1. Mapenzi kitu ajabu, yakutia bumbuwazi
Yakufanya uwe bubu, kujibu huwa huwezi
Shubiri kwako zabibu, na vitamu huviwezi.
2. Wamkuta kaemewa, asemayo hayajuwi
Aumba akiumbuwa, aona maruwiruwi
Vigumu kumuopowa, na kwa ngisi kumvuwi.
▬▬▬▬▬▬▬▬ஜ۩۞۩ஜ▬▬▬▬▬▬▬
3. Hukumbuka ya zamani, yote walofanyiana
Nyumbani barabarani, ayaona kama jana
Akili yake ya nyani, aruka inagongana.
4. Wangoja nyota ya jaha, kutwa wewe unahaha
Mawazo yako silaha, akukwaaye usaha
Usifanyiwe msaha, waugeuza karaha.
5. Kalelewa kaleleka, utani kwake ni mwiko
Njiani yeye na kaka, hapokei mualiko
Ghadhabu zake za paka, hapendi maziko.
No comments:
Post a Comment