoni kuwa
utakuwa unamyima haki zake Vero kama ukihamishia mawazao yako yote kwa Happy.?Nina imani Vero
anakupenda kwa dhati ya moyo wake na nina imani vile vile hata wewe unampenda Vero sasa kwa nini
utake kumtesa hivi mtoto wa watu?
“Andrew unayasema haya yote kwa sababu huwezi kuingia katika viatu vyangu na kuona nini kilichomo
ndani.Nina imani kubwa hata wewe ungekuwa mahala pangu kwa sasa basi ungeweza kufanya kama mimi
ninavyofanya.Please Andrew naomba msaada wako katika hili.Ni lazima nionane na happy hivi
karibuni.”
“Nimekuelewa Patrick lakini bado moyo wangu una wasiwasi sana juu ya kinachoweza kutokea.hapo
mbeleni.nafahamu kuwa endapo utaingia matatizoni basi ni sote tutakuwa tuko katika matatizo.Tatizo
langu ni lako na lako langu ndio maana tunahitaji sana kushauriana kwa kina kabla ya kufanya
jambo.”
“Andrew najua una wasiwasi mwingi kuhusu mimi na Vero.Hilo ni kubwa linalokuumiza kichwa.Hata mimi
sijisikii vizuri kumtesa Vero binti aliyeyatoa maisha yake kwangu.Binti anayenipenda kwa dhati ya
moyo wake.Ni vero huyu huyu ndiye aliyeirudisha tena furaha ndani ya moyo wangu na kuliondoa wingu
zito la ukiwa lililokuwa limenifunika.Nampenda Vero lakini sina jinsi ni lazima nionane na Happy.”
Andrew aliinuka kitini akaiendea friji na kujimiminia mvinyo baridi akanywa mafunda kadhaa kisha
akamgeukia Patrick.
“Ok Patrick kwa sababu umekwishaamua basi hatuna budi kufanya hivyo.Mimi nitaianza kazi hiyo
kesho.Nitamtafuta mtu ambaye ataifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa.Usijali kuhusu hili rafiki
yangu”
Patrick alifurahi akainuka na kumkumbatia rafiki yake.
********************************************************************
Saa kumi na mbili za jioni Veronika alirejea katika shughuli zake na kumuaga mama yake kuwa
alikuwa akaienda kumwangalia Patrick anaendelaje.Ni siku ya tatu sasa toka Patrick atoke
hospitali.Hali yake haikuwa ikiendelea vizuri sana.Muda mwingi alikuwa akionekana ni mtu mwenye
mawazo mengi sana.Hali hii ilimpa wasiwasi mwingi Vero kiasi cha kumfanya awe karibu naye kila
wakai ili kujaribu kumchangamsha na kumrudisha katika hali yake ya kawaida.
Ingawa Patrick alijitahidi kwa kila jinsi ili Vero asione hali hii ya unyonge lakini mara nyingi
alishindwa na kujikuta akitoa machozi.Vero aliigundua hali hii na kwa kiasi kikubwa ikamuongezea
udadisi juu ya kinachoendelea .alijua ni lazima liko jambo ambalo linamchanganya Patrick .
‘Haloo sweetie”Alisema Vero baada ya kuingia ndani kwa Patrick
“Haloo vero, you are back”akasema Patrick
Vero akamfuata Patrick kitandani akamkumbatia na kumpiga busu zito.
‘Unaendeleaje mpenzi”
“Naendelea vizuriMungu ananisaidia sana.Muda si mrefu nitapona kabisa”
Baada ya kujuliana hali Vero alimwandalia Patrick Juice kisha yeye akaelekea jikoni kufanya
maandalizi ya chakula cha jioni.Patrick alipata faraja kubwa baada ya Vero kuwasili Ni wazi
Patrick husikia furaha kubwa moyoni awapo na Vero.
Ilimuuma sana baada ya kugundua kuwa bado alimpenda sana Vero lakini kwa ghafla Happy ametokea na
kuanza taratibu kuzihamisha hisia zake.
Chakula kiilpokuwa tayari kikawekwa mezani,wakala kisha wakapumzika na baadae wakaelekea kulala.
“Vero dear tayari umekwisha kata tiketi za kuingia Miss Tanzania Jumamosi?Patrick akauliza
“Tayari mpenzi Nimekwishaziandaa .Je utaweza kweli kwenda na hali hii?Naona kama hali yako inazidi
kudhoofia siku hadi siku”
“Usijali mpenzi wangu lazima nihudhurie hata iweje.Nina imani ndani ya siku mbili tatu zijazo hali
yangu itakuwa shwari”
Vero akanyamaza kimya akajaribu kuvuta kumbukumbu nyuma siku ile Patrick alipoanguka na kupoteza
fahamu alikuwa akitazama kipindi cha wagombea wa miss Tanzania .Hakutaka kukubaliana kuwa kuna
kitu chochote kinachoendelea baina ya Patrick na mashindano yale.Alijitahidi kuilazimisha akili
yake ikubaliane na taarifa ya daktari kuwa Patrick alipoteza fahamu kwa sababu ya uchovu mwingi
uliokuwa ukimkabili kiasi cha kuufanya ubongo wake ushindwe kufanya vizuri kazi yake.
‘Lakini pamoja na taarifa ile ya daktari lakini kuna kitu kiko moyoni mwa Patrick ambacho
kinamyima raha na na kuisumbua akili yake namna hii.Ni kwa sababu hiyo tu ndiyo maana amepoteza
furaha yote aliyokuwa nayo kabla.Chakula chenyewe mpaka abembelezwe.mara kadhaa nimemfuma mwenyewe
kwa macho yangu akilia.Ingawa anajitahidi sana kuificha hali hii lakini nimekwishafahamu .Anyway
nitajitahidi kumuuliza ili anieleze kama kuna jambo lolote linalomsibu.”
Veronika alizama ghafla katika mawazo.
“Unawaza nini mpenzi wangu”Patrick akauliza
“Nothing.Siwazi chochote zaidi yako.Unajua Patrick hali yako kwa sasa inanipa wasiwasi sana.Tangu
umetoka hospitali umebadilika.Ni kitu gani kinakusumbua mpenzi hebu niambie.Hali hii inanifanya
hata mimi nihisi kama vile ninaumwa pia.Au kama kuna kitu nimekukosea niambie Patrick ili
nijirekebishe.Tangu tumeanza mapenzi yetu sijawahi hata siku moja kukuona katika hali hii”
Vero akashindwa kujizuia akaanza kulia kwa kwikwi.
Patrick akamvutia Vero kwae akambusu na kumwambia
“Usihofu kitu baby hakuna kitu kingine kinachonisumbua .Kama daktari alivyosema kuwa natakiwa
kupumzika sana .Uchovu ndio uliopelekea tatizo lile kutokea.”
Alisema Patrick huku akizichezea nywele laini za Vero.
‘Hapana dear najua lazima kuna kitu kinachokusumbua akili na hutaki kuniambia”
“Wow my dear angel ,wewe ndiye maisha yangu.Wewe ndiye uliyeyashika maisha yangu.Nimekukabidhi
funguo za moyo wangu.Wewe ndie mfariji wangu,wewe ndiye furaha yangu,wewe ndiye kila kitu kwangu
sasa kwa nini nikufiche kitu?Hakuna kitu nimewahi kukuficha wewe mpenzi wangu na haitakuja tokea
nikawa na tatizo nikashindwa kukwambia.Sasa nisipokwambia wewe nitamwambia nani tena?”
Patrick alijitahidi kumtoa Vero wasiwasi aliokuwa ameanza kuwa nao juu yake na mara moja akaazimia
moyoni kubadilika kitabia ili Vero asije akaendelea kumdadisi.Taratibu akaanza kurudi katika hali
yake ya kawida ya ucheshi na uchangamfu mkubwa kitu ambacho Vero alikifurahia sana.
*****************************************************************
Ni juamamosi angavu ndaniya jiji la Dar es salaam,jiji lililjaa kila aina ya pilika na
purukushani.Jua lilikuwa likielekea magharibi na kulipisha giza lichukue nafasi yake.Jioni hii
iliwakuta Patrick na Veronika wakiwa katika pilika pilika za kujiandaa kuelekea katika
kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa taifa katika ukumbi wa Diamong jubilee.
Patrick ndiye aliyekuwa katika pilika pilika nyingi zaidi jioni hiyo.Siku hii ilikuwa ni moja kati
ya siku zake kubwa kabisa katika maisha yake.Ni siku ambayo aliamini ingemkutanisha tena na
kiumbe ampendaye kwa dhati ya moyo wake.Alikuwa ndani ya suti nzuri ya gharama kubwa.Suti hii huwa
anaivaa kwa nyakati maalum kama hizi.Hakika alikuwa amependeza vilivyo kijana huyu.Wakiwa katika
harakati z a kumalizia kujiandaa simu yake ikaita.Alkuwa ni Andrew.
“Haloo Andrew”
“Hallo Patrick vipi mko tayari?aliuliza Andrew huku akicheka kichinichini.
“Tupo tayari Andrew na muda wowote toka sasa tunaweza kuanza safari ya kuelekea ukumbini”
“Ok Patrick sisi tayari tumekwishajiandaa na muda wowote tutakuwa njiani kuelekea huko na
tutawasubiri nje ya ukumbi ili tuingie pamoja.Ila ndugu yangu nakuomba kitu kimoja katu
usihamaki.Wala usionyeshe aina yoyote ya mstuko pindi utakapomuona Happy.Najua tu lazima kunaweza
kutokea na kitu kama mstuko flani hivi ila tafadhali naomba ujaribu kujizuia kwa sababu pale
tutakuwa tuko na Vero na Vick kwa hiyo wanatakiwa wasihisi kitu chochote.Mimi nitakuwa macho
kuhakikisha kuwa hakuna kitu chochote kitakachoharibika “
“Usihofu Andrew nalifahamui hilo na niko makini nalo sana.naelewa leo ni siku ya kipekee maishani
mwangu.Ni siku ya kihistoria katika maisha yangu hivyo siwezi kuiharibu.”
Baada ya kumaliza kujiandaa na kuhakikisha kuwa wako safi wakaingia garini na kueleka Diamond
Jubilee.
**************************************************************
Ukumbiwa Diamond jubilee ulikuwa umefurika watu pasi mfano.Pamoja na ukumbi kufurika watu bado
watu walikuwa wakmiminika ukumbini hap kwa lengo la kushuhudia mchuano wa kumtafuta mrembo wa
Taifa atakayeliwakilisha Taifa katika mashindano ya dunia.
Patrick,Vero,Andrew na Vick waliwahi sana kuingia ukumbini na kuchukua moja kati ya meza za mbele
kabisa.Patrick moyo ulikuwa ukimdunda sana usiku huo,.Andrew alilifahamu hilo na hivyo akawa
makini sana katika kuakikisha kuwa hakuna kitu kitakachoharibika .Toka wameingia ukumbini Patrick
alikuwa kimya .
“Patrick are you ok?Vero liuliza baada ya kuona Patrick yuko kimya sana.
“Yes I’m ok Vero usihofu.”
Mara muongoza shughuli akatokea jukwaani na kuanza kutangaza.
“Mabibi na mabwana mliohudhuria mashindano haya makubwa ya urembo nchini napenda kuwakaribisha
sana katika usiku huu wa pekee kabisa kwetu sote.Ni usiku wa pekee kwa sababu leo tutaandika
historia mpya kabisa katika mashindano ya urembo hapa nchini na ulimwengu kwa ujumla.Kwa mwaka huu
kamati nzima ya Miss Tanzania imeazimia kufanya mabadiliko makubwa sana na nyie wote mlioko hapa
ndio mtakaokuwa mashahidi wa kile kitakachotokea usiku wa leo.Nasema karibuni sana katika usiku
huu na tujumuike sote mimi naitwa Mc Thora kwa wale ambao hawanifahamu..
“Mabibi na mabwana kabla hatujaendelea mbele na ratiba yetu ningependa kwanza kumkaribisha
jukwaani mkurugenzi mkuu wa Sean woris entertainments ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano
haya kwa mwaka huu Mabibi a mabwana makofi kwaaaa Mr Petty.s Woris”
Petty woris mkurugenzi wa sean woris entertainments akapanda jukwaani akiwa amevalia nadhifu
kabisa.
“mabibi na mabwana ,wageni waalikwa,viongozi mbali mbali na wote mliohudhuria mashindano haya
usiku huu asalam aleikhum.Ni furaha ilioje kwetu sisi kama Sean woris entertainments kudhamini
mashindano makubwa kama haya ya urembo hapa nchini.Kama wote mnavyoshuhudia mashindano ya mwaka
huu yamekuwa na utofauti mkubwa na mengine yaliyotangulia.maandalizi yake yamekuwa mazuri ,zawadi
zimeboreshwa na ushindani miongoni mwa washiriki umeongezeka mara dufu.Kwa kuwa ni mara yetu ya
kwanza kudhamini mashindano makubwa kama haya bado kunaweza kuwa na kasoro kadhaa ambazo nina
imani kwa kushirikiana na wadau wote wa urembo hapa nchini tutasaidiana kuzitatua.Nina imani bado
tutaendelea kudhamini na kuandaa matamasha mengi na makubwa zaidi hapa nchini ili kuzidi kuukuza
wigo wa burudani hususani sanaa hii ya urembo.Mwisho kwa niaba ya uongozi na wafanya kazi wote wa
Sean woris entertainments napenda kuwatakia wote utazamaji mzuri wa mashindano haya usiku
huu.Ahsanteni sana.”
Baada ya kumaliza akarudisha kipaza sauti kwa muongoza shughuli kisha akashuka jukwaani.
“mabibina mabwana huyo alikuwa ni mkurugenzi wa Sean woris entertainment ambao ndio wadhamini
wakuu wa mashindano haya kwa mwaka huu..Mabibi na mabwana kwa mujibu wa ratiba yetu kinachofuta
kwa sasa ni kuwatambulisha majaji wa mchuano huu ambao ndio watakaofanya kazi kubwa na ngumu ya
kutuchagulia mrembo mwenye sifa ya kuwa mrembo wa taifa.Majaji tulionao usiku huu ni
saba.Ningeomba jaji utakaposiia jina lako likitajwa basi usimame ili watu wakufahamu.Wa kwanza ni
Mr Ernest Namesha,wa pili ni ndugu Mecky ,tunaye pia Mr Boniventure Gregory,anayefuatia ni Mr
Samweli Nathaniel,tunaye pia dada yetu mpendwa usiku huu naye ni dada Esther mdee,pia tunaye Mrs
Coletha brown,tunaye vile vile bi Susan Abrahams na wa mwisho ni ndugu Jacob Lyimo.Hawa ndio
majaji wetu ambao watakuwa wakifanya kazi ngumu ya kumchagua mrembo wa Taifa usiku huu wa leo.”
“mabibi na mabwana baada ya kuwafahamu majaji wa mchuano hu wa leo sasa naomba niwalete kwenu
warembo wote 26 katika show maalum waliyoiandaa “
wimbo ukaanza kupigwa na warembo wakaanza kutoka huku wakicheza kwa stailiyenye kuvutia
sana.makofi nderemo na vifijo vikatawala ukumbini.Patrick alielekeza macho na akili yake yote
jukwaani na bila kukosea alimuona happy ambaye alikuwa amependeza kupindukia Jasho
likaanzakumtiririka akatoa kitambaa na kujifuta.Alikuwa imya kabisa.
Baada ya show ya warembo kukamilika ziliendelea burudani mbili tatu toka kwa wasanii mbali mbali
kisha muongoza shughuli akapanda jukwaani.
“Mabibi na mabwana baada ya kupata burudani hizo zakukata na shoka sasa naomba niwalete kwenu
warembo wote 26 ili muwatambue.Watapita hapa jukwaani mmoja mmoja .”
Warembo wakaanza kutoka nyuma ya jukwaa na kuanza kupita mbele ya watazamaji.Kidogo Patrick atamke
kitu baada ya kusikia jina la Happy likitajwa .Happy akapita jukwaani huku kelele za shangwe
zikisikika.Happy alikuwa akionekana kama malaika usiku huu.alikuwa amependeza vilivyo.Kila mtu
aliustaajabia uzuri wa binti huyu mwenye kila sifa ya kuwa mrembo wa Taifa na dunia.Kelele zile za
mashabiki zilizidi kumchanganya Patrick na kumfanya ahisi kuchanganyikiwa.Andrew alikuwa makini
sana kwa lolote ambalo lingeweza kusababisha uvunjifu wa amani kati yao.
Baada ya kupita jukwaani kujitambulisha kwa mashabiki zikafuata burudani za aina yake toka kwa
wanamuziki.Kisha Muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.
“mabibi na mabwana mambo yanazidi kupamba moto.Mambo ni bam bam na kama nilivyowaeleza toka mwanzo
kuwa Sean woris entertainment wameleta mageuzi makubwa katika mashidano ya mwaka huu .Kwa sasa
napenda kuwaleta kwenu warembo wote 26 wakiwa katika vazi la ufukweni.Mhh hapa pana kazi kweli
kweli .mabibi na mabwana hebu tuwashangilie hawa warembo wetu watakapokuwa wakipita jukwaani
katika vazi la ufukweni.”
Warembo wakaanza kupita jukwaani wakiwa katika vazi la ufukweni.Siyo siri walikuwa wamependeza
vilivyo.Baada ya kumaliza kupita na vazi la ufukweni zikafuata tena burudani halafu warembo wote
wakapita tena kwa mara nyingine na vazi la ubunifu.Kelele zilikuwa kubwa sana kila walipopita
warembo Neema wa Arusha na Happy wa Ilala.Warembo hawa walionekana kuchuana vilivyo.Kisha pita
na vazi la ubunifu muongoza shughuli akapanda jukwaani.
“mabibi na mabwana tayari tumewashudia warembo wetu 26 wakipita hapa mbele yetu wakiwa katika
mavazi tofauti tofauti.Kwa sasa ule wakati mliokuwa mkiusubiri kwa hamu kubwa unaelekea
kuwadia.Kwa hivi sasa tutakwenda kuwafahamu warembo 10 bora ambao wameonekana kufanya vizuri zaidi
.Naomba sasa nimkaribishe Mrs Coletha brown ili aje atutangazie wale warembo wetu kumi waliofanya
vizuri zaidi.Karibu sana mama.”
Mrs Coletha brown akapanda jukwaani akiwa na karatasi yenye majina ya warembo kumi waliofanya
vizuri na ambao wataendelea na mchuano.
“mabibi na mabwana napenda kuchukua nafasi hii kwanza kuwapongea waandaaji wa mashindano haya
ambayo kwa mwaka huu yameboreshwa kwa kiwango cha juu kabisa.
Mabibi na mabwana kazi yetu usiku wa leo imekuwa ni ngumu sana .Warembo wote wako katika hali ya
ushindani wa hali ya juu mno.Lakini tumeweza kuwapata wale kumi ambao ni bora zaidi na ambao
nitaenda kuwataja hivi punde.Nambari 12 Nelea shulo,nambari 9Saida abdi,nambari 4 Upendo
timelo,Nambari 20 Neema i,Nambari 11 Esther stevens,Nambari 6 Happy ,nambari 22 Elimeena
kimuo,nambari 26 bahati udhoka,nambari 16 Winifrida mwasajuki,na mwisho ni namba 13 genevieve
alphonse.”
Kelele za kushangilia zikasikika ukumbini.Warembo waliofika hatua ya kumi bora wakajipanga
mstari.wakapiga picha ya pamoja kisha zikafuata burudani .baada ya burudani mc akapanda tena
jukwaani.
“Mabibi na mabwana bado tunaendelea na mchakato wetu wa kuifikia ili hatua kubwa kabisa ambayo
kila mmoja wetu aliyeko hapa anahamu ya kuishuhudia.Kila mmoja anatamani amfahamu mrembo wetu mpya
wa Taifa.Kwa sasa tutaenda kuwatafuta wale watano bora ambao kutoka kwao tutampata mrembo
wetu.Atapanda tena Mrs Coletha kuja kututangazia warembo watano bora .”
mrs Coletha akapanda tena jukwaani akiwa ameongozana na watu wawili wa miraba mine wanaomlinda.
“mabibi na mabwana kama nilivyowaambia kuwa kazi yetu leo imekuwa ngumu sana hasa kutokana na
jinsi warembo wote walivyo na vigezo vya juu mno kiushindani.Lakini pamoja na wote kuwa na
ushindani wa juu tumeweza kufanikiwa kuwachuja na kupata wale watano ambao wameonekana kuwa ni
bora zaidi.
Warembo waliopita hatua ya tano bora ni mrembo nambari 16 Winifrida mwasajuki,nambari 20 Neema
i,nambari 13 Genevieve alphonse,nambari 26 Bahati udhoka na mwisho ni nambari 6 Happy .”
Kelele kubwa zikasikika zikishangilia.Kila mtu pale ukumbini alikuwa ameridhika na kazi
waliyoifanya majaji.Hakukuwa na aina yoyote ya upendeleo.Baada ya kuwatambua warembo wote
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora hatimaye kikafuata kipindi cha maswali.Ni Happy kibaho
tena ndiye aliyejibu swali vizuri zaidi na kuwafanya watu wote ukumbini kumshangilia kwa
nguvu.Kila mtu alikuwa akiamni kuwa Happy ni lazima angeibuka kuwa mrembo wa Taifa.patrick jasho
lilikuwa likimtiririka mwilini.alijitahidi kwa kila alivyoweza ili asiweze kuonyesha hali yoyote
ya utofauti pale mezani.Baada ya kipindi cha maswali kumalizika ikafuata burudani moja kisha
muongoza shughuli akapanda jukwaani.
“mabibi na mabwana ule wakati uliokuwa ukisubiriwa na kila mtu hapa ukumbini naona sasa
umewadia.huu ni wakati wa kumtambua mrembo wetu mpya wa Taifa.Napenda nichukue fursa hii
kuwashukuru sana majaji kwa kazi ngumu waliyoifanya usiku huu kwa kutuchagulia mrembo mpya wa
Taifa.Kabla sijamkaribisha jaji mkuu kuja kutangaza mshindi wa shindano hili napenda kumkaribisha
mrembo anayemaliza muda wake ili aweze kuongea machache na kuwaaga rasmi kabla hajalivua taji la
Miss Tanzania.”
Helen Daudi mrembo anayemaliza muda wake alipanda jukwaani huku akishangiliwa vilivyo.Alipewa
kipaza sauti na kusogea mbele.
“mabibi na mabwana ,wageni waalikwa,waheshimiwa majaji ,waandaaji na wadhamini wote wa mashindano
haya habari za usiku.Napenda kwanza kabisa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha mimi kutimiza
moja ya ndoto zangu nayo ni kuwa mrembo wa Tanzania.Nawashukuru vile vile wazazi wangu na ndugu
zangu kwa kunipa moyo toka katika hatua za awali za kinyang’anyiro hiki hadi nilipobahatika
kuchukua taji.Mabibi na mabwana kulivaa taji la Miss Tanzania ni mzigo mkubwa.Nimeshuhudia mimi
mwenyewe uzito wa taji hili kubwa la urembo hapa nchini.Yapo mengi ambayo unapaswa kulifanyia
taifa hili ukiwa kama mrembo wa Taifa.Kuna mazuri na magumu yake.Zipo changamoto nyingi ambazo
yakubidi upambane kufa na kupona ili uweze kushinda.Napenda kuishukuru kamati nzima ya Miss
Tanzaina kwa ushirikiano mkubwa walionipa katika kipindi chote nilichokuwa nimevaa taji
hili.Sintaweza kumtaja mmoja mmoja lakini napenda niwashukuru wote kwa ujumla.Napenda niwashukuru
vile vile wadau wote wa sanaa hii ya urembo hapa nchini kwa sapoti yao kubwa
waliyonipa.Wamenisaidia sana kuifahamu sanaa hii ya urembo vizuri.Nawashukuru pia wananchi wote wa
Tanzania kwa kunikubali Nawapenda wote na ninaahidi kushirikiana na mrembo atakayevaa taji hili
usiku huu katika yale yote mazuri niliyokuwa nimeyafanya kwani kulivua taji hili si mwisho wa
kuendeleza yale yote niliyokwisha yafanya wakati niko na taji.Mwisho kama binadamu kuna wakati
naweza kuwa nimemkosea huyu na yule kwa namna moja au nyingine.Napenda kuchukua nafasi hi kwa
dhati kabisa kuwaomba msamaha wale wote niliowakosea.Tusameheane na kuanzia usiku huu tuanze
maisha mapya.Ahsanteni sana.”
Alimaliza kutoa machache mrembo huyu akarudi katika kiti chake cha heshima huku akishangiliwa na
watu.’
“naam mabibi na mabwana huyo alikuwa ni mrembo anayemaliza muda wake.Na sasa ule wakati tuliokuwa
tukiusubiri kwa hamu kubwa ndio umewadia.Ni hivi punde tutaenda kumfahamu mrembo wetu mpya.Naomba
sasa nimwite Mr Jackob Evarist ili aweze kututajia washindi wetu.”
Mr jacob akapanda jukwaani.
“Mabibi na mabwana kama alivyotangulia kusema Mrs Coletha brown kuwa mchuano wa leo ulikuwa mgumu
sana.Tunamshukuru Mungu kuwa tumeweza kumpata mrembo wa taifa licha ya kuwa na wakati mgumu hasa
kutokana na kila mrembo alivyokuwa amejiandaa.Mabibi na mabwana nitaanza kuitangaza nafasi ya tatu
hadi moja.”
Alitulia kidogo kisha akaendelea.
“Nafasi ya tatu imekwenda kwa mrembo nambari 16 winifrida mwasajuki”
alitulia kwanza na kumpisha mrembo huyu apite mbele huku akishangiliwa.
“nafasi ya pili imekwenda kwa mrembo mwenye nambari 20 Neema Japheti”
Kelele za shangwe zikasikika.Neema binti mwenye ngozi nyeusi yenye kung’aa akapita jukwaani akiwa
ndani ya tabasamu kubwa.
“Na sasa mabibi na mabwana ni nafasi yakwanza.Nafasi ya kwanza imekwenda kwa mrembo mwenye nambari
6 Happy .”
Tangu ukumbi wa Diamond jubilee ujengwe hakujwahi tokea shangwe kubwa kama hii ya usiku huu ya
kuushangilia ushindi wa Happy.Mrembo huyu alifanikiwa kuzikonga nyoyo za watu vilivyo.
Patrick alishindwa kujizuia akainuka na kushangilia kwa nguvu sana.
Jukwaani Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Hakuamini kama ni yeye ndiye aliyetangazwa mshindi wa
shindano hili hasa kutokana na upinzani mkubwa uliokuwepo miongoni mwa washiriki.Watu
waliKumbatiana na kupeana mikono ya hongera kuashiria kukubaliana moja kwa moja na maamuzi ya
majaji ya kumchagua Happy kuwa mrembo wa Taifa.Kila mmoja aliamini kuwa happy alistahili kulitwaa
taji lile.
Baada ya kama dakika kumi hivi za hoi hoi na nderemo muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.
“mabibi na mabwana nafikiri hoi hoi hoi na nderemo hizi zote ni kuonyesha jinsi gani wote kwa
pamoja tunavyokubaliana moja kwa moja na maamuzi ya majaji.Happy kibaho ndiye miss Tanzania wetu
mpya.sasa kinachofuata ni mrembo anayemaliza muda wake kulivua taji na kumvisha mrembo mpya.”
Zoezi hili likafanyika huku likishangiliwa kwa nguvu sana.na baada ya zoezi hili kukamilika
muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.
“mabibi na mabwana tukio linalofuata sasa ni la kumkabidhi Miss Tanzania funguo za gari
lake.Tunamuomba mkurugenzi mkuu wa Sean woris entertainment ambao ndio wadhamini wakuu apande
jukwaani na kumkabidhi Miss Tanzania funguo hizo.”
Petty woris mkurugenzi wa Sean woris entertainment akapanda jukwaani na bila kupoteza muda
akamkabidhi happy funguo za gari ambalo ni zawadi ya kwanza kwa miss Tanzania.Akiwa katika
tabasamu pana sana alipita jukwaani huku akizipunga funguo hewani .Kelele za kushangilia
zilisikika.
Baada ya zoezi hilo zikafuata burudani mbili kisha mashindano yakafungwa rasmi na taratibu umati
wa watu ukaanza kuondoka maeneo hayo ya Diamond jubilee kila mmoja akiwa amesuuzika vilivyo na
ushindi wa Happy kibaho.
Happy sasa alikuwa akipiga picha na watu mbali mbali huku akisongwa na waandishi wa habari
wakitaka kufahamu mawili matatu ingawa mkurugenzi wa Miss Tanzania alijitahidi kuwazuia kwani
Happy angefanya mkutano na waandishi wa habari hapo kesho lakini haikusaidia kitu.
Patrick ambaye alionekana kuchanganyikiwa kadiri muda unavyosonga alitoa simu yake na kuanza
kubonyeza namba kisha akajitenga na akina Andrew ambao kwa sasa walikuwa wamesimama wakijiandaa
kuondoka.Patrick aliitumia njia ile ya kujifanya anapiga simu ili aweze kuondoka mahala pale bila
kutiliwa mashaka kwani lengo lake kuu lilikuwa kujaribu kupata nafasi ya kuonana na Happy.Andrew
alielewa mara moja nini kilichokuwa kikiendelea akawaomba waondoke mahala pale waelekee katika
magari.Lengo lilikuwa kuwatoa wasiwasi akina Vero.
Patrick sasa alikuwa akipigana vikumbo na waandishi wa habari ambao walikuwa wakichukua picha na
kumuuliza Happy maswali mawili matatu.Alijitahidi sana kupenya na hatimaye akajikuta yuko mahala
ambako anaweza kumuona Happy kwa ukaribu.Jasho lilikuwa likimtiririka na moyoni alikuwa na wasi
wasi mwingi lakini hii haikukumkatisha tamaa azma yake ya kuonana na Happy.Alikwisha azimia
hivyo.Alijisogeza taratibu na hakuna mtu yeyote aliyeweza kuwa na shaka naye kuwa si mwandishi wa
habari tena toka katika chombo cha habari kikubwa hapa nchi au nje ya nchi kutokana na muonekano
wake.
“Hongera sana Happy madame Tanzanie”Alisema Patrick wakati huo akiwa uso kwa uso na Happy.Happy
kwa wakati huo hakujua aliyekuwa akiongea naye .Alijua wote ni waandishi wa habari.Lakini neno
lile “Madame Tanzanie”linamstua na kumfanya ainue uso wake na kumtazama vizuri mtu yule aliye mpa
salamu ile.Kwanza alihisi sauti ile ni kama si ngeni masikioni mwake .mbele yake alikuwa amesimama
kijana nadhifu akiwa ndani ya tabasamu lenye kuonyesha aina Fulani ya wasi wasi.macho yake
yakakutana na macho ya Patrick na kwa kasi ya umeme kumbukumbu ya ghafla ikamjia kichwani
“Noooooo!!!!!!!!!!! Pa………..t…………….”
Akaanguka na kupoteza fahamu.
Kizaa zaa cha ghafla kikatanda hapo ukumbini.Kwa sekunde kadhaa ikatokea taharuki kubwa.Kila mtu
akapatwa mstuko kwa kitendo cha Miss Tanzania kupoteza fahamu ghafla.
Haraka haraka mabaunsa wakamwinua na kumkimbiza katika gari la wagonjwa ambalo lilikuwa limepaki
nje tayari kabisa kwa dharura kama hii.Kwa kasi ya ajabu gari lile likaondoka kuelekea Hospitali.
Watu waliokuwa bado wako ukumbini hawakuamini kilichotokea ghafla .Waandishi wa habari
wakalichukua tukio lile kama lilivyotokea.
Patrick nusura akili imruke kwa kitendo cha happy kupoteza fahamu.Taratibu alihisi kuishiwa nguvu
lakini tayari Andrew alikuwa ameshafika ,akamshika mkono na kumtoa nje ya ukumbi .
Saa kumi na moja asubuhi miss Tanzania Happy alizinduka.akaangaza huku na huku akatambua kuwa
alikuwa hospitali.Taratibu akaanza kukumbuka kilichotokea na kumfanya awepo pale mida
ile.Akalikumbuka tukio zima lililotokea usiku.
“Ooooh that’s him”Happy akajikuta akiongea kwa sauti na kuwastua watu waliokuwemo mle
chumbani.Miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatilia kwa karibu hali ya Happy ni mdogo wake Margreth
.Alikuwepo pia mkurugenzi wa Miss Tanzania pamoja na watu wengine kadhaa.Mara tu walisikia kuwa
ameamka mkurugenzi wa Miss Tanzania alimwita daktari ambaye alikuja na kumpima.Baada ya vipimo
vyote kuonyesha hakuna tatizo zaidi ya mstuko wa kawaida daktari alimuomba Happy aendelee
kupumzika na asibughudhiwe.Daktari akawaomba wote waliokuwa pale Hospitali kwa ajili ya Happy
waende kupumzika na kumwacha mgonjwa apumzike kwani bado alihitaji mapumziko ya kutosha.Ni
margreth pekee ndiye aliyebaki ili kumsaidia dada yake.Baada ya watu wote kutawanyika Happy
akageuza kichwa na kumwita margreth.
“my sister Pole sana”alisema Magie
“I’m ok magie.Magie I saw Patrick yesterday”
“Whaaaaat!!!!!!!!!!!!!!!!”akauliza margreth kwa mstuko.
“Sister are u ok?Magie akauliza tena.
“Sina tatizo magie ni kweli nilimuona jana wakati nikiongea nawaandishi wa habari alikuja mbele
yangu na kunisalimu .Alitaja kitu Fulani ambacho kilinifanya nistuke na nilipomtazama vizuri
alikuwa ni yeye.Nina hakika ni yeye kwani ni mtu ambaye yuko moyoni mwangu kwa miaka mingi na kila
siku ninaangalia picha yake hivyo siwezi kuwa nilifananisha.Ninaamini nilimuona Patrick na ndio
maana nikastuka hadi kupoteza fahamu.I’m confused Maggie .Totaly confused.”
Kimya kikatanda mle chumbani .
“Margreth tafadhali usije mwambia mtu yeyote juu ya habari hii.”
“Usijali sister siwezi sema”
“Sasa magie naomba unisaidie.”Akasema Happy .
“Nikusaidie nini dada”
‘nataka kuonana na Patrick”Alisema Happy huku macho yake yamefunikwa na machozi.
“Pumzika kwanza sister ukitoka Hospitali tutaongea kwa undani juu ya suala hili.Kwa sasa bado
unahitaji mapumziko ya kutosha na uhitaji kuwaza sana juu ya suala hili.”
“Thanks Maggie I understand “
mara mlango wa chumba alimolazwa Happy ukafunguliwa wakaingia wazazi wa Happy ambao walikuwa
safarini lakini kutokana na matatizo aliyoyapata mtoto wao ikawabidi waahirishe safari yao na
kurudi Tanzania haraka.mama yake akamkumbatia huku machozi yakiwatoka wote .baada ya kusalimiana
Happy akawahakikishia kuwa kwa sasa alikuwa akijisikia mzima kabisa na pengine mchana wa siku
hiyo angeruhusiwa kurudi nyumbani.
Wakiwa katika maongezi akaingia muuguzi akiwa na sinia la dawa.akawaomba radhi wote waliokuwa mle
ndani kuwa alihitaji kumuhudumia mgonjwa hivyo akawaomba watoke nje japo kwa dakika
kadhaa.alipohakikisha wote wametoka akamkaribia Happy .
“Samahani dada Happy ninaujumbe wako ambao nimeambiwa ni wa muhimu na nyeti sana .Aliyenipa
ujumbe huu amenionya kwamba nisikupe mahala penye watu .”
“Nani aliyekupa ujumbe huu?
“simfahamu ila ni kijana mmoja alikuwa amevaa suti ya nyeusi na hakujitambulisha jina lake .yeye
alisema ukishausoma tu utakuwa umefahamu.”
Yule nesi akatoa bahasha toka katika mfuko wake wa koti na kumpatia.baada ya kumpatia dawa muuguzi
yule alitoka na kumwacha Happy jasho likimtiririka.Hakujua ni nani aliyeleta ujumbe ule.
Aliishika bahasha ile na kuifungua taratibu.Ilikuwa ni kadi nzuri iliyomtakia uponaji wa
haraka.Ndani ya kadi ile kikaanguka kikadi kidogo .Akakiokota na kukisoma.Nusura apatwe na wazimu
baada ya kuisoma kadi ile.Margreth akaingia mara akastukia dada yake amesimama ghafla na
kumkumbatia.
“dada kuna nini?akauliza margreth kwa mshangao.
“Its Patrick”
“Patrick !!!!!!!!!!!!!!!”
“Yes .Look at this” akasema Happy akimuonyesha Margreth ile bussines card
“Mhhh”margreth akaguna
Wakati margreth akiisoma ile kadi mlango ukagongwa na likaingia kundi la warembo.wote wakafurahi
baada ya kumkuta Happy ni mwenye furaha namna ile.
**************************************************************
MISS TANZANIA AZIMIA JUKWAANI,HAPPY KIBAHO MISS TANZANIA MPYA,ZENGWE LATAWALA UKUMBINI MISS
TANZANIA AZIRAI,Hi vyo vilikuwa ni baadhi ya vichwa vya habari vilivyotanda katika magazeti mengi
kwa siku hiyo.Karibu magazeti yote yalijaribu kuandika kwa kina juu ya tukio la kuzimia kwa miss
Tanzania ukumbini,lakini hakuna hata gazeti moja lililoweza kuandika au kuufahamu ukweli juu ya
tukio lile.
Akiwa katika kibanda cha kuuzia magazeti asubuhi hiyo Andrew alinunua karibu kila gazeti
lililotoka siku hiyo na kupitia habari ya kuanguka kwa Happy .Lengo lake kubwa ni kutaka kufahamu
kama kuna mtu yeyote aliyeweza kumtilia shaka Patrick kuwa ndiye aliyekuwa chanzo cha tukio lile
la kuanguka Happy ukumbini.katika magazeti yote hakukuta habari yoyote iliyomuhusisha Patrick na
tukio lile.
Akatoa simu yake na kumpigia Patrick.
“Hallo shemeji”Simu ikapokelewa na Vero.
“Shemeji mambo vipi?habari za toka jana ?Andrew akauliza
“nzuri tu shemeji”
“Vipi jamaa bado kalala?
“Ameingia maliwatoni kidogo anakuja sasa hivi”
Muda huo huo Patrick akatokea Vero akampa simu na kumwambia Andrew anahitaji kuongea naye.
Hallow Andrew vipi?Alisema Patrick
“Poa Patrick vipi maendeleo lakini?
“Nashukuru Mungu Andrew naendelea vizuri.Hebu nipe habari’
“Habari ni ndefu kidogo lakini kwa ufupi tu ni kwamba leo sijalala kabisa.baada ya kuachana pale
ukumbini nikamrudisha Vick kwake halafu nikaanza kufuatilia Happy alipelekwa hospitali gani.Kwa
msaada wa rafiki yangu mmoja nilifanikiwa kujua mahala Happy alikopelekwa.Unajua walificha juu ya
mahala alikopelekwa Happy kwa sababu ya kuwakwepa waandishi wa habari.Alikuwa amepelekwa katika
hospitali moja ya kanisa maeneo ya msasani.Mpaka saa kumi na mbili nilikuwa pale hospitali na
ndipo nilipopata taarifa kuwa tayari Happy alikuwa amezinduka.Kuna nesi mmoja anafahamiana na
Vick pale na ndiye huyo aliyenipa msaada mkubwa sana.Nilimpa kiasi Fulani cha pesa yule nesi na
kumuomba aipeleke business card yako kwa Happy na kumwambia apige namba zile zilizoandikwa katika
business card hasa muda wa mchana.Yule nesi akajitahidi na kuifikisha kadi ile .Baada ya
kuhakikisha tayari ameipata mimi nikaondoka.Kabla sijafika nyumbani nikaona nipite kwanza katika
kibanda cha magazeti ili nione magazeti yanasema nini lakini hakuna chochote kibaya.Kwa hiyo
Patrick nina imani muda wowote Happy anaweza akakupigia simu.Mimi kwa sasa nakwenda nyumbani
kupumzika tutaonana baadae ila be carefull brother’
Patrick akavuta pumzi ndefu kisha akasema
“Sijui hata nikushukuruje Andrew kwa kitu ulichokifanya ila nasema thanks a lot.Dont worry I’ll be
careful.Bye see you later”
Patrick akakata simu kisha akaelekea jikoni ambako Vero alikuwa akiandaa stafstahi .alianza
kumsaidia Vero kuandaa mlo wa asubuhi kitendo ambacho Vero alikifurahia sana nakuamini tayari
Ptrick alikuwa amerudia hali yake ya kawaida.
Saa sita kamili mchana Happy akaruhusiwa kutoka hospitali.akiwa na furaha isiyokifani huku
ameongozana na mama yake pamoja na mdogo wake kipenzi Margreth bila kumsahau mwenyekiti wa kamati
ya Miss Tanzania akiwa na wajumbe kadhaa wa kamati hiyo pamoja na ujumbe wa watu toka sean woris
entertainment ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo walilakiwa na kundi kubwa la warembo
waliokuwa wakisubiri atoke kwani walikwisha taarifiwa kuwa angeruhusiwa mchana.Walitumia kama robo
saa kusalimiana na kupongezana vile vile kupeana pole kwa yaliyotokea. Kisha akapanda gari na
kuelekea nyumbani kwao.Happy alikuwa ni mwenye furaha sana mchana huo.Ni margreth pekee ndiye
aliyefahamu siri ya furaha ile aliyokuwa nayo dada yake.akiwa garini Happy akafumba macho kana
kwamba amelala lakini alikuwa amezama katika mawazo na mara akajikuta akitamka kwa sauti.
‘Thanks God I found him’
mama yake aliyekaa kiti cha mbele aligeuka na kumuangalia mwanae bila kusema kitu.
Margreth yeye alikuwa katika lindi la mawazo na hasa akijaribu kuvuta taswira ya kinachoenda
kutokea huko mbeleni.Anafahamu wazi kuwa katika dunia hii Patrick ndiye mwanaume pekee ambaye
Happy anampenda .Licha ya kupotezana kwa muda mrefu lakini bado taswira ya Patrick haikufutika
moyoni mwake.Kwa sasa Happy tayari ana pete ya uchumba ambayo amevishwa na mchumba wake ambaye
ni mmarekani mweusi aitwaye Mike cambel anayefanya kazi katika ubalozi wa Marekani hapa
nchini.Mike ni kijana anayependwa sana na kila mtu katika familia ya akina Happy .Pamoja na kuwa
na pete ya uchumba kidoleni bado Happy ameshindwa kuifuta kabisa kumbukumbu ya Patrick moyoni
mwake.Kuonekana kwa Patrick ni wazi kunaweza kusababisha mvurugano mkubwa ambao ni ngumu kujua
hatma yake.Ni wazi Mike alikuwa akimpenda Happy kupita maelezo.Hiki ni kitu kilichomuumiza sana
kichwa Margreth.
Baada ya mzunguko mrefu hatimaye wakawasili nyumbani ambako walilakiwa na kundi jingine la
warembo,ndugu jamaa marafiki na waandishi wa habari wote walifika kumpongeza na kumpa pole Happy
.Kisha salimiana na kupongezana Happy akaomba aachwe kidogo apumzike.
Happy akaoga na kupata chakula kisha akaingia chumbani kwake kupumzika.Kitu cha kwanza kabisa
ambacho alikifanya ni kuitazama tena ile business card kwa makini .akaichukua simu yake na
kuandika namba zile zilizoandikwa pale juu kisha akapiga.Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda kwa
kasi ya aina yake.Mikono ilianza kuloa jasho kwa wasi wasi.Hakujua angeongea nini baada ya
kuisikia sauti ya Patrick.Hakujua Patrick angekuwa katika hali gani mara atakapoisikia sauti
yake.Wakati akisuburi kujibiwa na sauti ambayo aliamini moja kwa moja ingekuwa ni ya Patrick
akasikia kitu ambacho hakukitarajia.Ilikuwa ni sauti ya mwanamke ndiye aliyepokea simu ile ya
Parick.
“hallow”Ilita sauti ya upande wa pili.
Happy mikono ilimtetemeka,akapatwa na kigugumizi cha ghafla kilichomfanya ashindwe kuongea.
“hallow nakusikia”Iliuliza tena ile sauti ya mwanamke.
Happy akashindwa ajibu nini akabaki ameiweka simu sikioni.
“Haloo nani mwenzangu?Iliuliza tena..Tayari Happy chozi lilikuwa likimtoka.Mara akasikia simu
ikikatwa.Kitendo kile kikamuuma akajitupa kitandani machozi yakimtoka.
“Oooh Lord why me???Why me God?I love Patrick .Yes ni yeye tu ndiye mwanaume ninayempenda kwa
dhati ya moyo wangu .Nimetengana naye muda mrefu sana na sielewi maisha yake kwa sasa.nadhani
anaweza kuwa na mke au girlfriend.Sielewi kama ninaweza vumilia nikisikia Patrick anamke.I’m her
only girl.Yes I know that.I know he loves me very much.’
Happy alikuwa kijisemea peke yake kwa sauti ndogo
“Patrick I’ll fight for you and I must win you back.You are mine Patrick .I lost you once and now
I’ve found you I’ll never loose you again”
Happy alikuwa akiongea peke yake maneno haya huku machozi yakimchuruzika.
Patrick leo huamki?alisema Vero huku akimtingisha Patrick ambaye alikuwa amelala tangu alipokula
chakula cha mchana.Patrick akajigeuza na kuangalia saa kubwa ya ukutani.Ilionyesha ni saa kumi na
moja jioni.
“Oh nimelala sana”
“Ni vizuri hata hivyo ukipata mapumziko ya kutosha”
Happy akaelekea jikoni akaleta juice na kummiminia Patrick katika glasi.
“Halafu nimekumbuka kuna mtu alikupigia simu nikaipokea lakini cha ajabu hakutaka kuongea kitu
chochote .Nimemuuliza zaidi ya mara mbili yeye ni nani lakini hakunijibu.”
Patrick moyo ukamruka.Kijasho kikaanza kumtoka .akaichukua simu na kuziangalia namba zilikuwa ni
ngeni kabisa kwake.Hakufahamu zilikuwa ni namba za nani lakini akahisi huenda Happy ndiye
aliyepiga.Kwa mujibu wa maelezo ya Andrew ni kwamba alimuelekeza Happy apige mida ya mchana.Bila
kukawia akaipiga ile namba.Simu ikailiita sana bila kupokelewa,ikakatika.Akapiga tena mambo yakawa
ni yale yale.Akapiga kwa mara ya tatu simu ikapokelewa.
“Hallow”Ilikuwa ni sauti tamu sana ya mtoto wa kike.kabla Patrick hajaongea lolote simu
ikakatika.Patrick akaipiga tena na safari hii akaambiwa kuwa simu anayopiga haipatikani.
Patrick akaitupa s