Saa kumi jioni nikiwa maeneo ya Kimandolu nikielekea Usa river katika baa iliyotulia ya Roterdam garden mahala panapofanyika vikao vya harusi yangu.Wanakamati walichagua mahala hapa kutokana na utulivu wake kwani kuna bustani nzuri na hata huduma zake ni nzuri sana.Nikiwa maeneo haya ya Kimandolu gari ikienda taratibu kutokana na magari mengi kukaa pembeni ya bara bara kwa muda mrefu kwa kupisha misafara ya viongozi wa jumuia ya Afrika mashariki waliokuwa na kikao chao hapa Arusha.Siku zote kunapokuwa na mikutano ya namna hii jijini Arusha huwa kunakuwa na adha kubwa kwa watumiaji wa bara bara hii ya Moshi Arusha kwa sababu ndio bara bara kuu waitumiayo viongozi hawa wakitokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA.Simu yangu inaita naitazama na kukuta ni Mr Cheleo mmoja kati ya wanakamati.
“Haloo kaka” nikasema
“Haloo ,uko wapi? Sisi tumeshafika tunakusubiri wewe tu.”
“Niko njiani kaka si unajua leo njia ilikuwa imefungwa.hawa viongozi walikuwa wanaondoka.Ndani ya dakika kumi nitakuwa nimefika hapo Usa river.”
“Ok kaka tunakusubiri”
Hiki kilikuwa ni mojawapo ya kikao cha maandalizi ya harusi yangu inayotarajiwa kufanyika muda wa kama mwezi mmoja ujao.Harusi ambayo kila mmoja wa rafiki zangu alikuwa akiisubiri kwa hamu sana.Nimekuwa mchangiaji mzuri wa harusi za rafiki zangu na kuhakikisha zinafana safari hii walikuwa wamepania sana kufanya sherehe ya harusi yangu kuwa ya kihistoria.
Tulipofika maeneo ya madukani gari zikaanza kwenda kasi na dakika tano baadae nikawasili usa river katika baa tulivu ya Roterdam.Nikapaki gari na kuelekea bustanini.Nikawasalimia wanakamati na kuwaomba radhi kwa kuchelewa kisha kikao kikaendela.Kilikuwa ni kikao kirefu .
Wakati kikao kikiendelea nikachukua simu na kumtumia mpenzi wangu Emmy ujumbe mfupi.Kwa siku tatu nilikuwa na shughuli nyingi na sikupata hata muda wa kuonana naye.Tuna kawaida ya kuonana karibu kila siku.Kwa sasa emmy anasome digrii ya sheria katika chuo kikuu cha Tumaini makumira.Kila jioni huwa ana desturi ya kupita kwangu na hata kama sipo kwa kuwa ana ufunguo wa nyumbani kwangu huwa ananisubiri mpaka nikirudi tunakaa wote kisha namrudisha kwake.
“Hallow sunshine,niko kwenye kikao hapa roterdam.Baada ya kutoka hapa nitapita kwako.Missing you soooo much.” Huu ndio ujumbe mfupi niliomtumia Emmy kipenzi cha moyo wangu.
Tukaendelea na kikao.Baada ya kama robo saa hivi tangu niutume ule ujumbe mfupi wa maandishi kwa mpenzi wangu Emmy simu yangu inaita kuangalia zilikuwa ni namba za emmy.Nikainuka na kwenda mbali kidogo ili niweze kuongea anaye.
“Halloo Darling “Nikasema kimahaba.kwani ndivyo tulivyozoea wakati tunaongea simuni.
Nusura moyo unipasuke kwa mstuko pale nilipoisikia sauti nzitoo ya kiume ikijibu.
“Mwanaharamu wewe,mpenda wake za watu.Huna hata haya unamwita nani Darling? Kumbe ndio mchezo wako huo wa kudandia dandia wanawake wa watu.Leo nimekupata.”
Nilibaki nimeduwaa kwa sekunde kadhaa nisijue nini cha kusema.sikuelewa yule jamaa alikuwa akimaanisha nini.Huku nikitabasamu nikauliza
“Mbona sikuelewi wewe.Unasemaje? samahani kama simu zimeingiliana “
‘Simu hazijaingiliana we juha.We si ndio Wayne? Wayne mkotela….
“yah ndio mimi” Nikajibu huku mapigo ya moyo yakienda kwa kasi baada ya yule jamaa kulitamka jina langu
“ Wewe si ndio umemtumia Sarafina ujumbe wa maandishi sasa hivi ukisema unakuja kumuona ukitoka kwenye kikao?
“Mi nimemtumia ujumbe Emmy na sio sarafina”
“sasa sikiliza we mjinga….”Nilihamaki baada ya kuitwa vile lakini nikavumilia nimsikie alichotaka kusema
“Iwe ni huyo Sara au Emmy kama unavyojua lakini nakwambia kuwa huyu ni mke wa mtu na mimi ndio bwana wake.”..
“Unasemaje wewe??..Nikauliza kwa hamaki
“Hebu mpe Emmy simu yake haraka.Mpuuzi wewe” Nikasema tena kwa hasira
“Mpumbavu wewe hivi nikwambie mara ngapi Hakuna Emmy Huyu anaitwa Sarafina.Kama alikwambia anaitwa Emmy alikudanganya.Huyu ni sarafina na mimi ndio mumewe,mimi ndio ninayemlipia hii nyumba anayoishi na ni mimi ndio niliyemtafutia katzi pale AICC na baadae nikamtafutia nafasi ya masomo pale Makumira.Mimi ndiye ninayemlipia ada na kila kitu.Mimi ndiye ninayemuweka mjini.Nilikuwa nje ya nchi nilikuwa napata taarifa kuwa kuna mtu anatembea na mke wangu nikjua ni utani.Leo ndio nimegundua kuwa ni kweli”
“Mjinga mkubwa wewe,huna hata haya mimi ndio ninayemlipia Emmy ada zote za masomo na hata nyumba anayokaa mimi ndiye ninayempa pesa za kulipia.Na kwa taarifa yako mpumbavu wewe,sasa hivi tuko katika maandalizi ya harusi yetu na kesho jumapili kanisani wanasoma tangazo la kwanza la ndoa yetu.Hivyo nakuomba usijaribu kwa namna yoyote ile kuleta upumbavu wako “ Tayari hasira ilikwisha nipanda nikatamka maneno yale kwa hasira.
“Sikiliza we mjinga yaani pamoja na kukueleza kote huku bado hunielewi sasa Emmy huyu hapa hebu ongea naye”
Nikasikia akimpa mtu simu na kumlazimisha
“Hebu ongea na huyu mbwa mwenzako mweleze ukweli mimi ni nani na mkanye akome kuanzia leo kukufuata fuata la sivyo nitamuulia mbali ,hanijui mjinga huyu” maneno haya nikayasikia kwa mbali.Mara nikasikia kitu ambacho sikukitegemea kukisikia maishani mwangu.Niliomba ardhi ipasuke niingie ndani.Nilitamani nijimalize pale pale.sikuona thamani tena ya kuendelea kuishi katika dunia hii.
Niliisikia sauti ile tamu na nyororo iliyozoea kuniburudisha kila siku na kunifanya nione kama niko peponi,sauti amabayo niliamini ni sauti nzuri kuliko zote duniani,sauti ya mpenzi wangu,bibi harusi mtarajiwa Emmy.Huku akilia kwa kwikwi akatamka maneno ambayo yalinifanya niichukie dunia na watu wake na hasa wanawake.
“Wayne I’m sorry mi ni mke wa mtu,na ninaomba usiendelee tena kumtukana mume wangu”
Ilikuwa ni kama niko ndotoni nikazubaa kwa sekunde kadhaa kisha nikajikaza kiume na kuuliza tena.
“Emmy is that you??…….
“Yes Wayne tafadhali leave me alone.Usinipigie simu tena.Mi nina bwana wangu”
Machozi yalikuwa yakinitoka.Sikuamini kile nilichokisika.
“Please Emmy tell me ur Joking”Nikasema tena huku machozi yakinitoka.
“My name is not Emmy…..Akashindwa kuendelea alikuwa akilia.Yule jamaa akachukua tena simu
“Sasa umeamini we kijana.Tafadhali usiendelee kumfuata fuata sarafina.Kitakachokupata usje kumlaumu mtu………..”Akasonya na kukata simu
Nikahisi miguu ikiisha nguvu nikaakaa chini.
Christopher rafiki yangu mkubwa alihisi lazima nitakuwa na tatizo akanifuata .Akastuka baada ya kunikuta nimekaa chini.
“Wayne.. “Akaita nikamuangalia sikuwa na nguvu hata za kujibu.
“Wayne una tatizo gani?
Akawaita wanakamati wote wakaja mbio na kuanza kunipepea.Nikaletewa maji nikanywa.Dakika kama tano hivi nikaweza kuongea
“Take me home” Nikamwambia Chris
“Wayne una tatizo gani.Twende hospitali” Akasema Chris
“No take me home” Nikasema huku nikijaribu kuinuka.Wakanisaidia kutembea hadi garini kisha Chris akawasha gari na kuondoka kunipeleka nyumbani.
Picha mbali mbali zikawa zinakuja na kupotea.Nilihisi kama vile niko ndotoni .Chris aliendesha kwa kasi bila kunisemesha.Tulipofika maeneo ya sanawari nikafungua mdomo na kumwambia Chris.
“Nipeleke kwa Emmy” Chris alikuwa akipafahamu anapoishi Emmy hivyo tulipofika maeneo ya Ilboru akakata kushoto na moja kwa moja akaelekea nyumbani kwa Emmy.
Alisimamisha gari nje ya nyumba ya Emmy.Sikuongea kitu nikafungua mlango nikashuka garini.Mlinzi wa kimasai alinifahamu hivyo aliponiona wala hakunisemesha nikapita zangu hadi ndani.Chris naye alikuwa akinifuata nyuma.Nilisimama mlagoni na kusikia watu wakinong’ona kwa ndani.Nikakinyonga kitasa na kuufungua mlango.Sebuleni nilimshuhudia Emmy akiwa kifuani kwa baba mmoja mnene wakiwa katika mahaba mazito.Pale pale nikaanguka na kupoteza fahamu.
****************************************************************
Nilizinduka na kujikuta mahala nisipopafahamu.Nilikuwa katika chumba chenye harufu ya dawa.Ndani ya chumba hiki kulikuwa na watu kadhaa.Mtu wa kwanza kumtambua alikuwa Chris.
“Pole sana Wayne”.Akasema huku akinishika kichwa.”Tafadhali usiinuke , endelea kupumzika.’Muda huo huo akaja daktari akiwa ameongozana na manesi wawili,nikajua tayari hapa nipo hospitali.daktari akanipima kisha akasema
“Kwa sasa unaendelea vizuri.Itabidi ulale hapa leo ili tuendelee kukuangalia zaidi”
Sikuwa na ubishi ingawa sikuhisi kuumwa sehemu yoyote ile zaidi ya kichwa kuwa kizito mno.Daktari akatoa maelekezo kadhaa kwa wale manesi akaandika pia katika kijikadi flani hivi kisha akatoka.Pale mlangoni nilisikia akiongea kama na kundi la watu.na dakika hiyo hiyo watu zaidi ya ishirini wakaingia mle chumbani.Walikuwa ni wanakamati ya maandalizi ya harusi yangu pamoja na baadhi ya rafiki zangu.Walinipa pole nami nikawahakikishia kuwa niko salama wakanitakia usiku mwema wakaondoka.pale hospitali nikabaki na Chris
“Chris nini kilitokea mpaka nikaletwa hapa?
Chris akanitazama kisha akajibu
“Wayne ulianguka ukapoteza fahamu ,ikanibidi nikulete hapa katika hospitali hii ya tanki la maji .Usijali kila kitu kinakwenda vizuri.Daktari anasema kesho asubuhi atakuruhusu”
Niliposikia kuanguka na kupoteza fahamu ,ndipo nikalikumbuka tukio zima lililotokea.Ghafla fahamu zikinipotea tena.
Nilirejewa na fahamu baadae sikujua hata ni saa ngapi.Ukiacha yule daktari mmoja aliyekuwapo mida ile sasa walikuwapo watatu.hali hii iliniogopesha sana.Nikaogopa pengine hali yangu si nzuri.Daktari mmoja mzee mwenye miwani akanisogelea na kuniuliza
“Wayne unajisikiaje sasa hivi?…
“Najisikia safi tu ila kichwa ndio kizito sana.Nahisi kama kizungu zungu kwa mbali”
“Ok sawa.Hali yako inaendelea vizuri,vipimo vyote vinaonyesha viko sawa ila unachotakiwa kwa sasa ni kujaribu kutokuwaza kitu chochote kinachoweza kukusababishia ukapoteza fahamu kwa mara nyingine.Jaribu kupata mapumziko ya kutosha na jitahidi sana kutokuwaza…..”
Nilimtazama yule daktari sikuwa na jibu la kumpa.Nafikiiri hakujua kitu gani kilichonipata.Hakuyaelewa maumivu yaliyokuwa moyoni mwangu.
“Ok dokta nitajitahidi”.Nilisema huku machozi yakinilenga.
Madkatari na wauguzi wakatoka na kuniacha chumbani mimi na Chris.hawakutaka Chris aniache peke yangu kwa kuwa waliogopa pengine ningeweza kujidhuru.
Niliinuka na kukaa kitandani.Chris akanisaidia nikakaa sawa.
“Chris I hate the world”Nikasema kwa sauti ndogo
Chris akanitazama akasema.
“Wayne jitahidi upumzike.Usiwaze lolote kwa sasa.Everything will be ok”
“No Chris.Nothing is ok.Emmy lied to me…………………”Nikasema huku machozi yakinitoka.
“Don’t cry buddy,be strong” akasema chris huku akinipiga piga mgongoni
“ I loved her .I loved her Chris more than I love myself.Lakini ona kitu alichonifanyia…..Nitauweka wapi uso wangu mimi?.”.Uso wote ulijaa machozi.Iliniuma kupita kiasi.
“Wayne lala kwanza.Tutaongea asubuhi” Akasisitiza Chris.
“No Chris siwezi lala wakati mwanamke niliyempenda amenisaliti….why me????? Why this pain???”
“Ok brother let it out……let it out….”Akasema Chris.
“Emmy amenidanganya muda wote huu kumbe ana bwana wake….”
“what!!!!!!!!” Akahamaki Chris
“Yah! ana bwana wake.Ndiye yule tuliyemkuta amelala naye kwenye sofa pale sebuleni kwake.Kwa mdomo wake mwenyewe ameniambia nisimsumbue yeye ana mume wake na haitwi Emmy anaitwa Sarafina”
Chris akainuka na kuanza kuzunguka mle chumbani huku ameshika kichwa.
“Is this true brother”Akauliza
“Yah..kwa mdomo wake amenitamkia maneno haya….It hurt Chris it hurt so much.”
“Mwanaharamu huyu…….”Akasema Chris kwa hasira
“Kesho ndoa yetui inatangazwa kanisani kwa mara ya kwanza…….nikashindwa kuendelea.Nilishindwa kujizuia kuangusha machozi.
“Wayne its gonna be ok.Jitahidi ulale then kesho tutayaongea mambo haya.Usiwaze sana kilichotokea.Hii ni mitihani tu ya maisha”
Chris alijaribu kwa kila njia kunibembeleza ili niweze kuwa katika hali yangu ya kawaida lakini kwa hali halisi jinsi ilivyo ni ngumu sana.
Ni Jumatano ya wiki hii tumetoka kuandikisha ndoa kanisani na kesho tangazo la kwanza linaanza kusomwa.tayari maandalizi yote ya harusi yamekamilika .Nitauweka wapi uso wangu mimi.Niatawaeleza nini watu wanaoisubiri harusi yangu??Nitawaleleza nini wazazi na ndugu zangu? Simlaumu mtu.Emmy nilimchagua mwenyewe.Hakunichagulia mtu yeyote.Iwapo ningechaguliwa na wazazi au mtu mwingine , ningekuwa na kila sababu ya kuwatupia mzigo wa lawama wao kwa uchaguzi wao usiofaa.Lakini hili lilikuwa ni chaguo langu mwenyewe..Huu ni mzigo wangu na inanibidi nisimame kidete niukabili.Nilijilaza kitandani na sijui hata saa ngapi nilipata usingizi
Saa tano asubuhi tayari nilikuwa nyumbani kwangu maeneo ya majengo.Nilikuwa najisikia mzima wa afya isipokuwa kichwa ndio kilikuwa kikiniuma kwa mbali.Chris ndiye aliyenichukua hospitali na kunirudisha nyumbani.
Mpaka sasa hivi hakuna mtu mwingine alikuwa akijua nini kilichotokea na kupelekea kupoteza fahamu na kulzwa hospitali zaidi yangu na Chris.Sikutaka kuharakisha kuliweka wazi jambo hili gumu.Nilitaka kuacha kwanza akili yangu itulie.Nilikaa kidogo sebuleni ,halafu nikamwambia Chris aniache nikapumzike.
“Brother naomba nikapumzike,halafu tutaongea jioni.Ila tafadhali naomba usimwambie mtu yeyote nini kilichotokea..”
‘Ok wayne nenda kampumzike ila tafadhali don’t do anything stupid”Akasema Chris huku akitoa tahadhari kwani madaktari walimuonya asikubali kuniacha peke yangu kwa kuhofa pengine ninaweza kujidhuru.
“C’mon Chris,I’m not a kid.Haya ni mambo ya kawaida katika maisha.Let me have a rest then I’ll know what to do next.”
“Ok wayne..nitapita mchana kukuangalia.Nikuletee chakula gani mchana?
“Nothing Chris.Usiniletee chochote.I don’t feel like eating anything.”
“Unatakiwa ule Wayne.unatakiwa uwe na nguvu.”
Sikumjibu kitu nikamtazama na kuondoka kuelekea chumbani kwangu.
Nilikaa kitandani,nikalifungua kabati langu na kutoa albamu kubwa la picha.Humu kuna picha nyingi ambazo nimepiga na emmy tangu tulipoanza mapenzi yetu .Picha yetu ya kwanza mimi na yeye ikanikumbusha tulikwenda picnic Ziwa Duluti.Ni siku tuliyofurahi sana.Siwezi kuisahau siku hii.Nikaendelea na kuzifunua picha nyingine.Wakati nikiendelea na kuzitazama picha simu yangu inalia.Alikuwa ni mama yangu.
“mama shikamoo” nikamsalimu
“Marahaba baba ,hamjambo”
“hatujambo mama,vipi mnaendeleaje?
“Huku wote wazima.Ni baba yako tu ndio kichwa chake kile kinamsumbua sana lakini anaendelea vizuri”
‘Mpe pole sana “Nikajibu kwa ufupi.
“Vipi mkwe wangu hajambo?
Nikasita kujibu.
“eenh jamani hajambo mama mkwe? Mama akauliza tena baada ya kuona sijamjibu
“Hajambo mama”Nikajibu huku nikiuma meno kwa hasira.Mwanamke huyu amewadanganya hadi wazazi wangu.Iliniuma sana.
“nashukuru kama ni mzima.Vipi mnaendeleaje na maandalizi ya harusi?
“mama maandalizi ni mazuri.Tunaendelea vizuri”
“sawa baba.Leo huku wamesoma Tangazo la kwanza..Hivi ninavyokwambia watu wanajiandaa isivyo kawaida,kila ndugu anataka aje kwenye harusi yako.”
Sikuwa na cha kusema.Machozi yalikuwa yananitoka.
“Mama nashukuru.Nitakupigia baadae tutaongea vizuri zaidi”
“Sawa baba”
Nilikata simu na kuitupia kitandani.hasira zikanipanda.
“Damn you Emmy…..”
Nilizungunguka zunguka mle chumbani nikijaribu kuwaza na kuwazua bila kupata jibu.Nikatoka na kurudi sebuleni.Nikafungua kabati ninamoweka cd na kuchukua moja ya cd niipendayo sana ya mmoja kati ya wanamuziki mahiri kwenye mziki wa bongo fleva,Hamis mwinjuma au Mwana F.A .Huu wimbo wake niliona ni kama vile alinitungia mimi kwa sababu ulinihusu mimi.Ubeti wa pili ndio uliniumiza zaidi ukanifanya niurudie tena na tena
“hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?/
watu wana watu wao wengine toka zamani/
ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako/
wadogo usoni wanahifadhi wazee wako/
sijui ni dhiki au tamaa tu??/
watoto wanaanika njaa tu/
hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu/”
Mamneno haya yalinichoma moyo.Kijana huyu aliimba vitu vya kweli kabisa na yote aliyoyaimba yamenikuta mimi.
Nikarudi tena chumbani sikujua nini cha kufanya.Nilikuwa kama nimechanganyikiwa vile.Nikaona ni bora nijilaze kitandani na kijiusingizi kikanipitia.
Nilistuka na mlio wa simu iliyokuwa kichwani kwangu,alikuwa ni Chris.
“ Haloo” Nikasema
“Wayne umelala?”
“Yes nilikuwa nimelala”
“Ok sawa.sasa wayne naomba uwe na moyo mgumu na usihamaki tafadhali.Ni kwamba Emmy amenifuata na hapa nilipo niko naye na ni yeye ndiye alinisisitiza nikupigie simu hii.”
“Unasemaje Chris????? “Nikasema kwa ukali.Sikutegemea kusikia kitu kama kile.
“Wayne niko na Emmy hapa.amenitafuta na kuomba nafasi ya kuongea na wewe”
“Chris…………..”Nilidakia,sikutaka aendelee tana kunipa habari za yule baradhuli
“Chris tafadhali.Kama na wewe unataka tukosane hamna shida ila tafadhali naomba usinipe habari zozote kuhusu huyu mwanamke.”
Nikakata simu.Mwili wote ulikuwa unanichemka kwa hasira.Sikutaka kumsikia tena emmy katika maisha yangu.Nilikuwa na hasira mbaya mno kwa kitendo alichonifanyia na kama angekuwa karibu yangu sijui hata ningemfanya kitu gani.
“Hana haya mwanamke huyu.Kwa hiki kitu alichokifanya halafu leo anataka kuongea na mimi!! Aongee na mimi kitu gani? Kwanza si ana nguo zake humu .Zote nazipiga moto.Sitaki kumuona tena machoni mwangu huyu mwanamke.Amenifanyia kitendo cha kikatili sana.”
Nikalifungua kabati kwa hasira na kuanza kutoa ngo zote za Emmy.Nyingi nilimnunulia mimi mwenyewe na ni nguo za thamani kubwa.
“Nguo zote hizi nimegharamia malaki ya hela kumbe alikuwa akiniona mimi mjinga namna hii…….”
Nikazikusanya zote na kwa hasira nikaenda nazo katika shimo la taka taka na kuzichoma moto.Sikuondoka mpaka nikahakikisha zimeteketea kabisa kwa moto.
Nikarudi sebuleni na kuangalia kama kuna kitu chochote kinachoweza kumuhusu Emmy,nikaiskia geti linagongwa.haraka haaka nikafuta uso na kujiweka vizuri ili mtu asije gundua nilivyosawajika.
Nilifungua geti na kukuta ni rafiki yangu anaitwa Erasto.
“karibu Erasto “ilijilazimisha kuchangamka.
“Ahsante sana wayne”
“Nimekuja kukujulia hali ,niliambiwa na akina mangi jana ulipata matatizo ukalazwa hospitali” Akasema Erasto tukiwa tumekaa sebuleni
“tNdiyo,jana nilipatwa na matatizo tu ya mstuko nikaanguka na kupoteza fahamu.Ni mambo ya uchovu.Si unajua tena ,mambo yamekuwa meengi sana.” Nikadanganya.Sikutaka mtu yeyote agundue kilichotokea kati yangu na Emmy
“Du! Pole sana.lakini hivi sasa unaendeleaje?
“Kwa sasa naendela vizuri.Madaktari wamenipima na hakuna tatizo lolote,wameniomba niongeze muda wa kupumzika.”
Nilishukuru kwa erasto kuja kunitazama kwani kidogo kichwa changu kilitulia.Tuliongea na kucheka nikaona kichwa kinakuwa chepesi.Mida ya kama saa nane hivi Chris naye akaja akiwa amefungasha chakula,tukajumuika wote kula.Kwa masaa haya machache nilifarijika sana na kujiona kama vile sina matatizo.
Ilipata saa kumi na moja jioni tukiwa katika maongezi na rafiki zangu ,geti langu likagogwa.Nikainuka na kwend akumuona mgongaji.Nilistushwa na ujio usio wa kawaida wa mwalimu wangu wa dini.katekista Nzomola ndiye mwalimu wetu aliyetufundisha mafundishoya ndoa mimi Emmy na watu wengine kama nane hivi.
“Ouh Mwalimu,Shikamoo” Nikamsalimia kwa furaha,sikutaka kuonyesha aina yoyote ya mstuko kwa ujio wake.hajawahi kuja nyumbani kwangu hata mara moja.
“Marahaba Wayne.Habari za Jumapili?
“Nzuri katekista.”
“Leo sijakuona kanisani,hata mwenzio naye sikumuona “
“Leo sikuwa najisikia vizuri ndio maana sikuja.Si unajua mwalimu nyakati hizi mambo yanakuwa mengi “
Katekista akatabasamu.nikamkaribisha ndani.Nikamtambulisha kwa Chris na Erasto amabo baada ya kuona nimepata mgeni wakaaga na kuondoka.
“Ndio mwalimu karibu sana.hapa ndio nyumbani kwangu.”
“Ahsante nimeshakaribia.”
Kimya kikapita cha kama dakika moja hivi ,katekista akaanzisha maongezi
“Wayne nimekuja hapa ili tuzungumze juu ya matattizo yaliyotokea”
Kauli ile inanistua.
“Matatizo?” yapi hayo” ikauliza
“yaliyotokea kati yako na mwenzako”
“nani kakwambia kuna matatizo? Nikauliza tena
“Mwanzako amenifuata nyumbani .Tangu saa saba mpaka mida hii ndio tumeachana.Amekuja analia na kutaka tukae tuyaongee masuala haya”
Nilimtazama mwalimu yule kwa hasira mpaka akaogopa.
“Mzee Nzomola nakuheshimu mno kama mzee wangu,umenijenga sana kiroho.Lakini kwa hili lililotokea naomba usiingilie kabisa.Hakuna kitu tunachoweza kuongea hapa.Halafu mpaka hapa nilipo kichwa changu bado hakijatulia,bado nina hasira na hatuwezi kuongea lolote na tukafikia muafaka .Mzee wangu naomba uniache kwanza nitulie halafu kwa heshima yako nitakuita mimi mwenyewe tutakaa ,tutaongea.Usione kama nimekudharau mzee wangu ,hali niliyonayo sasa hatuwezi kuongea tukafikia muafaka.Niachie siku mbili tatu,kichwa kitulie halafu nitakutafuta mimi mwenyewe.Nakuahidi hivyo.”
Nashukuru mzee Nzomola alinielewa na akaondoka.
ilipoishia sehemu ya nne...
“wazee wangu nimewasikilza vizuri.Ujio wenu leo umenipa faraja sana.Sijui mmekuja na kitu gani lakini kwa kweli najiona mwepesi na mwenye furaha sana.Mmenisaidia kuutua mzigo mzito niliokuwa nimeubeba.Ahsanteni sana.Wazee wangu kwa kweli lililotokea ni pigo kubwa kwa moyo wangu.Nimeumia sana.Kwa kweli sikutegemea jambo kama lile kutokea kwa mtu kama Emmy tena kwa wakati kama huu.kama mzee pale alivyosema ni kwa maongozi ya Mungu niliamua kutumia busara zaidi katika suala hili.Sijamueleza mtu yeyote zaidi ya rafiki yangu wa karibu.Sikuwa na haraka ya kutaka kuutangazia ulimwengu nini Emmy kafanya.Sikutaka dunia imchukie.naamini kama mzee alivyosema ni tamaa za pesa ,mali na vitu vizuri vizuri ndio ilmponza.Iwapo ningeamua kumdhalilisha Emmy kwa kutangaza aliyoyafanya ,nisingekuwa nafanya hivyo kwake tu bali hata kwa wazee wake waliomlea katika madili mema,ndugu zake,ndugu zangu na hata wazazi wangu.Pamoja na yote yaliyotokea,machungu yote niliyoyapata,maumivu ya ndani na nje,bado ninathubutu kusimama nakutamka mbele yenu wazee wangu kuwa nimemsamehe Emmy na niko tayari kurudiana naye tena na mipango ya ndoa yetu kuendelea kama kawaida”
Hawakuamini ,wakanitaka nirudie tena kauli yangu.Nikarudia tena na kuwahakikishia kuwa Emmy nimemsamehe kwa moyo mmoja na wala sina kinyongo naye tena.
Wazee wakainuka na kuja kunipongeza.Kilikuwa ni kipindi cha furaha sana.Baada ya kupongezana baba yake mkubwa Emmy akasimama na kusema.
“Wayne wewe ni kijana wa ajabu .Katika kuishi kwangu mpaka nimefika uzee huu sijawahi kuona mtu mwenye moyo wa ajabu kama wako Wayne.laiti dunia ingekuwa na vijana 100 kama wewe basi pangekuwa ni sehemu nzuri sana kwa kuishi.Mimi binafsi sijui hata niseme kitu gani.Sijui hata nikushukuru vipi kwa ujasiri wa kumsamehe mwenzako.Narudia tena kijana unaongozwa na roho wa Mungu.Kwa ulimwengu wa sasa si rahisi mtu kumsamehe mwenzake aliyemfanyia kitendo kama alichokufanyia emmy.Ahsante sana kijana.ahsante sana wayne”
akanishika mkono tena.Akawageukia wazee wengine na kuwaambia kuwa ni wakati muafaka kwa Emmy kuitwa .Ikapigwa simu na baada ya kama dakika kumi hivi Emmy akaingia ndani.Moyo wangu ukastuka tena baada ya kuiona sura ya Emmy ikiwa na macho mekundu yaliyovimba ikiashiria jisni alivyokuwa akilia.hakutaka kuniangalia usoni.Uso wake alikuwa kuinamisha chini.Nilishindwa kuwa na hasira nikamuonea huruma.
ENDELEA.......................................................................................................
Baba mkubwa wa Emmy akasimama na kuongea machache.
“Kijana wetu Wayne,na ndugu wote ambao mko hapa leo,napenda kuchukua nafasi hii kuongea machache kwa sababu mengi yamekwisha semwa na nisingependa kuyarudia tena.Tumemsikia kijana wetu alivyosema.Toka ndani ya moyo wake amekubali kumsamehe Emmy .Kwa kuwa kijana wetu Wayne si mtenda kosa basi hatuna budi sasa kumpa nafasi mtenda kosa yeye mwenyewe kwa mdomo wake akiri kosa na kuomba msamaha kwa mchumba wake,wazazi wake na kwa Mungu wake.Emmy uwanja ni wako ,waangukie wazazi wako uwaombe msamaha pamoja na mchumba wako”
Kimya kikatanda mle sebuleni.Emmy huku akilia akainuka na kwenda kupiga magoti mbele ya baba yake na kulia akiomba kusamehewa.Baba yake akamshika kichwa na kumuombea kwa Mungu amsamehe na kumtangulia katika kila jambo alifanyalo,halafu akatangaza kuwa tayari amemsamhehe mwanae kwa kosa alilolifanya.Emmy akaenda tena kwa mama yake na kuomba msamaha kama alivyofanya kwa baba yake.Naye halikadhalika akamsamehe.Kazi ikawa kwangu.Akasita kuja kwangu pale tulipogonganisha macho.Nadhani ni nafsi yake ilikuwa ikimsuta kwa mambo aliyoyafanya.Wazee wake wakamuangalia kwa ukali hali iliyomlazimu kujikaza kisabuni na kunisogelea.akapiga magoti mbele yangu na kunishika miguu.
“Wayne, nakosa hata neno la kusema.Nashindwa nikwambie kitu gani cha kuweza kulifuta doa nililoliweka moyoni mwako kwa tamaa zangu.Nimekuumiza Wayne,na sistahili hata huruma yako.lakini pamoja na hayo yote niliyokufanyia naomba ufahamu kitu kimoja kuwa toka ndani ya moyo wangu bado nakupenda sana na ninaomba msamaha wa dhati kabisa .Naomba unisamehe na tuendelee na mipango yetu ya ndoa kama tulivyokuwa tumepanga.naahidi sintafanya tena kosa kama hili katika maisha yangu.nakuahidi kuwa mke mwema kama utanisamehe.naomba msamaha wako Wayne..”
Emmy macho yalikuwa yamejaa machozi,akilia kwa kosa alilokuwa amelifanya.Hata mimi ilikuwa ikiniuma sana na nilikuwa nikijiuliza mara mbili mbili kama ni kweli nimeamua kwa dhati kumsamehe? Nikakubaliana na moyo wangu kuwa nikubali kumsamehe.Nikamshka mkono nikamuinua na kumtazama usoni.
“Emmy,nakubali ulinikosea.Lakini kama tunavyofundishwa kila siku nav iongozi wetu wa dini na kama maandiko yanavyosema kuhusu kusamehemana,mimi kwa moyo wangu wote nimekubali kukusamehe.Nakuombea kwa Mungu naye akusamehe na tuendelee na mipango yetu ya ndoa kama kawaida “
Maneno yale machache yakampa Emmy faraja kubwa na kumfanya ainuke na kunikumbatia kwa furaha.Sebule yangu ikageuka sehemu ya furaha kubwa.Watu tukashikana mikono na kupongezana.Lilikuwa nitukio kubwa na la kihistioria katika maisha yangu.Vinywaji vikaletwa tukaendelea kuburudika hadi ilipotimu saa mbili za usiku tukaagana wakaondoka.Walipoondoka nikabaki mwenyewe nikitafakari juu ya kilichotokea.Pamoja na kumsamehe Emmy lakini bado roho yangu haikuwa ikimtazama kama nilivyokuwa nikimtazama hapo zamani.
“Hivi ni kweli roho yangu imekubali kwa dhati kumsamehe Emmy kwa kitu alichonifanya?? Nikajiuliza tena kwa mara ya pili.Saa chache zilizopita sikutamanai kkumuona tena Emmy katika maisha yangu kuokana na kitendo kile lakini sasa nimeaua kumsamehe.
“Kwa vile nimamua kumsamehe acha tu nimamehe.Nahisi amekiri toka moyoni mwake.”Nikajisemea mwenyewe.
Maisha mapya yakaanza tena.Penzi letu likaonekana kama vile limechipua upya.Upendo ukaongezeka mara dufu.Enmmy alionekana kuba