Mama: Mwanangu hebu mpigie simu baba yako mwambie chakula tayari.
Mtoto: Sawa mama
Basi mtoto akampigia simu babayake lakini hakumpata
Mtoto: Mama simpati
Mama: Basi subiri kama baada ya dakika tano mpigie tena inawezekana ni mambo ya network hayo.
Baada ya dakika tano mtoto akampigia tena baba yake
Mtoto:Mama mimi baba simpati simu yenyewe anapokea mwanamke
Mama: kha! sawa mwanangu niachie mimi hili suala wewe nenda kale.
Baada kama ya dakika30 baba akabisha hodi akakaribishwa na bonge la kibao hajakaa vizuri akapigwa na sufuria mara mwiko ikawa ni balaa kwa kwenda mbele mume akazidiwa mara majirani wakaja kuamulia ugomvi,lakini majirani walipofika wakakamkuta mume yuko chini ya sofa hoi bin taabani
Mama: Hivi we wa kunifanyia mimi hiviyaani unakwenda kwa wanawake zako na kuniacha mimi hapa nyumbani? mwanangu hebu waambie majirani yule mwanamke alipo pokea simu alisemaje?
Mtoto: Alisema simu uliyopiga kwa sasa haipatikani jaribu tena baadae!
.............................
NICE WAYS OF ANSWERING BORING QUESTIONS.
-1st Q: Unaenda tao na hii mvua?
A: Hapana. Naenda na ile ingine!
-2nd Q: Kwani umesuka nywele?
A: Hapana. Nime'change kichwa!
-3rd Q: Kwani gari imeanguka?
A: Hapana. Ni dere' amei'park upside down!
-4th Q: How was ua night?
A: Sijui. Nilikuwa nimelala!
-5th Q: Hio gazeti ni ya leo?
A: Hapana. Ni yangu!
-6th Q:(H.O.D.) Umemwona prefect?
A:(student) Hapana. Sikuwa namtafuta!
-7th Q: News za leo zinasemaje?
A: Sijui. Sijaongea nazo!
..............................
MTEJA MFALME
Jamaa kapata kazi ya kuuza duka, siku
moja bosi wake kaingia ghafla dukani
kakuta ubishi mkali na kijana wake
anamtukana mteja. Akaamulia ugomvi,
mteja akaondoka;
MWENYE DUKA: Leo mi nakufukuza kazi,
mara ngapi na kuambia kuwa mteja ni
mfalme na analosema mteja ndio sahihi?
Kamwe usimbishie mteja, anachosema
wewe kubali, kwani utapata kovu gani
ukikubali?
JAMAA: Mteja yule kaja hapa akaanza
kusema mwenye duka hili, punguwani
hana akili
...........................
Panya alimeza kipande cha dhahabu mwenye
dhahabu akachanganyikiwa na kuamua
kumkodi mpelelezi mmoja ili aje amuue
panya aliyemeza dhahabu.
Mpelelezi alipofika alikuta panya zaidi ya 500
lakini alishangaa kumuona panya mmoja
kajitenga,ndipo alipomkamata na
kumuua,alipompasua akakuta kipande cha
dhahabu akamkabidhi mwenyewe.Yule
jamaa alipigwa na butwaaa huyu mpelelezi
alimjuaje yule panya ikabidi amuulize.
Jamaa:aisee we mkali,ulijuaje kama huyu
ndiye panya aliyemeza dhahabu?
Mpelelezi:- hawa panya nao ni kama raia
Watanzania wakiwa na mali hujitenga na
wenzao.
.............................
NAUZA DUNIA
MLEVI 1: Mi naweza kukununulia dunia
MLEVI 2: Huwezi
MLEVI 1: Nasema NAWEZA
MLEVI 2: Huwezi kwa sababu siuziiii
.......................
NILIKUWA NAKOJOA KISIRISIRI
Mlevi alikuwa anakojoa kando ya barabara,
mgambo akamzukia;
MGAMBO: We acha kukojoa funga zipu haraka.
Mlevi akafunga zipu haraka, mgambo akaondoka.
Mlevi akaanza kucheka
JIRANI: Sasa unacheka nini? MLEVI: Mi mtoto wa mjini bwana, yaani
nimemdanganya mgambo hivihivi?
JIRANI: Umefanya nini?
MLEVI: Nimefunga zipu lakini nikaendelea kukojoa
kisiri kwenye suruali mpaka nimemaliza,
na yule fala wala hakutambua.
...........................
Dongo janja alitumwa dukani na mama yake
kwenda kununua njegere. Akiwa njiani njegere
moja ilidondoka ikabiringika.
Alipoona hivyo akasema,
"Ahaa, kumbe mnajua kutembea!"
Akazimwaga zote chini huku akisema, "mimi natangulia mtanikuta nyumbani"
Alipofika nyumbani akaulizwa na mama yake,
"njegere ziko wapi?"
Naye akajibu,
"zipo njiani zinakuja!"
Mama akabaki domo wazi!
.........................
DAH KUMBE SINA KISUKARI
ASANTE
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu
naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?....Mzee akatoa
kichupa na kijiko akaweka majimaji
yaliyomo kwenye kichupa kwenye kijiko
na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia
akatia yale maji mdomoni na
kuyazungusha zungusha mdomoni
akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au
chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano
nashukuru sana, dokta alinambia nipime
mkojo wangu kama ninakisukari, kumbe
sina asante bwana mdogo
.......................
MSHTAKIWA UMESEMAJE?
HAKIMU: Mahakama imekuona huna hatia
uko huru,
MSHTAKIWA: Nakushukuru sana bwana
hakimu nakuhakikishia sitarudia tena kosa
hili
...................
Mteja na Muuzaji.
Mteja:naomba chakula cha mbwa
Muuzaji:yuko wapi mbwa wako?
mteja:yuko nyumbani
Muuzaji:utanisamehe duka letu huwa
hatuwauzii wateja chakula cha mbwa bila ya
kumuona mbwa.
Zikapita siku mbili na mteja akaenda tena
dukani.
Mteja:naomba chakula cha paka
Muuzaji:Yuko wapi peke wako?
Mteja:yuko nyumbani
Muuzaji:samahani huwa hatuuzi chakula cha
paka bila ya kumuona paka mwenyewe;
Zikapita kama siku mbili mteja akaenda na
mfuko wa plastiki mpaka pale dukani;
Mteja:ingiza mkono wako ndani
Muuzaji:kwani kuna nini ndani?
Basi muuzaji akaamua kuingiza mkono
ndani ya ule mfuko
Muuzaji:kuna kuna kitu cha baridi?
Mteja:hicho ni kinyesi changu,nimekuja
uniuzie toilet paper.
..............
INAONEKANA WATANZANIA
MNAPENDA SANA TEMBO WENU
Askari wa wanyama pori alikutwa na
watalii katikati ya mbuga za wanyama
analia;
MTALII: Mbona unalia
ASKARI: Tembo kafa
MTALII: Hee ndio unalia hivi? Inaonekana
Watanzania mnapenda sana tembo wenu.
ASKARI: Hapana wamenipa kazi ya
kumchimbia kaburi na kumzika

No comments:
Post a Comment