mmmmh


oo

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

sms za vichekesho

AMRI KUMI KWA WAPENDAO OFA
1. Muheshimu anayekununulia
2. Muamkie mtoa ofa kabla hujakaa kitini
3. Uwe ndie mchekeshaji wa kikao, lakini usimkatishe mazungumzo anaetoa ofa
. Mtoa ofa akikutuma popote usikatae
6. Mtoa ofa akiupenda muziki fulani, we anza kucheza kwa bidii kabisa
8. Usinywe kwa pupa, kunywa mafunda madogomadogo
10. Mtoa ofa akitoa kichekesho cheka sana hata kama hakichekeshi
............................
...Uhali gani mteja wangu? Leo tunapeana discount kwa wanunuzi wote wa kuku. Nina kila aina za KUKU kama vile:
1.KUKUwaza
2.KUKUpenda.
3.KUKUmiss
4.KUKUona
5.KUKUalika
6.KUKUpigia
7.KUKUjali
8.KUKUngoja 9.KUKUsifu 10.KUKUsalimu.
11.KUKUtumia Sms.
12.KUKUlamba
13.KUKUsumbua
14.KUKUfil...
15.KUKUwanga
16.KUKUnyonya
17.KUKUtukana
18.KUKUtakia siku njema

Hebu niambie, unahitaji kuku gani?

................................
...MVUTA bangi alikwenda kwa
daktari na kumwambia.

“Mara nyingi huwa nazungumza na watu,
lakini cha kushangaza watu hao huwa
siwaoni, utanisaidiaje daktari?”

Daktari: “Ni wakati gani huwa inakujia
hali kama hiyo?”

Mvuta bangi: “Mara nyingi pale
ninapoongea nao kwa simu.”
.............................
...Hii imetokea huko Manzese Jijini D'salaam.
dogo mmoja umri 12, awaacha watu midomo wazi ni baada ya kuingia club na kuagiza bia ya "kilimanjaro" kama vyupa 11.

Kimbembe ni pale waiter alipokuja na kuhitaji malipo.

Mara Dogo" kazama mfukoni na kuchomoa bango la Kilimanjaro ambalo chini limeandikwa kwa maandishi makubwa:

"ONYO, HAIUZWI KWA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18"

(Hii ikiwa na maana wanapewa bure)
..............................
Jeuri dawa yake kiburi;

Gari imeondoka KARIAKOO kufika MANZESE konda akauliza kuna mtu anashuka?

Abiria 1 akajibu: "Tumeziacha nyumbani tuna mitandio tu."

kufika mbele..

abiria mwenye nyodo akawa anashuka UBUNGO MAZIWA. Akasema;

"Konda nashuka maziwa."

Konda akamjibu;

"Itabidi urudi mjini ukanunue Sidiria."
.....................
...Mzee bahili balaaaa...

Mtoto: Mama, nimemuomba baba hela ya kusuka akaninyoa nywele.
Mama: shukuru Mungu mwnangu, ungemuomba hela ya whitedent angekung'oa meno...!!
...............................
..TUWE MAKINI NA LUGHA 2NAZO 2MIA
mama na dokta
dokta;dah Mungu mkubwa mama.
mama;kwa nini dokta?
dokta;yani umezaa JEMBE mama
mama;(kazimia)
;kumbe dokta alimaanisha kazaa kidume hahahahahhahahahaha
....................
..Jamaa yangu mmoja alikuja kunitembelea kule Mburahati Madoto. Sasa wakati namsindikiza tukafika kituo cha madoto mwisho

kusubiri daladala. Mara jamaa yangu akanyewa na kunguru kichwani. Jamaa akaangalia juu alivyogundua amenyewa akamuona

kungulu usawa wake, jamaa akaangua kicheko sana yaani. Mi nilikuwa naona yote yanayotokea nikamuuliza “sasa unacheka nini

ndugu yangu wakati umenyewa?” Jamaa akajibu “We acha tu, afadhali bata hawapai angani kama kunguru”
....................
...Mama mmoja alimtuma mwanawe wa miaka sita (6) aende dukani akanunue unga robo na maharagwe. Wakati mwanae anatoka

akamwambia

Mama: Angalia magari barabarani siku hizi ajali nyingi

Mtoto1: Haya mama

Baada ya saa moja kupita mama akaona huyu mtoto atakuwa amepotea ama anacheza akamtuma mtoto mwingine akamuangalie na

amwambie arudi haraka. Wakati anatoka huyu mtoto mama akamkumbusha

Mama: angalia magari huko kuna ajali

Mtoto2: Haya

Mtoto huyu nae akaenda.

Baada ya saa jingine kuisha mama akatoka kwa hasira na kuwafata huko dukani. Alipofika barabarani kabla hajavuka kwenda

dukani akawaona watoto wake wamekaa katika matofali wanaangalia magari

Mama: (Kwa hasira) Nyi wa#@nz mnafanya nini hapa

Mtoto1: Tunaangalia magari

Mama: mitoto mijinga kweli, ndo nilichokutuma hicho?

Mtoto2: Usijali ndo nasubiri ajali niruidi
.....................
.Jamaa alipita sehemu isiyoruhusiwa katika kambi ya jeshi na akapewa adhabu ya kuhamisha tofali 1000!
Jamaa akajitahidi akabeba tofal 900 na akawa hoi! Na ghafla akakumbuka kuwa mkuu wa kambi ni rafik yake wamesoma pamoja,

akampigia simu.
Jamaa,”mkuu, vijana wako wamenipa adhabu ya kuhamisha matofali 1000!”
Mkuu,”hao wajinga kweli hawajui tunavyofahamiana! Wasikusumbue,mi ndo mkuu wao. Zirudishe palepale zilipokuwa mwanzo,

halafu uje ofisini tuonane.” Jamaa wacha alie.
............................
..NANI FALA ZAIDI?

BABA: Sikiliza Dogo akija mtu
kunitafuta mwambie nimesafiri
DOGO: Sawa baba...............
MGENI: Dogo baba yako yupo?
DOGO: Baba kasafiri
MGENI: Kaenda wapi?
DOGO: Ngoja nikamuulize................
DOGO: Mgeni anauliza umesafiri
umeenda wapi?
BABA:Mwambie nimeenda
Songea.........
DOGO: Baba kasema ameenda
Songea.
MGENI: Basi akirudi mwambie
anitaarifu..
......................
.TANGAZO!
kwa wasio na VING'AMUZI
majumbani Kwao!
kwetu tunaonyesha vpindi
vifuatavyo!
1-Taarifa ya Habari Tshs 250/=
2-Tamthilia ya ITV&STAR-TV Tshs
400/=
3-SPORTS BAR Tsh 300/=
4-WATOTO SHOW Tshs 150/=
5-CARTOUN Tsh 200/=

Tafadhali ukija uje na pesa kamili
Change hatuna.
na uje na mfuko wa kuwekea
NDALA..
...................
...Hii imetokea huko ujerumani ambapo daktari mmoja wa vichaa mwenye hospitali yake binafsi alikuwa anasafiri na vichaa

wake watatu wenye nafuu katika ndege ndogo toka mji mmoja kwenda mji mwingine.

Wakiwa hewani wagonjwa wawili walikuwa wanacheza cheza na kupiga kelele ndani ya ndege kwa nyuma wakati mmoja ametulia

kimya akiwa ameshika gazeti. Kelele zilikuwa zinasumbua kiasi fulandi ndipo Yule mgonjwa aliyekuwa kimya akaenda kwa

daktari mbele katika chumba cha kuongozea ndege na kuzungumza na daktari wao

Mgonjwa: Samahani dokta, nilikuwa nafikiri kama tungewapa mipira wachezee ili wapunguze kelele

Daktari: Ni sawa haina tatizo, wazo zuri sana

Yule mgonjwa akarudi nyuma kwa wenzie kisha baada ya kama dakika kumi hivi kule nyuma kulikuwa kimya kabisa. Daktari

akafurahishwa mno na ubunifu wa yule mgonjwa mmoja na kuona kuwa maendeleo yake ni mazuri.

Daktari akataka kuwapa pongezi kwa kukaa kimya, akamuita yule mgonjwa aliyetoa wazo na kumuuliza

Daktari: aisee! Wazo lako ni zuri sana, waambie wenzio kuwa tukifika nitawapa zawadi kwa utulivu wa leo

Mgonjwa: nilipata wazo zuri zaidi ya lile, nilipowapa mpira nikawafungulia mlango wakachezee barazani. Wakiingia ndani

nitawaambia. Shukrani dokta.
.........................
...Mama mmoja alimtuma mwanawe wa miaka sita (6) aende dukani akanunue unga robo na maharagwe. Wakati mwanae anatoka

akamwambia

Mama: Angalia magari barabarani siku hizi ajali nyingi

Mtoto1: Haya mama

Baada ya saa moja kupita mama akaona
 huyu mtoto atakuwa amepotea ama
anacheza akamtuma mtoto mwingine
akamuangalie na amwambie arudi haraka.
 Wakati anatoka huyu mtoto mama akamkumbusha

Mama: angalia magari huko kuna ajali

Mtoto2: Haya

Mtoto huyu nae akaenda.

Baada ya saa jingine kuisha mama akatoka
 kwa hasira na kuwafata huko dukani.
 Alipofika barabarani kabla hajavuka
 kwenda dukani akawaona watoto wake
wamekaa katika matofali wanaangalia magari

Mama: (Kwa hasira) Nyi wa#@nz mnafanya nini hapa

Mtoto1: Tunaangalia magari

Mama: mitoto mijinga kweli, ndo nilichokutuma hicho?

Mtoto2: Usijali ndo nasubiri ajali niruidi
......................
.Jamaa alipita sehemu isiyoruhusiwa katika
kambi ya jeshi na akapewa adhabu ya kuhamisha
tofali 1000!
Jamaa akajitahidi akabeba tofal 900 na
akawa hoi! Na ghafla akakumbuka kuwa mkuu
 wa kambi ni rafik yake wamesoma pamoja,
akampigia simu.
Jamaa,”mkuu, vijana wako wamenipa adhabu
 ya kuhamisha matofali 1000!”

Mkuu,”hao wajinga kweli hawajui tunavyofahamiana!
 Wasikusumbue,mi ndo mkuu wao. Zirudishe palepale
 zilipokuwa mwanzo, halafu uje ofisini tuonane.”
 Jamaa wacha alie.
........................
Vichaa waliambiwa watengeneze TV kwakutumia mabox.
Siku ya kuleta TV vichaa wote wakaleta mabox
 yao kasoro mmoja aliyekuja na karatasi.
Dokta akahisi amepona,akamuuliza we vp mbona
umeleta karatasi?
Kichaa: Hamna dokta hii ni FLAT SCREEN.
....................
..Jamaa aliingia hotelini:
JAMAA:
waiter nipe soda na mpe
kila mtu humu ndana soda,maana
wakati napata kinywaji lazma kila
m2 apate kinywaji.
Haraka sana waiter akagawa
vinywaji.
JAMAA:
waiter nipe supu na kila m2
mpe supu maana ninapokunywa
supu kila m2 lazma anywe supu.
Watu wakapewa supu tena safari
hii wakampigia makofi.
JAMaa:
waiter nipe bili,na kila m2 mpe
bili yake maana wakati nalipa bili
yangu lazma kila m2 alipe yake!
Vya bure hakunaaaaaaaaaa aa!
utaumiaaaaaaaa! akalipa yake na kwenda zake..
.....................
Shule ya singi JANJA JANJA...Ticha: Ni nani
 aliye muua mkwawa?
Dent 1: sio mimi ?
Dent2: wala sihusiki!.
Dent3:kwanz mi jana sikuja shule!!.
Ticha alipoona kuwa wanafunzi wote majuha ,
 akaamua kumwita mkuu wa shule awaulize tena
 mambo yakawa vile vile ndipo mwalimu mkuu akamwita
 mwalimu pembeni na kumuuliza hivi.
"HIVi UNA UHAkiKa MUUAJI YUPO DARASA HIli?..
...................
amaa alikuwa na wasi wasi kuwa mkewe si
 mwaminifu akapanga safari feki. Usiku
akamtafuta rafiki yake wakamfumanie kwa
 ushahidi. Wakanyata nyata na kufungua
 milango mpaka chumbani, jamaa na pisto
tayari mkononi, ile kufunua blanketi kweli
 wakamkuta bibie na mwanaume. Jamaa
kapandisha hasira anataka kumtwanga
risasi mgongoni.
MKE: Chonde chonde mume wangu subiri,
 huyu ndie mfadhili wetu, analipia ada
ya shule ya watoto, ndie aliyefanya mpango
ukapata kazi, ndie aliye nunua friji,
 home theatre, TV amelipia DSTV miezi
 sita,hata kodi ya nyumba sikukopa kama
 nilivyosema alilipa yeye.
MUME: Aise poleni mfunike blanketi vizuri
 asije akaumwa na mmbu.
...................
Bado tupo kwenye msiba wa ndugu zetu form
 four hivyo tuungane wote kwa kusema
"NECTA IMETOA NECTA IMETWAA, FORM FIVE
 WALIIPENDA LAKINI KITAA KUMEWAPENDAZAIDI,
 JINA LA NECTA LIHIMIDIWE MILELE AMINA!"
...................
Mbwa koko wawili walikuwa wanasaka chakula
 kwenye jalala mara ikapita Land Rover ya
FFU na ndani yake kuna mbwa wa Polisi;
 Mbwa koko mmoja akaangalia kwa uchungu
kisha akamwambia mwenzie, "Unaona wenzetu
 waliosoma, wale wanaenda kazini.
...............
Kulikuwa na washtakiwa watatu,
Mmasai, Mmakonde na Mchaga. Wote
waliukumiwa kufa/kuwawa kwa
kukutwa na madawa ya kulevya, kule
Jamhuri ya wa watu wa China. Serikali
ya China kwa kuzingatia mahusiano
mazuri na serikali ya Tanzania, askari
magereza akawashauri wachague jinsi
yanavyopenda kufa. Wakatakiwa
wachague aina tatu ya jinsi ya
kuuwawa. Aidha kwa bunduki, kupigwa
sindano ya virus vya aids/hiv. au
kunyongwa hadi kufa!!
Mmasai akafikiri sana akasema:
bwanya azkari, nipige pistori. Askari
wakafyatua risasi, Mmasai akafa...!
Mmakonde: Mimi bana achikari
ninyonge bachi, niuwawee. Mmakonde
akanyongwa hadi kufa.
Mchaga. Mimi nazubiri unipatie hiyo
injection ya viruzi vya aidz. Askari
magereza wakampiga sindano ya virus.
Ghafla mchaga akaanza kucheka,
akacheka akacheka sana. Askari
akashangaa na akamuliza unacheka
nini. Mchaga akajibu:
Wewe azkari mpumbafu zana. Aisee
babangu Mimi nimevaa kondom...
........................
Kuna jamaa moja alienda kuiba kuku alipoona
anafuatwa akakimbilia mtoni.. Alafu jamaa
 kufika mtoni akamtoa kuku manyoya kisha
akamrusha kwenye maji.. Watu walipofika
 wakamuuliza: kuku yuko wapi!?..
Akajibu kenda kuogelewa yule kule amenipa nguo zake nimshikie
akawaonesha manyoya, watu wote wakabaki midomo wazi
 kwa mshangao kuona kuku kweli anaogelea..
.........................
Mwlim wa CRE aliuliza,watu "wangapi wange penda kuenda mbinguni?"watu wote waka nyosha mikono except mmoja,mwlim akauliza

tena "wangapi wange pendakubaki?"ha­kuna alienyosha,mwli­m akamuuliza yule ambae hakunyosha wewe ungependa kuenda wapi?

mwnf"nyumb­ani."
..................
Mume mvivu aambiwa na mke wake :mume wangu si unisaidie kazi za bustani
MUME: kwani mi ni houseboy?
MKE: basi nisaidie kutengeza mlango
MUME: kwani mi ni carpenter?
MKE: basi nisaidie kutupa taka taka,:
MUME: kwani mi ni munisper?
(mume aliporudi jioni)mke wangu nani amesafisha bustani,akatengeza mlango na kutupa taka?
MKE:ni jirani ye2 swaleh lakini alinipa options mbili nimpe wali ama nilale nae,
MUME:hahaha,najua ulimpa wali,
MKE: Kwani mi ni hoteli?nililala nae kwa taarifa yako
........................
Wakiwa mbugani baba na mwanawe.
Dadi onaile mnyama!
Baba:c ninyani yule
mtot:na zile ki2 za blue ni nini
baba: ni tyre
nyumbani baba katoka safarini kajifunga taulo na mara kakaa vicvyo
mtot:dady tairi zako zimeisha upepo ona vile zimesinyaa huku akibofya
..................
Kuna makonde mmoja alienda kwa muuza chipsi
MTEJA.nikaangie chahani moja
MUUZAJI.tomato unataka?
MTEJA.tomato chili
MUUZAJI.akamuekea kila kitu............
MTEJA.akasusa kwa kusema...... Nchakwambia tomato chili chacha wewe umeweka chacha chitaki.......!
..................
Mwanafunzi makini...

Mwalimu wa somo la hesabu alimuuliza mwanafunzi wake
"Juma, kama kuna ndege mia kwenye mti, ukichukua bunduki yako
na kuwapiga ndege ishirini na saba, ndege wangapi watabaki kwenye mti?
Juma akamjibu "Hakuna ndege atakaebaki, wote wataruka na kukimbia
kwa kuogopa kishindo cha bunduki"
Mwalimu akamwambia " Hapana, watabaki ndege sabini na tatu. Hata hivyo
nimependa jinsi unavyofikiri mbali zaidi...uko makini.
Juma akamwambia "Mwalimu na mimi nina swali, kama kuna wanawake
watatu kwenye mgahawa wanakula 'cone icecream' mmoja anakula kwa
kuilamba, mwingine anakula kwa kuimega vipande na wa tatu anakula kwa
kuinyonya, unadhani ni yupi aliye olewa (mwenye mume) kati ya hao?
Mwalimu akamjibu "Bila shaka ni yule anaekula kwa kuinyonya"
Juma akamwambia "hapana mwalimu umekosea...ni yule mwenye pete ya ndoa,
hata hivyo na mimi nimependa sana jinsi unavyofikiri mbali zaidi..."
.........................
mama anamuuliza mwanaye,"we juma,hee!!alfajiri yote mbona unawahi shuleni leo?
juma:mwalimu wa bagia leo anakuja asubuhi nikichelewa nitakuta zimeisha
mama:pumbavu siyo kuwahi masomo bali bagia?
juma:ndiyo siwanasemaga elimu haina mwisho lakini bagia nikichelewa zinaisha..

mama hoi!!!!!!!!!!!!!!
......................
Jamaa anamatatizo kaingia kwa daktari
JAMAA=dokta ninatatizo huku chini
DOKTA=hebu vua tone
JAMAA=navua ila usunicheke ,plz dkt
usinicheke
DOCKTA=usijali mimi hii ndo kazi yangu siwezi
kumcheka mgojwa ,jamaa akavua suruari
kuonesha DUSHELELE(¡) yake ,basi dokta
kuona ustaarabu ukamshinda akaanza
kucheka kama dk3 hadi machozi yakamtoka
kwani DUSHELELE(uume) ya jamaa ni kadogo
kama betrii ya AAA(betrii za remote ya
TV)daktari alipomaliza kucheka mazungumzo
yakaendelea
DOKTA=enhee tatizo nini
JAMAA=imevimba toka juzi ,,dokta akazimia
pale pale
....................
NAKUPA HABARI NJEMA ZA KIAFYA

"Usiongee na Simu kwa Sikio la Kulia.
Usimeze Dawa kwa Maji ya Baridi.
Muda Mzuri wa Kulala ni baina saa 4 usiku hadi 10 alfajiri.
Hutakiwi Kula sana ifikapo saa 11 jioni nakuendelea.
Hutakiwi Kulala Pindi Utokapo Kula.
Simu inapokaribia Kwisha Chaji ni Hatari Kuitumia Kwani Mionzi huwa Effective Mara 1000.
Pendelea Kulalia Ubavu wa Kulia au Mgongo ili Kuepusha Matatizo ya Moyo.
..................................
..........aliumwa na Nyoka.akaanza kucheka hadimachozi yakamtoka.Juma akamwona akamwuliza,"mbona unacheka na umeumwa na

Nyoka?" Salim akajibu, "namcheka huyu Nyoka,juu nina UKIMWI !!"
...................
Wizi ulifanyika katika nyumba ya mpare na muhusika baada ya kufuatilia aligundua kuwa aliyemuibia ng’ombe wake alikuwa ni

Mmasai mmoja wa ng’ambo ya pili;

Mpare alifungulia kesi ya wizi na mahojiano mahakamani yalikuwa kama ifuatavyo:

* Mmasai: Wewe anasema mimi nimeiba hiyo Ng'ombe yako,
= Mpare: Ndiyo

* Mmasai: Niliingia kwa ile mlango ya nyuma ama ya mbele
= Mpare: Ya nyuma

* Mmasai: Imekosa, niliingia kwa ile mlango ya nyuma ya nyumba
* Mmasai: Nilipokuswaga ile ng’ombe dume alitangulia mbele au alikuwa nyuma
= Mpare: Uliswag Ng’ombe kwa nyuma

*Mmasai: Mekosa tena, Alienda kwa mbele ng’ombe akanifuata yenyewe.
* Mmasai: Je ile Ng’ombe alikuwa iko ngapi?
= Mpare: Ng’ombe walikuwa wako 7

*Mmasai: Amekosa kabisa, ng’ombe alikuwa ni 5 tu!!

TUFANYE WEWE NDO HAKIMU, HEBU TOA HUKUMU...!!
......................
Ki2ko ", Afisa mmoja alikwenda kwenye shamba la miti kukagua. Msimamizi akamwambia usingie muda huu! Afisa akatoa

kitambulisho cha kazi; "wewe ninani wa kunizuia? Jamaa akamwambia pita tu mzee..! Kupita tu akaanza kupiga makelele:

nyukiii! nakufaaa nyukiii, nisaidie, Jamaa akamjibu "Waonyeshe Kitambulisho
.........................
MUME: “Unajua mi unanishangaza sana, kila
 siku nakusikia mara useme TV yangu,
gari yangu, chumbani kwangu, watoto wangu,
sisi ni mke na mume, kila kitu ni chetu,
jirekebishe bwana.”
Mke akanyamaza kimnyaaaa anaendelea
 na shughuli zake za kupekua kabatini
 kama hasikii, na hakumjibu kitu mumewe!
MUME: Akamuuliza Kwa hamaki: "
Sasa hapo unatafuta nini?"
MKE: “Sidiria yetu!!!
..................................
Ukitaka kujua mwanamke sio ndugu yako soma hii hapa upate undani.
Jamaa karudi toka job mpole!
MKE: vipi leo mbona mapema na mpole?
MUME: ofisi yetu imeungua na watu wote wamekufa, MKE: ilikuwaje wewe ukapona?
MUME: nilikuwa chooni, jirani na ofisi najisaidia.
MKE: Loh masikini familia zao itakuw aje?
MUME: watalipwa milioni 100 kila mfiwa.
MKE KWA HASIRA: ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela..
................................
Wageni wengine noma.Mwenyeji: Utakunywa soda au chai?
Mgeni:Ntakunywa­ soda wakati nasubiri chai ichemke! Mwenyeji:Hapa kuna sprite na coca nikupe ipi?
Mgeni: Nipe coca sprite niwekee kwenye friji iendelee kupoa.
Mwenyeji: Nikupe mkate au maandazi?
Mgeni: Nipe maandazi kwanza mkate ntakula na chai ikichemka. ILIPOFIKA JIONI Mwenyeji: Nkuandalie chips mayai au kuku?
Mgeni: Niandalie chips kuku kwanza,mayai naomba unichemshie 10 tu ili nishushie na ile sprite.MGENI KAMA HUYU WEWE

UTAMFANYAJE?
.............................
CHEZEA PAKA WW?Jamaa alichukua paka wake na kwenda kumtupa mbali aliporudi nyumbani alimkuta paka amekwisha rudi,jamaa

alikasirika sana,Siku ya pili akamchukua na kwenda naye zaidi ya kilometa 50 akapiga chochoro za kutosha kisha akamtupa

akaanza safari ya kurudi nyumbani ,baada ya muda akampigia simu mkewe, Vipi Mke wangu huyo paka yupo?MKE: Ndiyo mume wangu

tena ametulia hapa kwani imekuaje? JAMAA: hebu mpe simu anieelekeze njia ya kurudi nimepotea.
.................................
Mfalme aliwaita w2 wake, akasema
shujaa atakaeogelea kwenye hili
bwawa la mamba nampa binti yangu,
mara akasikia pwaa jamaa kajitosa
kaogelea mpaka upande wa pli,
mfalme akasema nitakupa binti yangu
na mali, jamaa huku akihema kichiz
akasema sitaki binti yako wala
mali namtaka mtu
aliyenisukuma..
.................................
Mhindi aliambiwa amalizie methali za
Kiswahili;
1.Nyani haoni:- valise miwani
2.Debe tupu :- weka dengu
3.Maskini akipata :- itaacha iba
jumbani
4.Penye kuku wengi :- Chinja bili au
tatu
5.Asiyesikia la mkuu :- Peleka yeye
polisi
6.Penye wengi :- iko kutano ya CCM
7.Penye fujo :- hapo iko chadema
8.Bandu bandu? :- Baba yake Somji
iko Bombay
9.Simba mwenda pole :- Huyo
naogopa yanga banah
10.Chovya chovya :- mwisho yake
tapata mimba
11.Mficha uchi :- Bado janyoa huyo
.................................
Vituko shule za kayumba!!!
TICHA:Ok class,lets show the principal and the guests hw far we have reached...if i say small,you say

small,smaller,smallest,the class agreed...
TICHA: small
CLASS: small,smaller,smallest.
TICHA: big
CLASS: big,bigger,biggest.
TICHA: tight.
CLASS: tight,tighter,tightest.
TICHA(smiled): thats good.
CLASS: thats good,thats gooder,thats goodiest.
TICHA: ok.
CLASS: ok,okier,okiest.
TICHA: no.
CLASS: no,noer,noest.
TICHA: stop.
CLASS: stop,stopper,stoppest.
................................

Massawe aliongozana na binti
yake kwenda kwa mwanaume
aliyempa mimba huku akitweta
kwa hasira.
Walipofika ilikuwa hivi:-
KIJANA: Mzee ni kweli mimi
nimempa mimba binti yako, ila
akizaa dume nitakupa daladala
kumi, sheli 3, Maduka 5 na
milioni 50 za mtaji. Akizaa jike,
nitakupa supermarket 3,
mashamba 6 na milioni 40.
BINTI: Je mimba ikitoka?
Massawe: Nyamaza pumbavu we,
si atakupa nyingine...
.............................
DOGO: Baba kwani mimi nimetoka wapi?
BABA: Dah mwanangu mbona unaniuliza swali
gumu hivyo? Ene wei hebu kaa hapo nikuhadithie.
Mimi nilikutana na mama yako siku moja wakati
anatoka kazini, tulikutana kituo cha basi, mvua
kubwa ikaanza ikalazimika tuchelewe sana
kupanda basi, hivyo tukazoeana sana. Baada ya
kama miezi mitatu tukaona ni vema tuoane,
tukawaeleza wazazi wetu wakatukubali, harusi
ikafanyika, tena kubwa sana, tukaanza kuishi
pamoja na kwa kifupi ndio wewe ukapatikana.
Ukikua kidogo utanielewa nina maana gani
DOGO: Haya, ila mwalimu atanipiga
nisipomwambia kesho, katuambia wote tuwaulize
wazazi wetu tumetoka wapi. Mwalimu wetu kasema
yeye ametoka Bukoba
..............................
Jamaa akiwa ametulia beach mzungu akapita akamuliza jamaa "are u relax?
Jamaa hakuelewa akajib No, mzungu mwingine akamuliza vilele akajib No akaona hapa nasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja amekaa akamuliza
"are u relax? Mzungu akajib
"yes"
jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzako.....shenzi, muda wote huo nasumbuliwa kumbe we ndio relax.....
.........................
Mwalimu: Wee Dogo janja bingwa la kuchelewa darasani, naleo umechelewa tena darasani?
Dogo janja: mwalimu mbona leo nimewahi sana, nimekuja hapa ndo kipindi cha kwanza kinaisha.
Mwalimu: pumbavu zako kuja hapa mbele haya taja jamii moja ya mnyama anaeishi baharini na nchi kavu kwa wakati mmoja...
Dogo janja: haa hilo simpo sana mwalimu jibu ni Kaa

Mwalimu: Taja wengine watano wanoishi hivyo

Dongo janja:
1. Mamaake kaa,
2. Babaake kaa,
3. Kakaake kaa,
4. Dadaake kaa na
5. Mdogo wake kaa!.
...................................
Mtanzania, Mnyarwanda, na Mkenya walikamatwa
na madawa ya kulevya China. Wakaambiwa
adhabu ni mbili kifo au adhabu nyingine ambayo
wakiishindwa pia wanauawa.Wakaomba wapewe
hiyo adhabu
nyingine wajaribu bahati yao.Wakapelekwa
msituni wakaambiwa waingie msituni kila mmoja
kwa njia yake halafu kila mmoja arudi na matunda
kumi ya kufanana. Wakaingia msituni kila mtu njia
yake.
Mnyarwanda akarudi wa kwanza.Karudi na maepo
kumi.Akaambiwa adhabu ni kuyameza yote mazima
mazima moja baada ya jingine bila kufumba
macho
bila kulia wala kucheka wala kujitikisa! Akameza
la kwanza.Safi.Kumeza la pili akashindwa
kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi
akafa.
Wa pili Mkenya akaja.Ana vitunda vidogo vidogo
Kumi Vya kufanana Vidogo kama pipi.Akaambiwa
masharti.Akaanza kula bila kufumbua macho wala
kulia wala nini. Alipofika cha tisa akashindwa
kuvumilia akaangua kicheko!Akapigwa risasi pia
akafa.
Wakiwa kuzimu Mnyarwanda akamuuliza
Mkenya.. "Vipi wewe mbona ulishindwa kuvumilia
wakati ulibakisha kitunda kimoja tu?" Mkenya
akajibu: "Kaka, nilishindwa kuzuia kicheko maana
nilimwona Mtanzania anakuja na matikiti
maji!".....
................................
Mitoto isiyopenda shule bwana..! Mwizi aliingia ndani akaiba,
 wakati anaondoka Dogo akamdaka mguu, akamwambia ucpochukua na
 beg langu la shule napiga kelele..!
............................
Mwanafunzi M1 Wa Form IV  Akiwa Kwenye Chumba Cha Mtihani Wa Hesabu, Ghafla Baada Ya Dk 30 Akatoka Kwenye Kiti Akakaa Sakafuni. Msimamizi Akamuuliza Kwa Nini Umekaa Chini? Mwanafunzi Akajibu "Swali Hili La 9 Linasema SOLVE THIS QUESTION WITHOUT USING TABLE''.
Msimamizi  Hoi..! Chezea Shule Za Kata Wewe!.
......................
 
 Hii ni kwa wanachuo wote Tanzania"Kuanzia mwaka huu system imebadilika, ukubwa wa GPA ndio uta-determine urefu wa joho la mahafali"
kutakuwa na;
 joho kama sidiria 1.8-2.0,
 joho kama vest 2.1-2.4,
 joho kama shati 2.5-2.8,
 joho saizi ya mapaja 2.9-3.2,
saizi ya goti 3.3-3.5,
 saizi ya ugoko 3.6-3.9,
saizi ya unyayo 4.0-4.4 na saizi ya shela ya kuvuruta 4.5-5.0.
Imetolewa na TCU.Wajulishe na wengine pindi upatapo ujumbe huu. Jion njema.
.........................
Nirushie "500"
   au "400"
      au "300"
         au "200"
            au "100"
Kama huna nirushie salam,kama huna bac nirushie hata 'MAWE'..!!
..................................
Read More ->>

No comments:

visitors comments