mmmmh


oo

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

MAANA YA TABASAMU

Tabasamu ni dirisha linaloonesha nini kilichopo ndani ya moyo wa mtu, ni kitu kinachonyoosha kila kitu kuwa katika mstari ulioonyoka.
Ukiwa mtu wa kutabasamu unakuwa na marafiki wengi na ukiwa mtu wa ndita watu huanza kukukwepa.
Kila unapotabasamu kwa mtu yeyote ni ishara ya upendo, ni zawadi kwa yule mtu ni kitu kizuri.
Tabasamu ni kusema karibu, tabasamu ni uwezo ambao unaweza kuifanya siku ya giza kuwa siku ya nuru, huweza kufanya pasipo na upendo kuwa na upendo.MAANA YA TABASAMU?
Inagharimu misuli 17 tu kutabasamu na inakugharimu misuli 43 kuwa na ndita kwa nini ujizeeshe mapema?
Amani huanza kwa tabasamu!
Huwezi kuvaa ukapendeza bila kuvaa tabasamu, huwezi kuwa mrembo bila kuvaa tabasamu huwezi kuitwa beautiful one kama hujavaa tabasamu huwezi kuitwa handsome kama hujavaa tabasamu period!
Tafiti zinaonesha mtu anayetabasamu huwezi kuongeza miaka mingi katika maisha yake.
Hata hivyo watoto hujifunza kutabasamu kutoka kwa wazazi wao.

No comments:

visitors comments