Kipindi cha maswali na majibu kilimalizika katika kikao hiki cha nane cha mkutano wa nne wa bunge
la jamhuri ya muungano wa Tanzania.Maswali yote yaliyopangwa kuulizwa siku hii yalipata nafasi na
majibu muafaka toka kwa mawaziri husika.Kumalizika kwa maswali kukampa spika wa bunge Bi
Bernadetha makawala nafasi ya kusimama na kusema machache ikiwa ni pamoja na kutambulisha wageni
muhimu na kusoma matangazo mbali mbali ya kazi .WHITE HOUSE ROMANCE
Dakika takribani tano alizitumia katika kusoma matangazo ya kazi na kuwatambulisha baadhi tu ya
wageni waliohudhuria kikao hiki,halafu akamwita katibu wa shughuli za bunge siku hiyo ndugu Wilson
ndendeki aweze kuliongoza bunge kwa shughuli inayofuata.Akasimama na kutamka shughuli inayofuata
“Hoja binafsi za wabunge”
Baada ya kauli hiyo spika wa bunge akasimama na kutoa maelekezo mafupi.
“Waheshimiwa wabunge ,leo tutakuwa na hoja binafsi mbili.Ya kwanza inatoka kwa mheshimiwa mbunge
Romana salvatory inayohusu kufilisika kwa benki ya taifa ya vijana .Hoja ya pili inatoka kwa
mheshimiwa mbunge Marewa shawe inahusu uvunaji wa mazao ya misitu katika msitu wa Isambe..Kila
mtoa hoja amepewa muda usiozidi dakika sitini za kuwasilisha hoja yake.Kwa kuwa hatutakuwa na muda
wa kutosha wa kuanza kuzichangia hoja hii katika kipindi hiki cha asubuhi basi tutakaporudi mchana
tutaanza moja kwa moja kuchangia katika hoja zote mbili kwa pamoja.Kwa maana hiyo mnatakiwa muanze
kujiorodhesha kuchangia hoja hizi kuanzia sasa hivi ili tuone tutakuwa na wachangiaji wangapi
mpaka mchana.Naomba sasa nimwite mtoa hoja wa kwanza mheshimiwa Romana salvatory.Karibu sana
mheshimiwa” Spika akakaa katika kiti chake tayari kwa kuanza kuisikiliza hoja ya mheshimiwa
mbunge Romana mmoja kati ya wabunge vijana machachari mno .
Bunge lote lilikuwa kimya kabisa wakimsubiri mhesimiwa mbunge ainuke.Mheshimiwa Romana alikuwa
ameinamia meza yake bila kustuka hali inayomlazimu spika kusimama tena.
“Mheshimiwa mbunge ,tafadhali karibu uwasilishe hoja yako.”
Pamoja na mwito ule wa spika bado mheshimiwa mbunge alikuwa ameinamia meza yake.Wabunge wote
wakageuza vichwa vyao kumuangalia mheshimiwa mbunge yule kijana huku wengine wakidhani labda
amepitiwa na usingizi.Minong’ono na vicheko vya chini chini vikaanza kusikika..Spika akasema
“Waheshimiwa wabunge mlio karibu naye hebu tusaidieni kumstua hapo “
Mheshimiwa Salama awadh mbunge wa viti maalum akainuka na kwenda kumstua.Akamshika bega na
kumtikisa kidogo,lakini bado mheshimiwa mbunge hakuamka,akampiga piga mgongoni lakini bado
hakuonyesha dalili zozote za kustuka ndipo alipoamua kumuinua kichwa.Nusura aanguke kwa mstuko
alioupata.Mheshimiwa mbunge Roma alikuwa hana fahamu,jasho linamtiririka usoni na povu
mdomoni.Bunge lote linakumbwa na taharuki.Haraka haraka wabunge waliokuwa karibu wakamuinua na
kumtoa nje kumkimbiza katika zahanati ya bunge.Shughuli za bunge zikasimama kwa muda.Ni muda
mchache tu uliopita mheshimiwa mbunge Roma alikuwa mzima wa afya na alipata nafasi ya kuuliza
swali la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu,hakuonyesha dalili zozote za ugonjwa.Hali
iliyomtokea ilimpa wasi wasi kila mtu mle bungeni.
“Waheshimiwa wabunge naomba tukae…..” Ilikuwa ni sauti ya mheshimiwa spika akiwataka wabunge
watulie na shughuli za bunge ziweze kuendelea.Bado mazungumzo yaliendelea licha ya mwito ule wa
spika.
“Naomba utulivu ndani ya bunge tafadhali….waheshimiwa wabunge naomba tukae katika sehemu zetu ili
shughuli za bunge ziweze kuendelea.”
Taratibu wabunge wakaanza kurejea katika sehemu zao na mazungumzo yakapungua.
“Waheshimiwa wabunge,mwenzetu amepatwa na matatizo ya ghafla na amepelekwa katika zahanati yetu
ya bunge kwa huduma ya kwanza.Naomba tuwe watulivu wakati mwenzetu anapatiwa matibabu.Mtajulishwa
kila kitu juu ya maendeleleo yake baada ya uchunguzi wa kidaktari kufanyika.Kwa sasa naomba
shughuli za bunge ziendelee.Kwa kuwa mheshimiwa Roma ndiye aliyekuwa awe wa kwanza kuwasilisha
hoja yake asubuhi hii napenda sasa nimwite mheshimiwa Marewa aweze kuwasilisha hoja yake.Hoja ya
mheshimiwa Roma tutaipangia siku nyingine.Mheshimiwa marewa karibu uwasilishe hoja yako”
****************************************************************
Zahanati ya bunge ghafla ikageuka sehemu ya heka heka .Madaktari wa bunge walikuwa wakijitahidi
kwa kila walivyoweza kumpa huduma ya kwanza mheshimiwa Roma .Vipimo vya awali vilionyesha kuwa
shinikizo la damu lilikuwa juu isivyo kawaida na hata sukari ilikuwa imepanda mno.Pamoja na
jitihada zote za madaktari wa bunge bado hali ya mheshimiwa mbunge iliendelea kuwa mbaya
,ikamlazimu daktari mkuu wa bunge aamuru mheshimiwa spika aitwe.
Akiwa mezani kwake huku mheshimiwa mbunge Marewa shawe akiendelea kuwasilisha hoja yake,mhudumu
wa bunge akampelekea ujumbe wa kumtaka afike mara moja katika zahanati ya bunge.Bila kupoteza hata
sekunde spika akasimama na mheshimiwa aliyekuwa akiendelea kuwasilisha hoja yake akanyamaza
kumpisha spika wa bunge.
“waheshimiwa wabunge,nimepata taarifa toka kwa daktari wetu mkuu wa bunge akinitaka nifike mara
moja katika zahanati yetu.Naomba nimuachie naibu spika aweze kuendelea na shughuli zilizobaki za
bunge.”
Kitu cha kwanza alichotaka kufahamu mheshimiwa spika baada ya kufika katika zahanati ya bunge ni
hali ya mheshimiwa Roma.Daktari akamuomba waongozane hadi katika ofisi yake.
“Daktari hebu nieleze hali ya mbunge inaendeleaje? Anasumbuliwa na kitu gani? Akauliza mheshimiwa
spika .
“Mheshimiwa spika nimeona nikuite nikueleze ukweli kwamba hali ya mbunge si nzuri hata
kidogo.Vipimo vyetu vinaonyesha kuwa shinikizo la damu liko juu mno na hata sukari yake imepanda
sana.Mpaka sasa hivi bado hatujaweza kufanikiwa kushusha sukari wala shinikizo la damu.Hali ya
mbunge inaendelea kwa mbaya hivyo nashauri haraka sana tumuwahishe katika hospitali kuu ya St
Francis ili akachekiwe zaidi.”
Huku uso wake ukionyesha wasi wasi mheshimiwa spika akaamuru haraka sana mheshimiwa Roma
ahamishiwe katika hospitali ya St Francis.Ni kitendo ambacho hakikuchukua hata dakika kumi tayari
mbunge alikwisha pakiwa katika gari la wagonjwa na kukimbizwa St Francis hospital.
Madaktari na wauguzi walikuwa wamekwisha jiandaa kumpokea mheshimiwa mbunge.Walikwisha pigiwa
simu na ofisi ya bunge.Baada tu ya gari kusimama kitanda kinashushwa na mheshimiwa mbunge
akakimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Mara moja mheshimiwa Roma akaanza kupatiwa
matibabu.Kwa zaidi ya nusu saa juhudi zikaendelea za kuhakikisha hali ya mheshimiwa huyu kijana
kipenzi cha wengi inaimarika lakini bado hali yake ikaendelea kuwa mbaya na kuwashangaza hata
madaktari.Mwishowe madaktari wakafikia uamuzi wa kumuhamishia mheshimiwa Roma katika hospitali kuu
ya magonjwa ya moyo Tanzania Heart hospital iliyoko jijini Dar es salaam.
Zahanati ya bunge ghafla ikageuka sehemu ya heka heka .Madaktari wa bunge walikuwa wakijitahidi
kwa kila walivyoweza kumpa huduma ya kwanza mheshimiwa Roma .Vipimo vya awali vilionyesha kuwa
shinikizo la damu lilikuwa juu isivyo kawaida na hata sukari ilikuwa imepanda mno.Pamoja na
jitihada zote za madaktari wa bunge bado hali ya mheshimiwa mbunge iliendelea kuwa mbaya
,ikamlazimu daktari mkuu wa bunge aamuru mheshimiwa spika aitwe.
Akiwa mezani kwake huku mheshimiwa mbunge Marewa shawe akiendelea kuwasilisha hoja yake,mhudumu
wa bunge akampelekea ujumbe wa kumtaka afike mara moja katika zahanati ya bunge.Bila kupoteza hata
sekunde spika akasimama na mheshimiwa aliyekuwa akiendelea kuwasilisha hoja yake akanyamaza
kumpisha spika wa bunge.
“waheshimiwa wabunge,nimepata taarifa toka kwa daktari wetu mkuu wa bunge akinitaka nifike mara
moja katika zahanati yetu.Naomba nimuachie naibu spika aweze kuendelea na shughuli zilizobaki za
bunge.”
Kitu cha kwanza alichotaka kufahamu mheshimiwa spika baada ya kufika katika zahanati ya bunge ni
hali ya mheshimiwa Roma.Daktari akamuomba waongozane hadi katika ofisi yake.
“Daktari hebu nieleze hali ya mbunge inaendeleaje? Anasumbuliwa na kitu gani? Akauliza mheshimiwa
spika .
“Mheshimiwa spika nimeona nikuite nikueleze ukweli kwamba hali ya mbunge si nzuri hata
kidogo.Vipimo vyetu vinaonyesha kuwa shinikizo la damu liko juu mno na hata sukari yake imepanda
sana.Mpaka sasa hivi bado hatujaweza kufanikiwa kushusha sukari wala shinikizo la damu.Hali ya
mbunge inaendelea kwa mbaya hivyo nashauri haraka sana tumuwahishe katika hospitali kuu ya St
Francis ili akachekiwe zaidi.”
Huku uso wake ukionyesha wasi wasi mheshimiwa spika akaamuru haraka sana mheshimiwa Roma
ahamishiwe katika hospitali ya St Francis.Ni kitendo ambacho hakikuchukua hata dakika kumi tayari
mbunge alikwisha pakiwa katika gari la wagonjwa na kukimbizwa St Francis hospital.
Madaktari na wauguzi walikuwa wamekwisha jiandaa kumpokea mheshimiwa mbunge.Walikwisha pigiwa
simu na ofisi ya bunge.Baada tu ya gari kusimama kitanda kinashushwa na mheshimiwa mbunge
akakimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Mara moja mheshimiwa Roma akaanza kupatiwa
matibabu.Kwa zaidi ya nusu saa juhudi zikaendelea za kuhakikisha hali ya mheshimiwa huyu kijana
kipenzi cha wengi inaimarika lakini bado hali yake ikaendelea kuwa mbaya na kuwashangaza hata
madaktari.Mwishowe madaktari wakafikia uamuzi wa kumuhamishia mheshimiwa Roma katika hospitali kuu
ya magonjwa ya moyo Tanzania Heart hospital iliyoko jijini Dar es salaam.
*******************************************************
Kupitia matangazo ya moja kwa moja yaliyokuwa ywakirushwa na vituo mbali mbali vya televisheni na
hata redio Taifa zima liliweza kushuhudia na kusikia moja kwa moja kilichotokea bungeni.Uikuwa ni
mstuko mkubwa sana.Kutokana na ukuaji wa teknolojia,ka kipindi kifupi sana idadi kubwa ya watu
waliweza kupata taarifa ya kilichojiri bungeni. Kupitia mitandao ya kijamii,simu za mikononi,blogs
na vyombo vingine vya upashanaji habari taarifa ziliweza kuwafikia watu kwa haraka mno.Taarifa
kubwa iliyokuwa ikizunguka katika mitandano na jumbe za simu za mikononi ni kwamba Mheshimiwa Roma
amefariki dunia ghafla.Taarifa hii ilisababisha shughuli ziweze kusimama kwa muda.Taifa
likazizima.Watu wengi walikuwa na mapenzi makubwa kwa mbunge huyu kijana.Mheshimiwa Roma alipendwa
na watu wa rika zote bila kujali itikadi ya dini au vyama.Kuanzia shule za msingi hadi vyuo
vikuu,toka kwa muuza nyaya Kariakoo hadi kwa mkulima wa korosho kule Mtwara,toka kwa mvuvi wa
samaki Kigoma hadi kwa mfugaji ngorongoro.Wengi walikuwa na imani kuwa muda utakapofika basi huyu
ndiye angeweza kuwa raisi wa Tanzania na kuwakomboa watanzania katika maisha duni waliyokuwa
nayo.Hii ilitokana na uzalendo wa kweli aliouonyesha kijana huyu katka kipindi kifupi.
Taarifa zikaanza kusambaa tena kuwa mwili wa mheshimiwa Roma ulikuwa njiani kusafirishwa kwa
ndege kuja Dar es salaam.Makundi ya vijana yakaanza kukimbia kuelekea uwanja wa ndege wa Dar es
laam ili kuweza kuhakikisha kama taarifa hizi ni za kweli.
“Hatuwezi kukubali wametuulia raisi wetu….” Alisema kwa jazaba kijana mmoja aliyekuwa akikimbia
huku amevua shati na jasho likimtiririka mwili mzima akielekea uwanja wa ndege.
Kundi jingine la vijana watembeza bidhaa barabarani maarufu kama machinga lililokuwa na vijana
wapatao mia moja na zaidi nalo lilikuwa lilikimbia kuelekea uwanja wa ndege ilimradi kila mmoja
aliyeguswa na taarifa ile ya kustusha alitaka kuhakikisha kwa macho yake mwenyewe .
***********************************************************
Ndege iliyombeba mheshimiwa Roma ilitua katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.Kwa
haraka mgonjwa akashushwa nakupakiwa katika gari la wagonjwa na kukimbizwa katika hospitali kuu ya
magonjwa ya moyo Tanzania heart hospital.Waandishi wengi wa habari na wapiga picha walikuwa
wamejazana hapo uwanjani ili kuweza kujaribu kupata walau habari na picha za tukio hili ili kuweza
kuuhabarisha umma wa watanzania uliokuwa ukisubiri taarifa zenye uhakika kwa hamu kubwa.Kwa jinsi
ulinzi ulivyokuwa umeimarishwa na kwa tukio lenyewe lilivyokuwa la haraka ilikuwa ngumu kuweza
kuipata picha ya moja kwa moja ya mheshimiwa mbunge.Picha zilipigwa kwa kutumia kamera zenye nguvu
zenye kuweza kunasa tukio katika umbali mrefu.
Gari la wagonjwa likiwa limetanguliwa na piki piki ya polisi liliondoka kwa kasi hapo
uwanjani na kuwaacha watu wakiwa kimya na wengine wakiangua vilio wakijua ni kweli mpendwa wao
mheshimiwa Roma alikuwa amefariki dunia.
Tanzania heart hospital hospitali binafsi inayomilikiwa na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo
Dr Sandra Jeremy mpama,mtoto wa rais wa jamhuri ya muungano Tanzania ,ilikwisha taarifiwa juu ya
kuletwa kwa mheshimiwa mbunge hivyo madaktari na wauguzi waliwekwa tayari ili pindi tu mgonjwa
atakapofika basi aanze kushughulikiwa haraka iwezekanavyo..Hopsitali hii ni moja kati ya hospitali
kubwa ya magonjwa ya moyo katika ukanda huu wa afrika mashariki,iliyosheheni madaktari bingwa wa
moyo.Japo ni hospitali binafsi lakini inatumika kama hospitali ya rufaa kwa watu wennye maradhi ya
moyo.
Geti linafunguliwa na kuiruhusu piki piki ya polisi iliyoliongoza gari la wagonjwa lililombeba
mheshimiwa Roma kupita .Baada tu ya kusimama ,mheshimiwa akashushwa na kukimbizwa katika katika
chumba maalum cha wagonjwa mahututi.Kazi ya kumuhudumia ikaanza.
**************************************************************
Umati wa watu ulizidi kuongezeka katika kila dadkika.Hakuna aliyeruhusiwa kuingia ndani
hospitalini zaidi ya viongozi wachache wa serikali ambao hata nao hawakuweza kumuona mheshimiwa
Roma kwa sababu bado alikuwa akiendelea kupata matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi.Watu
walikaa nje ya jengo la hospitali wakiongozwa na waandishi wa habari waliokuwa wakijitahidi kwa
kila namna ili kuweza kupata taarifa za nini kilichokuwa kikiendelea mle ndani. Mpaka saa kumi
na moja za jioni bado hakukuwa na taarifa zozote toka ndani ya hospitali juu ya maendeleo ya
mgonjwa.Yapata saa kumi na mbili za jioni mheshimiwa spika wa bunge akawasili ,akafunguliwa geti
na kuingia ndani.Akiwa ameongozana na baadhi ya wabunge na maofisa wengine wa bunge waliweza
kuingia hospitalini hapo lakini taarifa aliyopewa ni kwamba bado hali ya mheshimiwa mbunge haikuwa
nzuri..Spika na ujumbe wake wakatoka humo hospitali na kuondoka kwa sababu hakukuwa na ulazima wa
wao kuendelea kuwepo hapo hospitali wakati bado mgonjwa alikuwa akipatiwa matibabu.
****************************************************************
WHITE HORSE HOTEL - DODOMA
“Na sasa tugonganishe glasi zetu kusherehekea ushindi mkubwa tulioupata.” Kila mmoja akainua glasi
yake ya mvinyo na glasi zikagonganishwa.
Ni katika hoteli tulivu ya white horse hoteli,hoteli yenye hadhi ya nyota tano ambayo ni baadhi
tu ya vigogo ndio huwa wanafikia hapa,katika chumba kikubwa chenye hadhi ya presidential suit
kilichopangwa na Mr Faidh al badir,mmoja kati ya wafanya biashara wakubwa sana nchini akiwa na
wabunge watatu wa bunge la jamburi ya muungano wa Tanzania na watu wengine wawili ,walikuwa
wakijipongeza.
“Mr Nkebo nimeamini wewe ni mtu hatari sana.Unajua bila wewe leo hii huyu kijana alikuwa
atuaibishe vibaya mno.Lengo lake lilikuwa kuutangazia umma kuwa sisi ndio tulioshiriki katika
kuifilisi ile benki ya Taifa ya vijana Tanzania.Lakini sasa kwisha habari yake…Na hili ni fundisho
kwake kuwa siku nyingine asijaribu kufuatilia mambo yasiyomuhusu” Ilikuwa ni kauli ya mheshimiwa
mbunge Nasoro ngimarwa.
“hahahahaaa….mimi ndio Nkebo bwana.Yule kijana mdogo sana hawezi kusindana na watu kama
sisi.Nilikwisha waambia kuwa msiwe na wasi wasi hata kidogo.Huu mswaada binafsi hauwezi
somwa.Najua wengine hamkuamini kabisa niliyokuwa nawaambia.Kwa wale ambao hamkuwa mkijua
kilichokuwa kikiendelea ni kwamba mheshimiwa Ngimarwa hapa alipata taarifa ya kuwapo kwa nia ya
kuwasilishwa hoja binafsi bungeni na mheshimiwa Roma juu ya kufilisika kwa benki ya vijana.Baada
ya utafiti tuligundua kuwa yule kijana tayari alikuwa na baadhi ya taarifa zinazotuhusisha sisi na
kufilisika kwa bennki ile na hata baadhi ya nyaraka ambazo zingeweza kutuweka sisi matatani
alikuwa nazo.Kitu cha kwanza kilichofanyika ni kupoteza ushahidi wote Ili hata kama lingetokea
pendekezo la kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguza sakata hili wasingeweza kutuhusisha
kabisa sisi na suala hili.Hilo lilifanikiwa .Pamoja na kufanikiwa huko bado kijana yule aliendelea
kuonekana hatari kwetu.Alikwisha tujua na hivyo asingeweza kuacha kutuandama.Nadhani mnajua jinsi
ambavyo anaungwa mkono na wananchi.Baada ya kuliona hilo tukaamua kuwa sasa kilichobaki ni kumuua
tu.Mpango ulianza kusukwa toka mkutano wa bunge uliopita.Tukagundua kuwa kijana yule anapenda
kufikia HD LODGE.Basi pale tukampatia kazi binti ambaye ndiye aliyeweza kumaliza mchezo wote wa
leo.Binti huyu ndiye aliyepangiwa kumuhudimia yule kijana na ndiye aliyeweka sabuni ambayo Roma
amaeogea leo.Sabuni hiyo ilikuwa na sumu kali ambayo hupenya na kuingia mwilini haraka sana mara
tu inapopakwa katika ngozi na kwa kawaida hii hufanya kazi taratibu na baada ya masaa manne toka
iingie mwili basi mgonjwa anaweza kufa.Kilichomuweka hai mpaka sasa hivi ni hizi dawa alizopewa
katika hositali ya St francis.Hizi zimechangia kumuweka hai mpaka sasa hivi.Lakini nawahakikishia
kuwa mheshimiwa huyu hawezi kufika asubuhi.Hata wafanye nini ni lazima atakufa tu.”
Wote wakampongeza Mr Nkebo kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya.Wakaendelea kujimiminia mvinyo
katika maglasi na kunywa kwa furaha na kutakiana maisha marefu.
*******************************************************************
Saa mbili za usiku ,katika hospitali alimokuwa amelazwa mheshimiwa Roma,Daktari bingwa wa magonjwa
ya moyo Dr Sandra Jeremy Mpama akajitokeza mbele ya waandishi wa habari waliokuwa wamekusanywa
katika chumba cha mikutano cha hospitali hiyo.Akakaa kitini na chumba chote kikawa kimya kabisa.
“Ndugu wandishi wa habari nimewaiteni hapa ili kuwapa taarifa fupi juu ya mgonjwa tuliyempokea
hapa leo mheshimiwa Roma .Taarifa ninayotaka kuwapa si nzuri....................................
“Leo mchana tumempokea mheshimiwa mbunge Roma akisumbuliwa na shinikizo la damu.Toka tumempokea
tumekuwa tukijitahidi kwa kila tuwezalo ili kuhakikisha kuwa mwenendo wa mzunguko wa damu mwilini
unakuwa wa kawaida lakini napenda kusema kuwa bado hali ya mbunge si nzuri.Napenda kuchukua nafasi
hii kukanusha uvumi ulioenea na unaoendelea kuenea kuwa mheshimia Roma amefariki dunia.Taarifa ya
ukweli ni kwamba mheshimiwa mbunge ni mzima japo hali yake si nzuri lakini napenda niwatoe hofu
watanzania kuwa mbunge wetu atapona kwa sababu anashughulikiwa na timu yetu nzima ya madaktari
bingwa wa moyo wakiongozwa na mimi mwenyewe.Narudia tena kuwatoa hofu watanzania kuwa mbunge wetu
ni mzima na anaendelea kupata matibabu.Kinachotakiwa ni kuzidi kumuombea ili Mweneyzi Mungu ampe
uponaji wa haraka.Ahsanteni.
Akamaliza Dr Sandra ,akainuka na kutoka humo ukumbini huku waandishi wa habari wakisimama kutaka
kuuliza maswali.
“Jamani Dokta hana muda wa kujibu maswali yenu.Bado wanaendelea na kazi.Subirini kwanza wamalize
kazo zao ndio mtapata muda mzuri wa kumuuliza maswali yenu”
Dr Kalufa akawaambia wandishi wa habari.
Alipotoka kuzunguma na waandishi wa habari ,Dr Sandra akarudi tena katika chumba cha uangalizi
maalum kuungana na madaktari wenzake.Bado hali ya mheshimiwa Roma haikuonyesha dalili zozote za
matumaini.Hili lilimuumza mno Dr Sandra.Akatoka na kwenda ofisini kwake akakaa kitini huku
akitafakari nini cha kufanya.Ugonjwa huu ulimshangaza mno.Baada ya kama dakika tano za tafakaroi
akachukua simu na kumpigia msaidizi wake.
“Susan ,naomba mtaarifu Spika wa bunge kuwa namuhitaji haraka hapa hospitali”
Muda wa dakika ishirini toka apate mwito ule wa haraka spika wa bunge akawasili
hospitali.Akapokelewa na moja kwa moja akapelekwa katika ofisi ya Dr Sandra.
“Mheshimiwa Spika,naomba kwanza nikuombe samahani kwa mwito huu wa haraka” akaanza maongezi Dr
Sandra
“Usijali Dr Sandra.Hii ni moja ya majukumu yangu ya kazi kuhakikisha wabunge wote wanapopatwa
na hali kama hii kupata matibabu na kupona.Nimeacha vikao vya bunge vikiendelea ili kuja
kuhakiksha kuwa mheshimiwa mbunge anapata tiba stahili kwa sababu ugonjwa wake umetustua mno.Vipi
maendeleo yake kwa sasa?
“Mheshimiwa Spika napenda niwe wazi kuwa tumejitahidi sana toka tulipompokea hapa mchana lakini
bado hali yake haionyeshi mabadiliko .Bado tunaendelea na uchunguzi wa nini kinachosababisha hali
hii.Mheshimiwa spika hospitali yetu ni kubwa na ya kuaminika katika ukanda huu wa afrika mashariki
na kati na imesheheni madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo.Pamoja na ukubwa na sifa hizo zote
tulizonazo napenda nitoe pendekezo kuwa mheshimiwa mbunge anahitaji kupelekwa nje ya nchi haraka
iwezekanavyo kwa matibabu zaidi.Mimi ni daktari bingwa wa moyo lakini kwa ugonjwa huu ninavyouona
hatuna njia nyingine zaidi a kumpeleka mgonjwa katika hospitali kubwa zaidi kwa uchunguzi
mpana.Kuna hospitali moja iko nchini Israel katika mji wa Haifa inaitwa Rambam medical center.Pale
wamesheheni mabingwa wa moyo na kuna vifaa vikubwa zaidi vya uchunguzi kuliko tuliyo navyo
sisi.Hospitali hii ni rafiki zetu na tumekuwa tukisaidiana mara kwa mara na hata kubadilishana
wataalamu.Nimekwisha ongea nao na wako tayari kumpokea mheshimiwa na kumsaidia”
Dr Sandra akamaliza na kumtazama Mheshimiwa Spika aliyekuwa amenyamaza akimsikiliza kwa makini
sana.Akainama kidogo akafikiri kisha akasema.
“Dr Sandra nakushukuru sana kwa jitihada zote unazozichukua kuhakikisha kuwa mbunge wetu
anapona.Mimi huyu mbunge ninamlea kama mwanangu Licha ya kwamba mimi ndiye kiongozi wake bungeni
lakni kama mzazi na kama mtanzania mwenye moyo wa uzalendo niko tayari kwa lolote lile linaloweza
kufanyika litakalomsaidia kijana huyu apone.Tatizo lililoko hapa Dr Sandra ni kwamba kuna taratibu
za kisheria ambazo ni lazima zifuatwe.Ingekuwa ni kwa ridhaa yangu basi ningekuruhusu sasa hivi
umuandae mgonjwa kwa safari.Kwa kuwa umeshauri hivyo ngoja na mimi nimpigie simu waziri wa afya
ambaye yuko hapa hapa Dar ili tukutane usiku huu huu na kuona nini cha kufanya.Yeye ndiye mwenye
dhamana ya kuamua nani na nani wapelekwe nje ya nchi kwa matibabu.”
Dr Sandra akamtazama Spika kwa makini sana kisha akasema kwa sauti ya taratibu.
“Nalifahamu hilo mheshimiwa Spika ,lakini kwa leo sidhani kama utaratibu huo una
nafasi.Kinachotakiwa hapa si utaratibu bali maamuzi ya haraka.Iwapo mtaanza kuvutana kuhusu
utaratibu kuna hatari ya kumpoteza mgonjwa.”
“Dr Sandra mambo ya kiserikali ni magumu .Siwezi kutoa uamuzi mimi mwenyewe hapa bila kufuata
taratibu husika.Ninachoomba nipe kama saa moja hivi iliniweze kukutana na waziri wa afya na tuone
tulifanyaje suala hili.”
Spika wa bunge akatoka ofisini kwa Dr Sandra kwa kasi.
Dr maneno kilugwa ,waziri wa afya katika serikali ya jamburi ya muungano wa Tanzania alikuwa
amejipumzisha katika mgahawa tulivu katika ufukwe wa bahari.Ni siku ya mwisho ya mkutano wa wadau
wa afya afrika,mkutano uliochukua takribani siku nne na uliomfanya asiwepo Dodoma katika vikao vya
bunge.Baada ya kazi ngumu iliyofanyika ya kuhakikisha kuwa mkutano ule unafanikiwa,Mheshimiwa
waziri ameamua kutoka na kwenda kujipumzisha sehemu tulivu.Mezani chupa kubwa ya mvinyo ilikuwa
imesimama .Dr maneno alikuwa amekaa peke yake akijaribu kuwazua hili na lile.hakutaka bughudha ya
aina yoyote ile.Wakati akiendelea kukata mvinyo taratibu simu yake inaita.Akaitoa mfukoni na
kuangalia.Alikuwa ni mheshimiwa Spika.
“Hallo mheshimiwa Spika”
“Mheshimiwa waziri uko wapi kwa sasa?
“Mimi niko sehemu Fulani napumzika.Kuna tatizo ganui mheshimiwa spika?
“Mheshimiwa waziri kuna tatizo kubwa linalomuhusu Mheshimiwa Roma.Hali yake bado si nzuri na
madktari wameshauri haraka sana apelekwe nje ya nchi.Kwa maana hiyo naomba ndani ya dakika kumi na
tano toka sasa tukutane hapo katika ofisi yangu ndogo.Fanya hima”
Kauli ile ya mheshimiwa Spika inamfanya mheshimiwa waziri wa afya nywele zimsisimke.
“Bastard!!!!!!!………..
“He’s still breathing….” Akanong’ona kwa ghadhabu Dr maneno.
“This cant be..” Akafoka tena kwa hasira.Akachukua simu yake na kupiga
“Halloo Mr Nkebo habari za saa hizi? Akasema Dr maneno huku amefura kwa hasira
“Habari nzuri Dr Maneno.Niko hapa na akina Faith,mheshimiwa Ngimarwa na wengine wote tunafurahia
ushindi wetu” Akasema Mr Nkebo huku akicheka kicheko cha chini chini.
“Mafurahia ushindi gani wakati mpaka sasa hivi Roma bado mzima? Bado anapumua na hivi saa Spika
kanipigia simu tuonane.Roma anatakiwa apelekwe nje ya nchi haraka iwezekanavyo.”
Kikapita kimya cha sekunde kadhaa halafu Mr Nkebo akasema kwa sauti kavu.
“Don’t let it happen.Roma must die tonight.Ukiacha Roma apelekwe nje ya nchi basi tumeumia.Kuna
mawili atapona na kuna hatari ikagundulika kuwa aliogea sabuni ya sumu.Uchunguzi ukifanyika
inaweza ikawa mbaya kwa upande wetu.Sasa fanya kila uwezalo,tumia madaraka yako yote kuhakikisha
kuwa Roma hapelekwi nje ya nchi.Ukifanikiwa kwa hilo basi Roma hafiki asubuhi.Ukiacha tu atolewe
nchini,tumekwisha.Do you understand that?
Dr maneno akapumua kwa nguvu kisha akajibu.
“I understand that.I wont let it happen……..”Akakata simu halafu kwa haraka akaelekea lilipo gari
lake akapanda na kuondioka kwa kasi.
Ili mchukua dakika kama kumi kuwasili katika ofisi ndogo ya spika.Usiku huu hakukuwa na
msongamanao mkubwa wa magari.Spika alikuwamo ofisini mwake akimsubiri.
“karibu sana mheshimiwa waziri.”
“Ahsante mheshimiwa Spika.Nimeitika mwito.Vipi hali ya bunge inaendeleaje? Akasema Dr maneno huku
akivuta kiti na kuketi
“Hali ya mbunge si nzuri na kila muda unavyozidi kwenda hali inazidi kuwa mbaya.Madaktari
wameshauri kuwa ili kuokoa maisha ya mheshimiwa roma inabidi haraka sana akimbizwe katika
hospitali kubwa nchini Israel.Suala la kumpeleka mgonjwa nje ya nchi lina taratibu zake za
kiserikali.Wewe ukiwa kama waziri wa afya una dhamana kubwa ya kuamua kuhusu wagonjwa wa kupelekwa
nje ya nchi.sasa nimekuita hapa ili tujadiliane kwa haraka nini cha kufanya ili mheshimiwa Roma
apelekwe nje ya nchi usiku huu.Kwa kuwa taratibu ni ndefu basi tunaweza andika kibali cha dharura
na usiku huu huu mbunge akapelekwa nje kwa matibabu halafu taratibu zingine zikafuatia wakati
tayari matibabu yanaendelea.”
Spika akamtazama Dr maneno aliyekuwa akisikiliza maelezo ya spika kwa makini .
“Mheshimiwa spika nafamu ni jinsi gani wote tulivyoguswa na tatizo hili la mheshimiwa
Roma.Ingekuwa ni kwa ridhaa yangu na yako hata sasa hivi mgonjwa angekuwa hewani akisafirishwa
lakini kuna taratibu za kiserikali ndizo hizo zinazoleta shida.Kusema ukweli kwa usiku huu mimi
siwezi andika kibali chochote labda hadi kesho ndipo ninaweza kuanza kulishughulikia suala
hili.Uliponipigia tu simu nimewasiliana na madkatari wa serikali ambao ni mabingwa wa moyo na
wamesema kuwa ugonjwa huo wa Mheshimiwa Roma unaweza kutibika humu humu nchini.Hakuina sababu ya
kumpeleke mgonjwa wa shinikizo la damu nje ya nchi wakati tunao wataalamu wetu wengi wa serikali
ambao ni mabingwa wa maradhi haya ya moyo.Hivi tunavyoongea maandalizi yanafanyika ili mheshimiwa
Roma ahamishiwe katika hospitali ya taifa ya muhimbili ambayo ina wataalamu wa hali ya juu
kabisa.”
Mheshimiwa waziri wa afya akasema kwa kujiamini.Spika akasimama na kumtazama Dr maneno kwa
hasira.hakutegemea katu kusikia jibu kama lile.
“waziri sijakuelewa vizuri,unasemaje?? Akauliza spika
“Nimesema hivi mimi kama waziri mwenye dhamana ya afya nimeagiza kuwa mheshimiwa mbunge ahamishiwe
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.Pale kuna wataalamu wa hali ya juu watakaoutibu ugonjwa
wake na tayari maandalizi yameanza kufanyika.Muda mfupi ujao nataka mheshimiwa mbunge ahamishwe
toka katika hospitali hiyo binafsi na kuhamishiwa katika hospitali ya serikali.Mbunge ni mtumishi
wa umma na hivyo atatibiwa katika taasisi za umma.Hospitali binafsi wao wanachofahamu ni pesa tu.”
Akasema Dr maneno kwa sauti iliyokuwa na aina Fulani ya ukali
Spika wa bunge akalengwa na machozi
“Siamini hayo unayoniambia Dr maneno.wewe unaelewa wazi kabisa uwezo mdogo wa hospitali zetu za
serikali na ndio maana wagonjwa wote wanapelekwa Tanzania heart hospital.sasa iweje leo uamuru
mheshimiwa mbunge ahamishwe toka katika hospitali ambayo inategemewa afrika mashariki na kati
umpeleke katika hospitali isiyo kuwa na uwezo wa juu katika tiba ya moyo?” Spika akauliza kwa
ukali
“Mheshimiwa Spika pale Muhimbili kuna kitengo cha moyo chenye mabingwa na hata wataalamu wa
kichina wako pale.Sioni tatizo lolote kwa mheshimiwa mbunge kutibiwa katika hospitali za
serikali.Mimi ndiye waziri wa afya na huo ndio uamuzi wangu.Nina imani pale atashughulikiwa na
madaktari wazalendo na atapona tu.”
“Ok nimekuelewa.we’re done in here.Unaweza kwenda.”
Waziri wa afya Dr maneno akatoka katika ofisi ya spika baada ya kuona tayari mheshimiwa spika
amekasirika.Spika wa bunge akafanya mawasiliano na mawaziri kadhaa lakini hakukuwa na hata mmoja
aliyeweza kumpa jibu lenye uhakika.Wote walisema wasubiri asubuhi ili waone ni jinsi gani ya
kulishughulikia suala hilo.Akatoka ofisini kwake na kumuamuru dereva wake kumpeleka hospitali
haraka iwezekanavyo.
Alipofika hospitali akafululiza kwa kasi hadi katika ofisi ya Dr Sandra.
“Dr mgonjwa anaendeleaje?”akauliza spika
“mgonjwa bado hali yake inazidi kuwa mbaya.Vipi umefikia wapi kuhusu suala lile?
“mambo magumu sana Dr.Nimetoka kuongea na waziri wa afya lakini tumshindwa kuelewana.Ameamuru Roma
ahamishiwe katika hospitali ya taifa ya muhimbili”
“Whaaaattttt!!!!????? …..akauliza Dr Sandra kwa mshangao.
“No its not true…These people are jocking” akalalama Dr Sandra
“Its not a joke Dr Sandra.Hivi tunavyoongea maandalizi yanafanyika na muda si mrefu mtatarifiwa
juu ya uhamisho huo”
Dr Sanra akamuangalia spika kwa macho makali.
“Mheshimiwa spika hivi mnajua mnachotaka kukifanya??
Spika hakujibu kitu.Dr Sandra akauliza tena.
“You are killing this young man…He’s going to die” machozi yakamlenga lenga
“Na wewe mheshimiwa spika umekubaliana na uamuzi huo?
“hapana sijakubaliana nao hata kidogo”
Dr Sandra akamtazama spika kwa makini sana halafu akasema.
“Mheshimwa Spika naomba unisikilize.Toka mheshimiwa Roma ameletwa hapa wewe ndiye kiongozi pekee
wa juu wa serikali uliyefika hapa na unayehangaika kuyapigania maisha ya mbunge huyu.Wewe ni
kiongozi jasiri.Ukiwa kama mzazi hutapenda kuona mbunge huyu kijana anafariki au kupata ulemavu wa
kudumu.Tukikubali hili litokee tutakuwa tumefanya kosa kubwa mno na pengo la kijana huyu
halitazibika kamwe.Kwa maana hiyo basi ninaomba kama kweli una nia ya dhati tushirikiane mimi na
wewe kuhakikisha kuwa hilo linalotaka kufanyika halifanyiki.Tuhakikishe mheshimiwa Roma ahamishiwi
Muhimbili na usiku huu huu anasafirishwa nje ya nchi.Are you ready for this?
Bila kusita spika wa bunge akajibu.
“Dr Sandra kwa kuyaokoa maisha ya kijana huyu niko tayari kwa lolote lile na hata kuhatarisha
maisha yangu,kazi yangu ilimradi Roma apone.”
“Good” Akasema Dr Sandra.Akamtazama tena spika halafu akasema
“Niliapa siku natawazwa kuwa daktari bingwa kuwa sintakubali hata siku moja kuona mgonjwa
akipoteza maisha kwa uzembe.Ndio maana ninapokuwa na mgonjwa huwa nafanya kila niwezalo
kuhakikisha namuhudumia hadi mwisho.Nimeumia sana moyoni kwa kitu anachotaka kukifanya waziri.Hii
inanipa picha ya wazi kuwa there is something going on here.”
“Kweli Dr Sandra haata mimi nimeanza kuhisi kitu kama hicho manake hii si kawaida.”
“Ok Usijali spika kwa vile umekubali kushirikiana na mimi basi napenda kukuhakikishia kuwa ndani
ya nusu saa ijayo tutamsafirisha mheshimwa mbunge.Litakalotokea litokee tu lakini bora tujaribu
kuliko kukaa na kusubiri kuhani msiba.Naomba sasa unisubiri hapo nje kama dakika tatu hivi”
Spika akatoka na kwenda kukaa katika masofa yaliyokuwa nje ya ofisi ya Dr Sandra.
Huku akipumua kwa nguvu Dr Sandra akachukua simu na kuzitafuta namba za baba yake Jeremy Mpama
raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
“ Hallo Sandra how are you my love” Ilikuwa ni sauti nzito ya mheshimiwa Rais Jeremy Mpama.
“I’m ok dady how are you? Dr Sandra akauliza
“I’m ok.Mbona sauti yako inaonyesha kama una tatizo? Is there anything wrong my love” akauliza
mzee Jeremy
“Yes dady I have a problem.”
“My love,nimekwisha kwambia kuwa ,wakati niko hai duniani sintataka hata siku moja tabasamu
likauke usoni mwako.wewe ndiye binti wangu wa pekee na niko tayari kufanya lolote lile kwa ajili
yako”
Tabasamu likaanza kujengeka usoni mwa Dr Sandra baada ya kauli ile
“Niambie nini tatizo? Akauliza Rais
“Daddy tatizo ni kubwa lakini kwako wewe si kubwa na linahitaji kauli tu badala ya nguvu.” Dr
sandra akasema
“Mbona unashindwa kulisema tatizo gani linakusumbua my love.Sema tu mimi ndiye baba yako na
nitafanya kama unavyotaka.
“Daddy nafikiri una taarifa juu ya mbunge aliyepatwa na matatizo leo bungeni”
“Yes nimepewa taarifa zake.Nilizipata taarifa hizo nikiwa katika mkutano na mabalozi na hata hivi
ninavyoongea na wewe niko na mkutano na wakuu wa mikoa ya Mbeya ,Iringa na Rukwa.Nimekosa hata
muda wa kufuatilia anaendeleaje.Nilipewa taarifa kuwa ameletwa hapo hospitalini kwenu.”
“Yes daddy.Tumempokea mchana na tumekuwa tukiendelea kumuhudumia.Kusema ukweli daddy ugonjwa wake
ni mkubwa na anatakiwa haraka sana apelekwe nje ya nchi kwa uchunguzi zaidi.Mpaka sasa bado
hatujafanikiwa kulishusha shinikizo la damu Nimeongea na mheshimiwa spika nikamueleza naye
akaongea na waziri mwenye dhamana yaani waziri wa afya kuhusu kumpeleka nje mheshimiwa mbunge
lakini waziri wa afya amekataa katu katu na ameagiza mgonjwa ahamishiwe katika kitengo cha
magonjwa ya moyo cha hospitali ya Muhimbili.Daddy please understand me kama akihamishiwa kule he’s
going to die.I wont let him die just like that.I need to fight for him.Daddy naumia mno kuona
mgonjwa akiteseka hadi kufa kwa uzembe.Nimekwisha ongea na rafiki zangu wa hospitali ya Rambam
iliyoko Haifa Israel na wamekubali kumpokea mgonjwa.daddy I want to take him out of country in 30
minutes.”
“In 30 minutes?? Akauliza Rais
“Yes daddy and one more thing I need your plane” Dr Sandra akasema kwa sauti ambayo haikuwa na
masihara hata kidogo.
Kimya kikatanda.Mzee Jeremy alikuwa katika tafakari nzito.hakujua afanye nini.Ombi la mtoto wake
lilimstua mno.
“Daddy are you there? Dr Sandra akauliza baada ya kuona baba yake yuko kimya.
“I’m here love” Akajibu Raisa kwa upole
“natafakari uzito wa ombi lako.Kwa nini lakini us………………..”
Dr Sandra akakamkatisha baba yake aliyekuwa akitaka kuongea
“daddy No..this is not politics.This is life of someone.You promised to give me anything I
want.That’s what I want.I need your plane to take me to Israel in 30 minutes.Am I going to get it
or not? Kama haiwezekani niambie ili nijue nifanye kitu gani haraka.”
Dr Sandra akauliza kwa msisitizo
Mzee Jeremy alimpenda mno binti yake wa pekee na alikuwa tayari kufanya lolote lile kwa ajili
yake.Aliuona msisitizo aliouonyesha binti yake na akaona kuna kila ulazima wa kumsaidia.Hakupenda
kumuudhi binti yake.
“ Sandra my love ninaelewa ni kwa jinsi gani unavyoumia kuhusu suala hili.Japokuwa ni suala gumu
lakini ninakubali kubeba dhamana hii kwa ajili yako.Jiandae ndani ya muda huo unaoutaka utaondoka
na ndege yangu .Nitaongea na balozi wa Israel hapa nchini na kumweleza dharura hii iliyotokea,na
vile vile nitaongea na rais wa Israel na kumfahamisha juu ya suala hili ili usije ukapata usumbufu
wa aina yoyote ile.”
“Thank you so much daddy.You did great.Talk to you soon.I love you”
Dr Sandra hakutaka maongezi tena marefu na baba yake.Akatoka kwa kasi na kumkuta spika wa bunge
akimsubiri hapo nje ya ofisi yake.
“Mheshimiwa Spika.Kila kitu kiko shwari.Ndani ya muda mfupi ujao tutamsafirisha mgonjwa nje ya
nchi.”
“wow !! Dr Sandra “ Akasema Spika kwa furaha iliyochanganyika na mshangao.
Dakika kumi na tano tu zilitosha kabisa kumuandaa mgonjwa tayari kwa safari ya kuelekea nchini
Israel.Gari la wagonjwa lilikuwa tayari,mheshmiwa Roma akapakiwa na safari ya kuelekea uwanja wa
ndege ikaanza.
Uwanjani ndege ya Rais ilikwisha wekwa tayari kwa amri ya rais.Mgonjwa akaingizwa ndegeni tayari
kwa safari.Dr Sandra akamkumbatia spika kwa furaha.
“Nashukuru sana mheshimiwa Spika kwa kukubali kuwa upande wangu.Nakuahidi nitafanya kila niwezalo
kuhakikisha mheshimiwa mbunge anapona”
Wakaagana ,Dr Sandra akapanda ndegeni,milango ikafungwa na muda si mrefu ndege ikapaa
**********************************************************
Timu ya madaktari toka kitengo cha magonjwa ya moyo hospitali ya taifa ya Muhimbili kinawasili
katika hospitali ya magonjwa ya moyo ya Tanzania heart hospital ili kumuhamisha mheshimiwa mbunge
Roma kama walivyoamriwa na waziri wa afya.Taarifa waliyoipata toka kwa msemaji wa hospitali
zinawachanganya na kumlazimisha mkuu wa msafara ule ampigie simu waziri wa afya.
“Mheshimiwa waziri,kuna mambo yamejichanganya hapa.Taarifa tuliyoikuta hapa hospitali inasema
kuwa mgonjwa amesafirishwa nje ya nchi”
“Unasemaje??? Akahamaki mheshimiwa waziri
“taarifa toka kwa msemaji wa hospitali hii ni kwamba mgonjwa tuliyemfuata hapa Mheshimiwa Mbunge
Roma,amepelekwa nje ya nchi akiongozana na daktari mkuu wa hospitali hii Dr Sandra mpama na
muuguzi mmoja..”
“No….. haiwezekani…Nisubirini nakuja hapo sasa hivi”Akasema waziri
Jasho lilikuwa likimtoka.
“Lazima kuna kitu kimefanyika hapa.Watakuwa wamemficha mgonjwa .Si rahisi kumsafirisha mgonjwa nje
ya nchi bila mimi kujua.Mgonjwa ni laziam yuko humo humo hospitalini. Nitakwenda na kikosi cha
askari na kufanya upekuzi hospitali yote.Najua ni lazima atakuwa amefichwa katika moja ya vyumba
vya hospitali hiyo.”
Haraka haraka akapanda katika gari lake na kuodnoka kuelekea hospitalini ambako aliwakuta
madaktari toka hospitali ya muhimbili wakimsubiri.
Msemaji mkuu wa hospitali ile akamhakikishia kuwa mheshimiwa mbunge amesafirishwa nje ya
nchi.Bado hakuamini akaamua kumpigia simu mheshimiwa Spika.
“Mheshimiwa spika una taarifa zozote juu ya kusafirishwa kwa mbunge Roma nje ya nchi?”
“Ndiyo Dr Maneno.Nina taarifa hiyo na mimi mwenyewe nimewasindikiza na kuhakikisha ndege
imepaa.”
Sura ya mheshimiwa waziri ikazidi kujikunja kwa hasira
“Sikutegemea mheshimiwa spika kama na wewe unaweza ukashiriki katika uvunjifu huu wa sheria za
nchi.Unafahamu wazi kuwa zipo taratibu za kufuatwa lakini nyie kwa makusudi kabisa mmekiuka
mamlaka na kuchukua uamuzi wa kumtorosha mgonjwa kumpeleka nje ya nchi bila kibali cha
serikali.Hilo ni kosa mheshimiwa spika na utatakiwa kulijibu.”
“Mhshimiwa waziri nimefanya ninavyotakiwa kufanya.Hata watanzania wakisikia nilivyofanya
watanipongeza badala ya kunibeza.” Akasema spika kwa sauti ya kejeli
“Mheshimiwa spika umefanya kosa kubwa na itakubidi ulieleze bunge ni kwa nini umefanya kitu cha
namna hii.Kwa kuwa umeonyesha dharau kwangu mimi kama waziri mwenye dhamana ya afya naahidi kula
nawe sahani moja.Mheshimiwa utanisamehe kwa hili lakini ni lazima tupambane ili heshima iwepo.”
Akasema waziri kwa hasira
“Waziri usinitishe kabisa.Huna lolote la kunifanya.Nenda kanishtaki kokote unakoweza lakini uwe
tayari kueleza ukweli juu ya ajenda yako ya siri inayokulazimisha ufanye juu chini kuyahatarisha
maisha ya mheshimiwa mbunge.”
“Sema uatakavyo spika,lakini ni lazima nile na wewe sahani moja” Akasema waziri na kukata simu
kwa hasira.
“Damn you………………” Mheshimiwa waziri akapiga ukuta kwa hasira.akainama akatafakari halafu kwa
hasira akaelekea lilipo gari lake.Kabla hajalifikia gari lake simu yake inaita.Alikuwa ni kamanda
wa polisi dar es salaam.
“Mheshimiwa waziri nimekutumia vijana kumi na tayari wamekwisha fika hapohospitalini kama
ulivyoelekeza.”
“ahsante sana kamanda” waziri akajibu kwa mkato.Akageuka na kuangaa angaza getii ambaki aliliona
gari la askari likiwa limepaki.Akanyoosha mkono na kumuita kiongozi wa msafara ule.
“Kazi ya hapa imekwisha na hivi sasa tutaongozana kuelekea uwanja wa ndege” Akaamuru waziri.
Gari ya polisi ikiitangulia gari ya wairi zilikwenda kwa kasi ya ajabu kuelekea uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere.Mheshimiwa waziri alikuwa amefura kwa hasira huku jasho likimtiririka.Alipofika
uwanjani alielezwa kuwa mheshimiwa Roma ni kweli amesafirishwa kwenda nje ya nchi kwa kutumia
ndege ya Rais kwa amri ya rais.
“This thing is more complicated than I thought” Akawaza mheshimiwa waziri wa afya huku
amejishika kiuno na jasho likimtiririka.Alikuwa akipumua kwa nguvu.Alihisi miguu inaihsha nguvu.
“wamefanikiwa kumsafirisha” Ilikuwa ni sauti y kiunyonge ya waziri wa afya akimfahamisha Mr Nkebo
katika simu.
“How could you let it happen Dr? Mr Nkebo akauliza kwa ukali
“Its complicated Mr Nkebo.It was an order from Mr President”
Mr Nkebo akapumua kwa nguvu.
“Unataka kuniambia rais ameshirikishwa katika hili?
“yah na ndiye aliyetoa ndege yake imsafirishe Roma.”Akasema waziri
Kimya kikapita halafu Nkebo akasema
“naona upepo umebadilika.Mchezo unaanza kuchezwa upya kabisa.hatuna jinsi safari hii ni lazima
tucheze na mheshimiwa rais”
“Mheshimiw Rais? Akauliza waziri
“yes Mheshimiwa rais” Akarudia tena Mr Nkebo.
“Nina imani kuwa huko aendako anaweza akapona.Atakapopona atakuja na nguvu mpya na mashambulio
makali japokuwa hatokuwa tena na ushahidi wa kutosha wa kutuhusisha sisi na benki ile.Lakini hilo
la kuharibu ushahidi bado halitoshi kutuhakikishia maisha ya utulivu,raha mstarehe.The guy is very
smart.Bado ataendelea kutufuata .kwa maana hiyo basi yatulazimu kujikinga mapema.Ni lazima
tumfanye mheshimiwa rais kuwa ngao yetu.Yeye ndiye mkuu wa nchi na akitukingia kifua basi hakuna
mwingine wa kutusumbua.”
“Mr Nkebo una mawazo mazuri sana,lakini bado sijakupata vizuri.How are we going to convince Mr
president to join us?” Akauliza waziri maneno
“ ahahahahaa its just simple Dr maneno.This is politics and you know what politics means.All
politicians are fighting for power so is Mr President”
“maneno yako yananipa matumaini makubwa Mr Nkebo.lakini bado nina wasi wasi kidogo na
kumshirikisha rais.”
“Dr Maneno usijali kabisa.Hilo ni jukumu langu na nitalifanikisha.Mimi ndiye nitakayekwenda
kuonana na rais.Kesho mheshimiwa rais anakuja Dodoma kwa vikao vya chama vitakavyoanza kesho
kutwa.Rais ananifahamu vizuri na akisikia niko Dodoma na ninahitaji kumuona basi atakubali haraka
sana.Sisi ndio wafadhili wa chama japokuwa hatutaki kujulikana moja kwa moja.Rais anatusikiliza
sisi.Nitaitumia fursa hiyo kutafuta kinga yake.”
“Nimekuelewa Mr Nkebo.Kama mtahitaji ushirikiano wowote toka kwangu msisite kunitarifu kwa
sababu sitegemei kuja Dododma hivi karibuni.mambo yaliyofanyika leo yamenitibua mno ,lakini
nimepata tumaini jipya kwa maneno uliyoniambia.”
“Usijali Dr maneno.Mimi ndiye Nkebo nisiyeshindwa na kitu chochote.See you then “
“good luck gentleman” akasema Dr maneno na kupumua kwa nguvu.tabasamu lenye Nuru likaanza
kujijenga tena usoni mwake.
“This is politics…………………..” Akanong’ona taratibu.
Wakati haya yote yakiendelea,katika ukumbi mdogo wa hoteli ya Dodoma palace hotel kikao kilikuwa
kikiendelea.Mbunge Damiani mwamba alikuwa ndiye mwenyekiti wa kikao hiki kilichowakutanisha baadhi
ya wabunge wa chama tawala na wenye nguvu bungeni na katika chama,pamoja na baadhi ya viongozi na
watendaji wa chama waliokuja mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya chama.
Damiani Mwamba alikuwa ni mmoja kati ya wabunge matajiri aliyewahi kushka nyadhifa mbali mbali
serikalini na katika chama.Amekuwa mbunge kwa miaka karibu ishrini sasa na bado wananchi wake
walikuwa wakimpenda na kumtaka aendeleee kuwasemea kama mbunge wao.Maendeleo aliyoyaleta jimboni
mwake yalikuwa ni ya kutiliwa mfano.Maji yalitiririka katika kila kijiji,bara bara zote zilikuwa
safi na zilizopitika kwa muda wa mwaka mzima bila matatizo,Zahanati zilijengwa katika kila
kata,umeme uliwaka katika kila kijiji .Alihmiza ujenzi wa viwanda vidogo vidogo vilivyoleta ajira
kwa mamia ya vijana,isitoshe aliwaleta wawekezaji wakubwa kuwekeza katika kilimo na uwekezaji
mkubwa.Haya ni baadhi tu ya mafaniko yaliyopatikana jimboni kwake na kumfanya awe ni mfano wa
kuigwa miongoni mwa wabunge.Ukaribu wake na Mheshimiwa Rais Jeremy mpama ulikuwa si wa kuulizwa
kwa sababu walisoma wote shule moja na huko ndiko walikoanzia shughuli za siasa.Kwa muda wa miaka
kumi na sita amekuwa waziri katika wizara mbali mbali hadi pale rais alipolivunja baraza lake la
mawaziri na yeye kuushangaza umma kutokurudi tena katika baraza la mawaziri.Hakuna ajuaye ni kwa
nini Mheshimiwa damian hakupewa uwaziri tena.Pamoja na kutopewa uwaziri katika serikali ,bado
mheshimiwa Damiana ameendelea kuwa na nguvu kubwa katika chama na bunge.Idadi kubwa ya viongozi wa
chama na serikali walikuwa upande wake.
“Ndugu wajumbe ,karibuni sana katika kikao hiki cha leo.Hiki ni moja tu ya vikao vyetu vya
kawaida ambavyo tutaendelea kukaa na kujadili mwenendo wa siasa hapa nchini.Kikao cha leo ni kwa
ajili ya kukumbushana baadhi ya mambo bila kusahau mkakatiwetu wa kuchukua urais katika uchaguzi
mkuu ujao ambao umekaribia sana.nawashukuru ndugu wajumbe kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya na
mnayoendelea kuifanya kila siku.Nguvu yetu katika chama imeongezeka,idadi ya wajumbe wanaotuunga
mkono imeongezeka na hivyo kuzifanya mbio za kinyang’anyiro cha mgomea urais ndani ya chama kuwa
nyepesi sana kwa upande wetu.Nina imani tutashinda.Imani kwa wananchi na kwa wanachama imeongezea
na inaendelea kuongezeka licha ya kuwa kuna upinzani mkubwa kati yangu na rais.Vile vile kuna watu
ambao kidogo wanakuiwa ni tishio ingawa hawajaweka bayana dhamira zao za kugombea nafasi
hiyo.Mmoja waoni huyu kijana Roma.Kijana huyu ana nguvu sana katika jamii na hasa kwa vijana ambao
ndio wapiga kura wengi.Ikiwa ataweka nia ya kugombea kijana huyu ni tishio mno.Hatumuombei mabaya
lakini ikiwa kama atapona anaweza kuwa tishio kwetu.Lakini hawezi kutusumbua kwa sababu nguvu yake
katika chama bado ndogo.Kitu cha msingi kwa sasa ni kuanza kuchunguza wenzetu kambi ya rais
wanajiandaa vipi na nguvu yao ikoje.Mchakato huu ni lazima tuanze mapema sana.Sina wasi wasi na
utendaji wenu kwa sababu kazi yenu tayari inaonekana.Tunakotakiwa kuongeza nguvu kwa sasa ni kwa
wajumbe wa mikoani .Intakiwa tujiimarishe kule zaidi ii kusiwe na taizo la uungwaji mkono”
WHITE HOUSE ROMANCE SEHEMU YA SABA
ILIPOSHIA SEHEMU ILIYOPITA
Dr Sandra akahisi kijasho kikimtoka baada ya taarifa ile ya Dr Jacob.Akakohoa kidogo kutafuta
sauti halafu kasema
“Dr Jacob nashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na ugunduzi mliogundua.Kwa ufupi tu ni kwamaba
huyu mgonjwa ni mwanasiasa.Ni mbunge ambaye anapendwa na watu wengi .Kupendwa huko kumemfanaya awe
na maadui wengi vile vile.Nina imani hata sumu hiyo iliwekwa makusudi na maadui zake kisiasa.Dr
Jacob naomba mfanye kila linalowezekana ili mgonjwa huyu apone kwa sababu ni tumaini la
wengi.Naomba vile vile asiruhusiwe mtu yeyote kuja kumuona mgonjwa zaidi yangu mimi au
nitakayemruhusu kwa sababu watu hawa waliofanya hivi hawatasita kumfuata Roma hadi huku .”
“Usihofu kitu Dr Sandra.Hopitali yetu ina usalama mkubwa na hakuna mtu yeyote anayeweza kuja
kufanya kitendo chochote kibaya hapa.hata hivyo tutafanya kama ulivyoomba na hatutamruhusu mtu
yeyote kwenda kuonana na mgonjwa.Kwa sasa operesheni inaandaliwa na baada ya masaa mawili tutakuwa
tumeanza na tutakutaarifu kila kitu kitakavyokuwa kikiendelea.Naahidi kumshughulikia mgonjwa huyu
kwa kila namna tunayoweza ili apone kwa heshima yako.Hospitali yako na yetu zimekuwa marafiki kwa
muda mrefu sasa,kwa hiyo naomba uwe na amani ya moyo”
Dr Sandra akatabasamu ,akaagana na Dr Jacob akatoka kuelekea madukani kwa ajili ya kujinunulia
vitu vichache vya kutumia kwa muda atakaokuwa hapo Haifa
ENDELEA...........................................................................................
.
Ni saa mbili za usiku katika ikulu ndogo mjini Dodoma rais wa Tanzania Mzee Jeremy Mpama akiwa na
rafiki yake mkubwa ,mfanya biashara maarufu na kada wa chama Mr Nkebo, katika bustani ya ikulu
ndogo .Walikuwa wakipata chakula cha usiku huku wakibadilishana mawili matatu.Ni mr Nkebo ndiye
aliyeomba kuonana na Mzee Mpama kwa usiku huu .Jeremy Mpama hakuweza kukataa ombi la Mr Nkebo kwa
kuwa ni mmoja kati ya watu muhimu na anaowaheshimu sana.Ni kwa sababu ya kutambua umuhimu wake
ndio maana usiku huu rais alivunja ratiba zake ili kupata wasaa wa kuonana na kada huyu wa chama
“Mr President tumepotezana sana siku za karibuni” Akasema Mr Nkebo huku ajimimnia mvinyo katika
glasi yake
“Ndiyo Mr Nkebo kwa miezi kama mitatu mine iliyopita imekuwa ni kipindi cha kazi nyingi
kwangu.Nimekuwa na ziara nyingi za kimataifa na ndio maana nimekuwa sipatikani mara kwa mara.Leo
uliponipigia simu kuwa uko Dodoma na ukaomba kama nina nafasi tuonane nilifurahi sana kwa kuwa ni
muda hatujaonana.Vipi biashara zinaendaje?
“Mr President biashara zinakwenda vizuri licha ya kushuka kwa thamani ya shilingi na kuongezeka
kwa bei ya mafuta katika soko la dunia bado tunafanya biashara nzuri” Akasema Mr Nkebo
“Hilo la kushuka kwa thamani ya shilingi yetu linatuumiza vichwa mimi na viongozi wenzangu
serikalini.Nina imani tutafanikiwa kuifanya shilingi yetu iwe na thamani tena”
“ndiyo Mr Pesident nakuamini utafanikiwa katika hilo.Naamini kwa watu uliowapa dhamana ya
kulishghulikia suala hiloni wachapa kazi hodari .”
Mzee Jeremy akacheka kidogo akainua glasi yake ya mvinyo nakupiga funda dogo.
“Mr President vipi upepo wa kisiasa unakwendaje ?manake naona vuguvugu la urais limeanza kupamba
moto”
“Yah! Mr Nkebo upepo wa kisiasa si mbaya japokuwa kuna changamoto nyingi na vikwazo vingi
lakini sina wasi wasi na kuteuliwa tena na chama changu kugombea urais kwa awamu ya pili”
“Hata mimi Mr president sina wasi wasi na hilo lakini kwa hali tuliyopanza kuiona kwa sasa
inaonekana hamasa ya kuwania uteuzi hii imeongezeka sana ndani ya chama.Japo hatujui bado nani na
nani wana nia ya kuwania uteuzi huo lakini tayari dalili zimekwisha anza kujionyesha na ni dhahiri
unaweza ukakumbana na upinzani mkali sana.”
“Nakubaliana na wewe Mr Nkebo upinzani utakuwepo.Lakini hebu nipe picha halisi ya upepo
unavyouona Mr Nkebo kwa sababu wewe ni mshauri wangu mzuri sana katika mambo kama haya”
Sura ya Mr Nkebo ikapambwa na tabasamu pana.Akainua glasi yake akapiga funda kubwa halafu
akasema.
“Mr President tayari ndani ya chama kuna watu wamekwisha anza kutengeneza makundi ya kuhakikisha
kuwa wanashinda katika uteuzi huo.” Kauli ile inamfanya Mzee Jeremy kujiweka sawa na kumsikiliza
Mr Nkebo kwa makini.
“jana usiku nilipata taarifa toka katika moja ya vyombo vyangu vya taarifa kilichokuwapo katika
kikao kimoja cha siri kilichoendeshwa katika hoteli ya Dodoma palace .Mr Damian Mwamba tayari
amekwisha anza mbio za kuwania uteuzi huo.Na kwa taarifa zenye uhakika tayari amekuwa na uungwaji
mkono wa kuridhisha toka kwa wajumbe.Timu aliyoiteua ifanye kazi hii inafanya kazi yake kwa
umakini na usiri mkubwa na kusema ukweli hawalali.Wanafanaya kazi usiku na mchana.Mr Damian
hajaanza mbio hizi jana wala juzi.Ameanza kitambo sana.Wakati akitafuta uungwaji mkono katika
miongoni mwa wajumbe wa chama ,amekuwa pia akijijengea jina katika jamii.Kwa hivi sasa jina la Mr
Damiani linatajwa sana katika orodha ya watu weye sifa na uwezo wa kuiongoza nchi hii.Amekuwa
akitoa misaada mbali mbali katioka mashule,kwa wanafunzi,vikundi vya akina mama na vijana,amejenga
mashule na kila linapotokea suala lolote la ktaifa amekuwa mstari wa mbele sana.Si kwamba
namuhofia Mr Damiani lakini kwa kasi anayokwenda nayo ndiyo iliyonisukuma kutaka kuonana na we ili
tujadili kwa kina kuhusu suala hili.”
Mheshimiwa Rais akapumua kwa nguvu na kumuangalia Mr Nkebo usoni.Alionyesha uoga wa dhairi kwa
maneno yale aliyoambiwa. Nkebo akanywa tena funda lingine la mvinyo halafu akaichukua chupa na
kumimina tena mvinyo katika glasi yake.Mzee Jeremy alikuwa kimya kabisa.
“Mr president,wewe ni rafiki yangu,umeshanisaidia katika mambo mengi sana kwa hiyo kunapokuwa na
suala lolote lile ambalo ninajua si zuri kwa upande wako ni lazima nikwambie.Kuna kitu umekifanya
jana ambacho kwa kweli lilikuwa kosa ingawa hukulifahamu.Ni kuhusu yule mbunge Roma.nadhani
utakuwa umepata wasaa wa kutazama televisheni kuanzia jana na kuona ni jinsi gani suala la ugonjwa
wake limeviteka vichwa vya watu.Mr President yule kijana ni tishio kubwa kwa sasa.Ugonjwa wake huu
wa ghafla umenistua mno baada ya kuona ni jinsi gani anavyopendwa na watu.Sikufichi mheshimiwa
rais yule kijana ana nguvu kubwa katika jamii.Nchi yote ilizizima baada ya taarifa kusambaa kuwa
amefariki dunia.Kasi anayokuja nayo inaleta wasi wasi mwingi.Kijana huyu atakuwa na hatari kubwa
iwapo atataka agombee urais.Kwa mujibu wa marekebisho ya katiba yaliyofanywa,tayari Roma
anaruhusiwa kikatiba kugombea urais.Na nina imani kuwa hiyo ndiyo nia yake kwa sababu huko mitaani
anadiriki kuitwa rais wa wanyonge.Naelewa nguvu yake katika chama si kubwa lakini anaweza
kushawishiwa kujiunga na chama pinzani ili agombee urais na kama akifanyua hivyo mheshimiwa rais
basi shughuli itakuwa ngumu.Kuna uwezekano mkubwa kijana yule akatwaa nchi.Mheshimiwa rais kosa
ulilolifanya ni kutoa ndege yako kumsafirisha Roma na kuyaokoa maisha yake.Ilitakiwa kijana yule
afariki dunia jana.kama angeondoka usoni pa dunia jana ile basi uwanja wa mapambano ya uras
ungetuhakikishia ushindi upande wetu.”
Mheshimiwa Rais akatoa kitamba ana kujiuta jasho lililoanza kumtoka.akatwaa glasi yake akapiga
funda kubwa na kumgeukia Mr Nkebo.
“Kweli leo nimeamini Mr Nkebo wewe n rafiki yangu wa kweli.Hakuna katika watu wangu wa karibu
aliyekuja na kunieleza mambo uliyonieleza leo.hakuna hata mmoja aliyeweza kugundua hatari iliyoko
mbele yetu.Nashangaa hata hawa washauri wangu wa mambo ya siasa ni kwa nini wamekaa kimya wakati
kumbe kuna hatari kubwa inatukabili.Nadhani hata hawa washauri wangu watakuwa tayari
wamesharubuniwa na ndio maana wamekaa kimya na kusubiri kuanguka kwangu.Kuhusu yule kijana Roma
mimi sikuwa nimejua kama ni kijana hatari.Iwapo ningejua kama ana nguvu ndani ya jamii basi
nisingekubali kutoa ndege yangu impeleke huko Israel akatibiwe.Vile vile lilikuwa ni ombi maalum
la Binti yangu.Unajua Mr Nkebo mimi nina mtoto mmoja tu na mara nyingi huwa sipendi kumuona akiwa
na huzuni moyoni.Yeye ndiye furaha yangu .kwa maana hiyo nilimuahidi kumpa chochote atakachohitaji
ili kumrudishia furaha yake.Alichokiomba ilikuwa ni ndege yangu na sikuweza kumkatalia kwa sababu
nilikwisha muahidi.Kutokana na majukumu mengi yanayonikabili nashindwa kupata muda hata wa
kufuatilia mambo ya siasa yanavyokwenda nchini .mambo yote yanayohusu mwendendo mzima wa siasa
nimeyakabidhi kwa washauri wangu wa mambo ya siasa.Wameniudhi mno.Haiwezekani wakashindwa kuwa na
taarifa kama hizi wakati kila kitu wanacho.Nimewapa nguvu na kuwawezesha kwa kila kitu ili
kuhakikisha kuwa bado ninaendelea kuwa na nguvu na hatimaye kupata ridhaaya kuongoza tena kipindi
kijacho.Ahsante sana Mr Nkebo kwa taarifa yako.Hapa nilipo nahisi kuchanganyikiwa sijui hata
nifanye kitu gani” Akasema Mzee Jeremy.Huku akitabasamu Mr Nkebo akasema
“Mr President usipate shida yoyote mimi nipo nitakuelekeza nini cha kufanya kama utakuwa tayari
kufuata ushauri wangu”
“Kwa nini inifuate ushauri wako Mr Nkebo wakati wewe ndiye uliyekuja kunifumbua macho? Nielekeze
nifanye nini.Tena kuanzia sasa ningeomba uwe ndiye mshauri wangu wa siri wa mambo haya ya siasa.”
“kama nilivyokwisha kueleza Mr President mimi nipo hapa na niko tayari kukushauri na hatimaye
kuhakikisha kuwa unashinda katika awamu ijayo .Lakini kazi hii siwezi kuifanya mimi peke yangu
.Kitu cha kwanza tunachotakiwa kukifanya ni kuunda timu ndogo ya watu ambayo itafanya kazi ya
kuchunguza mwenendo wa siasa na kuangalia nini tufanye ili tuweze kupata ushindi ambayo itakubidi
mheshimiwa rais uiwezeshe ili iweze kufanya kazi zake kikamilifu bila kugundulika.Timu hii itakuwa
ya watu sita ambao nitakupa majina yao.Ni watu ambao inakupasa uwaamini kwa sababu ni wataalamu
katika michezo hii ya kisiasa.Kitu cha pili ambacho tutakifanya baada ya kuunda timu hii ni
kuwanyamazisha wale wote wanaoonekana kuwa na nguvu kisiasa na kuhatarisha urais wako kwa kipindi
kingine.”
Mzee Jeremy akamtazama Mr Nkebo halafu akauliza.
“Kuwanyamazisha kivipi?
“Mr resident politics is a dirty game and to win this game you need to play dirty too” Akasema Mr
Nkebo.
“Bado sijakuelewa Nkebo hebu nifafanulie vizuri”
“Mheshimiwa rais ninaposema kumnyamazisha mtu yeyote mwenye kuwa na nguvu kisiasa nina maana ya
kumpunguzia nguvu yake aliyonayo na wakati mwingine ikibidi hata kumuondoa katika uso wa dunia hii
iwapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.Kazi hii si kazi rahisi ,inahitaji umakini na wataalamu
wa hali ya juu mno ndiyo maana nikasema inabidi tuwezeshwe ili kufanikisha shughuli kama hizi.Kwa
kuanzia ,tutaanza na wale ambao tayari wamekwisha onyesha wazi dhamira zao za kuwania urais kama
Mr Damian na huyu kijana Roma.Sisi tutawashughulikia bila hata ya mtu yeyote kuhisi kuwa unahusika
kwa namna yoyote na wao.Ninakuhakikishia Mheshimiwa rais kuwa hakuna mtu atakayejua nini
tunakifanya “
Sura ya mheshimiwa rais ikajenga tabasamu pana baada ya uchambuzi wa kina wa jinsi mambo
yatakavyoendeshwa ili kuwamaliza wabaya wake kisiasa.Mpaka wanamaliza maongezi Mzee Jeremy
akamkabidhi rasmi Mr Nkebo jukumu zima la kuhakisha kuwa wale wote wanasiasa wanaoonekana kuwa na
nguvu ndani na nje ya chama na ambao wanaonyesha dhamira ya wazi ya kugombea urais wanamalizwa
kimya kimya.Rais alimuahidi Nkebo kumuwezesha yeye na kamati yake kwa kila kitu
watakachohitaji,kama vile ulinzi na fedha.Saa saba za usiku Mheshimiwa Nkebo akatoka maeneo ya
ikulu ndogo akisindikizwa na walinzi maalum kuelekea katika hoteli aliyopanga.
Siku ya tano toka mheshimiwa Roma ameletwa katika hosopitali hii ya Rambam medical center mjini
Haifa Isarel.Operesheni aliyofanyiwa ili kuondoa sehemu za mwili wake zilizokuwa zimeharibiwa na
sumu ,ilifanikiwa .Madaktari walifanikiwa kuyaokoa maisha ya mbunge Roma.Dr Sandra Mpama hakuweza
kuizuia furaha aliyonayo baada ya kufanikiwa kupambana na kuokoa maisha ya mgonjwa.Kwake huo
ulikuwa ni ushindi mkubwa.Siku zote amekuwa ni mtu wa kuyapigania maisha ya wagonjwa wanaopelekwa
katika hospitali yake hadi mwisho.Moyoni alijipongeza kwa ujasiri aliokuwa nao wa kuweza
kumsafirisha Roma nje ya nchi japo kuwa alikumbana na vikwazo vingi.
Hali ya Roma ilikuwa ikiendelea vizuri siku hadi siku.Licha ya hali yake kuonyesha maendeleo
mazuri ,bado alikuwa katika uangalizi maalum wa kidaktari na kwa muda huo wote hakuna
aliyeruhusiwa kuonana naye.Dr Sandra alikuwa akipewa taarifa mara kwa mara juu ya maendeleo ya
mgonjwa wake.Siku hii Roma aliamka vizuri mchangamfu na anayeweza kuongea vizuri.Madaktari
wakampima na kuona kuwa tayari hakukuwa na hatari yoyote inayomkabili,Dr Sandra akapewa taarifa
kuwa sasa anaweza kuoanana na mgonjwa na bila kuchelewa akaenda hospitalini hapo.Alimkuta Roma
ameaala kitandani
Daktari aliyekuwa akimuhudumia Roma akamtambulisha Dr Sanndra.
“Roma huyu ni Dr Sandra Mpama toka katika hospitali ya moyo ya Tanzania heart hospital.Ni yeye
ndiye aliyekuleata hapa siku ile ukiwa hujitambui.Kwa kiasi kikubwa yeye ndiye shujaa
aliyefanikiwa kuyaokoka maisha yako kwa sababu baada ya kuona kuwa ugonjwa wako ulikuwa mgumu
kutibika katika hospitali yao ikabdii fanye uamuzi wa haraka haraka wa kukuleta huku .Tunamshukuru
mno dokta huyu kwa ujasiri wake.”
Roma alikuwa akitabasamu asiyaamini macho yake.Alikuwa akifahamu kwa kifupi kuwa ugonjw
auliokuwa ukimsumbua ni shinikizo la damu lakini Hakuwa ameambiwa ni jinsi gani alivyofika pale
katika hospitali ile na ni nani aliyempeleka.Alitamani ainuke na kwenda kumkumbatia Dr Sandra
mwokozi wake lakini hakuwa bado na nguvu za kuweza kufanya hivyo.
Dr Sandra aliiona furaha aliyokuwa nayo Roma na kwa kuwa hakuwa na nguvu za kuinuna akamfuata
pale kitandani ,akamkumbatia huku naye machozi yakimtoka akiwa haamini kama ni kweli kijana yule
kipenzi cha wengi alikuwa amepona.
“Thank you God” Akamshukuru Mungu.
“Dr Sandra sijui nikushukuruje kwa namna ulivyoyaokoa msiaha yangu.Wewe ni daktari wa kweli” Roma
alisema huku naye machozi yakimlenga lenga.
“Usijali Roma haya yote ni maongozi ya Mungu.yeye ndiye anayepanga kila kitu kiwe.Sifa zote na
utukufu tumrudishie yeye”
Dr Sandra akaenda kukaa katika kiti kilichokuwa pembeni ya kitanda.Kwa sasa walikuwa wawili tu
chumbani.Dr Sandra yeye alikuwa akiipitia ripoti ya madaktari kuhusu maendeleo ya mgonjwa lakini
Roma bado aliendelea kumtaama Dr Sandra kwa makini.
“Dr Sandra nafurahi mno kukuona .Nilipopata fahamu na kugundua kuwa siko nyumbani nilijiona
mkiwa sana.Sikujua kama ulikuwa uko hapa na mimi.Kwa sasa unakaa wapi? Roma akauliza
“Kwa sasa ninakaa Leonardo hotel” Dr Sandra akajibu.
“Nani anakulipia gharama za hoteli na kila kitu? Roma akauliza tena
“Gharama zote ninalipa mwenyewe? Sandra akajibu huku akitabasamu .Roma akamwangalia kwa mshangao.
“Unalipa mwenyewe? Akauliza.
“Ndiyo mheshimiwa ninalipa mwenyewe.Kwani kuna ubaya wowote?
“hakuna ubaya Dr Sandra ,ila kwa kawaida gharama hizi hulipwa na serikali .”
Dr Sandra akacheka kidogo halafu akasema
“Usijali mheshimiwa Roma.Mimi nitalipa tu si gharama kubwa za kunishinda.”
“Ina maana serikali hawajui kama nimefuatana na wewe huku? Roma akauliza
“Mheshimiwa Roma kuna mambo mengi ya kuongea lakini kwa sasa naomba ujitahidi kwanza upone ,upate
nguvu za kutosha halafu tutakaa na kuongea.
Huku akitabasamu Roma akasema
“Dr Sandra huku tuko ugenini hivyo naomba mambo ya uheshimiwa tuyaweke pembeni.Niite Roma
inatosha.”
Dr Sandra akatabamu na kumuendea Roma pale kitandani.
“Dr Sandra ulisema unaitwa Sandra Mpama?
“Ndiyo. Sandra Mpama? Akajibu Sandra huku akitabasamu
“Are you related in anyway with Mr Jeremy Mpama ?
Kicheko kidogo cha chini chini kikamtoka Dr Sandra
“He’s my father”Akajibu kwa ufupi
“Your father??? Roma akauliza kwa mshangao
“yes.He’s my father.”
Roma akakaa kimya kidogo.
Kumbe ni mtoto wa Rais.Sura yake si ngeni machoni mwangu.Ni kama nimeshwahi kumuona
sehemu.Nadhani tumeshakutana mara kadhaa katika dhifa za kitaifa ikulu.Sasa nimeshapata picha kuna
kipindi niliwahi kusikia kuwa kuna hospitali kubwa na nzuri ya maradhi ya moyo imefunguliwa
inaongozwa na mtoto wa rais.baadhi ya watu walikuwa wakihoji alikoweza kupata fedha za kujenga
hospitali hiyo kubwa na ya kisasa.Hospitali hii ndiyo iliyoniokoa.Daktari wake ndiye aliyeyaokoa
maisha yangu..Lakini kuna kitu bado kinanisumbua akiliyangu.Iweje niletwe huku Israel kwa
shinikizo la damu,ugionjwa ambao hospitali zetu nyumbani zina uwezo wa kuutibu? Japokuwa
ninaendelea vizuri lakini nahisi ni kama upotevu wa fedha za serikali.Au kuna ugonjwa mwingine
mkubwa na wanashindwa kuniambia? Yawezekana kuna kitu wananificha.Haiwezekani nipoteze mamilioni
ya fedha kwa ajili ya kutibiwa shinikizo la damu nje ya nchi.lakini kama ni ugonjwa mwingine